Intelijensia Kuhusu Maandamano ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Intelijensia Kuhusu Maandamano ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by We know next, Jan 6, 2011.

 1. W

  We know next JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naomba kuuliza swali hili kwa wote waliohusika kusababisha Mauaji ya Arusha Jana.

  Je Familia zenu na jamaa zenu wapo salama??

  My Take: Kwa hasira ya Watanzania walio wengi, kitendo cha mauaji ya raia wema Arusha, kinaleta hali tete sana kwa familia za wahusika waliosababisha hayo yote;

  - Je familia zenu zitalindwa na Polisi zinapojichanganya na jamii nyingine ktk Public places?
  - Je si mnafahamu kuwa waliofariki na kuumizwa huko Arusha wana ndugu na jamaa zao kama nyie?
  - Je mlipokuwa mnafanya hayo maamuzi, mliyafikilia hayo? Au mlijiona mnaishi Kisiwani ambapo hamtafikiwa?
  - Kama mlifumba macho, basi subirini muone, kwani hali mmeisababisha wenyewe! Uchungu wa Mwana aujuaye mzazi!!
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa polisi nchini Said Mwema kusitisha ghafla maandamano ya Chama Cha Chadema huko mjini Arusha ambayo yalishapata kibali kutoka kwa Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha ni dhahiri kuna mkubwa fulani aliyeshinikiza na leo anainamisha kichwa chini kwa kuona matokea ya kutumia zaidi nguvu ya dola kukandamiza haki za wananchi badala ya kutumia utaratibu wa utashi wa mazungumzo ya pande zote mbili kwa amani kama walivyoomba chadema hapo awali au kuyaacha maandamano na mkutano uishe kwa amani.

  Mfalme Suleman wa taifa la Waisrael alipoambiwa aombe kitu cho chote kwa Mungu katika utawala wake, yeye aliomba Mungu amjalie kipaji cha hekima na burasa. Aliomba kitu ambacho kwa wengi wa watawala wetu wa leo ni kitu adimu kukifikiria Mungu awajalie. Kwa hakika alichagua fungu lililo bora na adimu sana. Wengi wetu wanaomba usiku na mchana Mungu awajali kupata utajiri na heshima na kutawala bila mipaka. Lakini Mfalme Suleman anaheshimika katika historia ya wafalme wengi kwamba ni mmoja aliyejaliwa hekima na busara sana katika utawala wake licha ya udhaifu wake aliokuwa nao. Naam busara na hekima ndio sifa njema ya kiongozi bora, na yuko makini kufikiria athari zake kabla hajaagiza utumiaji wa nguvu dhidi ya raia wasio na hatia na wanaaoandamana kwa amani.

  Maji kadiri ya nature na wataalamu wa fisikia wanajua the force of gravity, maji hayawezi rudi mlimani, na hilo hata kwa mwenye akili changa anajua. Kwa vyo vyote mwenye kulazimisha maji yarudi mlimani yalikotoka kinyume cha nguvu ya asili yake kufuata mreremko basi kwa vyo vyote akili yake haija kaa sawa. Kwa maana busara na hekima inakosekana kwa kiasi kikubwa. Kiongozi mwenye hekima na busara atatumia busara na hekima kutambua nature ya maji kufuata mkondo wake hadi baharini. Busara na hekima kwa pamoja vitaongoza mkondo wa maji yaendelee na safari yake kwa utulivu wote.

  Kulazimisha maji yarudi yalikotoka haiwezekani. Inawezekana kuyasimamisha kwa muda mahala fulani na ujue wazi wakati huo yanakusanya nguvu. Yatatoboa njia nyingine ya kupita na pengine nguvu yake ikizidi itavunjilia mbali kizuizi ulichoweka ili mradi safari yake inaendelea. Hapo kutakuwa na athari kubwa kwani mimea na udongo na vitu vingine ambavyo ni kando ya mtu vitaadhirika katika dhoruba itakayoletwa na maji, na baadhi kusombwa katika dhoruba hiyo.

  Kama maji hayo yasingezuiwa madhara yanayotokana na nguvu ya kusukuma yaendelee na safari yake yangeepukika. Kwa maana hiyo hapa ni common sense tu ambayo imo ndani ya hekima na busara.

  Tuna mifano hai kama ya Mzee Ruksa kwa busara yake alipoona maji kuzidi nguvu katika harakati za kudai mageuzi aliruhusu na kuongoza mageuzi na hakukutokea madhara kama tunayoona sasa katika utawala huu. Sijui tumekulia jeshini hivi tunafikiria siasa ni nguvu badala ya majadiliano ya kupata hoja ya kukubaliana?

  Wanafalsafa husema kukaa kimya bila kutolea msimamo wako katika jambo fulani maana yake ni kwamba unakubali au unapinga ila unao woga wa uwazi. Hii ni kasoro kubwa, na ngoja ngoja huumiza matumbo kama wahenga walivyotuachia usemi huu. Hatima ya ngojangoja huumiza matumbo ndo yaliyojilia huko Arusha.

  Heshima ya jiji la arusha laweza shuka hadhi yake tokana na kukosa burasa katika mambo ya kawaida tu yanayotaka haki za raia zizingatiwe, kwani jiji hilo linaitangaza Tanzania katika mengi. Hayo yanatokea Arusha kuna mambo ya siri yaliyofichika ili kulinda maslahi ya wachache, si matakwa ya wananchi. Kuibuka ghafla kutafuta makafia ya kusaidia kuongoza jahazi lisiendelee kuzama tokana na dhoruba kali, wakati dalili za dhoruba uliziona na kwa sababu zako binafsi uliidharau hiyo, tunaweza tafsiri kama ni kutapatapa kwa mfa maji.

