J. Mnyika: How and Why did you loose Ubungo 2005?

mimi sijui ukweli kwa ndani, ila tuliokuwapo ubungo wakatu huo tulimpigia kura (au tudanganyana?)
(hearsay) Keenja aliamua kuishika manzese, na sehemu zilizo highly populated akatilia msisitizo kwa kila hali, kuanzia khanga, tshirts, kofia mpaka sherehe na vikao vya usiku(niliona baadhi). Sikuona tshirt ya mnyika.
Mnyika alizunguka sana tangu mwanzo, jimbo zima akaeleweka vizuri kabisa, akapendeka, Keenja alikwama mwanzoni kabisa ila mwishoni akawateka watu kwa mshtukizo kwa ahadi na zawadi, wakamuhama mnyika.
hiyo ni hoja tuliojipa wakati ule baada ya kuona kura hazikutimia.
Anyway, bado tunajua wewe ndio ulifaa. Ukitumia nguvu ile hadi mwisho pia safari hii mtapata. Labda asije keenja. aje kijana kama wewe toka ccm.

Haika,

Mimi muda ule nilikua bado niko Sinza na kwa karibu nilikua na mawasiliana na kambi ya huyu Mh.Mbunge (Aliyetarajiwa)Bwn.Mnyika.
Tatizo kubwa lilikua Kujiaamini kupia kiasi kwa kambi yake,hasa kutokana na ifluence ya ujana (maana wengi walikua vijana na wapiga kula wa maeneo yale ni vijana) ya kamati nzima.
Ila walisahau kitu kimoja,ukitulia maanani maeneo hasa maeneo ya manzese na kata zake za sinza.wenye viti wengi wa serikari za mtaa walikua ni kutoka ccm na walikua na mipango mingi ya kupata kula iwe kwa harari ama kuiba kwani mamlaka mengi yalikua chini yao hivyo kufa uibaji kura pale URAFIKI HALL kua rahisi unlike vijana ambao wao ni wapiga kula tu waendao vituoni na kupiga kula na kwenda zao vijiweni kusubiri majibu na kupiga kula.
Wenye viti hao wengi hasa wa kata ya sinza madukani alinunua vijana wengi katika ile kamti ya Mnyika na fedha zote zilitoka kwa Muheshimiwa aliye pata huo Ubunge.
Lakini all in all bwana Mnyika na kamati yake walijitahidi sana ila wenzao waliwashinda kwa mbinu ila Ubunge kwakweli alipata kutokana na HOJA za kweli toward maendeleo ya ukweli .
 
Ni kweli lakini jamaa wa Chadema walijiamini sana na walishaona hakuna tena .....ni wao tu maana nao walijipanga sawa sawa..ila sidhani kama walikuwa na iwiano sawa wa maeneo na vitongoji ndilo kubwa lilimuangusha dogo...ila kwa sasa anazidi kukomaaa hope 2010 itakuwa mpambano mkali sana sana kwa yeyote toka CCM.....ajinoe tu na kujifua zaidi kwenye nyanja zote ni hazina isiyopingika....na lulu ing'aaayoo labda anunuliwe tuu.............la sivyoo tumtegemea sana .......
 
Mnyika njoo hapa utupe statistics kwenye uchanguzi wako ulioshindwa..number dont lie,tunaweza kukusaidia pesa maana we've same interest na ninaamini utafanya makubwa maana you have nothing to loose kuwamaliza mafisadi na ndio roho yako itakuwa imeridhika na sisi pia,nakuhakikishia nitamake sure kama number zako ni nzuri na ninaona unaweza ku flip hilo jimbo nitakutafutia at least a million shillings kwa ajiri ya campaign yako,unajua hiyo ni pesa ndogo sana huku states....pls tup analysis what happened?
 
Hivi Hili Kaulizwa Mnyika Au Yeyote Anaweza Kumjibia? Me Naona Mnyika Angejibu Then Wengine Tufwate....
 
Yohana wa Mnyika,

Ndugu yangu naomba leo nikuulize swali gumu na very personal.

Kulitokea nini Ubungo 2005 ukashindwa kuchukua Ubunge wa jimbo?

