Intelijensia Kuhusu Maandamano ya CHADEMA

Intelijensia Kuhusu Maandamano ya CHADEMA

Mgeni wageni wafanyibiashara wawekezaji ni nini hii? hivi unaweza ukamtegemea jirani kuendeleza familia yako huu ni wazimu hapo ndipo unadhihirisha hadharani jinsi ulivyo na akili finyu tegemezi Wakaribishe basi kwa mkeo hao wageni wawekeze ili usiaibike
Kipindi cha jky tulisoma tulitibiwa na misingi endelevu ya maendeleo aliiweka! Hatukuwa Na mgeni wala mwekezaji Hakika umelogwa na aliye kuloga kafa JITAMBUE!
 
'Kwa roho mbaya tu na kwa nia isiyoyatakia mema Tanzania, viongozi wa Chadema wakahakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa lazima na hata yangeruhusiwa na polisi basi fujo lazima zingetokea ili kuwatisha hao wawekezaji waone kuwa Tanzania si pa kuwekeza.' Polisi wamepewa mamlaka ya "Kuruhusu au kutoruhusu' maandamano na katiba ipi? Polisi wako juu ya katiba ya nchi hii wanatoapa kuilinda? Polisi walihitimu lini na wapi kozi ya unajimu kwamba "hata yangeruhusiwa (Maandaamano) na polisi basi fujo lazima zingetokea" Ukweli unabaki palepale kwamba haki ya kuandamana inayotolewa na katiba kamwe haiwezi kumilikishwa kwa kikundi kidogo cha wahalifu waliovishwa sare mnaowaita polisi. Andengenye ni mpumbavu asiyejua kusoma alama za nyakati. Amejikomba serikalini mpaka inaboa. Na ukichunguza vema watu watatu wanapaswa kuwajibika kwa yaliyotokea Arusha nao ni Waziri wa mambo ya Ndani, IGP aliyekurupuka kama mtu aliyetoka usingizini kuzuia maandamano na RPC Andengenye ambaye nina mashaka na uwezo wake wa kufanya maamuzi. Maana maamuzi aliyoyafanya Arusha kwa zaidi ya mara moja yamewachonganisha na kuhatarisha usalama wa maaskari wake na wananchi kwa jumla. Naona Katiba mpya itabidi iliangalie hili ili Marais wajao wasiendelee kutuchagulia wehu kuongoza asasi nyeti. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hizo ndio sababu ambazo hazipingiki, kulikuwa kuna umuhimu gani wa kufanya maandamano wakati kuna wageni? tena ni wawekezaji muhimu? kama si kuwatisha?

Mhh kaka wewe ni Mtanzania, Mbona mawazo yako hayako kizalendo???????????
 
mi si mtetezi wa hao mafisadi maana nipo tofauti nao sana kwa jinsi uamuzi wa mwema na hao mafisadi wengine mimi naunga mkono maandamano ya chadema coz wanaonesha uzalendo mkubwa kwetu sisi watantania,na hoa waliokufa huko Arusha ni wazalendo tena lazima wakumbukwe na hao majerui Mungu awaponye haraka ameni.:A S 100:😛layball::A S-danger::lol::biggrin::scared:
 
Hizo ndio sababu ambazo hazipingiki, kulikuwa kuna umuhimu gani wa kufanya maandamano wakati kuna wageni? tena ni wawekezaji muhimu? kama si kuwatisha?

Wawekezaji gani wakati wananchi wanaendelea kufa kwa umasikini. Tunaposema nchi hii inaongozwa kwa kufuata sheria za nchi zingine huoni. you have to think more and more, ila kwako wewe unanufaika na mfumo ndo maana unaona njia zote zinazotumiwa na Chadema ni feki.

Mkuu Zomba, Uliza wangapi wananufaika na hii system kama si wewe na wachache mnaosahau kuwa kuna binadamu wengine kama wewe ambao wanahitaji elimu, maji, barabara au hata kiongozi wa kuwaonyesha njia tu inatosha.
 
:mad2:
Mkuu wa polisi nchini Said Mwema kusitisha ghafla maandamano ya Chama Cha Chadema huko mjini Arusha ambayo yalishapata kibali kutoka kwa Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha ni dhahiri kuna mkubwa fulani aliyeshinikiza na leo anainamisha kichwa chini kwa kuona matokea ya kutumia zaidi nguvu ya dola kukandamiza haki za wananchi badala ya kutumia utaratibu wa utashi wa mazungumzo ya pande zote mbili kwa amani kama walivyoomba chadema hapo awali au kuyaacha maandamano na mkutano uishe kwa amani.

Mfalme Suleman wa taifa la Waisrael alipoambiwa aombe kitu cho chote kwa Mungu katika utawala wake, yeye aliomba Mungu amjalie kipaji cha hekima na burasa. Aliomba kitu ambacho kwa wengi wa watawala wetu wa leo ni kitu adimu kukifikiria Mungu awajalie. Kwa hakika alichagua fungu lililo bora na adimu sana. Wengi wetu wanaomba usiku na mchana Mungu awajali kupata utajiri na heshima na kutawala bila mipaka. Lakini Mfalme Suleman anaheshimika katika historia ya wafalme wengi kwamba ni mmoja aliyejaliwa hekima na busara sana katika utawala wake licha ya udhaifu wake aliokuwa nao. Naam busara na hekima ndio sifa njema ya kiongozi bora, na yuko makini kufikiria athari zake kabla hajaagiza utumiaji wa nguvu dhidi ya raia wasio na hatia na wanaaoandamana kwa amani.

Maji kadiri ya nature na wataalamu wa fisikia wanajua the force of gravity, maji hayawezi rudi mlimani, na hilo hata kwa mwenye akili changa anajua. Kwa vyo vyote mwenye kulazimisha maji yarudi mlimani yalikotoka kinyume cha nguvu ya asili yake kufuata mreremko basi kwa vyo vyote akili yake haija kaa sawa. Kwa maana busara na hekima inakosekana kwa kiasi kikubwa. Kiongozi mwenye hekima na busara atatumia busara na hekima kutambua nature ya maji kufuata mkondo wake hadi baharini. Busara na hekima kwa pamoja vitaongoza mkondo wa maji yaendelee na safari yake kwa utulivu wote.

Kulazimisha maji yarudi yalikotoka haiwezekani. Inawezekana kuyasimamisha kwa muda mahala fulani na ujue wazi wakati huo yanakusanya nguvu. Yatatoboa njia nyingine ya kupita na pengine nguvu yake ikizidi itavunjilia mbali kizuizi ulichoweka ili mradi safari yake inaendelea. Hapo kutakuwa na athari kubwa kwani mimea na udongo na vitu vingine ambavyo ni kando ya mtu vitaadhirika katika dhoruba itakayoletwa na maji, na baadhi kusombwa katika dhoruba hiyo.

Kama maji hayo yasingezuiwa madhara yanayotokana na nguvu ya kusukuma yaendelee na safari yake yangeepukika. Kwa maana hiyo hapa ni common sense tu ambayo imo ndani ya hekima na busara.

Tuna mifano hai kama ya Mzee Ruksa kwa busara yake alipoona maji kuzidi nguvu katika harakati za kudai mageuzi aliruhusu na kuongoza mageuzi na hakukutokea madhara kama tunayoona sasa katika utawala huu. Sijui tumekulia jeshini hivi tunafikiria siasa ni nguvu badala ya majadiliano ya kupata hoja ya kukubaliana?

Wanafalsafa husema kukaa kimya bila kutolea msimamo wako katika jambo fulani maana yake ni kwamba unakubali au unapinga ila unao woga wa uwazi. Hii ni kasoro kubwa, na ngoja ngoja huumiza matumbo kama wahenga walivyotuachia usemi huu. Hatima ya ngojangoja huumiza matumbo ndo yaliyojilia huko Arusha.

Heshima ya jiji la arusha laweza shuka hadhi yake tokana na kukosa burasa katika mambo ya kawaida tu yanayotaka haki za raia zizingatiwe, kwani jiji hilo linaitangaza Tanzania katika mengi. Hayo yanatokea Arusha kuna mambo ya siri yaliyofichika ili kulinda maslahi ya wachache, si matakwa ya wananchi. Kuibuka ghafla kutafuta makafia ya kusaidia kuongoza jahazi lisiendelee kuzama tokana na dhoruba kali, wakati dalili za dhoruba uliziona na kwa sababu zako binafsi uliidharau hiyo, tunaweza tafsiri kama ni kutapatapa kwa mfa maji.

Hekima na busara huzaa mafanikio ya uongozi bora, lakini machafuko ni udhaifu wa uongozi ambao wanajiona ni watawala. Cha msingi wengi wa viongozi wetu ni watawala badala ya kuwa viongozi. Kiongozi bora ataongoza maji yafuate mtiririko wake yaendako.
 
For Andrew James Tice Canada here
For Gopalakrishnan Balachandaran (India)here

Make the corpse walks. Fiks baab kubwa wametuona wabongo kama wafu vile wanakuja na watu wa uongo, hao ni marafiki zao na wame negotiate kuwavisha uhusika ili wavute mshiko, sasa hapo intelijensia kazi yake ni nini? Kuchunguza fujo za raia na kuacha maslahi ya taifa yakihujumiwa? Huyu Luteni Kanali Sultani jk kajigawia mshiko kiulaini!
 
Mods, hii thread niliianzisha mimi kwa post hiii hapa chini, vipi mmechakachuwa? Yaani hata ma mods mnachakachuwa threads?

Viongozi wa Chadema walilazimisha maandamano yafanyike licha ya kuombwa na Mkuu wa Polisi Tanzania kuwa yasifanyike kwa sababu tu:

Walikuwa na nia ya kuwatisha wawekezaji wakubwa duniani ambao wapo Tanzania, huko huko Arusha kwa sasa.

Wawekezaji hao, wakiongozwa na Dhirubhai Ambani walikuwa Tanzania kwa nia ya mapumziko na biashara na kutazama mandhari ya Tanzania na uwezekano mkubwa wa kuwekeza Tanzania.

Kwa roho mbaya tu na kwa nia isiyoyatakia mema Tanzania, viongozi wa Chadema wakahakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa lazima na hata yangeruhusiwa na polisi basi fujo lazima zingetokea ili kuwatisha hao wawekezaji waone kuwa Tanzania si pa kuwekeza.

Yote hiyo, ni kwa sababu tu, ya chuki zao binafsi walizozijenga baada ya kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita.

Hakuna mantiki yoyote kwa wana siasa walio mahiri kulazimisha maandamano yafanyike wakati kuna wageni, tena wawekezaji muhimu ambao hakuna nchi katika hii dunia yetu ya sasa isiotaka wawepo au watembelee kwao.

Viongozi wa Chgadema kwa ajili tu ya chuki zao binafsi, wakaona hii ndio fursa ya kuipakaza matope (kama si m*v*) Tanzania. Walijuwa kuwa wawekezaji wakubwa kama hawa wanapokuja tena kwa idadi kubwa kama iliowasili hapa, lazima kuna waandishi wa habari wa kimataifa hususan wa mambo ya kibiashara na pia kuna watu wa intelijensia za kibiashara ambao misafara kama hiyo huwa hawakosekani.

Kwa namna ya maisha tunayoishi wa Tanzania au kwa mpenda amani yoyote, hata kama mna ugomvi wenu wa ndani, ajapo mgeni, tena ambae anaweza kuleta manufaa nyumbani kwenu, huwa mnasitisha ugomvi kwa siku mbili tatu mpaka mgeni aondoke. Haya hutokea hata majumbani mwetu, tukipapurana na bahati nzuri au mbaya mgeni akibisha hodi basi mara nyingi kwa wenye akili husitisha kupapurana kwao, wakamhudumia mgenina ikibidi kupapurana, wataendelea mgeni akisha ondoka.

Leo Chadema wameonyesha sura gani ya nchi yetu, kwa kulazimisha maandamano yaliyositishwa na Mkuu wa Polisi, mbele ya hawa wageni?

Nna uhakika, sura walioionyesha si nzuri, lakini, ni matumaini yangu kuwa wenyeji, waliowaalika hawa wageni, wataweza kuwafahamisha ukweli ulivyo na wataridhia si tu kuja tena kutembelea Tanzania, bali na kuwekeza kwa wingi, kwani kwa sasa bado tunahitaji mitaji ya nje.

Nawaomba wa Tanzania walaani kitendo cha viongozi wa Chadema baada ya kuuelewa huu ukweli wa kwanini hawa viongozi walilazimisha maandamano yafanyike.

Mungu awalaze popote apendapo Marehemu waliofarik.
 
Wawekezaji gani wakati wananchi wanaendelea kufa kwa umasikini. Tunaposema nchi hii inaongozwa kwa kufuata sheria za nchi zingine huoni. you have to think more and more, ila kwako wewe unanufaika na mfumo ndo maana unaona njia zote zinazotumiwa na Chadema ni feki.

Mkuu Zomba, Uliza wangapi wananufaika na hii system kama si wewe na wachache mnaosahau kuwa kuna binadamu wengine kama wewe ambao wanahitaji elimu, maji, barabara au hata kiongozi wa kuwaonyesha njia tu inatosha.

Kuna awamu yeyote katika Tanzania kumetowa wahitimu wengi zaidi wa chekechea, primary, sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya ualimu vyuo vikuu zaidi ya huu wa Kikwete?

Kuna awamu yeyote katika Tanzania iliopeleka madaktari wengi kwenda kuongeza ujuzi na kuwa madaktari bingwa zaidi ya huu wa Kikwete?

