Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Hizo zoooote porojo.

Ukweli ni kwamba walikuwepo wote wanne kwa wakati mmoja Tanzania hii, mwenyeji wao akiwa Kikwete. Obama, Bush, Clinton na Jimmy Carter. Hata kwenye maziko ya Mandela haijatokea hiyo Huyo ndiyo Kikwete. Kumbuka hilo.

Record.

Kwel kuitetea ccm kazi, Mkuu sijaona POINT hapa kwenye maelezo yako zaidi ya kuzunguka zunguka tuu!! Lete facts na kwa bahati mbaya sana watanzania wenyewe hali halisi tunaiona kwa macho yetu haiitaji uwe na digrii kuyafaham mengne lete hoja zenye nguvu mkuu.....kajipange kisha urudi tena!!
 
mjenga nami nakuunga mkono kwa asilimia mia moja na zaidi. lakini sikilizia jinsi wajinga watakavyokushukia....ila usivunjike moyo, penye ukweli sema tu.
Ndugu zangu watanzania wenzangu, kupitia jamvi hili, kwa heshima na taadhima nichukue fursa hii kumwandikia Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, kwanza kumpa pole kwa majukumu mazito aliyonayo katika kulitumikia taifa lake. Ninampa pole kutokana na kutambua ugumu wa majukumu aliyonayo.

Kwa nafasi yake, yeye ndiye wa kutupiwa lawama zote pale mambo yanapokwenda si sawa. Pia ni mtu wa kupongezwa pale mambo yanaponyooka. Hii ni kawaida kwani wahenga walikwushasema kuwa mkubwa ni jalala.

Ndugu zangu watanzania wenzangu, mimi leo ningependa kuzungumzia kazi nzuri ambayo Rais Kukwete ameifanya ambapo hata kama baadhi yetu tutaibeza, ukweli utajidhihirisha.

Kikwete, katika kipindi cha miaka 9 amefanya yafuatayo mazuri;
1. Uchumi; amefanya mabadiliko kwenye kilimo ambapo wakulima wengi kwasasa wanalima kisasa na kwa msaada wa pembejeo za ruzuku.

Walau imesaidia taifa kuwa na akiba ya chakula cha kutosha hivyo kutokuwa na hofu ya wananchi kufa njaa. Kilimo cha umwagiliaji kimeongezeka, kilimo cha biashara kimekua. Mabadiliko ya sheria ya uwekezaji angalau yamewezesha nchi kuanza kunufaika na kodi ya uzalishaji ingawa bado si kwa kiasi kikubwa. Uboreshaji wa huduma za kibenki, mikopo ya saccos, uboreshaji wa njia za uchukuzi kama barabara, vivuko, reli kwa kununua vichwa na mabehewa, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege e.g. Rungwe, Katavi, Gombe, DSM. n.k.

2. Kisiasa; Ni katika kipindi cha Kikwete ambapo uhuru wa shughuli za kisiasa umetolewa. Watanzania sote ni mashahidi kwamba vyama vya siasa vimekuwa huru kiasi kwamba baadhi vimeshindwa kuutumia uhuru huo ambapo baadhi vimeishia kuitisha maandamano, kukitisha chama cha mapinduzi na kutishia uvunjifu wa amani kama mbinu ya kutaka kutimiza adhma zao za kisiasa.

Ni wakati huu ambapo majukwaa ya siasa yametumika kuvitukana na kuvidhalilisha vyombo vya dola kwamba havina lolote. Ni wakati huu ambapo wanasiasa wa vyama pinzani wameachwa kuichambua serikali kwa kadiri ya hazina ya maneno iliyoko vinywani mwao.

Ni wakati huu ambao hakuna mwanasiasa aliwekwa kizuizini kwa kutoa kauli zenye kuhatarisha usalama wa nchi. Wanasiasa baadhi yao walifikia hatua ya kutisha kuwa wanao uwezo wa kuifanya nchi isitaealike, hakuna aliyeshughulika nao.

Aidha ni wakati huu ambao siku moja watu walikuwa wakishuhudia chama fulani kimeitisha maandamano nchi nzima kisha muitisha maandamano akakimbilia South Africa! Kiukweli ni wakati unaelekea mwishonu lkn kwa wanasiasa hasa wa upinzani mtaukumbuka!!!

