Jaji Chande: Wananchi hawana imani na taasisi zinazotoa haki

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Siku tatu baada ya Tume ya Kutathmini Mfumo wa Haki Jinai ianze kazi yake, imesema Tanzania kuna mmomonyoko na upungufu wa imani za wananchi kwa taasisi zinazotoa haki.

Tume hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti, Jaji mstaafu Mohammed Chande na Makamu wake, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue ilianza kazi Februari 6, mwaka huu.

Kuundwa kwa tume hiyo Julai 20, mwaka jana kulitokana na kukithiri kwa malalamiko ya wananchi dhidi ya taasisi zinazotoa haki na mfumo wa haki jinai nchini.

Akitangaza kuundwa kwa tume hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan alisema: “Nimeunda kamati ya watu 12 na Sekretarieti yenye watu watano.

“Kamati hii itaongozwa na Jaji Mstaafu Mohamed Chande ndio Mwenyekiti na Makamu wake atakuwa mstaafu Balozi Ombeni Sefue,” alisema.

Akizungumza kuhusu tume hiyo jijini Dar es Salaam leo Februari 8, 2023, Jaji Chande amesema zipo changamoto zinazojulikana katika mfumo huo, ikiwemo ucheleweshwaji usio wa lazima wa kesi mahakamani.

“Lingine linalojulikana na ucheleweshwaji wa upelelezi, jukumu letu ni kuja na mapendekezo ya kutatua matatizo haya," amesema.

Lakini, amesema matokeo mazuri ya tume hiyo yanategemea michango ya hoja na mapendekezo ya wananchi, hivyo aliwataka kujitokeza kufanya hivyo.

“Tunataka tuainishe mambo ambayo ni sugu kwenye mfumo wa haki jinai hasa yanayojirudia. Tunataka mfumo utende haki na taasisi ziongeze weledi, ufanisi na ubora.

“Tutafikia vipi hatua ya kuwa na wafungwa ambao wakitoka magerezani wanakuwa wamejifunza na hawarudii makosa yaleyale, haya yote yatatokana na mapendekezo ya wadau," amesema.

Alipoulizwa iwapo tume hiyo itashughulika na wanaotajwa kutenda makosa kupitia taasisi zao, Jaji huyo amesema kazi inayofanywa nao ni kutathmini mfumo wa taasisi na sio mtu.

“Kwenye utendaji wa taasisi hatupimi utendaji wa mtu mmoja mmoja, kwa sababu upimaji wa utendaji kila taasisi na kila mmoja ana mamlaka yake ya nidhamu," amesema.

Badala ya kutuhumu kupitia majukwaa ya kisiasa, amewataka wanasiasa na wananchi wote kutoa mapendekezo na tuhuma zao wakiwa na ushahidi kwa tume hiyo kupitia majukwaa mbalimbali iliyoyaanzisha.

Hata hivyo, amesema tayari kwa siku tatu walizoanza kazi wameshakutana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Bara na Zanzibar na jana walikutana na Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Kulingana na Jaji Chande, wiki ijayo makamishna wanane wa Jeshi la Polisi watakutana na tume hiyo na alitoa wito kwa vyombo vya habari kwenda kufanya nao mahojiano watakapomaliza mazungumzo na tume hiyo.

Mbali na taasisi tano ilizopewa kuangalia mfumo wa haki jinai ndani yake ambazo ni Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), DCEA, Jeshi la Magereza na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, amesema taasisi nyingine zinazohusika na utoaji haki zitatazamwa pia.

“Tunachoangalia ni kuwa na mfumo mmoja chini ya taasisi mbalimbali lengo ni kuboresha mfumo na taasisi zenyewe, "Rais Samia ana azma kubwa ya kusukuma hili gurudumu la kijinai litende haki kwa wananchi," amesema.

Amesema tume hiyo inatarajia kutembelea mikoa 14 na wilaya 30 katika kazi zake ilizopangiwa kuzitekeleza kwa siku 120 na kwamba kila kundi litahojiwa.

Alipoulizwa kuhusu watu kutokuwa na imani na wajumbe hao, amesema ni vigumu aliyeteuliwa kujieleza, lakini mageuzi hufanywa na mtu aliye ndani na siyo nje.