Jimbo la Ubungo, liko Dar Es Salaam, mji mkubwa Tanzania. Nakadiria kuwa karibu 50% ya wakazi wa Ubungo ni "middle class", wasomi na wenye kupenda maendeleo na si rahisi kubabaishwa na siasa za CCM.

Sasa najiuliza leo, nikiwa najikumbusha ninavyokufahamu na hata kwa kusoma Waraka mbali mbali ulizoandika, ni kitu gani kilisababisha Ubungo kuangukia mikononi mwa CCM?

Je ilikuwa ni wizi wa kura?
Je ilikuwa ni hongo, rushwa na takrima?
Je ilikuwa ni uwezo mdogo wa kifedha kwako na Chadema kupambana na CCM?
Je ilikuwa ni kukosekana kwa mikakati na mipango mizuri kujitangaza na hata kuendesha kampeni na kuweza kukonga na kuteka nyoyo za Wana-Ubungo?
Je ilikuwa ni Ujana na ukosefu wa ujuzi wa michuano ya kisisasa?
Je ulishindwa kujiuza kisera na kiitikadi kwa Wana-Ubungo?
Je ni kwa kuwa ulikuwa Chadema na si CCM, CUF, TLP, NCCR au chama kingine cha siasa?
Je mlikanyagana viatu na wagombea wa vyama vingine na kuishia kumpa Keenja ushindi wa bure?

Kumbukumbu zangu zaniambia kulifunguliwa kesi ya Uchaguzi.

Lakini najiuliza tena, kijana mahiri kama wewe ulishindwaje kulichukua jimbo la Ubungo kwa nguvu kubwa na kuishia kwenda mahakamani?

Nikiangalia Ubungo na wakazi wake, kama Chadema na wewe kama mgombea, mngekuwa na mikakati mizuri, suala la uhamasishaji na kukonga nyoyo lingekuwa ni rahisi.

Ubungo imezungukwa na taasisi za Elimu ya juu nyingi. Anzia UDSM, Ardhi, Maji, DIT, kuna mashirika na taasisi zenye maendeleo makubwa na watu wenye upeo mkubwa wa mawazo, je ilishindikana vipi kujiuza kwa hawa watu haswa waalimu na wanafunzi ili waeneze Injili ya Mnyika na Chadema?

Najua wanafunzi ni wapita njia, lakini je walitumika japo kusaidia kufanya kampeni na kulipeperusha jina la Mnyika na Chadema? au nao walikuwa wagumu kuuziwa na kununua bidhaa ya Mnyika na Itikadi na Sera Chadema?

Je 2010 inavyokuja unatarajia kugombea tena? kama utagombea, ni mambo gani ambayo unafikiri ni lazima uyafanye ili ujipatie Ushindi wa Tsunami?

Najua mikakati mingine ni siri yako ya moyoni na chama chako na ni mapema sana kumwaga mchele kwenye kuku. Lakini kama Mwana Jamii mwenzako na Mwanaharakati, inabidi niulize na nikuulize kati yetu ili kama kulikuwa na makosa, tuyarekebishe, kama ni kujenga mikakati, basi tukusaidie ili Bunge letu lipate Mwana JF wa pili (au zaidi ikitegemea wale wanaojificha!) baada ya Zitto.

Kwa wewe na Zitto, tambueni kuwa pamoja na JF kuwa imetapakaa dunia nzima, lakini ni Jimbo moja mahiri ambalo mnalihitaji kwa nguvu sana!

La mwisho, katika jimbo la Ubungo, ni kata ngapi na kuna madiwani wangapi ambao ni wa Chadema au Upinzani?

Nasubiri majibu yako na hata ya wengine ambao wanafahamu kwa undani kilichotokea 2005.

Kaka Mchungaji

Ujumbe mzito huu, naomba upitie hii hotuba yangu hapa ambayo niliitoa mwaka 2006: http://www.chadema.net/hotuba/mnyika/hotuba_4.html

Mjadala huu umeuibua wakati mwafaka katika kipindi hiki ambacho nimeanza kuandika kitabu. Nawatakia mjadala mwema

JJ
 
2010 hakuna hela za EPA, hakuna mabavu ya Nkapa, hakuna kampeni za Malecela, may be wapinzani wataanza kuwika!!!! Lakini mpaka sasa sielewi kwa nini Dar yote iko chi ya CCM!!!

