Hamad Chande: Umasikini umepungua Tanzania

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imetajwa kuwa kwenye kiwango kizuri cha upatikanaji wa chakula kutokana na kuwepo kwa takwimu sahihi za hali ya maisha katika kaya, hali iliyopelekea kiwango cha umasikini wa chakula kushuka nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akifungua Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 15 ya Mradi wa Utafiti wa Kupima Hali ya Maisha zinazojumuisha Tafiti za Kilimo Katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (LSMS-ISA), uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema Programu hiyo ya utafiti iliyoanza 2008 ambayo ilifadhiliwa na Benki ya Dunia, imeweka alama sio tu katika uzalishaji wa takwimu muhimu za hali ya maisha katika kaya bali pia takwimu zilizozalishwa zimekuwa nyenzo muhimu za kutathmini sera na programu zinazotekelezwa na Serikali, taasisi binafsi na wadau wa maendeleo.

"Kiwango cha umasikini kwa sasa kimepungua hasa umasikini wa upatikanaji wa chakula, chakula kipo kwa wingi cha kutosha ambapo sisi watanzania leo tunalisha mpaka nchi jirani" amesema Chande.

Moja ya mipango ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Tanzania inakua Baba wa mataifa mengine kwa kuyalisha chakula na ndiyo maana aliridhia kuratibu Mkutano mkubwa unaohusu Usalama wa Chakula Barani Afrika AGRF 2023, ambao ulifanyika Septemba 2023 Dar es salaam
 
Back
Top Bottom