3. Kijamii; Rais Kikwete amejitahidu kuimarisha huduma za kijamii kama usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, Ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa gesi asilia huko Mtwara ambapo sote tunajua jinsi wanasiasa walivyoupinga na kufanya kila aina ya uchochezi ili usifanikiwe, leo tunashuhudia mradi unelekea kujamilika.

Miradi ya maji vijijini imetekelezwa kwa kasi awamu hii. Upande wa elimu mafanikio yako wazi ambapo ongezeko la ajira za walimu, ongezeko la shule za msingi na sekondari na pia ujenzi wa vyuo vikuu kwa ujumla vimetokea wakati wako.

Maboresho ya mishahara kwa wafanyakazi yamefanyika wakati wako. Kwa upande wa afya, siyo siri ununuzi wa vifaa vya kisasa mahospitalini walau umefanyika wakati huu kwa kiwango cha kuridhisha, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kupitia TASSAF, hospitali za mikoa kuwa za rufaa, mapambano dhidi ya malaria na UKIMWI, uzuiaji wa vifo vya mama wajawazito, juduma bure za matibabu kwa wazee (bado changomoto katika utekelezaji), maboresho ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo sasa ina uwezo wa kutibu magonjwa ambayo awali matibabu yake yalipatikana nje yanchi n.k.

4. Kimataifa; Kwanza amejitahidi kukwepa mitego ya maadui zetu waliotaka kuliingiza taifa vitani kwasababu za chuki binafsi na wivu kutokana na nchi yetu kuanza kukua kiuchumi kwa kasi. Mfano wa nchi hizo sote tunao. Kikwete alijua kwamba vita kwasasa siyo kipaumbele cha nchi ingawa uwezo wa kuwachapa hao maadui zetu tunao.

Alifanya uamuzi mzuri na wa kizalendo. Isingekuwa rahisi kwa Rais asiye busara kuacha kuiingiza nchi vitani dhidi ya Rwanda, Malawi na Kenya wakati ambao nchi hizo zilionesha wazi kuichokoza Tanzania. Ni busara ya kiwango cha juu aliyonayo Kikwete hata kufanikiwa kuukwepa mtego huo.

Pia amejitahidi kusuluhisha migogoro katika nchi mbalimbali kama vile ule wa Kenya mwaka 2008, wa Sudan ya Kusini, Congo DR, Comoro, Afrika ya kusini (wa ndani ya ANC). Amekuwa na ushawishi mkubwa kwa mataifa makubwa kwa kuifuata sawasawa sera mama ya taifa ya kutofungamana na upande wowote kwa lengo la kuiepusha nchi kuwa na uadui unaotokana na mivutano baina ya mataifa makubwa.

Katiba mpya; Jambo hili halijaisha, tumwombe Mungu liishe salama!. Sote ni mashahidi juu ya umahiri alionao Kikwete katika namna anavyolihandle swala hili muhomu kwa mstakabali mwema wa taifa letu. Siyo siri swala hili limegubikwa na mambo mengi lkn mbaya na hatari inayoonekana ni kuibuka kwa kundi la watu linaloipinga katiba iliyopendekezwa.

Sina tatizo na kupingwa huko ola nina tatizo na sababu za kuipinga. Mfano wengi wanadai kuwa katiba pendekezwa imekiondoa kipengele cha uadilifu, si kweli kwani kipengele hicho kipo isipokuwa kiliondolewa kwenye Ibara inayohusu tunu za taifa na kuwekwa kwenye ibara ya maadili ya mtumishi wa umma. Kiukweli uadilifu siyo tunu kwa tafsiri yake bali ni swala la uadilifu.

Tunu ni kama vile Lugha ya kiswahili,amani, muungano n.k. Swala la katiba limeingiliwa na siasa kiasi kwamba watu hawajadili tena kwa uchungu wa kulinda misingi ya utaifa wetu bali kwa maslahi na kupata upenyo wa kisiasa.

Ninaamini kwa umakini wa Rais wetu atasimamia na hatimaye tutapata katiba yenye maslahi mapana ya historia ya taifa letu hasa Muungano, udugu na amani.

My take; Pamoja na mafanikio hayo wapo baadhi ya watanzania ambao wameendelea kubeza kwa namna yoyote ile. Baadhi yao wamediriki kukashifu kwa matusi na kumdhihaki Kikwete kwa lugha mbaya kabisa. Ni kweli hakuna binadamu aliyetimilika kwa kufanya bila kukosea.