Dar yote bado iko chini ya CCM kwa sababu wapiga kura wengi bado ni mbumbumbu !!! Utawaona kwenye mikutano ya hadhara wamejaa lakini usidhani kwamba watapiga kura kwa wapinzani. Nahisi ukifanya sensa ya wapiga kura wa Dar es Salaam utagundua uelewa wao wa mambo ya siasa na jinsi nchi inavyoendeshwa kwa ujumla hauna tofauti kubwa sana na ule wa wale wa mikoani. Wengi wao wanapenda kusoma magazeti ya udaku, badala ya kusoma yale yanayoelemisha. Internernet access ndio kabisaa wala usizungumzie.

Mbaya zaidi, hao "middle class" wa Dar wengi wao, ama kwa kukata tamaa kwa jinsi nchi inavyoendeshwa au vinginevyo ni wavivu kweli kwenda kupiga kura! Siku ya kupiga kura kwao ni public holiday na wengi wao wakunywa tu pombe, au kufanya starehe zao zingine mpaka asubuhi. Only a few of them go to vote! And in most cases some of them go to the ballot without knowing wagombea wa ubunge ni kina nani.....Wanawajua wale wa urais tu!

Safari bado ni ndefu na ngumu kuliko tunavyofikiria.
 
Wakuu

Nawashukuru wote mliochangia huu mjadala unaoendelea hasa wale mlioonyesha wazi kuwa mliniunga mkono kwenye uchaguzi uliopita na bado mtaendelea kuniunga mkono kwa namna moja au nyingine.

Pamoja Tutashinda

JJ
 
I love numbers too!!

Kulinganisha kura za Urais na Ubunge kule Ubungo:

Wote waliojiandikisha:
313765

Idadi ya kura zote za Rais:
152525

Idadi ya kura halali za Rais
149037

Kura zilizokataliwa:
3288

Kura za Kikwete:
107733

Ubungo:

Wote waliojiandikisha
313765 (ni idadi ile ile na inakubaliana na ile ya kura za Rais, kwani ni wapiga kura wale wale)

Idadi ya Kura zote za Ubunge181305

Idadi ya kura zote za Keenja
93,473

Idadi ya kura zote za Mnyika
45164

Idadi ya kura zote za Minja
28412

Idadi ya kura za wagombea wengine
4933

Kura zilizoharibika
9323

Hebu tuangalie namba hizo na kuzipa maana:

Tofauti ya kura halali za Rais na Wabunge:
181305-149,037 = 32,268

Ina maana gani:

a. Kwenye uchaguzi ambapo mpiga kura anapiga kura za Rais na Mbunge, ni kwanini wapiga kura 32,268 hawakupiga kura ya Rais?
b. Kwa vile uchaguzi wa 2005 kiongozi aliyekuwa maarufu sana Kikwete alikuwa kwenye karatasi ya kupigia kura, inawezekana vipi watu zaidi ya elfu thelathini wasipige kura upande wowote ule, lakini wakapiga kura kumchagua Mbunge?
c. Kama makaratasi 32,268 hayakurudishwa yakiwa na kura za Rais, makaratasi haya yalienda wapi? Kwa sababu kura za Urais zilizoharibika ni 3288 tu. Kama hazikurudi na hazikurekodiwa, hawa 32,268 waliopiga kura ya Ubunge ni kina nani?

Tofauti ya Keenja na Mnyika
Keenja's 93,473 – Mnyika's 45,164 = 48,309

Tofauti ya kura zao na tofauti ya kura za rais

48,309 -32,268 = 16041

Kura zilizoharibika kwenye Ubunge: 9323

Ina maana gani?

a. Kama wapiga kura ya Ubunge wangekuwa idadi ile ile ya waliopiga kura Rais yaani 149,037 (kitu ambacho kina make sense ukizingatia kuwa kivutio kikubwa cha uchaguzi wa 2005 kilikuwa ni Kikwete)

Basi,

Keenja angeshinda, 93,473 ma hivyo kuacha kura 55,564 kugombaniwa na wapinzani.

Na kama Mnyika bado angepata kura zile zile 45,164 na yeye angeacha kura 10400 kugombaniwa na Minja:

Sasa kama Minja angepata kura 28,412 na wapinzani wengine kupata kura 4933 kama inavyooneshwa, basi tungekuwa na upungufu wa kura – 22,945

Sasa kura hizo wangezielezeaje?

