ISIS yatafuta kiki kupitia Uislam

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
845
Asalam Aleikum..!

Nasikitika kusema kuwa watu wengi hawajajua kuwa waislam ndo target kubwa ya magaidi. ISIS sio waislam kwa sababu hakuna muislam mwenye akili timamu atakayeweza kwenda kulipua Madina. Hii inadhihirisha wazi kwamba ISIS, Al Qaeda na wengineo wako after something else na sio kwa ajili ya dini.

Uislam ni salama na umejitenga mbali na upuuzi unaofanyika kwa jina la Uislam. Kwa akili ya kawaida tujiulize kwanini hao wanaojiita waislam wanalipua ndani ya misikiti, wanaua katika miji ya waislam?

Ndugi zanguni nawaombeni tuuweke Uislam mbali na upuuzi huu na tuwaone hao magaidi ni wapuuzi wasio na akili ambao wanafurahia kumwaga damu za watu wasio na hatia. Angalieni kule Syria hao ISIS wakiteka mji wanaua wanaume wote na kuwateka wanawake na kuwafanya watumwa wa ngono.

Mimi ni muislam na kamwe siwez kuwasaport wala kuwafurahia magaidi kwa sababu dini yangu hairuhusu unyama unaofanywa na Magaidi.

Wasalam
 
Asalam Aleikum..! nasikitika kusema kuwa watu wengi hawajajua kuwa waislam ndo target kubwa ya magaidi. ISiS sio waislam kwa sababu hakuna muislam mwenye akili timamu atakayeweza kwenda kulipua Madina, hii inadhihirisha wazi kwamba ISIS,ALKAIDA na wengineo wako after something else na sio kwaajili ya dini. UISLAM ni salama na umejitenga mbali na upuuzi unaofanyika kwa jina la Uislam. kwa akili ya kawaida tujiulize kwanini hao wanaojiita waislam wanalipua ndani ya misikiti?wanaua katika miji ya waislam,. Ndugi zanguni Nawaombeni Tuuweke UISLAM mbali na Upuuzi huu na tuwaone hao magaidi ni wapuuzi wasio na Akili ambao wanafurahia Kumwaga damu za watu wasio na hatia. Angalieni kule syria Hao ISIS wakiteka mji wanaua wanaume wote na kuwateka wanawake na kuwafanya watumwa wa ngono. Mimi ni muislam na kamwe siwez kuwasaport wala kuwafurahia magaidi kwa sababu Dini yangu hairuhusu unyama unaofanywa na Magaidi. Wasalam
wewe ni muongo, tunaishi na waislamu na wanashabikia wakristo kuuawa eti ni makafir, Kwa hiyo uislamu ni ugaidi kabisa, si ndo nyie mkiuwa kafir Kwa kujilipua mnaenda peponi na kupewa wabikra 72 na juice tamu?
 
Katika Quran hakuna hicho ulichokieleza ila Quran inasema kwamba Atakaeua nafsi moja isiyo na hatia ni sawa na ameua ulimwengu mzima na atakayeiokoa nafsi moja ni sawa na ameuokoa ulimwengu mzima. Pia quran inasema kuwa tusiwacheke na kuwakejeli wanaoabudu wengine Zaidi ya Allah. sasa sijui hao wanaoua wapate mabikira 72 wanasoma Quran Gani ama wanafata muingozo gani,na nahisi hao unaowasikia wakikupa habari hizo ni wale waislam majina. kumbuka Kuitwa Rashid hakumfanyi mtu kuwa muislam. Shukran
 
Asalam Aleikum..!

Nasikitika kusema kuwa watu wengi hawajajua kuwa waislam ndo target kubwa ya magaidi. ISIS sio waislam kwa sababu hakuna muislam mwenye akili timamu atakayeweza kwenda kulipua Madina. Hii inadhihirisha wazi kwamba ISIS, Al Qaeda na wengineo wako after something else na sio kwa ajili ya dini.

Uislam ni salama na umejitenga mbali na upuuzi unaofanyika kwa jina la Uislam. Kwa akili ya kawaida tujiulize kwanini hao wanaojiita waislam wanalipua ndani ya misikiti, wanaua katika miji ya waislam?

Ndugi zanguni nawaombeni tuuweke Uislam mbali na upuuzi huu na tuwaone hao magaidi ni wapuuzi wasio na akili ambao wanafurahia kumwaga damu za watu wasio na hatia. Angalieni kule Syria hao ISIS wakiteka mji wanaua wanaume wote na kuwateka wanawake na kuwafanya watumwa wa ngono.

Mimi ni muislam na kamwe siwez kuwasaport wala kuwafurahia magaidi kwa sababu dini yangu hairuhusu unyama unaofanywa na Magaidi.

Wasalam
Mkuu mm kila siku nawapinga hao Isis humu jukwaani na najitahidi sana kuwafahamisha watu juu ya mafundisho ya uislamu dhidi ya ugaidi!! Isis wale ni vimbwa vya motoni
 
wewe ni muongo, tunaishi na waislamu na wanashabikia wakristo kuuawa eti ni makafir, Kwa hiyo uislamu ni ugaidi kabisa, si ndo nyie mkiuwa kafir Kwa kujilipua mnaenda peponi na kupewa wabikra 72 na juice tamu?
Uislamu Unasemaje Juu ya Ugaidi?
Uislamu, Dini ya rehma, hauruhusu ugaidi. Katika Qur-aan, Mwenyezi Mungu Amesema:
“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni
makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu Huwapenda wafanyao uadilifu.” (Qur-aan, 60:8)
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakataza askari dhidi ya kuwaua wanawake na watoto,[ 90 ]na alikuwa akiwashauri:
((...Msisaliti, msizidishe sana, msimwue mtoto mchanga.))” [ 91 ]
Alisema pia:
((Mwenye kumuua mtu aliye katika mkataba na Waislamu, hataipata harufu ya Peponi, ingawa harufu yake hupatikana mpaka katika umbali wa mwendo wa miaka arubaini.))[ 92 ]
Kadhalika, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kutoa adhabu ya moto.[93 ]
Kuna wakati aliorodhesha dhambi ya kuua kuwa ya pili miongoni mwa madhambi makubwa,[ 94 ]
hata akatahadharisha hilo juu ya Siku ya Hukumu, (( Kesi za mwanzo kuhukumiwa baina ya watu ka tika Siku ya Hukumu zitakuwa ni zile za umwagaji damu. 95 )) [ 96 ]
Waislamu huhimizwa hata kuwa wakarimu kwa wanyama na wamekatazwa kuwadhuru. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema siku moja:
((Mwanamke aliadhibiwa kwa sababu alimweka paka kifungoni mpaka akafa. Kwa minajili hii, aliangamiziwa Motoni. Wakati alipomweka kifungoni, hakumpatia paka chakula wala kinywaji, wala hakumwacha huru ale wadudu wa ardhini.)) [ 97 ]
Pia alisema kuwa kuna mtu alimpatia kinywaji mbwa aliyekuwa na kiu kikali, hivyo Mwenyezi Mungu Alimsamehe madhambi yake, kwa kitendo hiki. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Je, sisi hulipwa kutokana na ukarimu wetu kwa wanyama?” Alijibu:
((Kuna malipo kwa ukarimu kwa kila mnyama hai au mwanaadamu.))
[ 98 ]
Zaidi ya hayo, wakati wa kuchinja mnyama kwa ajili ya chakula, Waislamu wameamrishwa kufanya hivyo katika namna inayopelekea hofu ndogo na mateso madogo sana kwa mnyama, kadiri itakavyowezekana. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Mnapomchinja mnyama, fanyeni katika njia iliyo bora zaidi. Mchinjaji akinoe kisu chake kwa ajili ya kupunguza mateso ya mnyama.)) [99 ]
Kutokana na mwangaza wa haya na mafundisho mengine ya Kiislamu, kitendo cha kuchochea khofu katika nyoyo za raia wasio na ulinzi, uharibifu wa majengo na mali, ulipuaji mabomu na kuwalemaza wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia, yote haya yamekatazwa, tena ni matendo ya kuchukiza kwa mujibu wa Uislamu na Waislamu. Waislamu wanaifuata Dini ya amani, huruma na msamaha, na wengi hawahusiani na matukio ya vurugu ambayo baadhi yamehusishwa na Waislamu. Ikiwa Muislamu mmojawapo atajihusisha na kitendo cha kigaidi, mtu huyo atakuwa katika hatia ya kukiuka sheria za Uislamu.
[90 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1744, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 3015
[91 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1731, na
At-Tirmidhiy, Na, 1408
[92 ]Imeandikwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy, Na. 3166, na Ibn Majah, Na. 2686
[93 ]Iko ndani ya Abu Daawuud, Na. 2675
[94 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 6871, na Swahiyh Muslim Na. 88
[95 ]Hii inamaanisha kuua na kujeruhi
[96 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 1678, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 6533
[97 ]Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim Na. 2422, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 2365
[98 ]Hadiyth hii ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imeelezwa kwa kirefu hapo nyuma. Imesimuliwa ndani ya Swahiyh Muslim
Na. 2244, na
Swahiyh Al-Bukhaariy Na. 2466
[99 ]Imeandikwa katika Swahiyh Muslim, Na. 1955 na At-Tirmidhiy,
Na. 1409
 
