Mbunge kuleta maendeleo katika jimbo lake haiwezekani

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,035
Wadau nawasabahi.

Nimekuwa nawafuatilia Wabunge wengi kuona ni Maendeleo gani wamewapelekea Wapiga kura wao katika Majimbo yao. Ukweli sijaona Maendeleo yote ktk Majimbo yote yaliyoletwa na Mbunge bali Maendeleo yanapelekwa na SERIKALI kupitia Wizara zake.

Waziri au RAIS anapotembelea JIMBO Mbunge nae hujumuika na Wananchi na kuomba Maendeleo kwa huyo Waziri au Rais .Mchango pekee wa Mbunge ktk kuleta maendeleo ni kupiga kelele zake akiwa Bungeni na bado anaweza kupiga Kelele kwa nguvu zake zote na Maendeleo yasipelekwe.

Mfano mdogo tu
Je Maendeleo gani Wabunge hawa wameyapeleka ktk Majimbo yao?
1.Jimbo la Kawe
2.Jimbo la Ubungo
3.Jimbo la Kigamboni
4.Jimbo la Sumbawanga Mjini
5...
6....
Ni Ukweli Usiopingika Mbunge Kama Mbunge hawezi kuleta MAENDELEO ktk Jimbo.
 
Nini kazi ya Mbunge ?

In short zaidi ya kufikisha mawazo ya anaowawakilisha Huko kwenye Kutunga Sheria na Sera.., Mbunge anaweza kufanya lobbying kwa urahisi kusaidia maendeleo yake yeye na raia wenzake jimboni kwake.. (he is just part of the equation)

Ingawa practically usitegemee mwanasiasa wa sasa akakusaidia siasa ishakuwa platform ya kupata kura kwenda kula (ni wananchi wenyewe kama social beings wanaoweza kujiendeleza) na haya yanaweza kuwa rahisi iwapo kuna good infrastrucure
 
Kazi ya mbunge sio kuleta maendeleo.
Ni kutunga sheria na kuishauri serikali kuhusu mambo mbalimbali jimboni na nchini. Serikali ndio inaleta maendeleo.
Ndio maana serikali ikimnyanyapaa mbunge hawezi hata kuchimba shimo la choo. Ataonekana anafanya uchimbaji wa madini ya changarawe bila kibali.

Ni hayo tu.
 
Mbunge kamwe hawezi kupeleka maendeleo jimboni kwake kwa sababu hana fungu lo lote la fedha. Ingekuwa kuna mfumo wa utawala wa majimbo hilo lingewezekana kwa sababu angekuwa na fungu analolisimamia.

Hivyo katiba mpya ni muhimu kupeleka mamlaka kwa wananchi na si kumwachia Rais ambaye kwa sasa ni mungu mtu!
 
Bunge ndilo linapanga bajeti ya nchi
 
Mbunge kamwe hawezi kupeleka maendeleo jimboni kwake kwa sababu hana fungu lo lote la fedha. Ingekuwa kuna mfumo wa utawala wa majimbo hilo lingewezekana kwa sababu angekuwa na fungu analolisimamia.

Hivyo katiba mpya ni muhimu kupeleka mamlaka kwa wananchi na si kumwachia Rais ambaye kwa sasa ni mungu mtu!
Mbunge ni sehemu ya baraza la madiwani na huko kuna mambo mengi sana ya maendeleo huamuliwa
 
Wadau nawasabahi.

Nimekuwa nawafuatilia Wabunge wengi kuona ni Maendeleo gani wamewapelekea Wapiga kura wao katika Majimbo yao. Ukweli sijaona Maendeleo yote ktk Majimbo yote yaliyoletwa na Mbunge bali Maendeleo yanapelekwa na SERIKALI kupitia Wizara zake.

Waziri au RAIS anapotembelea JIMBO Mbunge nae hujumuika na Wananchi na kuomba Maendeleo kwa huyo Waziri au Rais .Mchango pekee wa Mbunge ktk kuleta maendeleo ni kupiga kelele zake akiwa Bungeni na bado anaweza kupiga Kelele kwa nguvu zake zote na Maendeleo yasipelekwe.

Mfano mdogo tu
Je Maendeleo gani Wabunge hawa wameyapeleka ktk Majimbo yao?
1.Jimbo la Kawe
2.Jimbo la Ubungo
3.Jimbo la Kigamboni
4.Jimbo la Sumbawanga Mjini
5...
6....
Ni Ukweli Usiopingika Mbunge Kama Mbunge hawezi kuleta MAENDELEO ktk Jimbo.
Nakuunga mkono kwa hoja yako nzuri ikumbukwe nje ya luwa na mbunge haitoshi kufanya maendeleo yaje jimboni , pamoja na kelele zote bungeni haitoshi kufanya jimbo kuendelea kama tu serikali haitamuunga mkono mbunge asilimia 80% ya maendeleo ya yanategemea sana serikali iunge mkono hoja ya mbunge japo baadhi ya wabunge wamekuwa wakijitoa Kwa fedha zao wenyewe mfanao Mh.Josephat Gwajima ametoa hela yake kujenga kivuko Cha Tegeta machinjioni ila hazitoshi kumaliza kero za wananchi ,hivyo basi tusiache kuunga mkono selikali.

Tunapaswa kuunga mkono serikali na kuacha kukata tamaa Kwamba mbunge fulani haleti maendeleo jimboni pamoja hoja za mbunge zenye nguvu , hazitoshi kuleta maendeleo kwa wananchi.
 
Hii thread imeletwa na mbunge mchovu.

Bila shaka hujatimiza ahadi zako kwa wananchi halafu unaleta ngonjera
 
Mkuu kazi ya bunge ni kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kuisimamia serikali.
Kuisamamia serikali ndiko kuleta maendeleo pia, kama wabunge wakiweza kuisamimia serikali vizuri kupitia kamati za bunge na mbunge mmoja mmoja vipaumbele vitakuwa sahihi, miradi itafanywa kwa kasi, itakamilika kwa wakati na ubora na pia uvujaji mapato hautakuwepo.
 
Mkuu uko sahihi 👍👏🆒
 
Back
Top Bottom