ITV yaanika kila kitu na ushahidi wa kutosha kuhusu mauaji ya mwandishi huko Iringa

kwa namna moja hili jambo linatusikitisha sana, ila kwa namna nyingine ni kama ukombozi unaanza kupatikana waandishi walio wengi ni wanafiki sana wakiongwozwa na wa clous. Kina kibonde na kina hando ni wachumia tumbo kila kukicha kujipendekeza kwa jk. Hawaongeagi ukweli ni unafki kwa kwenda mbele hata leo kwenye kusoma magazeti walikuwa wanyonge sana. Baadhi ya waandishi acheni kujipendekeza kwa selikari simamieni kwenye haki mnawaponza waandishi wa maana kama daud mwang'onda waandishi makini.
 
Mkuu markj sijui hawa jamaa wanaakili gani hata kifo jamaaa wanashabikia....aghraaaa! Lakini Mungu atawajibu tu siku moja.

tangu naanza kupumua hii dunia, hakuna kitu nisichokipenda na ambacho nakichukia kama uonevu wa mabavu ya aina hii, na hasa mtu kujiona yeye ndo top kwakuwa tu ati yuko kwenye idara fulani ya uongozi au kazi husika! daaah! siku ya mwisho hii tabia katika dunia ntamshitakia mungu kwa kweli.
 
...Mkuu hii tume uchwara inayoongozwa na Mwema kamwe haitawaita hao jamaa wawili watoe ushahidi na si ajabu wanaweza kabisa kunyamazishwa ili kuficha ukweli wa kile kilichojiri katika mauaji ya Mwangosi.
una uhakika gani kama wanafaa kuwa mashahidi?mtu yeyote anaweza kujitokeza na kusema ameona yote yalio tokea
 
Kuna watu wanailaumu sana CDM hapa. Jamani CDM ina kosa gani? Hao polisi wanatumwa na CDM kufanya haya wanayoyafanya? Mimi si mwana CDM lakini naona nchi inaelekea kwenye vita kali. Hatupo tayari kusikia na kukubali ukweli wa damu hizi zinazomwaga hivi.

Watanzania tuugane kwa pamoja bila kujali chama na kuyakataa mauwaji haya. Hii nchi sii ya CCM wala CDM. Tanzania ni yetu wote. Kwamba tunauwawa kinyama hivi sii sawa.

Hili jeshi letu linaonyesha kuwa na upungufu mkubwa kuanzia kwenye rushwa, kuonea wananchi na kuwabandikia makesi, kuwanyanyasa watu, na kuwaua raia wasio na hatia.

Kama tuna serikali ya kweli ijitokeze na kusahihisha mambo. Isipofanya hivyo CDM ina haki ya kuendelea kuwahamasisha watanzania kupigania haki zao. Uhai ni haki ya kila mmoja wetu aliopewa na Mungu. Polisi hampi mtu uhai, hivyo hana haki ya kutoa uhai.

Tuungane tupiganie uhai wetu. Mungu mrehemu na kumlaza pema ndugu yetu Daudi Mwangosi na marehemu wote, apumzike kwa amani Amina
 
Hao mashahidi wamepandikizwa, na unaposema alipigwa bomu kwa nyuma utumbo ukatoka na akakatika vipande vipande,hilo ni bomu gani,la machozi au RPG. Mimi nashaka sana na hao mashahidi wako, lazima watakua wametumwa kudanganya umma. Sisi tunasubiri uchunguzi ufanyike kwanza.

unaelewa maana ya jina majebere au umejiita tu?
 
Nimefurahishwa na Helen Kijo Bisimba Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu yeye amesema kutoa matamko sasa basi, bali wao wanakwenda moja kwa moja kuifungulia kesi Serikali ya Tanzania kwenye Mahakama za kimataifa. hili ndilo ninalotaka kulisikia mimi na siyo porojo
 
Hao mashahidi wamepandikizwa, na unaposema alipigwa bomu kwa nyuma utumbo ukatoka na akakatika vipande vipande,hilo ni bomu gani,la machozi au RPG. Mimi nashaka sana na hao mashahidi wako, lazima watakua wametumwa kudanganya umma. Sisi tunasubiri uchunguzi ufanyike kwanza.