Katika Quran hakuna hicho ulichokieleza ila Quran inasema kwamba Atakaeua nafsi moja isiyo na hatia ni sawa na ameua ulimwengu mzima na atakayeiokoa nafsi moja ni sawa na ameuokoa ulimwengu mzima. Pia quran inasema kuwa tusiwacheke na kuwakejeli wanaoabudu wengine Zaidi ya Allah. sasa sijui hao wanaoua wapate mabikira 72 wanasoma Quran Gani ama wanafata muingozo gani,na nahisi hao unaowasikia wakikupa habari hizo ni wale waislam majina. kumbuka Kuitwa Rashid hakumfanyi mtu kuwa muislam. Shukran
Uislam unafungamana na Ugaidi wewe unajisumbua tu kuutetea kila mtu anajua vikundi vya kiislamu vya kiuuaji vinavyofanya kazi ya kuua watu wasiokuwa waislamu.
 
Islamic States ndiyo waislam original,wewe mtoa post ni kafiri tu
Fikiri kabla ya kuandika comment kama huna uhakika na kinachoendelea bora kukaa kimya. Kinachoendelea no propaganda ya kuwafanya waislam waonekane wako hivyo nakushangaa kama in muislam kweli Kuunga mkono ISIS
 
Naonaga post kama hizi pale ambapo waislam wameshambuliwa ila wamewateketeza na kuwatesa kinyama yazzids sijaona matamko kama haya.

Wamefanya mauaji Paris na kwingineko sijaona matamko kama haya zaidi waislam mmekua mkiwapa pongezi kwa kuwaua makafiri na kupigana jihad ya ala leo wanachezea kiwanja cha nyumbani povu jingi.

Shame.
 
Asalam Aleikum..!

Nasikitika kusema kuwa watu wengi hawajajua kuwa waislam ndo target kubwa ya magaidi. ISIS sio waislam kwa sababu hakuna muislam mwenye akili timamu atakayeweza kwenda kulipua Madina. Hii inadhihirisha wazi kwamba ISIS, Al Qaeda na wengineo wako after something else na sio kwa ajili ya dini.

Uislam ni salama na umejitenga mbali na upuuzi unaofanyika kwa jina la Uislam. Kwa akili ya kawaida tujiulize kwanini hao wanaojiita waislam wanalipua ndani ya misikiti, wanaua katika miji ya waislam?

Ndugi zanguni nawaombeni tuuweke Uislam mbali na upuuzi huu na tuwaone hao magaidi ni wapuuzi wasio na akili ambao wanafurahia kumwaga damu za watu wasio na hatia. Angalieni kule Syria hao ISIS wakiteka mji wanaua wanaume wote na kuwateka wanawake na kuwafanya watumwa wa ngono.

Mimi ni muislam na kamwe siwez kuwasaport wala kuwafurahia magaidi kwa sababu dini yangu hairuhusu unyama unaofanywa na Magaidi.

Wasalam

Tena wakikupata wewe, watasema unaongea kama kafiri wanakuchomoa kichwa fasta!! Inawezekana wewe ndie huujui Uislam na ulifundishwa nusu tu!!
 
Islamic States ndiyo waislam original,wewe mtoa post ni kafiri tu
mleta mada yuko sahihi na nikweli kabisaa hamna hata aya moja ktk qurani inayotaka watu wauane....na ukisoma vzr historia ya uislamu utagundua maswahaba wengi walikuwa wakiabudia miti na vitu vinginevyo sa lau kama mtume Angekuwa na msimamo kama wa isis wakuua kila asiyekuwa muislam je hao maswahaba Wangeingia vp ktk uislamu maana angewaua wotee!! dini ya uislamu inavyofahamika tofauti na ilivyo na mtu akitaka kuufaham uislam kwa elimu basi ni lzm akae chini asome mfano uislamu unazingatia haqi za jirani ambae si muislam tena haqi hizoo ametufundisha mtume sasa he lau kama mtume angekuwa muuaji kama Osama bin laden je hata hizo haqi za jirani asiye muislam angezifundisha? tafadhali ndugu zetu ktk utu na ubinadamu acheni dhana potofu dhidi ya uislamu!! uislamu haukubaliani kabisa na vitendo vya kigaidi
 
Tena wakikupata wewe, watasema unaongea kama kafiri wanakuchomoa kichwa fasta!! Inawezekana wewe ndie huujui Uislam na ulifundishwa nusu tu!!
mm nishawasema sana kweny mimbali msikitini ...mm ni sunni na nimesoma dini tofauti na wao wanaobeba misimamo bila ya elimu!!
 
Back
Top Bottom