Jaji Mkuu Profesa Juma awataka Majaji na Mahakimu kutendea haki Kesi za Uchaguzi ili Mahakama isigeuzwe kichaka cha Wanasiasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,930
141,894
Akizungumza kwenye kikao cha kutoa elimu ya namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi kwa majaji na mahakimu, JM Prof Juma amewataka watendaji hao kutoa haki kwa wakati.

Profesa Juma amesema mahakama inapaswa kutoa haki ili isionekane kama tawi linaloweza kutumiwa na Wanasiasa.
Semina hiyo imefanyika mjini Morogoro.Chanzo: ITV habariMaendeleo hayana vyama!

====

Jaji Mkuu ataka kesi za uchaguzi ziwe kwa uwazi haki na bila upendeleo

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amewataka Majaji na Mahakimu kutoa maamuzi ya kesi zinazohusu uchaguzi kwa uwazi, haki na bila upendeleo wowote ili kulinda heshima ya Mhimili wa Mahakama.

JAJI MKUU LEO.jpg

Akifungua mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani yaliyoanza jana Septemba 02,2020 mjini Morogoro, Jaji Mkuu amesema ni uwazi na kufuata sheria tu ndiyo vitaongeza imani ya wananchi kwa Jaji au Hakimu na kwa Mahakama kwa ujumla.

“Kazi yetu na maamuzi yetu yaongozwe na sheria pamoja na ushahidi unaotolewa mbele yetu na si vinginevyo”, alisisitiza.

Aliwataka Majaji na Mahakimu kufahamu kuwa mashauri yanayotokana na Uchaguzi Mkuu hutumiwa na wananchi katika kupima na kutathimini utendaji kazi wa Mahakama ya katika maeneo mbalimbali ya utoaji haki.
tr.jpg


Alisema katika kipindi cha uchaguzi wananchi hupima uhuru wa Jaji au Hakimu mmoja mmoja na pia hupima uhuru wa Mahakama kwa ujumla.

“Ingawa wananchi wengi huwa hawafuatilii mashauri ya kawaida ya jinai na madai, hali hubadilika wakati wa mashauri ya uchaguzi ambapo hufuatilia taratibu zote zinazohusu kesi za uchaguzi”, alisema.

Akizungumzia mafunzo hayo, Jaji Mkuu amewataka Majaji kuibua maeneo ya uchaguzi yanayohitaji maboresho kwa lengo la kuboresha kanuni hizo ili mashauri ya uchaguzi yamalizike kwa wakati na hivyo kujenga Imani ya wananchi kwa Mahakama.

Alisema Majaji ni viongozi hivyo maamuzi yao hushawishi kuboreshwa kwa sheria au kubadilishwa kwa sera zinazohusu masuala ya sheria na haki.
trrrrrr.jpg

“Tuchukulie mafunzo haya kama fursa ya pekee ya kuibua maeneo ya uchaguzi ambayo yanahitaji maboresho Zaidi, alisema.

Alisema mafunzo hayo yatawasaidia Maafisa hao wa Mahakama kuwa katika hali ya utayari wa kupokea, kusikiliza na kumaliza mashauri yote ya uchaguzi ndani ya muda mfupi na pia mafunzo hayo ni muhimu katika uimarishwaji wa uchaguzi ulio huru na wa haki.

Mafunzo ya nmana bora ya uendeshaji wa kesi za uchaguzi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kwa nyakati tofauti yanawahusisha Maafisa wa Mahakama wa ngazi mbalimbali wakiwemo Majaji, Wasajili, Mahakimu na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji.
 
Wenye akili wameanza kujitoa kwenye huu mtego wamebaki yule mkuu wa tume ya uchaguzi katibu mkuu wa fisiemu na yule mwenda pole.
 
Akizungumza kwenye kikao cha kutoa elimu ya namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi kwa majaji na mahakimu, JM Prof Juma amewataka watendaji hao kutoa haki kwa wakati.

Prof Juma amesema mahakama inapaswa kutoa haki ili isionekane kama tawi linaloweza kutumiwa na Wanasiasa.

Semina hiyo imefanyika mjini Morogoro.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Kwa Lissu kila goti litapigwa.....ile kesi ya Lissu bado ipo?
 
Akizungumza kwenye kikao cha kutoa elimu ya namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi kwa majaji na mahakimu, JM Prof Juma amewataka watendaji hao kutoa haki kwa wakati.

Prof Juma amesema mahakama inapaswa kutoa haki ili isionekane kama tawi linaloweza kutumiwa na Wanasiasa.

Semina hiyo imefanyika mjini Morogoro.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
ilimradi kama siyo ile lip service yake ya siku zote basi sawa...
 
..hakosi shughuli zote za ikulu.

..hata kuapisha mabalozi na yeye yumo.

..kupokea midege ya Magufuli yumo.

..sasa huyu ni Jaji Mkuu kweli?

..Ni kiongozi wa mhimili unaojitegemea?
Kwani akihudhuria anavunja sheria yoyote bwashee?!
 
lissu kila siku ana sababu ya kukosa mahakamani
Mahakamani huko Kuna nini,kesi zenyewe za kutengenezwa kwa Sheria za kupitishwa kwa miswaada ya hati za dharura kuwanyazisha wengine na kuwalinda wengine
 
Ni ujinga mtupu kutegemea mahakama huru katika mazingira ya udikteta. Udikteta uondoke kwanza. Na udikteta hauondolewi katika sanduku la kura. Watanzania wenywe siku wakichokwa katika umoja wao, basi watauondoa.
Akizungumza kwenye kikao cha kutoa elimu ya namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi kwa majaji na mahakimu, JM Prof Juma amewataka watendaji hao kutoa haki kwa wakati.

Profesa Juma amesema mahakama inapaswa kutoa haki ili isionekane kama tawi linaloweza kutumiwa na Wanasiasa.

Semina hiyo imefanyika mjini Morogoro.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi mpaka awakumbushe ina maana wao hawajui wajibu wao? Walipataje hiyo kazi? Aisee kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom