Nilijiona ninapitia magumu kumbe kuna watu ni hustlers zaidi yangu

Spartacus boy

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
1,574
3,133
Habari za Jumapili wanajukwaa,

Maisha hayajawahi kuwa mepesi na hayatakuja kuwa mepesi. Ugumu wa maisha ninaamini ulianza punde tu mara baada ya wale watu wawili kula tunda pale bustanini. Kilichofuata baada ya hapo kila mtu anajua.

Baada ya kumaliza elimu ya chuo nikarudi home kujipanga upya. Niliweka plan zangu za kujiari kupitia saving za boom na plan nyngne za kutafuta mtaji nikiwa kitaa. Mambo hayakwenda sawa kama nilivyodhania.

Anuani ya makazi walinipiga chini, sensa nayo niliangukia kidevu kwenye sakafu.

Life likawa gumu lakini uhakika wa kula ulikuwepo maana wazazi wangu hawakuwa na noma kwani me licha ya kuwa nmerudisha mpira kwao lakini nilikuwa najiongeza Kwa deiwaka mtaani ,kuchoma mkaa ,kufua nguo za watu nk.

October basi mwaka jana ikatokea nafasi za kazi kwenye kampuni moja huku kwetu. Niliapply vizuri tu bila hata kwenda stationery ( vijana tujiongeze kutumia simu zetu vizuri) . Baada ya kama siku tano hivi baada ya kutuma maombi nikapigiwa simu ya kwenda kwenye interview.

Umbali wa Toka home hadi hapo ni kama km 20 hivi (haipungui). Nikicheki sina nauli nina sh. 1500/= tu yaani buku jero. Na toka mchakato unaanza sijawahi muambia mtu maana nilishajifunza baada ya kufeli mara kadhaa kwani nilikuwa nawaambia watu kila kitu kunihusu. Hapa hata mama sikumuambia kabisa. Nilimdanganya kuwa kuna mahali naenda. Anaulizia ni wapi me nikawa namjibu ya kuwa nitakuambi.

Sasa changamoto ni nauli. Basi nikapanga ya kuwa hapa ni kutembea tu ya mguu ila itabidi nisafiri siku moja kabla ya siku ya usaili.

Nikadamka saa kumi usiku huyo lengo ni kuwa asbh niwe nimefikia kwa ndugu yangu anayekaa karibu na hiyo kampuni anipe hifadhi( naye nilimdanganya nakuja kufanya nn ila nikamuambia kuna mishe nafuatilia)

So mama alishangaa niko serious bhn.. nimeamka saa kumi najiandaa nipo sebuleni natoa simu kwenye chaji akaamka akanipa elfu mbili jumla nikawa na elfu tatu na mia tano. Lakini ikawa haitoshi nauli kabisa.

Wazee Kijijini kwetu ni misitu minene balaa mpaka unafika na inatisha ila niliamua kusafiri muda wa usiku ili nisionewe huruma na mtu. Nikifka salama saa tatu asbh . Buku mbili nikanunulia bundle nikazama humu jf jukwaa la ajira kule nikakutana na uzi mmoja unazungumzia maswali ambayo ni huyokea mara kwa mara kwenye interview.

JF ibarikiwe sana maana kila nilichokisoma mule basi nikakutana nacho vilevile. Majibu mengine nilijibu kutokana na uelewa wangu. Nikatoka kwenye interview nikijisemea ya kuwa hapa nimeua. Nikarudi home Kijijini kuendelea na issue nyingine nikisubiri week mbili nilizopewa kama kuna majibu ya kuitwa kazini .
 
Basi nikazidi kukaza hizo week mbili nimalizie kulima shamba langu ( licha ya kuwa jobless lakini nilikuwa ninelima shamba la mahindi ili nisiwe idle tu).

Pia nikafanya kibarua ambachi nilipata 13,000/=
Akili yangu ilikuwa inanituma ya kuwa hiyo hela ndo nauki ya kuendea kazini ,safari hii hautembei kwa miguu tena ( wakuu Kuna faida ya kujinenea mambo mema)
Week ya kwanza ikapita, week ya pili ikaanza; jumatatu jumanne, jumatano ,alhamis tu hakuna cha simu wala nini ila nikazidi jipa imani ya kuwa nitapigiwa kesho simu ya kuitwa .

