Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,525
- 1,523
Yohana wa Mnyika,
Ndugu yangu naomba leo nikuulize swali gumu na very personal.
Kulitokea nini Ubungo 2005 ukashindwa kuchukua Ubunge wa jimbo?
Jimbo la Ubungo, liko Dar Es Salaam, mji mkubwa Tanzania. Nakadiria kuwa karibu 50% ya wakazi wa Ubungo ni "middle class", wasomi na wenye kupenda maendeleo na si rahisi kubabaishwa na siasa za CCM.
Sasa najiuliza leo, nikiwa najikumbusha ninavyokufahamu na hata kwa kusoma Waraka mbali mbali ulizoandika, ni kitu gani kilisababisha Ubungo kuangukia mikononi mwa CCM?
Je ilikuwa ni wizi wa kura?
Je ilikuwa ni hongo, rushwa na takrima?
Je ilikuwa ni uwezo mdogo wa kifedha kwako na Chadema kupambana na CCM?
Je ilikuwa ni kukosekana kwa mikakati na mipango mizuri kujitangaza na hata kuendesha kampeni na kuweza kukonga na kuteka nyoyo za Wana-Ubungo?
Je ilikuwa ni Ujana na ukosefu wa ujuzi wa michuano ya kisisasa?
Je ulishindwa kujiuza kisera na kiitikadi kwa Wana-Ubungo?
Je ni kwa kuwa ulikuwa Chadema na si CCM, CUF, TLP, NCCR au chama kingine cha siasa?
Je mlikanyagana viatu na wagombea wa vyama vingine na kuishia kumpa Keenja ushindi wa bure?
Kumbukumbu zangu zaniambia kulifunguliwa kesi ya Uchaguzi.
Lakini najiuliza tena, kijana mahiri kama wewe ulishindwaje kulichukua jimbo la Ubungo kwa nguvu kubwa na kuishia kwenda mahakamani?
Nikiangalia Ubungo na wakazi wake, kama Chadema na wewe kama mgombea, mngekuwa na mikakati mizuri, suala la uhamasishaji na kukonga nyoyo lingekuwa ni rahisi.
Ubungo imezungukwa na taasisi za Elimu ya juu nyingi. Anzia UDSM, Ardhi, Maji, DIT, kuna mashirika na taasisi zenye maendeleo makubwa na watu wenye upeo mkubwa wa mawazo, je ilishindikana vipi kujiuza kwa hawa watu haswa waalimu na wanafunzi ili waeneze Injili ya Mnyika na Chadema?
Najua wanafunzi ni wapita njia, lakini je walitumika japo kusaidia kufanya kampeni na kulipeperusha jina la Mnyika na Chadema? au nao walikuwa wagumu kuuziwa na kununua bidhaa ya Mnyika na Itikadi na Sera Chadema?
Je 2010 inavyokuja unatarajia kugombea tena? kama utagombea, ni mambo gani ambayo unafikiri ni lazima uyafanye ili ujipatie Ushindi wa Tsunami?
Najua mikakati mingine ni siri yako ya moyoni na chama chako na ni mapema sana kumwaga mchele kwenye kuku. Lakini kama Mwana Jamii mwenzako na Mwanaharakati, inabidi niulize na nikuulize kati yetu ili kama kulikuwa na makosa, tuyarekebishe, kama ni kujenga mikakati, basi tukusaidie ili Bunge letu lipate Mwana JF wa pili (au zaidi ikitegemea wale wanaojificha!) baada ya Zitto.
Kwa wewe na Zitto, tambueni kuwa pamoja na JF kuwa imetapakaa dunia nzima, lakini ni Jimbo moja mahiri ambalo mnalihitaji kwa nguvu sana!
La mwisho, katika jimbo la Ubungo, ni kata ngapi na kuna madiwani wangapi ambao ni wa Chadema au Upinzani?
Nasubiri majibu yako na hata ya wengine ambao wanafahamu kwa undani kilichotokea 2005.

Last edited by a moderator: