ISIS yatafuta kiki kupitia Uislam

ISIS yatafuta kiki kupitia Uislam

swali lako ntakujibu kama utaniambia ni nani anaepaswa kufuatwa kati ya Muhammad ibn wahab wa karne ya 18 na Prophet Muhammad (pbuh) .?
Kaa kimya kama hujui WAHHABISM utajiabisha bure.

SOMA hapa -->
Wahhabism is noted for its policy of "compelling its own followers and other Muslims strictly to observe the religious duties of Islam, such as the five prayers", and for "enforcement of public morals to a degree not found elsewhere"
 
wewe ni muongo, tunaishi na waislamu na wanashabikia wakristo kuuawa eti ni makafir, Kwa hiyo uislamu ni ugaidi kabisa, si ndo nyie mkiuwa kafir Kwa kujilipua mnaenda peponi na kupewa wabikra 72 na juice tamu?
bora umemtumbua hawa ni laana ya ngono tu na mabikra wakufikirika mpaka wanaua watu wasio na hatia. Hao ni waislamu kabisaaa japo siwezi walaumu waislamu wote maana wengine wana roho nzuri
 
mleta mada yuko sahihi na nikweli kabisaa hamna hata aya moja ktk qurani inayotaka watu wauane....na ukisoma vzr historia ya uislamu utagundua maswahaba wengi walikuwa wakiabudia miti na vitu vinginevyo sa lau kama mtume Angekuwa na msimamo kama wa isis wakuua kila asiyekuwa muislam je hao maswahaba Wangeingia vp ktk uislamu maana angewaua wotee!! dini ya uislamu inavyofahamika tofauti na ilivyo na mtu akitaka kuufaham uislam kwa elimu basi ni lzm akae chini asome mfano uislamu unazingatia haqi za jirani ambae si muislam tena haqi hizoo ametufundisha mtume sasa he lau kama mtume angekuwa muuaji kama Osama bin laden je hata hizo haqi za jirani asiye muislam angezifundisha? tafadhali ndugu zetu ktk utu na ubinadamu acheni dhana potofu dhidi ya uislamu!! uislamu haukubaliani kabisa na vitendo vya kigaidi
uzuri saizi mnalipuana wenyewe mpaka misikitini mwenu na bado mtashikishana adabu tuu
 
Vipi kuhusu alshabab walivyoua hapo Kenya?! Mbona sikuona matamko kama haya ya kulaani?
 
Wa kiislamu wanauana wao kwa wao kwa sababu ya makundi ya madhehebu ya kishia na sunni.wakimalizana huko watugeukie as wakristu na mayahudi.khaaa,naiona dunia iliyo salama bila waarabu na waislamu
 
Katika Quran hakuna hicho ulichokieleza ila Quran inasema kwamba Atakaeua nafsi moja isiyo na hatia ni sawa na ameua ulimwengu mzima na atakayeiokoa nafsi moja ni sawa na ameuokoa ulimwengu mzima. Pia quran inasema kuwa tusiwacheke na kuwakejeli wanaoabudu wengine Zaidi ya Allah. sasa sijui hao wanaoua wapate mabikira 72 wanasoma Quran Gani ama wanafata muingozo gani,na nahisi hao unaowasikia wakikupa habari hizo ni wale waislam majina. kumbuka Kuitwa Rashid hakumfanyi mtu kuwa muislam. Shukran
mkuu kwenye hii point umekosa shabaha My name is Green Bird and I am not a terrorist
 
