Iramba ni nyumbani kwa Mawaziri watatu lakini inazidi kudorora!

Mkuu umechemsha zile ni nyumba za miti na siyo tembe(miti na nyasi), kwa hiyo hali ya maisha ya Singida na Manyara, Arusha na Kilimanjaro zinalingana mkuu?
Ni miti manyazi na udongo SIO CEMENT. Wewe unaziona kwa barabarani mimi nimeingia ndani ayake hadi na kulala.
 
Dr Dorothy Gwajima hana mpango wa kugombea na hamtakaa kumuona akija kugombea huko. So kuwa na amani
 
Du. Tatizo mie darasa la saba na hao wote ni Maprof sijui nitawshindaje?
Sifa ya kuwa Mbunge ni kujuwa kusoma na kuandika. Musukuma na Lusinde (Kibajaji) ni darasa la saba. Jah People yule wa Makambako ni darasa la nne. Kwahiyo hakuna cha kujitetea hapo.
 
hajaonja ladha ya nyama pori! Ilikuwa Ndalichako na Mpango itakuwa Gwajima?
Unamfahamu Dr Dorothy Gwajima? Hicho chuma achana nacho wewe.Huyo mama ni 100% mtendaji siyo Mwanasiasa. Wala msiumize kichwa kuhusu yeye. Muda wake ukimalizika hataenda huko Iramba kugombea Ubunge.
Mark my words
 
Atakuwa Katibu Mkuu Kiongozi ama?
 
Prof. Kitila Mkumbo kwa Mwaka 2025 nina uhakika hana lake Jimbo la Ubungo.

Mwaka 2020 aliingizwa kibabe na hangeshinda. Dr. Dorothy Gwajima - Mnyiramba wa Tarafa ya Shelui naye anaonesha kunogewa na siasa - hakika atagombea Jimbo la Iramba. Dr. Mwigulu Nchemba (Mamba Kinani) ameendelea kujiamini na kujijenga katika siasa za Kitaifa kwa sababu Jimboni hana tena mpinzani.

Wabunge wa kweli Iramba hawataki siasa wapo kimya - sio kuwa wana hofu lakini pia wamevaa utashi wa dhati ya mioyo yao. Hawataki mgawanyiko.

Sasa hawa wabunge ambao wote ni Mawaziri kuna maendeleo yeyote wanaweza kujivunia kuiletea Iramba? Prof. atasema ooooohhhh yeye ni wa Ubungo lakini tunajua moyo wake upo Iramba ila kiwiliwili ndiyo kipo Ubungo. Hakika imeshapita miezi saba sasa tangu hawa watu waingine uongozini lakini hamna chochote ambacho angalau kinaonesha nia njema waliyonayo kwa Iramba.

Dkt Mwigulu anataka ifike 2023 ndiyo aanza kuchacharika kuwahadaa wananchi. Prof. Kitila vipi mbona wakati hujawa Waziri Jimbo la Iramba ndiyo ilikuwa mahali pako pa kutalii?

Imekuwaje tangu upate ubunge wa kupachikwa na Mwendazake Ubungo na Uwaziri huo huku Iramba umepashit kabisa! Tukueleweje? Au ndiyo ulitaka tu kututumia kama ngazi? Hauna tofauti na Dkt Mwigulu!

Dr. Dorothy Gwajima nina uhakika ukipunguza mbwembwe kidogo tu 2025 unachukua hili Jimbo. Ninakufahamu vizuri na wewe ninajua unanifahamu vema ukisoma tu hapa utajua ni nani kaandika. Njoo mwka 2025 Iramba inakuhitaji - ili ufanikiwe anza mapema - kama ambavyo uliibadili Hospitali ya Wilaya yetu ikawa ya viwango wakati upo kama incharge hapa nina uhakika wewe una cha kujivunia Iramba kuliko hata Dkt. Mwigulu. Anza sasa - weka mipango murua na ufanyie kazi ili Jimbo hili liwe lako mwaka 2025 tuachane na hao wenzio wenye ndoto za URais kila kukicha.

Ninawashauri wote - kama mtaendelea kuwa kimya bila kuiongelea Iramba hakika mkianza mwaka 2023 tutajua fika mnaanza kujipendekeza ili mkubalike 2025. Sisi tunataka muanze sasa, mgombane sasa kwa kuoneana wivu huyu kaahidi hiki, yule kaahidi kile, huyu kaleta kile, yule kawaleta wadau wa maendeleo wale.

Anzeni kugombania nafasi mapema ili jimbo letu lichangamke! Acheni kuogopana nyie Wanyiramba!
Mkuu hapo pa Mamba Kinani ndio nani au ni mambo ya kurudia shule?
 
Aliyekuambia Waziri,au Mbunge analeta maendeleo jimboni,alikudanganya,
Waziri yoyote hawezi kujiamulia kwamba Mimi kijiji Changu lazima nipeleke umeme,zahanati,shule,Waalimu,balabala,hivi vitu ni sera,vinaamuliwa na baraza la mawaziri,na watendaji wa wizarani kwa kuangalia vipaumbele,na kugawa kila sehemu ya nchi ipate,Arusha,na Moshi hazikuendelea kwa vile mawaziri na wabunge wenye hasiri ya huko,"walipereka"maendeleo,wao wabunge na mawaziri hawakupereka Mali,walionyesha njia,vision na kutoa uongozi,wakawaweka wananchi pamoja,shule zikajengwa,kwa nguvu ya wananchi na wafadhili,biashara zikaanzishwa,wafanyabiashara wakapata usaidizi wa karibu kutoka kwa viongozi,na mambo yakatokea,
Mbeya,Kagera walifanya hivi pia.
Mkitegemea Hao viongozi wenu watakuja kujenga zahanati na shule,na huduma za maji kwa pesa yao ya mifukoni mtasubili mpaka Yesu Arudi
 
Umeathirika na "la" badala yake unaweka "ra"
 
Ilikuwa Chato, sasa naona Iramba inataka kushika usukani. Sisi wa Mamsera tutaendelea kumlilia Mungu atufanyie wepesi.

Wanataka Mwigulu aipendelee Iramba kwa kiwango kikubwa wapate cha kuongea kama walivyoisakama Chato na Raisi JPM
 
Hawa Ndio kwanza wamepewa vyeo na ni lazima bosi wao wamridhishe ili wawe sehemu ya anaowaamini.

Sidhani kama kwa sasa wanawazia majimbo, wana ilani ya kurasa 303 inawategemea wao. Huyo Mkumbo ndio mtafsiri halisi wa Tanzania ya viwanda.

Gwajima anapigwa vijembe kwamba haiwezi wizara akili yake ipo kazini. Mwigulu anajikita katika kuununua upendo wa Mzee JK na Rais sidhani kama anawazia jimbo kwa sasa.

Mwigulu ananunue upendo kwa Jk ? Unamjua vizuri Mwigulu na JK ni kama Ridhwani kikwete na JK , Mwigulu ni mtiifu kwa viongozi wake na jamii kwa ujumla

natamani mngeweza Kumfahamu Mwigulu nje ya siasa ni binadamu na nusu na kwanza ndio Waziri anaengoza kwa kupendwa na wabunge wenzie na System kwa sababu hanyanyui mabega na ni mwenye msaada kwa wenzie
 
Asante kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom