ITV yaanika kila kitu na ushahidi wa kutosha kuhusu mauaji ya mwandishi huko Iringa

...what will it take to open our minds..!?

TUZIDISHE MAOMBI NA SALA..
 
shauri hili halina hadhi ya kwenda the hague, kosa hili halijadondokea kwenye any of the four crimes under the icc statute...can you say this is a widespread and systematic attack against civilian population within the meaning of the icc statute? ili tuseme hii ni crime against humanity? bado haijafikia hadhi hiyo, halafu hata hivyo, bado nchi yetu inayo room kupelekea watu mahakamani kwa at least mwaka mmoja ndio reasonable before the icc gets in...kuna principle kweney article 17 of the icc statute inaeleza principel ya complimentarity, na kama watu watapelekwa mahakamani kwa nia ya kuwashield tu au kama selikali itakuwa serious etc...kwa hili, hawa wataangukia kwenye mahakama zetu hizihizi tu bro.

mkuu ubungoubungo tks 4 your mchango. ktk thread yangu uliyoikariri nilisema neno "in case" kwamba huko mbeleni km mambo haya yataleta masahibu km yaliyotokea kenya kwa wale ocampo six. all in all nashkuru kwa data zako mkuu.
 
Mkuu majebere naomba nikuulize maswala haya
1. Nipe majibu ya tume iliyoundwa juu ya wale watu waliouwa pale songea wakati walipokuwa wakienda kwa rc
2. Niambie umeanza lini kusikia malalamiko ya watu wa nyamongo juu ya polisi kufanya mauaji ya watanzania wenzetu na hata kufikia hatua ya polisi hao kutupa miili ya marehemu barabarani? Je ni hatua gani zilichukuliwa hata baada ya kamati kuundwa?
3. Niambie jana jimbo la bubu-zanzibar makamu wa rais alikuwa na mkutano wa hadhara je zanzibar hakuana sensa? Au zanzibar si tanzania au hizi sheria zinalimitation
4. Jana kulikuwa na tamasha la fiesta mwanza mpaka sa 3 usiku, je mwanza sio tanzania? Hakuna sensa?/
5. Unafahamu kuwa morogoro wilaya ya mvomero amos makala (mb) anaendelea na mikutano yake kama kawaida je mvomero sio tanzania hakuna sensa? Hakuna sensa?
6. Unafahamu kwamba polisi na chadema walikubaliana kutokufanya mikutano lakini waliruhusiwa kufanya mikutano ya ndani na kufungua matawi, je tukio lile lilitokea katika mkutano upi?
7. Niambie ni polisi gani aliyechukuliwa hatua tangu mwakyembe alipoanza kulipoti juu ya mkakati wa baadhi ya watu kutaka kumuua hata kutaka kumuua kwa sumu, na ndipo baadaye mwanahalisi kuja kueleza kwa upana wake, je ni nini kilifanyika?
Nijibu hayo kwanza maana nona unaleta masihala hapa
 
Nimekosa la kusema kabisa.Nakubaliana na pendekezo la kuanzisha kitengo cha Records za matukio ya uhalifu dhidi ya binadamu pale CDM ili hapo baadae watu hao washughulikiwe maana kwa serikali ya sasa hawatafanywa lolote.Wakati ukifika ule utetezi eti nilikuwa natimiza maagizo ya wakubwa hautapata nafasi.Tushikamane 2015 tuirudishe serikali kwa wananchi wenyewe vinginevyo tutakufa wengi tunajiona.
 
kuna mashahidi wawili ambao ni waandishi wa habari waliokuwa na marehemu MWANGOSI (JANA- KATIKA UVUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA-IRINGA, MUFINDI) wakati anakamatwa na mapolisi shahidi walikuwa wanaelezea tukio zima itv news usiku huu (sa 2 ) wa kwanza anasema
"marehemu alikamatwa na mapolisi 8, wakampiga sana na marungu kwa mda mrefu kila upande wa mwili wake, akatokea polisi wa nyota tatu akawasihi hao polisi 8 wamwachie marehemu lakini haikufaa kitu akatokea polisi mmoja akaja kwa nyuma ya yule aliyekuwa akiwazuia wasiendelee kumpiga marehe akamfyatulia risasi marehemu na kumtawanya utumbo na bomu hilo likamvunja mguu hata huyo polisi aliyekuwa akiwazuia wasimuue.

Shahidi wa pili anasema
Yeye (huyo shahidi-ambaye pia ni mwandishi wa habari)alipoona marehemu anapigwa alikimbilia kutoa taarifa kwa mkuu wa mapolisi waliokuwa katika eneo hilo la tukio huyo mkuu wao alikuwa katika gari akiwa kafunga viooo huyo shuhuda ambaye naye ni mwandishi alipofika hapo akagonga kioo cha gari ili huyo afisa wa polisi afungue, alipofungua huyo mwandishi akamweleza tafadhali naomba msaada wako mkuu yule anayepigwa pale ni mwandishi wa habari, tafadhali naomba msaaada wako huyo afisa hakumsikiliza akarock kiooo.