“Mimi nilikuwa mahakamani, maboresho ya mahakama yanafanywa na watendaji wa taasisi hiyo. Jukumu letu ni kutathmini na kupendekeza na jambo kubwa ni methodolojia gani itakayoingia kwenye pendekezo," amesema.

Baada ya kuteuliwa kwa wajumbe wa tume hiyo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga amependekeza sheria 31 zipitiwe ili kufanikisha uboreshwaji wa mfumo huo.

Mapitio ya sheria hizo, yanatokana na kile alichoeleza kuwa zina changamoto zinazochagiza kasoro katika mfumo wa haki jinai nchini, hivyo tume hiyo ina wajibu wa kuzipitia.

“Tunaamini kuteuliwa kwa wajumbe hao ni dalili kwamba kamati itaanza kazi hivi karibuni, tunapendekeza iweke kipeumbele cha kuboresha sheria mbalimbali,” amesema.

Amezitaja sheria hizo na miaka yake kwenye mabano ni Sheria ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (2015), Sheria ya Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (2007), Sheria ya Kudhibiti Uhujumu Uchumi sura ya 200, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (1985) na ile ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu (2008).

Kwa mujibu wa Anna, sheria nyingine ni kanuni za adhabu sura ya 16, makosa mtandaoni (2015), huduma za vyombo vya habari (2016), sheria ya mtoto namba 21 (2009), sheria ya kuzuia utakatishaji fedha (2006) na sheria ya jeshi la polisi na huduma zaidizi sura ya 322.

Nyingine ni sheria ya ushahidi sura ya sita, sheria ya uvuvi sura ya 279, sheria ya uhamiaji sura ya 54, magezeza sura ya mwaka 1967, sheria ya wakimbizi sura ya 37 sheria ya tawala za mikoa (1997), sheria ya mamlaka ya mapato Tanzania sura ya 399 na sheria ya uchawi sura ya 18.

MWANANCHI
 
Swala la Polisi, waangalie Elimu

Wasio fit na mfumo wastaafishwe kwa manufaa ya nchi, walipwe mafao ya muda waliotumika.
Waajiriwe wapya, wasomeshwe upya

Wapewe vifaa vya kazi.

Polisi Post zijengwe upya, sehemu za mahabusu ziwe safi.

CCTV camera ziwekwe kwenye vituo vyote vya polisi

Mahojiano yawe yanafanyika chumba maalumu, ambacho mtu atarekodiwa sauti na video.

Polisi wawekeze nguvu kutafuta ushahidi bila kuumiza watu.

Magereza mapya yajengwe

Mfumo wa Wanyapara uondolewe, ibaki kazi ya Askari jela.

Mfumo wa chakula gerezani ubadilishwe.

Wafungwa wafanye kazi za kulipwa
 
Hongera Rais Samia
 
Una akili mno mpaka unakera
 
Mahakama nayo ina tatizo la Elimu, kuna mahakimu, hawajui kazi yao ya kuinterplate sheria, hivyo watu wengi hufungwa na mahakama za mwanzo, wanakuja ponea mahakama ya rufaa, huku ni kutesa watu wasio na hatia.

Ajira za Ujaji zianishwe, ziombwe, usaili ufanyike hadharani.
Wataopita Rais achague 5. Apeleke Bungeni Bunge limpe 3 ambao atachagua 1 ka

Majaji, mahakimu ambao hawana sifa wasitaafishwe kwa manufaa ya nchi. Walipwe chao waangalie kitu kingine.

Elimu kwenye masuala ya sheria iangaliwe upya.
 
Yupo sahihi kabisa na huyu Mzee huwa anaongea hivi mara kwa mara sijui kama wahusika wanalifanyia kazi...
 
mama DSamia, tumeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, tumeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, tumeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mpka lini? Chande alitokkkkkkkkkkkfanya ubunifu gani kuimarisha haki katika mahakama? Alifanya ubunifu gani kukabiliana nan rushwa mahakamani> Upotezji waedha tu!
KATIBA MPYA NDIO JIBU! rais asiwe na mamlaka ya kuteua majaji. Majaji wafanyiwe usaili wa wazi, televised one kama kenya wanavyofanya. Utapata watu competent kabisa
 
Back
Top Bottom