Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Hiyo ipo hasa kwa watu wenye umri mkubwa ni mambo ya dawa za asili mara nyingi anachukuliwa mgonjwa husika anawekwa ndani alafu sehem ya paa inatobolewa kidogo anapigwa na ule mwaga wa jua akiwa ndani hapo ndio anakata roho vingnevyo ataoza na harufu juu
Hii si vampire/zombie?

Maana katika movies tunaona ndio waathirika wa mwanga wa jua.

Dunia!
 
We usiyeamini usiombe yakukute, huko kwetu ipo dawa mtu akiitumia hafi mpaka apigwe mwale wa jua kutokea kwenye paa, yaani mtauguza mpaka atatoa funza kichwa kinaongea tu. Inabidi mtoboe bati au kama ni nyumba ya nyasi mnazitoa usawa wa alipolala jua likipenya ndio anaweza kufa kawaida. Hii sikusimuliwa nilijionea kabisa mtu mpaka anaoza hawezi kusogea lakini anaongea kawaida kabisa.
Zombies/Vampiers??

Hii Dunia hii!
 
Haya ni mazindiko ya kiafrika, roho haikai kwenye mti ila anafanya zindiko anaungana na ule mti ukitaka kumuua ni mpaka ule mti ufe kwanza. Hizi zilitumika kama kinga enzi zile watu wanatekwa maporini safari za miguu hamna magari. Zipo nyingi ambazo nimewahi kuziona in action ni kama;
1. Dawa ya mbio- hii kulikuwa na jambazi sugu wanamtafuta kila wakija akitoka mbio hata mbwa hawafati hiyo speed ya jamaa.

2. Kukosekana kwenye hatari- hii mtu akija akudhuru anakuwa hakuoni, walihangaika na huyo mtu mpaka wakaamua kuua mwanae kwa hasira baada ya kumkosa muhusika kila wakati.

3. Dawa ya kurusha ngumi- hii ukimpiga mtu ngumi anazikwa, inafanya kazi pale tu unapokuwa unaonewa lakini ukianzisha ukorofi utapigwa kama ngoma.

4. Dawa ya kurusha jiwe au fimbo - hii kama mtu kakukimbia na huwezi mpata basi ukichukua kitu chochote ukarushia uelekeo wake humkosi, hata awe mbali wa viwanja 3 vya mpira.

Na zingine kibao kwa nyie watoto wa miaka ya 90 na 2000 hamuwezi elewa.
Doh!

I’m in love na hii African technology 👏

Salute sana kwa wazee (wahenga) 🙌
 
sasa magu kaingiaje kwenye hili
Angeweka roho kwenye miti leo tusingekua na majanga yafuatayo

1)Chawa wa mama,
2)Deni ni stahimilivu,
3)Mama amekomesha mafisadi,
4)Mama:kuna watu wanaiba pesa za serikali,
5)Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake,
6)Garama za vifurushi,
7)Chadema kugeuka CCM ndogo, (wanatumika kutuhadaa wananchi huku ccm ikitafuna nchi kwa amani)
8)Chanjo za corona
9)Dp world
Mengine utaongeza na wewe
 
Mimi naamini kwa 100%
Kwetu Mpimbwe huko Katavi wilaya ya Tanganyika mila hii ipo.
Sio mti tu, kuna maji, mnyama, mmea, shallow graves n.k.
So sishangai huyo ndugu yako kusema hayo.
Mie mwenyewe siku nikiamua kuzindika mwili wangu, naenda tu home kwa bibi, mambo yanakuwa safi.
Sema masharti yake ndio yananishinda
Masharti yake yakoje, Kama hutojali?

Kwenye family yako yupo/wapo waliofanyiwa?


Nimependa kwa kweli. Heshima kwao wazee!

🙌
 
Tuna Mzee wetu hapa tunamuuguza kwa muda mrefu miaka mitatu sasa tunampambania nae alipata tatizo kuparalalaizi mpaka sana yupo ICU hali yake sio nzuri miguu yake imeanza kuoza

Imenibidi kuandika thread hii humu sababu siku mbili hizi tumepigiwa simu huko kijijini kwamba Mzee wetu twende huko kijijini wanafamilia wote tukafanye mambo ya Mila twende na kondoo wawili inasemekana Mzee wetu Kuna miti miwili ndio aliweka roho yake

Kwahiyo tutaendelea kupoteza muda kumuuguza atakufa mpaka aoze mwili wote inatubidi tuende tukafanye mambo ya Mila maana tukimuacha aoze mwili mzima ndio afe hali hiyo itakuja kumkuta mwanafamilia
Itakuwa alimeza hirizi dawa ya kinga za kichawi wasimdhuru sasa hawezi kufa mpaka atapishwe atateseka sana inabidi mkubali tu muende itakuwa zindiko lipo hapo mkitoa atakufa apumzike na mateso Kwa kweli mambo ya kinga machale mwilini kufa unatesekana sana
 
Kivipi ni mkataba na shetani?

Wewe umejuaje ni mkataba na shetani?
Jambo lolote linalohusu mila/jadi,ni lazima zihusishe ushirikina kwa namna moja au nyingine,hiyo ni ibada ya Shetani.Iwe ni kujipatia kinga/ulinzi au jambo lolote linalohusiana na hayo,na kwakuamini unafanikiwa,huko ni kuingia mkataba na Shetani,mwisho wa siku itakugharimu tu.
 
Hakuna ajabu yoyote ila ni elimu, hio haina tofauti na uhai uliofichwa kwenye sindano na vidonge kwani usipochomwa au kumeza unakufa na ukitumia unapona.
Hivyo kuna tofauti gani na aliyelinda uhai wake kutumia mti?

Nikupe mfano mwingine,
Huyo mzee hata ingetokea ajali asingekufa kirahisi, Je ipi teknolojia bora kati ya hiyo ya kujikikinga na miti au vitu na teknolojia ya Airbag ambayo inapunguza risk wakati wa ajali?
Sasa kama ni nzuri na haijakaa kimaajabu ajabu Kwa nini haifundishwi hadharani ili mradi watu wengi wapate kujifunza na kuielewa
 
Jambo lolote linalohusu mila/jadi,ni lazima zihusishe ushirikina kwa namna moja au nyingine,hiyo ni ibada ya Shetani.Iwe ni kujipatia kinga/ulinzi au jambo lolote linalohusiana na hayo,na kwakuamini unafanikiwa,huko ni kuingia mkataba na Shetani,mwisho wa siku itakugharimu tu.
Hii tafsiri inaishia anga la Afrika tu si ndio?

Maana kule kwa wenzetu Mila zao zinaitwa Dini, marehemu wao (mizimu kwetu) wanaitwa watakatifu.

Na huu ujuzi wa kwamba mila na tamaduni hizi ni kuingia mikataba na shetani umeupatia wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom