Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 265
- 241
Prof. Kitila Mkumbo kwa Mwaka 2025 nina uhakika hana lake Jimbo la Ubungo.
Mwaka 2020 aliingizwa kibabe na hangeshinda. Dr. Dorothy Gwajima - Mnyiramba wa Tarafa ya Shelui naye anaonesha kunogewa na siasa - hakika atagombea Jimbo la Iramba. Dr. Mwigulu Nchemba (Mamba Kinani) ameendelea kujiamini na kujijenga katika siasa za Kitaifa kwa sababu Jimboni hana tena mpinzani.
Wabunge wa kweli Iramba hawataki siasa wapo kimya - sio kuwa wana hofu lakini pia wamevaa utashi wa dhati ya mioyo yao. Hawataki mgawanyiko.
Sasa hawa wabunge ambao wote ni Mawaziri kuna maendeleo yeyote wanaweza kujivunia kuiletea Iramba? Prof. atasema ooooohhhh yeye ni wa Ubungo lakini tunajua moyo wake upo Iramba ila kiwiliwili ndiyo kipo Ubungo. Hakika imeshapita miezi saba sasa tangu hawa watu waingine uongozini lakini hamna chochote ambacho angalau kinaonesha nia njema waliyonayo kwa Iramba.
Dkt Mwigulu anataka ifike 2023 ndiyo aanza kuchacharika kuwahadaa wananchi. Prof. Kitila vipi mbona wakati hujawa Waziri Jimbo la Iramba ndiyo ilikuwa mahali pako pa kutalii?
Imekuwaje tangu upate ubunge wa kupachikwa na Mwendazake Ubungo na Uwaziri huo huku Iramba umepashit kabisa! Tukueleweje? Au ndiyo ulitaka tu kututumia kama ngazi? Hauna tofauti na Dkt Mwigulu!
Dr. Dorothy Gwajima nina uhakika ukipunguza mbwembwe kidogo tu 2025 unachukua hili Jimbo. Ninakufahamu vizuri na wewe ninajua unanifahamu vema ukisoma tu hapa utajua ni nani kaandika. Njoo mwka 2025 Iramba inakuhitaji - ili ufanikiwe anza mapema - kama ambavyo uliibadili Hospitali ya Wilaya yetu ikawa ya viwango wakati upo kama incharge hapa nina uhakika wewe una cha kujivunia Iramba kuliko hata Dkt. Mwigulu. Anza sasa - weka mipango murua na ufanyie kazi ili Jimbo hili liwe lako mwaka 2025 tuachane na hao wenzio wenye ndoto za URais kila kukicha.
Ninawashauri wote - kama mtaendelea kuwa kimya bila kuiongelea Iramba hakika mkianza mwaka 2023 tutajua fika mnaanza kujipendekeza ili mkubalike 2025. Sisi tunataka muanze sasa, mgombane sasa kwa kuoneana wivu huyu kaahidi hiki, yule kaahidi kile, huyu kaleta kile, yule kawaleta wadau wa maendeleo wale.
Anzeni kugombania nafasi mapema ili jimbo letu lichangamke! Acheni kuogopana nyie Wanyiramba!