Uislamu Unasemaje Juu ya Ugaidi?
Uislamu, Dini ya rehma, hauruhusu ugaidi. Katika Qur-aan, Mwenyezi Mungu Amesema:
“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni
makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu Huwapenda wafanyao uadilifu.” (Qur-aan, 60:8)
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakataza askari dhidi ya kuwaua wanawake na watoto,[ 90 ]na alikuwa akiwashauri:
((...Msisaliti, msizidishe sana, msimwue mtoto mchanga.))” [ 91 ]
Alisema pia:
((Mwenye kumuua mtu aliye katika mkataba na Waislamu, hataipata harufu ya Peponi, ingawa harufu yake hupatikana mpaka katika umbali wa mwendo wa miaka arubaini.))[ 92 ]
Kadhalika, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kutoa adhabu ya moto.[93 ]
Kuna wakati aliorodhesha dhambi ya kuua kuwa ya pili miongoni mwa madhambi makubwa,[ 94 ]
hata akatahadharisha hilo juu ya Siku ya Hukumu, (( Kesi za mwanzo kuhukumiwa baina ya watu ka tika Siku ya Hukumu zitakuwa ni zile za umwagaji damu. 95 )) [ 96 ]
Waislamu huhimizwa hata kuwa wakarimu kwa wanyama na wamekatazwa kuwadhuru. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema siku moja:
((Mwanamke aliadhibiwa kwa sababu alimweka paka kifungoni mpaka akafa. Kwa minajili hii, aliangamiziwa Motoni. Wakati alipomweka kifungoni, hakumpatia paka chakula wala kinywaji, wala hakumwacha huru ale wadudu wa ardhini.)) [ 97 ]
Pia alisema kuwa kuna mtu alimpatia kinywaji mbwa aliyekuwa na kiu kikali, hivyo Mwenyezi Mungu Alimsamehe madhambi yake, kwa kitendo hiki. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je, sisi hulipwa kutokana na ukarimu wetu kwa wanyama?” Alijibu:
((Kuna malipo kwa ukarimu kwa kila mnyama hai au mwanaadamu.))
[ 98 ]
Zaidi ya hayo, wakati wa kuchinja mnyama kwa ajili ya chakula, Waislamu wameamrishwa kufanya hivyo katika namna inayopelekea hofu ndogo na mateso madogo sana kwa mnyama, kadiri itakavyowezekana. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mnapomchinja mnyama, fanyeni katika njia iliyo bora zaidi. Mchinjaji akinoe kisu chake kwa ajili ya kupunguza mateso ya mnyama.)) [99 ]
Kutokana na mwangaza wa haya na mafundisho mengine ya Kiislamu, kitendo cha kuchochea khofu katika nyoyo za raia wasio na ulinzi, uharibifu wa majengo na mali, ulipuaji mabomu na kuwalemaza wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia, yote haya yamekatazwa, tena ni matendo ya kuchukiza kwa mujibu wa Uislamu na Waislamu. Waislamu wanaifuata Dini ya amani, huruma na msamaha, na wengi hawahusiani na matukio ya vurugu ambayo baadhi yamehusishwa na Waislamu. Ikiwa Muislamu mmojawapo atajihusisha na kitendo cha kigaidi, mtu huyo atakuwa katika hatia ya kukiuka sheria za Uislamu.
[90 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1744, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 3015
[91 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1731, na
At-Tirmidhiy, Na, 1408
[92 ]Imeandikwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy, Na. 3166, na Ibn Majah, Na. 2686
[93 ]Iko ndani ya Abu Daawuud, Na. 2675
[94 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 6871, na Swahiyh Muslim Na. 88
[95 ]Hii inamaanisha kuua na kujeruhi
[96 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1678, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 6533
[97 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 2422, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 2365
[98 ]Hadiyth hii ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imeelezwa kwa kirefu hapo nyuma. Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim
Na. 2244, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 2466
[99 ]Imeandikwa katika Swahiyh Muslim, Na. 1955 na At-Tirmidhiy,
Na. 1409
simulizi yako ni nzuri lakini nenda kasome uislmu unasemaje au kama quran itakuwa vema usiseme vitu kwasababu fulani atafurahia hapana haki ifiautwe kasome ustadh. Mimi ni green Bird and I am not a Terrorist
 
Wale sio waislam,uislam ni AMANI.Kama mtume Muhammad,angekuwa auwa watu ovyo,uislam usingeeneya dunia nzima.
Umejeribu vema ila usimkufurishe uislamu umekataza jambo hili tusome uislamu ni mtamu ukiujua My name is Green Bird And I am not a Terrorist
 