Majebere kaa ukijua hii dunia sote tunapita... Jaribu kuwa na moyo wa kibinaadamu kidogo, Hata kama unafaidika na huu mfumo lakini umefikiria maisha ya watanzania wenzako huyo marehemu ameacha watoto wanne (4) na mke, just imagine angekuwa na kaka yako huyo marehemu gafla from no where familia yake imeyumba, mtu hakuwa na silaha, wala hakuwa na jiwe zaidi alikuwa na kamera yake ya kazi lakini wewe bado unajifanya kiziwi sawa mkuu UBARIKIWE SANA.
 
una uhakika gani kama wanafaa kuwa mashahidi?mtu yeyote anaweza kujitokeza na kusema ameona yote yalio tokea

Wewe endeleza ligi mkuu.. lakini Mungu ni mwema, uliwahi kusikia Mungu ameshindwa?? Endeleza masihala katika maswala ya uhai wa watu.
 
Hata kama ana chama siyo tatizo. Hakuwa anafanya kazi za chama chake. Kwani hana hadhi ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa???????????
 
Tatizo sio polisi, tatizo hiki chama kisichotii sheria za nchi. kifo ni just matokeo ya huu ukaidi.
We mtu unaejiita tume ya katiba toa undava wako hapa, tangu uifahamu CHADEMA ni kifo gani kimewahi kusababishwa na CHADEMA?, hizo ni njama za maksudi za CCM kudhohofisha upinzani. The ERGUE inawasubiri wauwaji hawa
 
BEWARE OF POLICEMEN! Polis wetu wamegeuka wauaji.

Mbona mauaji walianza Zamani Sana Mkuu...


Huyu Askari Masikini ndio katumwa tu japo pichani anaonesha kusikitika sana na huzuni imemjaa sana sana sasa afanyeje na hali ishatokea nadhani siku zijazo nafsi yake itamsuta na atakuja sema kila kitu hata kama kupitia mtu mwingine... Namuombea atubu nadhani hata hayo magwanda alilazimishwa tu kuyavaa haonekani kama yeye ni FFU The Killer

2nd September 2012 22:05 akishuhudia.jpg
(1 of 4)
 
Mtu mmoja kasema waandishi wawe na msimamo ila kama sio wa akina '' ULI". Mimi nachelea kwani mimi ni mmoja wa akina ULI, kuna mahali hawa jamaa wa media hawakutendea haki. Baadhi yao walikuwa wanaripoti tofauti na hali halisi, ama kwa "kutumiwa" au kwa kutofahamu. Sasa hili linawahusu wao. None other than themselves know what transpired leading to the demise of our fellow Tanzanian. Watuhabarishe sisi jamii bila uoga. Mbona kibaka aliyechomwa moto humtaja hata jina. wasituambie uchunguzi unaendelea.

Mimi si mwanasiasa ila napenda kuanalyse mambo. Mbona kwenye mikusnyiko ya CDM ndiko tu watu hufa. Moja-aidha wanachafuliwa ili waonekane wana fujo ama wao wenyewe wana shida mahali.

Wanakufa ni sisi wananchi, mbaya kuliko yote na wale wanotaka kutuhabarisha ama uozo wa CDM au wa sirikali kupitia CDM.

Nini kifanyike, ili kunusuru hii hali?????????????????

Tushauriane kwa pamoja maana hata kwenda kwa mikusanyiko tutaogopa achilia mbali kuwa mwenyewe na kujikuta "Mabwe".
 
Majebere kaa ukijua hii dunia sote tunapita... Jaribu kuwa na moyo wa kibinaadamu kidogo, Hata kama unafaidika na huu mfumo lakini umefikiria maisha ya watanzania wenzako huyo marehemu ameacha watoto wanne (4) na mke, just imagine angekuwa na kaka yako huyo marehemu gafla from no where familia yake imeyumba, mtu hakuwa na silaha, wala hakuwa na jiwe zaidi alikuwa na kamera yake ya kazi lakini wewe bado unajifanya kiziwi sawa mkuu UBARIKIWE SANA.
Haya maneno unatakiwa kumwambia Slaa sio mimi, lasivyo ataendelea kuhamasisha fujo na watu wasio na hatia wataendelea kuumia au kufa. Polisi wako kazini kutuliza ghasia kwa njia wanazo zijua wao. Na pia waandishi wa habari wanajua hatari za shughuli zao lakini wanachukua risk,haya ndio madhara yake.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom