johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,980
Maxence Melo Mkurugenzi wa Jamii Forums amesema Uvujishaji wa Taarifa uko zaidi Nje ya Mitandao kwa mfano Makaratasi ya Matokeo ya Mitihani Kufungia Maandazi na Chapati.
Mungu wa Mbinguni Ibariki JF 😂
---
Maxence Melo, Mkurugenzi wa Jamii Forum: Uhuru huu wa mitandao ambao tunaupima sasa hivi ndiyo ulioleta uwajibikaji, ambao unaonekana lakini umekuja kwa baadhi ya watu kutoka jasho wengine damu.
Mitandao ya kijamii na digitali kwa ujumla wake imetoka mbali imepitia milima, mabonde, kona kadhaa tumezikata, tumefanya vyema lakini tulipofika mitandao ina nguvu.
Kwa mfano kunguni waliokuwapo Chuo Kikuu cha Dodoma ingekuwa mwandishi ameenda ahoji, stori ingeishia palepale lakini ilivyotolewa mitandaoni hatua zikachukuliwa.
Kama mnakumbuka Azory Gwanda ambaye hadi sasa hatujui aliko ingawa kuna mtu aliyewahi kuwa waziri aliwahi kusema aliuwawa, pia kuna mwanahabari aliuwawa na Askari Polisi na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Iringa alisema waliofanya hivyo ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ndiyo walimuua kwa kitu chenye ncha kali.
Bahati nzuri, picha ya tukio zima ilipigwa na kupandishwa Jamii Forum kupitia mtu wetu tunayemuamini aliyehakikisha kuwa alikuwa eneo la tukio, ilisaidia hatua zichukuliwe lakini upotoshaji ulikuwa umeshaanza na kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka waandishi wengine wangelazimika kuandika kuwa wafuasi wa Chadema wamemuua mwandishi wa habari kwa kitu cha ncha kali.
Mitandao ya kijamii inatoa taarifa ila isipowalinda watoa taarifa hii inaweza kuwa nafasi hatarishi kwa wananchi pia inaweza kuwaumiza wengine.
Source: Mwananchi