Ndio maaana nawahuliza hao (Majebere, mwiba na wengineo) wapenda uozo na mauaji ya polisi wameyasikia haya (Ushahidi toka kwa watu wailiokuwa eneo la tukio)? na kuangalia tv... maana wao sijui wanamioyo gani hawa watu ni zaidi ya wanyama kila wakati wao ni kuwatetea polisi hata uweke ushahidi wazi kiasi gani.

Imeniuma sana wakuu SORRY KWA ALIYEKWAZIKA JINSI NILIVYOLIPOTI NI HASIRA JUU YA HAO WATU

mkuu aliyegongewa KIOO GARI alikuwa RPC wa IRINGA na akashusha kioo cha gari na baada ya mwandishi kumweleza akapandisha kioo.
Mimi inaniuma sana ,utadhani hao police wao wataishi milele,ila Mungu yupo
 
Mkuu kauli zake huyu mwandishi ndio zinafahamika, huyu ni mwanachama mtiifu wa CDM na hilo linafahamika. Kwa hiyo uandishi ilikuwa just cover tu.

Kwa hiyo ukiwa mfuasi wa Chadema ndiyo unastahili kuwaua? Jaribu kutumia akili japo unazo kidogo.
 
Mkuu majebere naomba nikuulize maswala haya
1. Nipe majibu ya tume iliyoundwa juu ya wale watu waliouwa pale songea wakati walipokuwa wakienda kwa rc
2. Niambie umeanza lini kusikia malalamiko ya watu wa nyamongo juu ya polisi kufanya mauaji ya watanzania wenzetu na hata kufikia hatua ya polisi hao kutupa miili ya marehemu barabarani? Je ni hatua gani zilichukuliwa hata baada ya kamati kuundwa?
3. Niambie jana jimbo la bubu-zanzibar makamu wa rais alikuwa na mkutano wa hadhara je zanzibar hakuana sensa? Au zanzibar si tanzania au hizi sheria zinalimitation
4. Jana kulikuwa na tamasha la fiesta mwanza mpaka sa 3 usiku, je mwanza sio tanzania? Hakuna sensa?/
5. Unafahamu kuwa morogoro wilaya ya mvomero amos makala (mb) anaendelea na mikutano yake kama kawaida je mvomero sio tanzania hakuna sensa? Hakuna sensa?
6. Unafahamu kwamba polisi na chadema walikubaliana kutokufanya mikutano lakini waliruhusiwa kufanya mikutano ya ndani na kufungua matawi, je tukio lile lilitokea katika mkutano upi?
7. Niambie ni polisi gani aliyechukuliwa hatua tangu mwakyembe alipoanza kulipoti juu ya mkakati wa baadhi ya watu kutaka kumuua hata kutaka kumuua kwa sumu, na ndipo baadaye mwanahalisi kuja kueleza kwa upana wake, je ni nini kilifanyika?
Nijibu hayo kwanza maana nona unaleta masihala hapa
Majibu karibu yote utayapata baada ya tume kufanya uchunguzi, vuta subira. Lakini kumbuka kuwa matukio yote yamefanyiwa uchunguzi lakini watanzania wanatabia ya kusahau haraka sana, hata hili tukio litasahaulika pamoja na kwamba uchunguzi utaisha na maelezo yote yatakuwepo.
 
Hao mashahidi wamepandikizwa, na unaposema alipigwa bomu kwa nyuma utumbo ukatoka na akakatika vipande vipande,hilo ni bomu gani,la machozi au RPG. Mimi nashaka sana na hao mashahidi wako, lazima watakua wametumwa kudanganya umma. Sisi tunasubiri uchunguzi ufanyike kwanza.

Uchunguzi unaofanywa na Police wenyewe, ukisimamiwa na wao wenyewe ili kubaini kama wao wenyewe wameua ! Mh, Mhhhhhh ! Mh ....Kwamba panya waende kuchunguza ili kubaini kama kweli panya hao wamekula mahindi !?? Mh !
 
