Intelijensia Kuhusu Maandamano ya CHADEMA

Intelijensia Kuhusu Maandamano ya CHADEMA

Nasubiri majibu ya makamba........

Hawa wetu hatuwapeleki kwa ocampo watakula raha magereza ya nje.. Hawa ni keko au karanga au maweni.. Tuu..
 
Mkuu, nakuunga mkono, tena mahakama ya ICTR hapo hapo arusha, hakuna haja ya kuwapeleka hadi Uholanzi ...
 
Huyu naona kaamka na mawazo mgando, hivi Ambani kuja Tanzania kunasimamisha Democrasia yetu au ndio ruhusa ya kufanya uhuni kwenye uchaguzi wa meya?

Kaka fikiria vizuri hata kama ww ni kada kama mie, kwani integensia ya polisi ilisema nini kama watakaidi? na je kwanini polisi walijiandaa na risasi za moto kuua watu wasio na hatia?

Hapa kuna umuhimu wa kuwafikisha wote pamoja ww unayeongea kwenye mahakama ya kimataifa mkajibu kwanini mmeamua kuwa wauaji
 
hawa ndio ndio tunawataka humu sio kina kishongo, dar es salaam, ms na wengine.........
safi sanamkuu hii kitu jk akisoma hataelewa kitu hapa........maana he cannot think beyond the next meal!!
 
IGP na Waziri wa mambo ya ndani wanawajibika kwa mauaji ya watanzania wenzetu huko Arusha. Naamini tukishakuwa na katiba mpya basi tutakuwa na uwezo wa kuwawajibisha watumishi wa umma watakao sababisha maafa kwa nchi yetu!
 
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.... hiki ni chombo mahsusi kinachohusika na ushauri wa mambo ya usalama ya mkoa....

@Kamakabuzi... Glory to God
 
Viongozi wa Chadema walilazimisha maandamano yafanyike licha ya kuombwa na Mkuu wa Polisi Tanzania kuwa yasifanyike kwa sababu tu:

Walikuwa na nia ya kuwatisha wawekezaji wakubwa duniani ambao wapo Tanzania, huko huko Arusha kwa sasa.

Wawekezaji hao, wakiongozwa na Dhirubhai Ambani walikuwa Tanzania kwa nia ya mapumziko na biashara na kutazama mandhari ya Tanzania na uwezekano mkubwa wa kuwekeza Tanzania.

Kwa roho mbaya tu na kwa nia isiyoyatakia mema Tanzania, viongozi wa Chadema wakahakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa lazima na hata yangeruhusiwa na polisi basi fujo lazima zingetokea ili kuwatisha hao wawekezaji waone kuwa Tanzania si pa kuwekeza.

Yote hiyo, ni kwa sababu tu, ya chuki zao binafsi walizozijenga baada ya kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi uliopita.

Hakuna mantiki yoyote kwa wana siasa walio mahiri kulazimisha maandamano yafanyike wakati kuna wageni, tena wawekezaji muhimu ambao hakuna nchi katika hii dunia yetu ya sasa isiotaka wawepo au watembelee kwao.

Viongozi wa Chgadema kwa ajili tu ya chuki zao binafsi, wakaona hii ndio fursa ya kuipakaza matope (kama si m*v*) Tanzania. Walijuwa kuwa wawekezaji wakubwa kama hawa wanapokuja tena kwa idadi kubwa kama iliowasili hapa, lazima kuna waandishi wa habari wa kimataifa hususan wa mambo ya kibiashara na pia kuna watu wa intelijensia za kibiashara ambao misafara kama hiyo huwa hawakosekani.

Kwa namna ya maisha tunayoishi wa Tanzania au kwa mpenda amani yoyote, hata kama mna ugomvi wenu wa ndani, ajapo mgeni, tena ambae anaweza kuleta manufaa nyumbani kwenu, huwa mnasitisha ugomvi kwa siku mbili tatu mpaka mgeni aondoke. Haya hutokea hata majumbani mwetu, tukipapurana na bahati nzuri au mbaya mgeni akibisha hodi basi mara nyingi kwa wenye akili husitisha kupapurana kwao, wakamhudumia mgenina ikibidi kupapurana, wataendelea mgeni akisha ondoka.

Leo Chadema wameonyesha sura gani ya nchi yetu, kwa kulazimisha maandamano yaliyositishwa na Mkuu wa Polisi, mbele ya hawa wageni?

Nna uhakika, sura walioionyesha si nzuri, lakini, ni matumaini yangu kuwa wenyeji, waliowaalika hawa wageni, wataweza kuwafahamisha ukweli ulivyo na wataridhia si tu kuja tena kutembelea Tanzania, bali na kuwekeza kwa wingi, kwani kwa sasa bado tunahitaji mitaji ya nje.

Nawaomba wa Tanzania walaani kitendo cha viongozi wa Chadema baada ya kuuelewa huu ukweli wa kwanini hawa viongozi walilazimisha maandamano yafanyike.

Mungu awalaze popote apendapo Marehemu waliofarik.

Hakika sasa naendelea ku prove CCM inaendelea kutawala kutokana na Ujinga wa Watanzania.Prof Mazrui aliwahi kusema pale Nkrumah kuwa Problem of Tanzania 80% are fool.Zoba usifikiri hata huo uhuru ulionao umeshuka bure,Kuna watu waliumia wakateswa wakapoteza maisha leo unaishi na kutoa pumba kwa sababu ya Marehemu babu zetu.
 
Kuna jamaa kwenye thread moja huko ameyapa jina mauaji haya kuwa ni MAUAJI YA JK ya Arusha!...na ndivyo yanavyopaswa kuitwa!
 
Msisahau pia uongozi wa CDM kwa makusudi mazima wakijua kitakachotokea wakawahamasisha watu kupingana na Polisi. Leo wao wako nje, wale wasio na anuani wangali wanasota ndani. Inajulikana wazi utendaji wa vyombo vyetu vya dola, lakini watu wanajifanya hawajui na kuwahamasisha watu kuingia katika mambo ambayo yatawagharimu. Ni mara ngapi watu wamekuwa wahanga wa maandamano Tanzania mmewahi kusikia mtu kawajibishwa? ikiwa kweli tunawapenda watu wetu basi na tuwalinde kwanza. lakini ikiwa ndio njia ya kupandia tuwawache waendelee kupanda mpaka nchi itakapofikia kuwa kama Somali.

(nawasisitiza tena ndugu zangu Watanzania -haijalishi ni wananchi ama walio katika vyombo vya dola. TUACHE KUTUMIKIA MATAKWA YA WANASIASA)
 
kwa hiyo wakija wageni ndio Tanzania haiwi tanzania na Demokrasia inatakiwa ifichwe? Hivi hujasikia watu wanafanya maandamano kwenye G7 meetings ambako ndiko wageni wengine muhimu wapo? Yaani tuuze uhuru wetu kwa ajili ya kuogopa wageni.

Yeye mwenyewe ni MGENI ndio maana analalama kama lile jini lililotolewa kwenye kifungo ndania ya chupa na mvuvi
 
Kuna jamaa kwenye thread moja huko ameyapa jina mauaji haya kuwa ni MAUAJI YA JK ya Arusha!...na ndivyo yanavyopaswa kuitwa!

mkuu...naongeza kidogo tu.... MAUAJI YA JK ya Arusha-2011...
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiangalia Ramani inayoonesha maeneo yote ya Hifadhi ya Taifa ya Mbuga za Wanyama Serengeti, alipowasili kwenye kituo kidogo cha Hifadhi ya Taifa Serengeti Mkoani Mara leo,Makamu wa Rais yupo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa ajili ya Mapumziko mafupi. Wa pili kushoto Mke wa Makamu wa Rais Mama Aisha Bilal na kushoto Mkuu wa kituo cha Hifadhi ya Taifa Serengeti Mtango G.G. Mtahiko.
 
Asisahaulike OCD Mr. Zuberi kwa kumpiga Mbunge virungu wakati vijana wake wenyewe walimchagua Mr. Lema. Ushahidi kura za kituo cha Polisi kati Arusha.
 
Kikwete hana namna yoyote ya kukwepa lawama za mauaji haya
 
Salaam wana JF,

Tumeshuhudia ya Arusha na mengine mengi kabla ya hayo, swali nauliza; Je, thamani ya wanajamii mbele ya polisi ni pale wanapowasaidia kuwakamata wahalifu tu?
 
Msisahau pia uongozi wa CDM kwa makusudi mazima wakijua kitakachotokea wakawahamasisha watu kupingana na Polisi. Leo wao wako nje, wale wasio na anuani wangali wanasota ndani. Inajulikana wazi utendaji wa vyombo vyetu vya dola, lakini watu wanajifanya hawajui na kuwahamasisha watu kuingia katika mambo ambayo yatawagharimu. Ni mara ngapi watu wamekuwa wahanga wa maandamano Tanzania mmewahi kusikia mtu kawajibishwa? ikiwa kweli tunawapenda watu wetu basi na tuwalinde kwanza. lakini ikiwa ndio njia ya kupandia tuwawache waendelee kupanda mpaka nchi itakapofikia kuwa kama Somali.



(nawasisitiza tena ndugu zangu Watanzania -haijalishi ni wananchi ama walio katika vyombo vya dola. TUACHE KUTUMIKIA MATAKWA YA WANASIASA)


Acha uongo wewe mchana kweupe Mkuu!

Nani aliyesema kuwa kuna watu wanasota ndani?...eti wasio na anwani...crap!
Watu wote walioshikwa na kuwekwa ndani wamewekewa dhamana jana wako makwao, na jumla yao ni 41..
Usiupotoshe umma wa wasomaji kwa taarifa za hisia!
If you are not sure, better keep out of rail!

 
Wee zomba post yako ingekuwa na maana kama polisi wangewaacha chadema wafanye maandamano na fujo kutokea.
 
Kwa kweli wote wako nje ya dhamana, mimi nilikuwepo mahakamani. Labda kama kuna watuhumiwa wa issue nyingine sio raia wema wa maandamano.
 
Back
Top Bottom