Hivyo basi: Walishindwa kuinflate kura za Rais kwa sababu isingeingia akilini bila kuinflate kura za Wabunge. Hivyo ni rahisi kubadili idadi ya kura za Wabunge kuliko za Rais ili kuondoa tatizo ambazo nimelionesha hapo.

Sasa akili mukichwa.

Source: Tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa : http://www.nec.go.tz
 
Nadhani tumsubiri mwenyewe ila mimi nilishamshauri huko nyuma hana uwezo wa kumshinda Keenje Ubungo atafute jimbo la mikoani kama mwenzake Zitto.
In Africa, democracy is not voting, but counting the votes - January Makamba, Tanzanian (Ikulu)

Sam,

Huyu jamaa alisema hivyo kweli?

Nakumbuka ali-quote pia "A million flies cannot be wrong, they eat shyt" katika kuelezea the voting habits of majority of Tanzanians.
 
I love numbers too!!

Kulinganisha kura za Urais na Ubunge kule Ubungo:

Wote waliojiandikisha:
313765

Idadi ya kura zote za Rais:
152525

Idadi ya kura halali za Rais
149037

Kura zilizokataliwa:
3288

Kura za Kikwete:
107733

Ubungo:

Wote waliojiandikisha
313765 (ni idadi ile ile na inakubaliana na ile ya kura za Rais, kwani ni wapiga kura wale wale)

Idadi ya Kura zote za Ubunge181305

Idadi ya kura zote za Keenja
93,473

Idadi ya kura zote za Mnyika
45164

Idadi ya kura zote za Minja
28412

Idadi ya kura za wagombea wengine
4933

Kura zilizoharibika
9323

Hebu tuangalie namba hizo na kuzipa maana:

Tofauti ya kura halali za Rais na Wabunge:
181305-149,037 = 32,268

Ina maana gani:

a. Kwenye uchaguzi ambapo mpiga kura anapiga kura za Rais na Mbunge, ni kwanini wapiga kura 32,268 hawakupiga kura ya Rais?
b. Kwa vile uchaguzi wa 2005 kiongozi aliyekuwa maarufu sana Kikwete alikuwa kwenye karatasi ya kupigia kura, inawezekana vipi watu zaidi ya elfu thelathini wasipige kura upande wowote ule, lakini wakapiga kura kumchagua Mbunge?
c. Kama makaratasi 32,268 hayakurudishwa yakiwa na kura za Rais, makaratasi haya yalienda wapi? Kwa sababu kura za Urais zilizoharibika ni 3288 tu. Kama hazikurudi na hazikurekodiwa, hawa 32,268 waliopiga kura ya Ubunge ni kina nani?

Tofauti ya Keenja na Mnyika
Keenja’s 93,473 – Mnyika’s 45,164 = 48,309

Tofauti ya kura zao na tofauti ya kura za rais

48,309 -32,268 = 16041

Kura zilizoharibika kwenye Ubunge: 9323

Ina maana gani?

a. Kama wapiga kura ya Ubunge wangekuwa idadi ile ile ya waliopiga kura Rais yaani 149,037 (kitu ambacho kina make sense ukizingatia kuwa kivutio kikubwa cha uchaguzi wa 2005 kilikuwa ni Kikwete)

Basi,

Keenja angeshinda, 93,473 ma hivyo kuacha kura 55,564 kugombaniwa na wapinzani.

Na kama Mnyika bado angepata kura zile zile 45,164 na yeye angeacha kura 10400 kugombaniwa na Minja:

Sasa kama Minja angepata kura 28,412 na wapinzani wengine kupata kura 4933 kama inavyooneshwa, basi tungekuwa na upungufu wa kura – 22,945

Sasa kura hizo wangezielezeaje?

Hivyo basi: Walishindwa kuinflate kura za Rais kwa sababu isingeingia akilini bila kuinflate kura za Wabunge. Hivyo ni rahisi kubadili idadi ya kura za Wabunge kuliko za Rais ili kuondoa tatizo ambazo nimelionesha hapo.

Sasa akili mukichwa.