Inawezekana katika utendaji wake kuna mahali amekosea hata hivyo sidhani kama anastahili kulaumiwa kiasi hicho. Ninawaambia ndugu zangu watanzania wenzangu, tutamkumbuka Kikwete siku moja!. Wanasiasa hasa wa vyama pinzani iko siku mtamkumbuka Kikwete!.

Waropokaji msio na staha katika kauli zenu mtamkumbuka Kikwete!. Na kwako Mheshimiwa Rais, nikusihi usokate tamaa, endelea kuchapa kazi kwani kama ni ng'ombe umebakiza kipande cha mkia tu!. Ulishawashinda tayari mbona!. Up to this moment, you are the winner Sir!.

Cha muhimu malizia kazi zako na Mungu Baba Mwenyezi atakulipa kwa kazi nzuri uliyowafanyia watanzania. Jifunze kwa Prof. Muhongo, aliyekuwa waziri wako ambaye pamoja na mazuri yote aliyoyafanya mwisho wa siku watanzania wasio shukurani walimwandalia manila na kumnyonga kisiasa hadharani!.

As you signing off Sir keepon praying for your nation ili kikombe cha siasa chafu ya wasaka madaraka hali mikono yao ikinuka rushwa, kiliepushe taifa kuingia kwenye machafuko.
 
Watakuja watu kubeza hayo mafanikio. Mimi huwa nnawaambia wachanganye awamu zote waone kama Kikwete hajafanya zaidi ya wote.

Kweli Kikwete kafanya mambo mengi saana mazuri kwake na familia yake na chama chake.
Kama mauaji ya albino,Kuanguka kwa reli ya kati na TAZARA mwisho ni maisha maguum kwa kila mtanzania mwenye pato la chini na kati.
 
kipimo cha uongozi wenye mafanikio ni ule unaolenga na kupigania kupunguza matatizo ya kijamii, adha, kero, makali na ugumu wa maisha kwa jamii unayoiongoza, kwa kutumia busara ulio nayo kupanga na kugawanya rasilimali za kijamii kwa utaratibu ulio muafaka wenye manufaa ya uhakika kwa jamii.

Pamoja na sifa zoote hizo kwa bwana kikwete, mimi nilimshangaa sana mwanzoni tu, siku ya uteuzi wa baraza la mawaziri 60! Ninaomba kufahamu hapo busara iliyotumika ililenga kitu gani?
 
hii ni shida tosha ya kutojua na kutafsiri uchumi madhubuti, na kwa kweli naona Dalili Zote ambazo TANZANIA inaelekea kwenye arab spring syndrome, ya wana nchi kwenda na ku revolt against its leaders, utaringaje na university 40, wakati absorption rate ya wahitimu kwenda kazini ni only 2% , unatangaza kazi ya vacancy 70 wanakuja 14000 kwa interview, just because wanaenda kwenye interview kupita Barabara ya lami basi Nchi imesonga mbele , huu ni uaji, leo tumekopa na Deni hili watamaliza watoto wa chekechea leo, kwanini hatuoni hayo, mbona mimi nasikia uchungu na kadi yangu ya ccm Mfukoni? Indication ya takwimu ya kuwa Nchi ni fastest growing economy ni machungu ambayo hayana maana bila kuwa na Chembe za good leadership, moreover 90% ya fastest growing economies ziko Afrika na wote wanauza non renewable resources kama sisi dhahabu , nasikitika kuona Nchi hii tumepotea kiasi cha kupitiliza, na huku tunangalia Tofauti kubwa Kati ya tajiri na Masikini ikiongezeka na uchumi wa matajiri wachache ukitumiwa kama statistics za kujivunia, this is madness
Leo ilula, Jana ikwiriri, jana geita, mbeya etc this trend is getting worse and worse
 
Kumbeeee... Amekusikia! Hbr yako ni zao la utafiti kwa walengwa au ripoti za ikulu na wizara mbalimbali?
 
Kila kiongozi including Nyerere ana mazuri na mabaya/kasoro, hakuna aliye kamili
Ni kuangalia mizani tu, kipi kimezidi, mazuri au kasoro. Si malaika hawa!
 
Back
Top Bottom