Mkuu majebere naomba nikuulize maswala haya
1. Nipe majibu ya tume iliyoundwa juu ya wale watu waliouwa pale songea wakati walipokuwa wakienda kwa rc
2. Niambie umeanza lini kusikia malalamiko ya watu wa nyamongo juu ya polisi kufanya mauaji ya watanzania wenzetu na hata kufikia hatua ya polisi hao kutupa miili ya marehemu barabarani? Je ni hatua gani zilichukuliwa hata baada ya kamati kuundwa?
3. Niambie jana jimbo la bubu-zanzibar makamu wa rais alikuwa na mkutano wa hadhara je zanzibar hakuana sensa? Au zanzibar si tanzania au hizi sheria zinalimitation
4. Jana kulikuwa na tamasha la fiesta mwanza mpaka sa 3 usiku, je mwanza sio tanzania? Hakuna sensa?/
5. Unafahamu kuwa morogoro wilaya ya mvomero amos makala (mb) anaendelea na mikutano yake kama kawaida je mvomero sio tanzania hakuna sensa? Hakuna sensa?
6. Unafahamu kwamba polisi na chadema walikubaliana kutokufanya mikutano lakini waliruhusiwa kufanya mikutano ya ndani na kufungua matawi, je tukio lile lilitokea katika mkutano upi?
7. Niambie ni polisi gani aliyechukuliwa hatua tangu mwakyembe alipoanza kulipoti juu ya mkakati wa baadhi ya watu kutaka kumuua hata kutaka kumuua kwa sumu, na ndipo baadaye mwanahalisi kuja kueleza kwa upana wake, je ni nini kilifanyika?
Nijibu hayo kwanza maana nona unaleta masihala hapa
Unadhani hawakuelewi, wanaelewa sana, nafsi zinawauma pia, Mtu hawezi kufanya uchunguzi kwa jambo linalomhusu mwenyewe. na hivi wanajua sisi watanzania ni watu wa kuburuzwa tu, utasikia " ... jambo hilo liko mahakamani, ... Uchunguzi umekamilka, ... Police wametoa maelezo ya kina ... nk" Nimeona picha iliyotumwa CNN, nimeona picha ambazo mwana JF ameweka humu JF, hakuna haja ya tume. Walioua wameonekana hadharani, aliyeshika Limashine la kuulia ameonekana. sasa habari za kutuuliza kama ni bomu tuseme ni la aina gani, sasa huo ni utani. Ni kwamba Police wameua mwandishi wa habari, na haikuwa sawa kufanya hivyo kwasababu mwandishi huyo hakuwa na kinga yoyote, alikuwa anahangaika tu kujiokoa.Nina mashaka pia na akili au mafunzo wanayopata hao "POLISI JAMII, ULINZI SHIRIKISHI, UTII BILA SHURUTI ... " na mbwembwe kibao wanazotuletea siku hizi. Hivi wanaambiwa mashine hizo ni za kufanyia nini ? Maana ni lazima kuna boss wao anayewapatia mashine na maelekezo ! so Mheshimiwa commited, waambie issue hapa siyo kuwa nani ameua, NO, aliyeua kajulikana, labda mtu ajitetee kwa kusema Mashine ile ilijilipua nk, na hakuna msamaha, KWANINI ALIMLENGESHA MTU TUMBONI ??