Source: Tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa : http://www.nec.go.tz

Mzee wewe ni kichwa basi tu, laiti viongozi wetu wangeondoa ubinafsi wangetafuta vichwa kama hivi vichambue mambo nchi yetu ipige hatua!

Ulivo zinyambua hizo number mhhhh.. uende mbali ndugu! si watu wote tungeweza ziona na kuzifanyia kazi haraka haraka na hata kugundua dosari hizo, ofcourse hailezeki nini kilitokea hapo!
 
I love numbers too!!

Kulinganisha kura za Urais na Ubunge kule Ubungo:

Wote waliojiandikisha:
313765

Idadi ya kura zote za Rais:
152525

Idadi ya kura halali za Rais
149037

Kura zilizokataliwa:
3288

Kura za Kikwete:
107733

Ubungo:

Wote waliojiandikisha
313765 (ni idadi ile ile na inakubaliana na ile ya kura za Rais, kwani ni wapiga kura wale wale)

Idadi ya Kura zote za Ubunge181305

Idadi ya kura zote za Keenja
93,473

Idadi ya kura zote za Mnyika
45164

Idadi ya kura zote za Minja
28412

Idadi ya kura za wagombea wengine
4933

Kura zilizoharibika
9323

Hebu tuangalie namba hizo na kuzipa maana:

Tofauti ya kura halali za Rais na Wabunge:
181305-149,037 = 32,268

Ina maana gani:

a. Kwenye uchaguzi ambapo mpiga kura anapiga kura za Rais na Mbunge, ni kwanini wapiga kura 32,268 hawakupiga kura ya Rais?
b. Kwa vile uchaguzi wa 2005 kiongozi aliyekuwa maarufu sana Kikwete alikuwa kwenye karatasi ya kupigia kura, inawezekana vipi watu zaidi ya elfu thelathini wasipige kura upande wowote ule, lakini wakapiga kura kumchagua Mbunge?
c. Kama makaratasi 32,268 hayakurudishwa yakiwa na kura za Rais, makaratasi haya yalienda wapi? Kwa sababu kura za Urais zilizoharibika ni 3288 tu. Kama hazikurudi na hazikurekodiwa, hawa 32,268 waliopiga kura ya Ubunge ni kina nani?

Tofauti ya Keenja na Mnyika
Keenja’s 93,473 – Mnyika’s 45,164 = 48,309

Tofauti ya kura zao na tofauti ya kura za rais

48,309 -32,268 = 16041

Kura zilizoharibika kwenye Ubunge: 9323

Ina maana gani?

a. Kama wapiga kura ya Ubunge wangekuwa idadi ile ile ya waliopiga kura Rais yaani 149,037 (kitu ambacho kina make sense ukizingatia kuwa kivutio kikubwa cha uchaguzi wa 2005 kilikuwa ni Kikwete)

Basi,

Keenja angeshinda, 93,473 ma hivyo kuacha kura 55,564 kugombaniwa na wapinzani.

Na kama Mnyika bado angepata kura zile zile 45,164 na yeye angeacha kura 10400 kugombaniwa na Minja:

Sasa kama Minja angepata kura 28,412 na wapinzani wengine kupata kura 4933 kama inavyooneshwa, basi tungekuwa na upungufu wa kura – 22,945

Sasa kura hizo wangezielezeaje?

Hivyo basi: Walishindwa kuinflate kura za Rais kwa sababu isingeingia akilini bila kuinflate kura za Wabunge. Hivyo ni rahisi kubadili idadi ya kura za Wabunge kuliko za Rais ili kuondoa tatizo ambazo nimelionesha hapo.

Sasa akili mukichwa.