Uislam unafungamana na Ugaidi wewe unajisumbua tu kuutetea kila mtu anajua vikundi vya kiislamu vya kiuuaji vinavyofanya kazi ya kuua watu wasiokuwa waislamu.
Umeongea bila ushahidi lete ushahidi twende sawa. My name Is Green Bird And I am not a terrorist
 
Unajua Unaweza Kuwatetea Ila Kwa Matendo ya Waislamu Yanayofanywa Mfano Tu Zanzibar hapo Inaniwia Vigumu kusema Magaidi Si Waislamu
Umenena vema lakini kumbuka kuna waislamu na waumini quran imesema kuwa waumini ndio watakao ingia Jannah usimuangalie muislamu anafanyaje tazama uislamu unatakaje. My name is Greed Bird and I am not a Terrorist
 
mleta mada yuko sahihi na nikweli kabisaa hamna hata aya moja ktk qurani inayotaka watu wauane....na ukisoma vzr historia ya uislamu utagundua maswahaba wengi walikuwa wakiabudia miti na vitu vinginevyo sa lau kama mtume Angekuwa na msimamo kama wa isis wakuua kila asiyekuwa muislam je hao maswahaba Wangeingia vp ktk uislamu maana angewaua wotee!! dini ya uislamu inavyofahamika tofauti na ilivyo na mtu akitaka kuufaham uislam kwa elimu basi ni lzm akae chini asome mfano uislamu unazingatia haqi za jirani ambae si muislam tena haqi hizoo ametufundisha mtume sasa he lau kama mtume angekuwa muuaji kama Osama bin laden je hata hizo haqi za jirani asiye muislam angezifundisha? tafadhali ndugu zetu ktk utu na ubinadamu acheni dhana potofu dhidi ya uislamu!! uislamu haukubaliani kabisa na vitendo vya kigaidi
kasome tena akhii unaonyesha umezaliwa kwenye uislamu lakini qurani hujaifahamu My name is Green bird and I am not a Terrorist
 
mm nishawasema sana kweny mimbali msikitini ...mm ni sunni na nimesoma dini tofauti na wao wanaobeba misimamo bila ya elimu!!
sheikh usijisifu mimi naona unahoja dhaifu wewe umesema uislamu umekataza kuuwa lakini qurani hiyo hiyo ndio imeruhusu vita na hakuna vita isiyokuwa na mauaji kasome surat anfal imetaja mpaka kuwaandalia nguvu makafir ukitaka tukuelewe tafuta hoja zenye mashiko lakini kuuwa uislamu umeruhusu japo sio kama wanavyofnya ISIS My name is Green Bird And I am not a Terrorist
 
Mkuu wewe ni mkweli ila unakosea katika ukosoaji wako.Dini ya uislamu inasema msiwapige wale wasio wapiga vita lau kama wanaleta hoja zao basi nanyi wapeni maibu kwa hoja wala msitumie lugha za kuudhi na matusi kwa sababu nyinyi mkiwatusi na wao watamtukana mola wenu mlezi.So kuna makundi kweli yanapigana na ukafiri ila sisemi kama ukristo ni ukafiri kwa sababu hata Allah anatambua kuwa wakristo(manaswara) wapo na wayahudi so ikiwa yeyote atakayekuwa si muislam akianza kuipiga vita uislamu hatuna budi nasi kujibu mashambulizi ya vita hiyo. Rai yangu ni kuwa hawa jamaa wanapigana jihadi wengi wao wanaleta siasa za kidunia katika dini ndio maana haipatikani suluhu yake asilani abadani.
Allaaahu kbaar katika maoni yote ni wewe umenena kwa busara na hoja zenye tija allaah akuzidishie My name is Green Bird And I am not a terrorist
 
