Interview ya MKUTA ni moja ya interview mbovu niliyowahi kuhudhuria katika maisha yangu

Nyamalapa

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
206
448
Mwitikio wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukimwi Tanzania (MKUTA)


Hawa jamaa niseme tu kwamba hawapo serious au hawajui nini wanatakiwa kufanya

Kama mwezi umepita walitangaza nafasi moja ya kazi wakanialika interview kupitia Zoom Meeting, chakushangaza kuna rafiki yangu mmoja nae aliniambia amealikwa nao tena muda uleule ambao nimealikwa mimi.Hiki kitu kilinishangaza sana lakini nikasema anyway ngoja nione wamejipangaje.

Siku ya usaili ikafika nikaingia kwenye meeting kupitia link waliyonitumia daaah aiseeee kuingia tu baada ya dakika 15 kabla ya usaili kuanza nilichoka na kuchoka na ilibaki kidogo tu nijitoe kwenye ile meeting lakini nikasema anyway ngoja nifanye tu.

Tulikua watu si chini ya 10 na nafasi ni moja tu halafu kibaya zaidi wakati mwezio anajielezea wote mnamsikia wakati anajieza

Sasa just imagine wewe ndo mtu wa mwisho kuhojiwa je ni bundle kiasi gani unapoteza pasipo sababu za msingi, kweli mnanipotezea bundle langu kwa kusikiliza majibu ya mwenzangu ambayo hayanihusu ???

Mlikua na uwezo wa kumpangia kila candidate muda wake maalum wa kumuhoji

Kitu kingine ambacho kilinishangaza eti baada ya kuhojiwa oral interview palepale tukatakiwa kufanya na written interview kwa kujibu maswali kisha kuwatumia palepale huku wakituona na walikua hawataki tufanye offline, yani walikua wanataka tufanye huku wanatuona wote daaaah huu upuuzi wa kiwango cha lami kabisa....Si bora wangetualika tu kwenye darasa moja tukafanya written kisha ndo ije ifuate oral siku nyingine kwa watakaofaulu written.

Kama wataona huu uzi wangu nadhani watajirekebisha mana wana lack professionalism kwa kiasi kikubwa sana.

Jifunzeni hata kwa wenzenu basi jinsi wanavyoendesha saili zao

Am done.
 
Mtaka cha uvunguni sharti ainame. Ila kama mnaenda kudeal na wagonjwa si ndio itakuwa balaa. Vumilia Tu pengine ni usumbufu mdogo2. Zipo taasisi nyingi zinajiamuliq tu mambo yao hovyohovyo
 
Ukifika sasa zile za utumishi ata candidate hamruhisiwi kuzungumza wakati mkisubiri kuingia kufanyia interview. Ni vitu za hovyo sana
 
Mm sio mtabiri ila mtoa post unaonekana haujawa shortlisted..pole kwa kupoteza time kwa ajira za mchongo
 
Ulichosema ni kweli mkuu, nami nilikuwa mmoja wapo utaratibu wao haukuwa mzuri kwa kweli. Unatumia bando zaidi huku unasikiliza wengne ambao hakukuwa na ulazima wa kuwasikiliza.
Bora na wewe uliliona hili
 
Back
Top Bottom