Tarakilishi
JF-Expert Member
- May 19, 2013
- 2,180
- 2,453
Haha, mimi pia nilikuwa katika wajinga kama ww hapo zamani wa kusoma biblia kwa lengo la kukosoa. Nachukua kiaya kimoja tu nakifanyia analysis nafanya judgent bila kujali muktadha wa kilichokuwa kinazungumzwa. Nimefanya jitihada na kuisoma dini yangu vema hususani quran inazungumziaje dini za uyahudi na ukristo, sirudii tena ujinga wa kukejeli hovyo. Naona wakristo nao hawajasoma Quran na hata biblia yenyewe hawajasoma. Nina uhakika mtu akisoma Biblia kuanzia mwanzo mpaka mwisho hususani agano la kale hatakuja kuinua mdomo humu kusema ooh quran sijui nini maana MUNGU aliyepo kwenye agano la kale ndiye huyo aliyepo kwenye Quran atakaebisha hajui Biblia wala Quran haijui! Wakristo wengi hawajui Kitabu chao, lau wangekisoma kisha wakaisoma quran wangegundua kuwa quran Inasadikisha yaliyokuwepo kabla yake ambayo kimsingi utayapata kwenye Torati, zaburi na Injili kama zilivyotajwa katika quran.Zamani kabla sijaifaham vizur dini yangu nilikuwa na mtindo kama wako wa kupick zile aya/maandiko katika biblia ambayo nilikuwa nayaona kama hayaeweki kisha naanzisha mjadala bila kujua mwanzo wa maandiko hayo na sababu gani yapo. Bt alhamdulillah baad ya kuusoma uislam na kuuelewa nimefahamu kuwa hata hiyo tabia ya kukosoa na kutafuta kasoro katika imani za watu hairuhusiwi na Allah amekataza hivo. so najua one day hata wewe utakuna kuelewa kama kweli unataka kuelewa ila kama umeweka chuki moyoni basi kamwe hutoelewa jambo