Iringa: Ahukumiwa miaka 30 baada ya kushauriwa kumbaka dada yake wa kuzaliwa ili apate utajiri

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Huko Iringa Mahakama ya wilaya ya Kilolo imemhukumu Frank Kigomba miaka 30 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi laki 5 kwa kosa la kumbaka dada yake wa kuzaliwa kwa maelekezo ya mganga wa kienyeji ili awe tajiri.

Matukio ya kubaka, kuua na kutafta utajiri sasa yamehama kutoka kanda ya ziwa na kuhamia nyanda za juu kusini.

Kuna jamaa mwingine alimbaka mama yake kisha baba yake akaenda kumtolea dhamana na jamaa akatoweka hajulikani alipo hadi sasa.

---
Mkazi wa Kijiji cha Kising’a wilayani Kilolo, Frank Kigomba (31) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na kulipa fidia ya Tsh. 500,000 kwa kosa la kumbaka dada yake wa tumbo moja mwenye umri wa miaka 15.

Akizungumza na waandishi wa habari, Januari 23, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema tukio hilo la ubakaji lilitokea Januari 2, mwaka huu na kwamba tayari lilifikishwa mahakamani na hukumu imetolewa.

Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo alienda chumbani kwa ndugu yake na kumuita, akimtaka amsaidie kuingiza mbao ndani ya pagale la nyumba anayojenga na kisha akamkamata kwa nguvu na kumvua nguo, kabla ya kumuingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali.

“Uchunguzi ulibaini kuwa mtuhumiwa huyo alishauriwa na mganga wa kienyeji kuwa akifanya mapenzi na ndugu yake atapata utajiri, alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka lake na kukiri kosa; na kuhukumiwa kifungo hicho,” amesema.

Katika tukio lingine amesema Isaya Lucas (25), amehukumiwa miaka 30 jela baada ya mahakama kuthibitisha kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 katika tukio la Aprili 4, 2022.

Amesema matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto hasa ubakaji na ulawiti mkoani Iringa yameendelea kuwa changamoto kwa sababu mbalimbali zikiwemo imani za kishirikina, magonjwa ya afya ya akili pamoja ulevi wa kupindukia na kuiomba jamii kutoa ushirikiano kuyadhibiti.

Chanzo: Mwananchi
 
Niungefurahi sana kama wangebadilisha sheria waende mbali zaidi... na hao ''waganga'' nao wahukumiwe vifungo sawa na mkosaji.
 
Huko Iringa Mahakama ya wilaya ya Kilolo imemhukumu Frank Kigomba miaka 30 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi laki 5 kwa kosa la kumbaka dada yake wa kuzaliwa kwa maelekezo ya mganga wa kienyeji ili awe tajiri.

Matukio ya kubaka, kuua na kutafta utajiri sasa yamehama kutoka kanda ya ziwa na kuhamia nyanda za juu kusini.

Kuna jamaa mwingine alimbaka mama yake kisha baba yake akaenda kumtolea dhamana na jamaa akatoweka hajulikani alipo hadi sasa.

ACHA kufananisha Kanda ya ziwa na vitu vya ajabu mkuu, lake zone kwa mauaji ni no 1 Tanzania
 
Mbakaji yupo sahihi ili uupate utajiri lazima ufate maelekezo la sivyo utaishia kuusikia
Basi tu washamfunga ila bila hivyo alikuwa anaenda kuwa tajiri
Niwasihi vijana tujitahidi kufuata maelekezo tuwe matajiri
Umasikini ni laana ni shida,mateso ,manyanyaso ,,umasikini unakila aina ya shida ndani yake...
 
Mkazi wa Kijiji cha Kising’a wilayani Kilolo, Frank Kigomba (31) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na kulipa fidia ya Sh500,000 kwa kosa la kumbaka dada yake wa tumbo moja mwenye umri wa miaka 15

Akizungumza na waandishi wa habari, Januari 23, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema tukio hilo la ubakaji lilitokea Januari 2, mwaka huu na kwamba tayari lilifikishwa mahakamani na hukumu imetolewa.

Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo alienda chumbani kwa ndugu yake na kumuita, akimtaka amsaidie kuingiza mbao ndani ya pagale la nyumba anayojenga na kisha akamkamata kwa nguvu na kumvua nguo, kabla ya kumuingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali.

“Uchunguzi ulibaini kuwa mtuhumiwa huyo alishauriwa na mganga wa kienyeji kuwa akifanya mapenzi na ndugu yake atapata utajiri, alifikishwa mahakamani na kusomewa shitaka lake na kukiri kosa; na kuhukumiwa kifungo hicho,” amesema.

Katika tukio lingine amesema Isaya Lucas (25), amehukumiwa miaka 30 jela baada ya mahakama kuthibitisha kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 katika tukio la Aprili 4, 2022.

Amesema matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto hasa ubakaji na ulawiti mkoani Iringa yameendelea kuwa changamoto kwa sababu mbalimbali zikiwemo imani za kishirikina, magonjwa ya afya ya akili pamoja ulevi wa kupindukia na kuiomba jamii kutoa ushirikiano kuyadhibiti
 
Na mganga naye alitakiwa kufungwa,maana kesho atamshauri mtu mwingine,kama ataachiwa huru mtaani...
 
Back
Top Bottom