JOHN Chibuga (31), mkazi wa Kijiji cha Bugolola wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, ambaye Desemba 9, mwaka jana aliachiliwa kwa msamaha wa Rais, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Aidan Nziku, alidai kuwa Chibuga alimvamia Mdala Mangu (34), mkazi wa Ukerewe akiwa nyumbani kwake na kumkata kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kuiba simu ya mkononi na kukimbia.
Hukumu hiyo ilitolewa Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe, Lucas Nyahega, aliyesema kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani huko haukutia shaka, mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa kukusudia na hivyo mahakama inamhukumu kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka 30.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nziku akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 15, 2023 katika Kijiji cha Kakerege, wilayani Ukerewe.
Alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa la namna hiyo kwa mara ya pili ambapo awali alihukumiwa kwa kosa la kuvunja duka usiku na kuiba, hivyo kutiwa hatiani na Mahakama ya Mwanzo Nansio kisha kuachiliwa huru Desemba 9, 2023 kwa msamaha wa Rais.
Alidai kosa hilo la unyang'anyi wa kutumia silaha ni kinyume cha kifungu namba 287(A) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura 16 (2022), hivyo kuiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi yake ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea kutokana na kosa linalomkabili, aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hakuwa na fedha ya kujikimu baada ya kutoka gerezani, ndiyo sababu ya kupora.
Source - Nipashe