  Hekima na busara huzaa mafanikio ya uongozi bora, lakini machafuko ni udhaifu wa uongozi ambao wanajiona ni watawala. Cha msingi wengi wa viongozi wetu ni watawala badala ya kuwa viongozi. Kiongozi bora ataongoza maji yafuate mtiririko wake yaendako.
   
 3. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  habari ni ndefu naomba wachangiaji wasi ku quote waki reply
   
 4. comson

  comson JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hawa watachapwa na mungu
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 6. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Haina ulazima wowote kutumia nguvu waliyoitumia hawa polisi wetu. Na ndivyo walivyo kama vile wao ugumu wa maisha hauwahusu... Gap linaongezeka kati yao na Raia.
   
 7. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ni ndefu lakini amejitahidi kunyambua na kufanya aeleweke! Nimempa tano...........
   
 8. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  true
   
 9. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Yeah hapo ni kweli kabisa mkuuu...nyinyi ndio tunawahitaji humu ndani sio watoa pumba
   
 10. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  safi sana. imekaa vyema. aliyeshinikiza ni jk
   
 11. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena mkuu
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Candid Scope kama unaweza tuma hii kitu kwa wahaririri wa Mwananchi,Raia Mwema, Tz Daima ama Mwanahalisi wachape kwenye gazeti zao.
   
 13. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2011
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Greater thinkers hivi ni kweli RZ1 na wenzake wa UVCCM wana mamlaka ya kutoa tamko juu ya mauaji ya Arusha???? Naombeni mnijuze
   
 14. m

  mams JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni wakati gani kiongozi anatakiwa aamue jambo muhimu kwa masrahi ya wengi, na kama hana uhakika ni bora akae kimya.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa Chadema walilazimisha maandamano yafanyike licha ya kuombwa na Mkuu wa Polisi Tanzania kuwa yasifanyike kwa sababu tu:

  Walikuwa na nia ya kuwatisha wawekezaji wakubwa duniani ambao wapo Tanzania, huko huko Arusha kwa sasa.

  Wawekezaji hao, wakiongozwa na Dhirubhai Ambani walikuwa Tanzania kwa nia ya mapumziko na biashara na kutazama mandhari ya Tanzania na uwezekano mkubwa wa kuwekeza Tanzania.

  Kwa roho mbaya tu na kwa nia isiyoyatakia mema Tanzania, viongozi wa Chadema wakahakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa lazima na hata yangeruhusiwa na polisi basi fujo lazima zingetokea ili kuwatisha hao wawekezaji waone kuwa Tanzania si pa kuwekeza.

  Yote hiyo, ni kwa sababu tu, ya chuki zao binafsi walizozijenga baada ya kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita.

  Hakuna mantiki yoyote kwa wana siasa walio mahiri kulazimisha maandamano yafanyike wakati kuna wageni, tena wawekezaji muhimu ambao hakuna nchi katika hii dunia yetu ya sasa isiotaka wawepo au watembelee kwao.

  Viongozi wa Chgadema kwa ajili tu ya chuki zao binafsi, wakaona hii ndio fursa ya kuipakaza matope (kama si m*v*) Tanzania. Walijuwa kuwa wawekezaji wakubwa kama hawa wanapokuja tena kwa idadi kubwa kama iliowasili hapa, lazima kuna waandishi wa habari wa kimataifa hususan wa mambo ya kibiashara na pia kuna watu wa intelijensia za kibiashara ambao misafara kama hiyo huwa hawakosekani.

  Kwa namna ya maisha tunayoishi wa Tanzania au kwa mpenda amani yoyote, hata kama mna ugomvi wenu wa ndani, ajapo mgeni, tena ambae anaweza kuleta manufaa nyumbani kwenu, huwa mnasitisha ugomvi kwa siku mbili tatu mpaka mgeni aondoke. Haya hutokea hata majumbani mwetu, tukipapurana na bahati nzuri au mbaya mgeni akibisha hodi basi mara nyingi kwa wenye akili husitisha kupapurana kwao, wakamhudumia mgenina ikibidi kupapurana, wataendelea mgeni akisha ondoka.

  Leo Chadema wameonyesha sura gani ya nchi yetu, kwa kulazimisha maandamano yaliyositishwa na Mkuu wa Polisi, mbele ya hawa wageni?

  Nna uhakika, sura walioionyesha si nzuri, lakini, ni matumaini yangu kuwa wenyeji, waliowaalika hawa wageni, wataweza kuwafahamisha ukweli ulivyo na wataridhia si tu kuja tena kutembelea Tanzania, bali na kuwekeza kwa wingi, kwani kwa sasa bado tunahitaji mitaji ya nje.

  Nawaomba wa Tanzania walaani kitendo cha viongozi wa Chadema baada ya kuuelewa huu ukweli wa kwanini hawa viongozi walilazimisha maandamano yafanyike.

  Mungu awalaze popote apendapo Marehemu waliofarik.
   
 16. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zombe

  Endelea kulala tukipata Uhuru tutakuamsha.
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wewe kweli ZOBA
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hizo ndio sababu ambazo hazipingiki, kulikuwa kuna umuhimu gani wa kufanya maandamano wakati kuna wageni? tena ni wawekezaji muhimu? kama si kuwatisha?
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana, lakini nadhani ukweli umeuelewa na utauzingatia.
   
 20. c

  chibidula Member

  #20
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nafikiri uelewa wako ni tatizo, maandamano ya Chadema yalipangwa toka lini na hao wageni wamekuja lini?
   
Loading...