.....mm sijalijua hata kundi moja lakiislamu linalopigana na makafiri na kama ww unalijua Mkuu nitajie!! makundi yote yanayopigana hivi sasa yameasisiwa na alqaeda hivyo ukisema yapo makundi yanapigana kweli dhidi ya makafir maana ake unatambua kuwa alqaeda wanachofanya ni sahihi!! wanazuoni wa kiislamu kutoka duniani kote wametahadharisha vikundi vya kigaidi! wamewataka waislamu wajiweke mbali na hivi vikundi kwani ni venye kuuchafua uislamu pia ktk hivi vikundi watu hawana maarifa ya dini (elimu) na ndo maana wanafikia mpk kuteka mabinti kuwasilimisha kwa lazma kisha kuwaoa kwa lazima
lakini kama utakuwa ulifuatilia vema hao wanaokataza sasa hivi ndio walituambia kuwa afughanistan ni jihaad na tuende tukaungane na mujahideed na aliyekuwa akitoa msaada mkubwa wa kivita ni Osama Ibn Laden na hawa wanaotutahadharisha na haya makundi ndio waliotupatia nasaha za kwenda kujiunga na ndugu zetu waislamu wa afghanstan My name is Green Bird and I am not a Terrorist
 
Acha unafiki wewe wale ndio wanafuata dini ya uislam na watampga yyte ambae anapnga au hatekelezi maandiko!!Eb kakisome kitabu chenu ukimalize ukielewe
AF uje kujibu haya
Kwanini hawataki kuigeuza quaran" kwa lugha za husika kama kiswahili au kingereza n.k ili kila MTU a some aielewe!!mnatetea eti utapunguza swawabu!!
2.Wazinzi wakikamatwa mwanamke inabidi apgwe mawe ,mbona hampgi
3. Wasio waamini uislam mnawaita kafiri,na kadiri yenu kafiri hatakiwi wala Hana haki ya kuishi
Wanachofanya IS wapo sawa kadiri ya maandiko yenu !!Huwez kuyapnga hayo makundi wakati dini yenu ndo inasema hivo!!
Kumbuka tu kilichotokea Kenya!! Wale wanatekeleza kilichoandkwa!!
umejitahidi kuelezea hisia zako japo umetumia jazba kiasi.
kwanini hawataki kuigeuza quran kwa lugha za husika kama kiswahili n.k ? jibu quraan ipo ya kiswahili ila wewe ni mvivu kuitafuta ingia hapa>>>>quranitukufu.net
wazinzi wakikamatwa mwanamke inabidi apigwe mawe mbona hampingi ? Jibu sio mzinifu mwanamke ndio apigwe mawe hapa wote wawili hukumu yao ni kupigwa mawe mpaka wafe tena hadharani ikiwa ni wanandoa lakini ikiwa sio wanandoa hukumu yao ni >>>>Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini.
Wasio waamini uislam mnawaita kafiri,na kadiri yenu kafiri hatakiwi wala Hana haki ya kuishi? Ushaidi upi ulioutumia kuwa uislamu unamnyima haki kafiri kuishi je mjomba wake mtume alikuwa muislamu mbona hakuuliwa hindu na wengine wengi ukisoma historia hawakuwa waislamu na waliishi katika miji ya kiislamu punguza jazba.
Kumbuka tu kilichotokea Kenya!! Wale wanatekeleza kilichoandkwa ? wapo ni masheikh na niwachawi lakini ukifika muda wa sala huwa wanaacha madudu yao na kwenda kusali so alshabaab kuacha mapigano na kwenda kusali sio hoja ya msingi lete hoja zenye mashiko My name is green bird And I am not a Terrorist
 
Dini yenyewe ilienea na kukua kwa kumwaga damu(jihhad)
wana historia tu watanielewa hapa.
Wapi ushahidi uislamu haukuenea kwa upanga ila kisasi kililipwa kwa upanga je unajua mtume hakupigana vita yeyote katika mji wa makkah kabla ya hijra? My name is Green Bird and I am Not a Terrorist
 
Wewe sio mwana historia, usingelishangaa hili sheikh wangu.
samahani mkuu nilikuwa sijakuelewa na hizo historia zenu za kuwa watu mulianza kuwa manyani. My name is Green Bird and I am Not a Terrorist
 
Back
Top Bottom