Source: Tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa : http://www.nec.go.tz

Kaka

Superb! Huu ndio ulikuwa msingi mkuu wa kesi ya uchaguzi. Baada ya kufungua kesi, miezi michache baadaye nilikutana na kigogo mmoja wa Tume ya uchaguzi, nikamuuliza maswali haya haya. Mara ya kwanza akatoa sababu rahisi tu, kwamba watu hawakupenda kupiga kura ya Urais. Nikamwambia sasa mbona karatasi zao hazikuwepo katika kura zilizoharibika? Akajikanyaga, hakupata majibu. Akabadili topic. Tulikuwa pale ubalozi wa Marekani. Nikarudia tena kumwuliza, akanyamaza. Nikaelewa si kosa lake, ni kosa la waliomuagiza. Sitamtaja kwa jina huyu mkuu,mmoja wa vigogo wa juu kabisa wa NEC. Lakini aliponyamaza nilimwambia maneno ambayo najua mpaka leo ataendelea kuyatafakari. Nilimwambia kwamba kesi ya uchaguzi ubungo inapigwa danadana kwa kuwa Tume mtapaswa kwenda kujiueleza mahakamani kuhusu hizi tofauti. Nikamueleza pia nimepitia maeneo mengi yaliyokuwa na upinzani mkali ka mchezo kama haka kamefanyika. Nikamwambia, kila njia itatumika kuficha hii siri ya mwaka 2005, lakini ipo siku Tanzania itapata mabadiliko ya yaliyofichika yatafichuliwa. Nikamwambia kwa heshima yake aanze kujiandaa kuunga mkono mabadiliko hayo, arekebishe mambo katika uchaguzi mkuu 2010 ama sivyo historia itakuja kumhukumu

JJ
 
Nadhani kama alivyosema Koba.. namba hazidanganyi... sasa hii kesi ya Ubungo imefikia wapi? au bado wanajaribu kutafuta ufafanuzi wa kura hizo elfu 30,000?
 
Wee Mnyika, hayo magwanda ya kimgambo ya nini tena? Nyinyi Chadema kwa nini mnapenda sana kuwaiga CCM na migwanda gwanda yao ya kimgambo. I hope Kitila yeye huwa havai hiyo migwanda.....
 
Kaka

.... Nilimwambia kwamba kesi ya uchaguzi ubungo inapigwa danadana kwa kuwa Tume mtapaswa kwenda kujiueleza mahakamani kuhusu hizi tofauti. Nikamueleza pia nimepitia maeneo mengi yaliyokuwa na upinzani mkali ka mchezo kama haka kamefanyika.
JJ

...dont tell me kesi haijaiisha mpaka leo,kama ni kweli basi tumekwisha maana hata 2010 itakuwa mchezo ndio huo huo.
 
Mnyika kaza buti tu kijana, wanasema "like a spring, the beginnings of all things are small" nguvu ya wananchi itakufikisha!
 
Mnyika naomba ufuate ushauri wangu. Tafuta jimbo ambalo your vote will be counted. Mama Anne angekuwa kama wewe asingekuwa mbunge hivi sasa. Ilikuwa ni rahisi sana kumburuza Yona kuliko huyo ambaye wewe unadhani utamshinda. Au ombea Mungu asigombee. Na kwa taarifa yako CCM haiwezi kukubali kushindwa kirahisi majimbo ya Dar kwani huo ndiyo utakuwa mwanzo wa kushindwa kitaifa. Vyua hayo magwanda yako halafu uingie mikoani, ukienda na hayo magwanda kila mtu atakuogopa. Unapoenda kuomba kura inabidi uende kiungwana siyo kimgambomgambo.
 
Duh, Ama kweli J.J Mnyika umeipata fresh!...Magwanda tena imekuwa issue!...itabidi mkuu utafute Ngwsuma la nguvu na shurti ushomekee hasa..maana mikoani PeDeGee (President Director General) ndio inalipa..
 
halafu aoteshe kakitambi kadogo aonekane hana shida (joking)
mi ningependa uwe mbunge wa dar es salaam. mtafutane wengi mshike dar e salaam yote.
 
Kwa hiyo swala la ukabila halikuwa na nafasi kubwa kama ilivyodhaniwa na baadhi ya wachangiaji kwa sababu ingekuwa hivyo basi Minja ndio angeshika nafasi ya pili, au sio?
Ikumbukwe pia kuwa CHADEMA iliweka wachaga Kigamboni na Kawe lakini hawakulamba kitu.
 
je ni nini kinakwamisha kumalizika kwa kesi hii,au ndio wanasubiri uchunguzi wa tume.kama kesi ya msingi ni idadi ya kura,hapa inamaana ccm ndio wanaendesha hii kesi kwa kubuy time.
lakini kama nakumbuka vizuri hizi kesi zina muda maalumu wa kumalizika.
 
Back
Top Bottom