Unajua palipo na Ukweli uwongo hujitenga, Uwongo na Ukweli kamwe havifungamani.
zile rhehotoric zoote kumbe hamna kitu. jamaa walifikiri wairani ni wazembewazembe watu wa kuwapeleka peleka kumbe wapi, jamaa wako very smart katika hili game la diplomacy.
kiufupi nilikuwa nikifuatilia hii ishu kwa karibu sana ,kitu nilichojifunza ni kwamba kumbe diplomacy ni kama game flani ya chess au draft, unasukuma kete hii kisha unasubiri mwenzako asukume kete ile.
Kwa mfano ukiangalia toka Mwanzo Wairani walisukuma kete yao ya kwanza mwaka 2003 kwa kusimamisha kueinrich uranium.Wakatulia kimyaa huku Mmarekani akiendelea kuipata joto ya jiwe Irak.
Then akaingia raisi Ahmednejad madarakani, wakati huo wamarekani wako bussy kwelikweli Iraki.jamaa akasukuma kete nyingine akasema Irani ina haki ya kuendelea kueinrich uranium kwa ajili ya umeme kulingana na mkataba wa IAEA.
Western countries wakaja juu wakasema hawaiamini Irani, wakasukuma kete yao ya economic incentives kuivutia Iran iache kueinrich Uranium.Wairani wakasema hili haliwezekani kwa sababu huko mbeleni hakuna guarantee yoyote ya nchi za kimagharibi kubeba jukumu la kuipa Iran einriched Uranium kwa ajili ya mitambo yake ya kuzalishia umeme.
Wazungu wakasukuma kete ya vikwazo wakaitwanga Irani vikwazo mara ya kwanza. Wairani wakasukuma kete ya support kwa nchi zisizofungamana na upande wowote(non-aligned movement countries),nchi zikatoa matamko kwamba zinaunga mkono tekinolojia ya nyuklia kwa Matamizi ya Amani.wakati huohuo Irani ikasukuma kete ya diplomacy kwa adui wa marekani hugo Chavez,kukawa kuna alliance ya kuipinga marekani kwa sauti kubwa kwenye UN, (kumbuka hotuba ya chavez alivyomuita Bush shetani katika UN general assembly).
Then Wamarekani na wenzi wao wakakusanya nguvu wakacheza kete yao nyingine hatari sana, wakawatwanga wairani vikwazo kwa mara ya pili. kuona hivi wairani wakaona hali ngumu ikawabidi wajipange kisawasawa ili kukontrol gemu, wairani wakasema tutasolve ishu yetu Na IAEA,jamaa wakacheza kete yao nyingine, wakafanikiwa kuwaconvice IAEA kwamba hawana mradi wa Mabomu ya Nyuklia. IAEA wakatangaza wakasema hatujaona dalili za mabomu ya Nyuklia Iran.
Hii iliwaudhi wakubwa, wakawa sasa wanatapata ili kupata credibility ya kuwatwanga Wairani vikwazo kwa mara ya tatu.
sasa this Time uroho wa Wamarekani wa kutawala dunia ukaingilia kati gemu nzima, wakakwaruzana na Urusi kuhusu mpango wa kuweka Anti ballistic missile Polland. warusi wakaja juu wakasema hii ni kujaribu kupunguza nguvu (detterance) za ballistic missile za warusi na mabomu yao ya Nyuklia, Warusi wakaanza kuqustion ajenda ya Wamarekani.
Wairani wakacheza kete yao nyingine, this time ukaandaliwa mkutano wa caspian sea nation, wakamwalika Putin kwenda Tehran, jamaa akaenda wakakubaliana kwamba mataifa yenye kushirikiana caspian sea wasiruhusu ardhi yao kutumika na taifa lingine kumpiga mmoja wao, Hii ikawa ni kete ngumu kwa Wamarekani na wenzi wao;
Then hatujakaa sawa Wamarekani Wakamuita Dalai Lama aliye ukimbizini(kiongozi wa kiroho wa jimbo la tibet -uchina) Congress wakampa nishani ya juu ya heshima, hii kitendo iliwaudhi Wachina vibaya mno, wakaanza kususia hata mikutano ya kuiwekea vikwazo Irani.
Then sasa mafuta yakaanza kupanda bei kwa kasi ya ajabu,pipa moja likafikia hadi dola 99, hii ikawa ni situation ngumu.maana kila Marekani akitishia hali ya shari kwa irani pipa la mafuta linaongezeka bei,
Sasa naona wamarekani wamegundua kwamba hili gemu walilomchezea saddam husein limekuwa taffu kwa Wairani,wameamua sasa kuweka wazi mambo ambayo mimi naamini wanayafahamu fika ila ujeuri tu.
wanatafuta namna ya kusave face.
ila sasa nadhani wameelewa kwamba uwongo hata uupake mafuta namna gani utabaki kuwa uwongo tu