Kesho yake nilipata kibarua cha siku cha kupiga ngano malipo ni elfu saba. Basi kwa kuwa huwa sichagui kazi nikaenda. Piga ngano balaa. Mida ya saa jmi hivi jioni nikaona napigiwa simu na namba ngeni.

Hr:haloo za jioni
Mimi: salama kabisa. (Huku moyo unapiga kite)
Hr: Tunaongea na mtu fulani (ambaye ni mimi)
Mimi: ndiyo ndio mimi kabisa
Hr: Anhaa ulifanya interview katika kampuni xxxx
Mimi: Ndiyo
Hr: hongera,umechaguliwa katika nafasi uliyoomba na unatakiwa kufika kazini kwa ajili ya semina Jumatatu ijayo
Mimi: (Huku nikiongea jwa utulivu) Samahani nina swali
Hr: uliza
Mimi: Je ,ninavyokuja nije na vitu vipi?
Hr: Njoo na kadi ya bank,kitambulisho cha NSSF Namba ya NIDA.
Mimi: Ahsante!

Wakuu nilifurahi balaa. Jumatatu nikawasili kazini na Mambo mengine yako powa mpaka leo..
 
Habari za jumapili wanajukwaa,

Maisha hayajawahi kuwa mepesi na hayatakuja kuwa mepesi.Ugumu wa maisha ninaamini ulianza punde tu mara baada ya wale watu wawili kula tunda pale bustanini. Kilichofuata baada ya hapo kila mtu anajua.

Baada ya kumaliza elimu ya chuo nikarudi home kujipanga upya . Niliweka plan zangu za kujiari kupitia saving za boom na plan nyngne za kutafuta mtaji nikiwa kitaa. Mambo hayakwenda sawa kama nilivyodhania.

Anuani ya makazi walinipiga chini, sensa nayo niliangukia kidevu kwenye sakafu.

Life likawa gumu lakini uhakika wa kula ulikuwepo maana wazazi wangu hawakuwa na noma kwani me licha ya kuwa nmerudisha mpira kwao lakini nilikuwa najiongeza Kwa deiwaka mtaani ,kuchoma mkaa ,kufua nguo za watu nk.

October basi mwaka jana ikatokea nafasi za kazi kwenye kampuni moja huku kwetu. Niliapply vizuri tu bila hata kwenda stationery ( vijana tujiongeze kutumia simu zetu vizuri) . Baada ya kama siku tano hivi baada ya kutuma maombi nikapigiwa simu ya kwenda kwenye interview.

Umbali wa Toka home hadi hapo ni kama km 20 hv (haipungui). Nikicheki sina nauli nina sh. 1500/= tu yaani buku jero . Na toka mchakato unaanza sijawahi muambia mtu maana nilishajifunza baada ya kufeli mara kadhaa kwani nilikuwa nawaambia watu kila kitu kunihusu. Hapa hata mama sikumuambia kabisa. Nilimdanganya kuwa kuna mahali naenda. Anaulizia ni wapi me nikawa namjibu ya kuwa nitakuambi.

Sasa changamoto ni nauli . Basi nikapanga ya kuwa hapa ni kutembea tu ya mguu ila itabidi nisafiri siku moja kabla ya siku ya usaili.

Nikadamka saa kumi usiku huyo lengo ni kuwa asbh niwe nimefikia kwa ndugu yangu anayekaa karibu na hiyo kampuni anipe hifadhi( naye nilimdanganya nakuja kufanya nn ila nikamuambia kuna mishe nafuatilia)

So mama alishangaa niko serious bhn.. nimeamka saa kumi najiandaa nipo sebuleni natoa simu kwenye chaji akaamka akanipa elfu mbili jumla nikawa na elfu tatu na mia tano. Lakini ikawa haitoshi nauli kabisa.

Wazee Kijijini kwetu ni misitu minene balaa mpaka unafika na inatisha ila niliamua kusafiri muda wa usiku ili nisionewe huruma na mtu. Nikifka salama saa tatu asbh . Buku mbili nikanunulia bundle nikazama humu jf jukwaa la ajira kule nikakutana na uzi mmoja unazungumzia maswali ambayo ni huyokea mara kwa mara kwenye interview.

Jf ibarikiwe sana maana kila nilichokisoma mule basi nikakutana nacho vilevile. Majibu mengine nilijibu kutokana na uelewa wangu. Nikatoka kwenye interview nikijisemea ya kuwa hapa nimeua. Nikarudi home Kijijini kuendelea na issue nyingine nikisubiri week mbili nilizopewa kama kuna majibu ya kuitwa kazini .
Hapo bado DP World haijachukua nchi... subiri utaona mengi!
 
Sasa kisa kilichobeba heading ya huu uzi ni kuwa nilivowasili kazini nikakukatana na home boy wangu fulani hivi ambaye story yake ilinigusa balaa mpaka nikajiona mimi ni mtoto balaa.

Ni hivi jamaa alituma maombi kama tulivyofanya sisi wote. Lakini wakati sisi tunaitwa kwenye interview jamaa hakupata simu kabisa. Sasa akawa anazidi sikia fununua ya kuwa watu wanapigishwa interview week mbili zote ila yeye ndo hivyo.

Sasa ilifika siku ya mwisho kabisa ya kufanya interview jamaa si ana taarfa zote akaona usinitanie..

Akaamua na yeye aje Hivyo hivyo kwenye interview hata kama hajaitwa. Na akicheki ni saa nane mchana. Akakodi pikipiki ya mtu ili awahi kbla muda haujaenda.

Paap huyo lakini njiani akapata ajali mbaya ya pikipiki. Tairi la mbele lilikatika yale mapanga ya rimu .
Jamaa akijicheki kaumia kidogo basi akawekeza pikipiki kwa mtu huyo akafika ofisini kachafuka balaa.

Tena kakuta watu washakula basi cha kwanza akaandika jina kale kwenye karatasi ya mahudhurio ya watakaopigishwa interview.

Wafanya usaili wakamshangaa wewe vipi hapa mbona hivyo na kwenye list yetu haupo?
Akawajibu ya kuwa kiukweli mimi niliomba lakini sijaitwa kwenye interview ila najaribu bahati yangu.
Basi wakasema sawa . Jamaa ikafika zamu yake akashuka nondo mpka wakashangaa wakamuuliza hivi haya unayoyaongea unayajua au umemeza.?

Jamaa kwa wenge akajibu me nimeyameza tu.
Basi akamaliza interview akaendelea kusubiri.

Guess what!! Jamaa akapapigiwa simu na kazi akapata kama sisi.
 
😍❤️
 
So si kisa kirefu sana ila jamaa alinifunza kitu sana.

Akazidi niambia ya kuwa hivi angeacha usaili upite afu asijilizimishe kuja basi angeumia siku zote ila baada tu ya kupiga usaili kwa kuforce basi roho yake ikawa nyeupe na hata kama ni angekosa basi asingeumia hata kidogo.
Jamaa tuko naye kazini na yuko humble balaa. Anapiga kazi
Afu uzuri zaidi ni kuwa ana manzi ake yuko naye toka kitambo. Kuna kipindi alijiari mambo yakaenda powa baadae hali ikawa mbaya zaidi. Lakini mwanamke bado akawa naye. Akarudisha mpira home lakini mwanamke bado yuko na yeye. Hadi sasa hivi mwanamke bado yuko na yeye.

*********
Vijana tuzidi pambana na tuzidi shikana mikono. Tujiongeze kufanya vitu tofauti tofauti na kujenga imani thabiti toka kwa watu na jamii.Mimi mwenyewe kupata tangazo la kazi ni kuwa kuna rafiki angu wa shida na raha ndio alinisanua na kunipa tangazo lake. Huyu ni zaidi ya ndugu kwangu. Na yeye alipata mchongo mzuri zaidi yangu ila sehemu nyingine.

Tuzidi kufanya vitu sahihi no matter what !
Vikwazo vipo na vitazidi kuwepo ila tukiwa vizuri basi itakuwa kama mkate mgumu mbele ya chai.

Huyu mwamba namkubali sana kwani nilijiona mimi ndo nateseka kumbe kuna wengine afadhali ya mimi

MWISHO.
 
Back
Top Bottom