Kuna awamu yeyote katika Tanzania ambayo imesambaza maji kwa wingi zaidi ya awamu hii ya kikwete?

Kuna awamu yeyote imekusanya kodi zaidi ya awamu hii ya kikwete?

Kuna awamu yeyote imeshusha utumiaji wa fedha za wafadhili katika bajeti ya Tanzania zaidi ya hii ya Kikwete?

Kuna awamu yeyote imesambaza huduma za afya na kufikia karibu zaidi ya wa Tanzania zaidi ya hii ya Kikwete?

Kuna awamu yeyote imewahi kuwaondoa madarakani na kuwashitaki kwa rushwa au ubadhirifu vigogo wa serikali na wengineo zaidi ya hii ya kikwete?

Kuna awamu yeyote ilioleta viongozi na wageni mbalimbali wa kuanzia maRais, wafanya Biashara, watu muhimu zaidi ya hii ya kikwete?

Yote hayo hamuyaoni? Au ndio agenda za siri?
 
Kwa namna ya maisha tunayoishi wa Tanzania au kwa mpenda amani yoyote, hata kama mna ugomvi wenu wa ndani, ajapo mgeni, tena ambae anaweza kuleta manufaa nyumbani kwenu, huwa mnasitisha ugomvi kwa siku mbili tatu mpaka mgeni aondoke. Haya hutokea hata majumbani mwetu, tukipapurana na bahati nzuri au mbaya mgeni akibisha hodi basi mara nyingi kwa wenye akili husitisha kupapurana kwao, wakamhudumia mgenina ikibidi kupapurana, wataendelea mgeni akisha ondoka.
Wewe kweli hayawani na mwendawazimu. Kama waasisi wa taifa hili wangekuwa wanafikiria kama wewe basi hadi leo hii tungekuwa chini ya wakoloni. Eti Sytem at Work! Ama kweli system hiyo unayoifanyia kazi imeoza, kama huo ndio ujinga uliotumwa kuusambaza.
 
Zomba kumbuka kwamba maandamano ya tarehe 5 Januari 2011 ni tarehe iliyopangwa na CHADEMA na Polisi kwa makubaliano. Hili la kuvizia wawekezaji ndo fujo ifanyike umelichakachua mkuu na unaonyesha wewe ni mweupe wa data na ni mwongo na mwepesi wa kusahau. Kama huna hoja mzee si lazima kuchangia.
 
Serikali ina mkono mrefu na hawana sababu ya kutolea ufafanuzi wa kina wanapozuia kitu kisifanyike. Wana namna na njia nyingi za kupata habari, za kuaminika na kusadikika na zisozo hivyo. Maamuzi mengine yanateghemea muda na kuepusha fadhaa inayoweza kupatikana, na nilimsikia Mwema akisema yawachwe kwa sasa. Jee, huoni kuwa hawa viongozi wanao kaidi amri ya Serikali ndio wakorofi?

Na ukorofi huo wanaoufanya ni kwa faida ya nani? Raia wengi Tanzania hatuungi mkono ufedhuli kwa Serikali. Raia wengi Tanzania hutuungi mkono Maandamano haramu. Raia wengi Tanzania hatuungi mkono chama kisicho kuwa na maamuzi ya amani. Raia wengi wa Tanzania hatuungi mkono siasa za ubabe.
unatuboa sana! naomba usiendelee kuchangia mada:alien:
 
.....IGP sijui anajiita Mwema au kitu gani hana utu wowote! Sijui aliambiwa polisi kazi yake ni kuumiza na kunyanyasa raia!!! ASHINDWE! sasa ona yaliyotokea,,,,,huyu wa kumtia Mbaroni na hana sifa za uongozi wa juu namna hiyo,,,ni ushemeji tu!
 
Kuelezea mambo ya awamu za JK bila mafanikio ku ji reflect kwenye maisha ya watanzania ni upuuzi. Ungeeleza hayo mambo ya awamu ya Jk yalivyochangia kuondoa umaskini wa kipato. Soma data za HBS(Household budget survey 2007) na MKUKUTA I na MKUKUTA II na pia Tanzania Development Vision 2025 uone tulipo kimaendeleo. Hapo ndipo utajua unayoyasema kuhusu awamu za JK hatujaona matunda yake. Umaskini haujapungua GDP ya Bara iko chini ku;liko ya Zanzibar na Inflation iko 12.2% wakati anapokea nchi JK Inflation ilikuwa single digit nakupa homework katafute na acha ushabiki wa kijinga. Nchi iko taabani acha kushabiakia majina eti awamu za Jk!!!!!!
 
Wewe Zomba acha kutubabaisha!!! Wawekezaji unawajua wewe!! Hao ni baadhi ya waporaji tu wa rasilimali za mama yetu Tanganyika mnaowaalika kila kukicha!!!! Let me tell you.... if you think you'll get away with this..... you are utterly wrong!!! You and your allies....... soon or later....... you shall pay for this squarely!!!!
 
Hizo ndio sababu ambazo hazipingiki, kulikuwa kuna umuhimu gani wa kufanya maandamano wakati kuna wageni? tena ni wawekezaji muhimu? kama si kuwatisha?

Wageni my ass! Hivi hayo mawazo yenu mgando watu wa CCM yataisha lini? Nidhamu ya woga, kujipendekeza pendekeza kwa matajiri wa kigeni, there is no free lunch in this World kwa taarifa yako. Mwekezaji anawekeza mahali amabapo anaamini atapata faida.

Nenda Congo DRC ukaone Wachina na Wamarekani wanavyotumia pesa nyingi kufanya utafiti wa madini (mineral exploration), je kuna amani kule? Mbona hawakimbii? Nenda Tarime kule kwenye mgodi wa North Mara, wazungu wana hawawezi hata kuzurura mitaani kwa kuhofia maisha yao, na wameshavamiwa na wananchi wa Nyamongo mara kwa mara, na mali zao kuharibiwa. Kuna mzungu alishawahi kupigwa risasi na wananchi kijijini akafa. Mbona hawaondoki? Nani kakwambia mahali penye faidi bepari huwa anaogopa?

Jamani Watanzania tuamke, hizi sababu za kijinga kijinga hizi za eti kulikuwa na akina Ambani wamekuja kutalii na kuangalia uwekezaji zimepitwa na wakati. Tubadilike.
 
Kuna awamu yeyote katika Tanzania kumetowa wahitimu wengi zaidi wa chekechea, primary, sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo vya ualimu vyuo vikuu zaidi ya huu wa Kikwete?

Kuna awamu yeyote katika Tanzania iliopeleka madaktari wengi kwenda kuongeza ujuzi na kuwa madaktari bingwa zaidi ya huu wa Kikwete?

Kuna awamu yeyote katika Tanzania ambayo imesambaza maji kwa wingi zaidi ya awamu hii ya kikwete?

Kuna awamu yeyote imekusanya kodi zaidi ya awamu hii ya kikwete?

Kuna awamu yeyote imeshusha utumiaji wa fedha za wafadhili katika bajeti ya Tanzania zaidi ya hii ya Kikwete?

Kuna awamu yeyote imesambaza huduma za afya na kufikia karibu zaidi ya wa Tanzania zaidi ya hii ya Kikwete?

Kuna awamu yeyote imewahi kuwaondoa madarakani na kuwashitaki kwa rushwa au ubadhirifu vigogo wa serikali na wengineo zaidi ya hii ya kikwete?

Kuna awamu yeyote ilioleta viongozi na wageni mbalimbali wa kuanzia maRais, wafanya Biashara, watu muhimu zaidi ya hii ya kikwete?

Yote hayo hamuyaoni? Au ndio agenda za siri?

Lord have mercy on this guy! Eti marais wa nje na wafanyabiashara wakubwa kutembelea Tanzania, so what>? Hivi unakumbuka JK wakati ameingia tu Ikulu alifanya ziara ya ghafla Muhimbili, bila taarifa, akakuta wagonjwa wamelala chini. Tukajua atakuja na suluhisho la tatizo hilo sugu. Nenda sasa hivi Muhimbili kajionee, wagonjwa bado wanalala chini. Kwa hiyo pia utamsifia kwamba ni rais wa kwanza kwenda Muhimbili kutembelea wagonjwa na kukuta wamelalala chini>? Kama anatembelea tu na kupigwa picha na waandishi wa habari, kisha yanaishia hapo inatusaidia nini sisi?

Think outside the box brother. Hatuko tena kwenye zidumu fikra sahihi za mwenyekiti!
 
zombe nakubaliana na wewe asimia mia, tena nadhani na tanesco inabidi wasikate umeme mpaka wageni waondoke....maana wageni wakiouna huu mgao wanaweza kubadili mawazo ya ku "invest" kwenye nchi hii.


jamani achaneni na hawa vilaza mtu anaandika post zaidi ya 700 anapongezwa 2 lazima ujue huyo mtu hatumii kichwa anatumia kiungo kingine kabisa hao ndio kina salva wamo humu na id kibao
 
Back
Top Bottom