Viongozi wa Chadema walilazimisha maandamano yafanyike licha ya kuombwa na Mkuu wa Polisi Tanzania kuwa yasifanyike kwa sababu tu:
Walikuwa na nia ya kuwatisha wawekezaji wakubwa duniani ambao wapo Tanzania, huko huko Arusha kwa sasa.
Wawekezaji hao, wakiongozwa na Dhirubhai Ambani walikuwa Tanzania kwa nia ya mapumziko na biashara na kutazama mandhari ya Tanzania na uwezekano mkubwa wa kuwekeza Tanzania.
Kwa roho mbaya tu na kwa nia isiyoyatakia mema Tanzania, viongozi wa Chadema wakahakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa lazima na hata yangeruhusiwa na polisi basi fujo lazima zingetokea ili kuwatisha hao wawekezaji waone kuwa Tanzania si pa kuwekeza.
Yote hiyo, ni kwa sababu tu, ya chuki zao binafsi walizozijenga baada ya kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita.
Hakuna mantiki yoyote kwa wana siasa walio mahiri kulazimisha maandamano yafanyike wakati kuna wageni, tena wawekezaji muhimu ambao hakuna nchi katika hii dunia yetu ya sasa isiotaka wawepo au watembelee kwao.
Viongozi wa Chgadema kwa ajili tu ya chuki zao binafsi, wakaona hii ndio fursa ya kuipakaza matope (kama si m*v*) Tanzania. Walijuwa kuwa wawekezaji wakubwa kama hawa wanapokuja tena kwa idadi kubwa kama iliowasili hapa, lazima kuna waandishi wa habari wa kimataifa hususan wa mambo ya kibiashara na pia kuna watu wa intelijensia za kibiashara ambao misafara kama hiyo huwa hawakosekani.
Kwa namna ya maisha tunayoishi wa Tanzania au kwa mpenda amani yoyote, hata kama mna ugomvi wenu wa ndani, ajapo mgeni, tena ambae anaweza kuleta manufaa nyumbani kwenu, huwa mnasitisha ugomvi kwa siku mbili tatu mpaka mgeni aondoke. Haya hutokea hata majumbani mwetu, tukipapurana na bahati nzuri au mbaya mgeni akibisha hodi basi mara nyingi kwa wenye akili husitisha kupapurana kwao, wakamhudumia mgenina ikibidi kupapurana, wataendelea mgeni akisha ondoka.
Leo Chadema wameonyesha sura gani ya nchi yetu, kwa kulazimisha maandamano yaliyositishwa na Mkuu wa Polisi, mbele ya hawa wageni?
Nna uhakika, sura walioionyesha si nzuri, lakini, ni matumaini yangu kuwa wenyeji, waliowaalika hawa wageni, wataweza kuwafahamisha ukweli ulivyo na wataridhia si tu kuja tena kutembelea Tanzania, bali na kuwekeza kwa wingi, kwani kwa sasa bado tunahitaji mitaji ya nje.
Nawaomba wa Tanzania walaani kitendo cha viongozi wa Chadema baada ya kuuelewa huu ukweli wa kwanini hawa viongozi walilazimisha maandamano yafanyike.
Mungu awalaze popote apendapo Marehemu waliofarik.