Hongera sana ITV nashauri 2015 baada ya Chadema kuchukua nchi kituo hiki kiwe ndiyo Television ya taifa and then kuifungia milele Tbc na wote wlioajiliwa Tbc wasiruhusiwe kuajiriwa sehemu yeyote Tanzania
 
una uhakika gani kama wanafaa kuwa mashahidi?mtu yeyote anaweza kujitokeza na kusema ameona yote yalio tokea
Ukijitambulisha kwa uwazi kama msemaji wa serikali/polisi watu watakuelewa ila kama unatoa mawazo yako kama individual ndio unapokuja mshangao wa wengi hapa JF
 
kuna mashahidi wawili ambao ni waandishi wa habari waliokuwa na marehemu MWANGOSI (JANA- KATIKA UVUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA-IRINGA, MUFINDI) wakati anakamatwa na mapolisi shahidi walikuwa wanaelezea tukio zima itv news usiku huu (sa 2 ) wa kwanza anasema
"marehemu alikamatwa na mapolisi 8, wakampiga sana na marungu kwa mda mrefu kila upande wa mwili wake, akatokea polisi wa nyota tatu akawasihi hao polisi 8 wamwachie marehemu lakini haikufaa kitu akatokea polisi mmoja akaja kwa nyuma ya yule aliyekuwa akiwazuia wasiendelee kumpiga marehe akamfyatulia risasi marehemu na kumtawanya utumbo na bomu hilo likamvunja mguu hata huyo polisi aliyekuwa akiwazuia wasimuue.

Shahidi wa pili anasema
Yeye (huyo shahidi-ambaye pia ni mwandishi wa habari)alipoona marehemu anapigwa alikimbilia kutoa taarifa kwa mkuu wa mapolisi waliokuwa katika eneo hilo la tukio huyo mkuu wao alikuwa katika gari akiwa kafunga viooo huyo shuhuda ambaye naye ni mwandishi alipofika hapo akagonga kioo cha gari ili huyo afisa wa polisi afungue, alipofungua huyo mwandishi akamweleza tafadhali naomba msaada wako mkuu yule anayepigwa pale ni mwandishi wa habari, tafadhali naomba msaaada wako huyo afisa hakumsikiliza akarock kiooo.

Ndio maaana nawahuliza hao (Majebere, mwiba na wengineo) wapenda uozo na mauaji ya polisi wameyasikia haya (Ushahidi toka kwa watu wailiokuwa eneo la tukio)? na kuangalia tv... maana wao sijui wanamioyo gani hawa watu ni zaidi ya wanyama kila wakati wao ni kuwatetea polisi hata uweke ushahidi wazi kiasi gani.

Imeniuma sana wakuu SORRY KWA ALIYEKWAZIKA JINSI NILIVYOLIPOTI NI HASIRA JUU YA HAO WATU
shukrani kwa taarifa hii mkuu,maneno hayo,tuliwaambia kina Zomba exactly kama hao mashahidi walivyosema,just by looking at the pictures,and knowing the police very well,basi I was right.They've said it exactly what we thought went down.
 
Uchunguzi unaofanywa na Police wenyewe, ukisimamiwa na wao wenyewe ili kubaini kama wao wenyewe wameua ! Mh, Mhhhhhh ! Mh ....Kwamba panya waende kuchunguza ili kubaini kama kweli panya hao wamekula mahindi !?? Mh !
mimi nikuulize, hakimu akifanya kosa hapelekwi mahakamani, au wao kesi zao zinasikilizwa na mtu tofauti? Kama kuna polisi wameua kwa kukusudia basi watashitakiwa, hii ndio kazi ya polisi hata kama watuhumiwa pia ni polisi.
 
shukrani kwa taarifa hii mkuu,maneno hayo,tuliwaambia kina Zomba exactly kama hao mashahidi walivyosema,just by looking at the pictures,and knowing the police very well,basi I was right.They've said it exactly what we thought went down.
naona bongo CSI mko wengi.
 
Ebana ehh, mimi naona niwaache mpaka kesho, hii ni mida ya kupata bia baridi sio wakati wa malumbano.
 
M4C sasa kutua dodoma,kwa ratiba iliyopo ni kwamba CDM sasa inajiandaa kufanya oparation Kubwa dodoma na wilaya zake zote sasa cjui wajamba zangu hasa waishio wilaya ya bahi wako tayari kufa wamesimama au kuendelea kuishi huku wamepiga magoti.WAANDISHI WA HABARI KUI UNGA MKONO SERIKALI KUWA CHADEMA NDIO WALIO SABABISHA MAUUAJI NA FIKIRI MTAKUWA HAMTENDEI HAKI MWNZENU.
 
Hivi hizi tume zina tusaidia nini?
Kila siku zinaundwa tume za kuchunguza matukio lakini zimekuwa ni tume za kutetea watuhumiwa tu!

Hao mashahidi wamepandikizwa, na unaposema alipigwa bomu kwa nyuma utumbo ukatoka na akakatika vipande vipande,hilo ni bomu gani,la machozi au RPG. Mimi nashaka sana na hao mashahidi wako, lazima watakua wametumwa kudanganya umma. Sisi tunasubiri uchunguzi ufanyike kwanza.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom