In Edward Lowassa, I trust...

In Edward Lowassa, I trust...

GQ,

Burden of proof iko wako maana wewe ndiye unadai eti yeye ni Jambazi, Fisadi ana majumba mengi na mali nyingi. Tuletee basi hivyo vyeti vya umiliki vya mali unazodai ni za Lowassa ndipo defense counsel wawasilishe majibu 🙂

Nyerere alishaonesha mashaka juu ya Lowasa. Watanzania wengi pia tunamashaka na usafi wake. Mtu asiyeaminika ni hatari kumrudisha katika uongozi wa nchi. Kwanza kwa nini alijiuzuru uwaziri mkuu kama alikuwa msafi? Sisi tunafahamu kuwa bunge ambalo ni mwakilishi wa wananchi lilimwona anauhusiano na Richmond baada ya kufanya uchunguzi.
 
Ina maana hatuhitaji mtu muadilifu?

Naona mapepo yamewaingilia watu hapa. Lowasa si alikuwa waziri mkuu. Na katika kipindi cha miaka miwili alichofanya ni kitu gani zaidi ambacho sasa hivi watanzania wanaki-miss???
 
labda mvua yake ingesaidia wakati huu wa mgao kujaza kina cha maji. napenda kujuwa katiba ya tanzania inasemaje kuhusu pm toka upinzani? maana upinzani wako nako waofaa, kama Zitto,Slaa,Mrema,Lipumba,Seif na wengineo.
 
Labda niseme hivi nieleweke.

Tatizo la Tanzania si Ufisadi, bali ni sisi watu wenyewe, tu wavivu, magoigoi na tumeridhika mno na mambo ya ajabu ajabu ambayo Serikali imelala kabisa.
Hapo pana ukweli kabisa. Tunategemea miujiza badala ya kujituma na kutumia mida wetu vizuri
Si siri kila Mtanzania ni fisadi kwa namna yake moja au nyingine. Leo watu wanatoa rushwa kama ni haki yao kutoa rushwa na ni jambo la kawaida ili wapate leseni au kibali cha gari.
Hili pia wengi huwa hatutaki kulikubali ingawa ndio ukweli halisi kuwa rushwa zipo kila angle ya maisha ya watanzania. Ukiendesha gari, ukiingia hospitali, bandarini, airport, kwenye biashara etc
 
rev.nakuunga mkono,
na ukitaka kujua bongo hakuna kichwa kama lowasa linapokuja suala la utendaji,angalia majibu kwenye posts zote hizi watu hawatoi mbadala wa lowasa,yaani hawamtaki tu kwasababu hawamtaki,ila hawana mbadala,kama wangekuwa nambadala wangeitikia mwito wako wa kusema mtu aseme anaemwona anafaa,
lowasa ni kifaa angalau kwa nchi yetu hii ilipofikia,tunahitaji mtu atakaetoa amri na watendaji wake wakajua anamaanisha anachosema,nani kama lowasa kwa sifa kama hiyo kwa sasa,watu hapa wamebaki kujadili sijui kaiba,nani hajaiba?hata tufanye nini hatuwezi kupata rais malaika,lazima atatoka miongoni mwa sisi binadamu tu,ndivyo Mungu alivyoamua,alitupa nchi tuzitawale wenyewe,
wengine hapa wanaojifanya kuujua uchafu wa lowasa ndio walewale walikuwa mstari wa mbele kutuamninisha jk alikuwa ndio chaguo la Mungu[labda kwakuwa sijui ni mungu yupi walimaanisha]
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Watanzania hawamuhitaji Lowassa labda uwe umepandwa pepo. Kuna vipimo vya maendeleo ya nchi kama vile GDP, debt ratio na mengine.

Vipimo hivi wakati wa Lowassa na wakati huu wa Pinda viko vilevile. Hivyo basi utendaji wao hauna tofauti.
 
Naona mapepo yamewaingilia watu hapa. Lowasa si alikuwa waziri mkuu. Na katika kipindi cha miaka miwili alichofanya ni kitu gani zaidi ambacho sasa hivi watanzania wanaki-miss???

Tuna-miss kupandisha mori katika kuchapa kazi na kufuatiliana usiku na mchana!
 
Naona mapepo yamewaingilia watu hapa. Lowasa si alikuwa waziri mkuu. Na katika kipindi cha miaka miwili alichofanya ni kitu gani zaidi ambacho sasa hivi watanzania wanaki-miss???
Zakumi,
Nadhani tatizo ni kwamba quality ya leadership in Tanzania has sunk so low that we are lowering the benchmark. Among the worst leaders we have Lowassa stands out as a better substitute.
 
Watanzania hawamuhitaji Lowassa labda uwe umepandwa pepo. Kuna vipimo vya maendeleo ya nchi kama vile GDP, debt ratio na mengine.

Vipimo hivi wakati wa Lowassa na wakati huu wa Pinda viko vilevile. Hivyo basi utendaji wao hauna tofauti.

Zakumi,

Pepo la uwajibikaji na kuchapa kazi limenipanda leo.

Nilikuwa nyumbani kwa wiki tatu, nikatalii nchi kwa kiasi fulani ili nijionee kile nilichokuwa nabezwa kila siku eti kubeba kwangu maboksi najua nini zaidi ya kutumia funguobao(keyboard).

What I saw in Tanzania ni Chaos, Disorder and Disorganization!

Hakuna efficiency, hakuna mwenye ku-demand accountability au kumhold mtu responsible, kila mtu anajifanyia anachotaka.

It is not about BOT statistics au zile za CIA factbook, bali ni reality on ground.

Watu wengi wana afya nzuri na uwezo wa kufanya kazi. Nilipoandika kuhusu Idlelism, watu walinijia juu, sasa kama ile ilikuwa ni kitu nilichokiona Dar, sasa nilipokwenda vijijini ndio zaidi. Wewe mtu akiamka asubuhi anaoga na saa moja na nusu anapuyanga kwenda kuunga Azimio la Kimpumu!

What we lack is decisive and strong leadership and Lowassa stands tall above all!

He can do it, I trust that he can deliver! It may not be the way we want it, and its impact will never be short term but long term!
 
Nyerere alishaonesha mashaka juu ya Lowasa..

mbona huyo nyerere hakuonesha mashaka kwa mkapa na alichofanya akiwa madarakani[kwa kubebwa na mbeleko ya chuma ya nyerere]mpaka leo tunamlaumu?ninachotaka kusema hapa ni kwamba hata nyerere pia alikuwa ni binadamu tu na pia alikuwa mwanasiasa,kwa hiyo akiwa kama mwanasiasa alikuwa na malengo yake na uamuzi wa kumkataa mtu na kumkubali mtu,sio lazima kila alichokikataa au kukikubali mchonga kiwe ndio reference point ya kila mkijadili ishu.mbona huwa hampigi debe kwa salim ambaye inajulikana mwalimu alimtaka tokea 1985?
 
rev.nakuunga mkono,
na ukitaka kujua bongo hakuna kichwa kama lowasa linapokuja suala la utendaji,angalia majibu kwenye posts zote hizi watu hawatoi mbadala wa lowasa,yaani hawamtaki tu kwasababu hawamtaki,ila hawana mbadala,kama wangekuwa nambadala wangeitikia mwito wako wa kusema mtu aseme anaemwona anafaa,
lowasa ni kifaa angalau kwa nchi yetu hii ilipofikia,tunahitaji mtu atakaetoa amri na watendaji wake wakajua anamaanisha anachosema,nani kama lowasa kwa sifa kama hiyo kwa sasa,watu hapa wamebaki kujadili sijui kaiba,nani hajaiba?hata tufanye nini hatuwezi kupata rais malaika,lazima atatoka miongoni mwa sisi binadamu tu,ndivyo Mungu alivyoamua,alitupa nchi tuzitawale wenyewe,
wengine hapa wanaojifanya kuujua uchafu wa lowasa ndio walewale walikuwa mstari wa mbele kutuamninisha jk alikuwa ndio chaguo la Mungu[labda kwakuwa sijui ni mungu yupi walimaanisha]

Naona mmejipanga kweli kweli. Lakini haisaidii... Huyo Lowassa tumeshamsahau. Tunajua yeye na rafiki yake Mburushi wamekusanya pesa ya kutosha ili kurejea, lakini bahati mbaya sana Mungu hapendi watu wake waingie utumwani. Kama mnampenda sana nendeni mkanywe naye kahawa. Sorry!
 
NAUNGA MKONO HOJA YA KUMREJESHA MADARAKANI MHE LOWASA!THE GUY WAS VERY CREATIVE!mradi wa maji Dar,kapigana na mkataba wa mkoloni kuchukua maji ya ziwa victoria sasa maji mpaka KAHAMA AKIWA WAZIRI WA MAJI,alifukuza city water kitu ambacho KAWAMBWA KASHINDWA KWA TRL,alianzisha njia TATU wakati wa foleni DAR.Ulinza shule za sekondari zilizojengwa kila kata mpaka makongoro mahanga anamshukuru kwani alijenga shule 38 za sekondari ukonga.LOWASA NA MAGUFULI NDIO VIONGOZI TUNAOWAHITAJI
 
Wewe kweli BONGOLALA...
 
Zakumi,
Nadhani tatizo ni kwamba quality ya leadership in Tanzania has sunk so low that we are lowering the benchmark. Among the worst leaders we have Lowassa stands out as a better substitute.

Performance Indicators zangu hazionyeshi kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri. Kiongozi mzuri ni lazima ajue kutumia resources zake vizuri na makini. Ujenzi wa shule za sekondari za kata ni kigezo kikubwa kuwa Lowassa hafai.
 
Mchungaji Kishoka,

Kama lengo ni kutuonyesha mtu mwenye ujasiri, ubabe, utashi, dhamira na udiriki, naweza kukubaliana na wewe. Ni kweli jamaa akiamua kufanya kitu hata kama ni ufisadi anahakikisha unakamilika, yatakayotokea mbele ya safari hayo hayajui.

Tatizo kubwa ni kwamba wananchi hatuna imani na Lowassa. Pamoja na kwamba hatuna ushahidi wa ufisadi wake, lakini na yeye alipoulizwa na Mwalimu Nyerere (RIP) mwaka 1995, alishindwa kujieleza chanzo cha utajiri wake na hata alipopewa nafasi ya kwenda Msasani kuonana na Mwalimu aliingia mitini (Ref. Barua ya Mzee Kasoli, iko hapa hapa Jamvini).

Yawezekana Lowassa ana sifa hizo ulizozitaja kwa kuwa zinamsaidia kufanikisha ufisadi wake na pia ana create fear kwa surbodinates wake ili wasije wakafungua midomo kuongelea ufisadi wake. Unajua ukiwa mbabe una create woga kwa surbodinates wako na hivyo unakuwa na surbodinates ambao ni akina YES SIR! Je, tunahitaji kiongozi wa namna hiyo?

Kwa mtazamo wangu Lowassa ni jamii ya Mkapa. Mkapa alitetea ufisadi wa ununuzi wa radar na ndege ya rais kwa nguvu zote pamoja na nchi wahisani kupiga kelele na kutushangaa. Only to find out that ilikuwa ni ufisadi na imekuwa hivyo kwenye mambo mengi sana, mengine mpaka yanatia kinyaa.

Zama za Mkapa mawaziri wote walikuwa mstari wa mbele kutetea deals kibao hata kama walikuwa wanaona kabisa kwamba hapa kuna harufu ya ufisadi. Mkapa akishasema hakuna waziri aliyekuwa anabisha, bali kwenda kutekeleza. Tulishuhudia akina Prof. Mwandosya wakitetea ununuzi wa radar, lakini leo ukiwauliza watasema hawakujua, si kweli, walijua lakini ubabe wa Rais uliwafanya wakae kimya.

NetGroup Solution waliingizwa pale ofisi za TANESCO kwa usimamizi wa FFU, pamoja na kelele zote zilizopigwa. Aliyesimama kuwatetea hao jamaa ni Mkapa huyo huyo mwenye ujasiri, udiriki, utashi na ubabe juu. Maokola Majogo aliondolewa Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwakataa NetGroup, akapelekwa Ofisi ya Makamu wa Rais ili akapumzike na baada ya hapo makaburu wakaingia kuendesha TANESCO.

I am saying, I dont have trust in Eddie. JK ana mapungufu yake, lakini kusema Lowassa ni bora, ni kujichimbia kaburi sisi wenyewe, esp, wale ambao ni walalahoi kama mimi. Matajiri watazidi kuneemeka pamoja na familia, sipendi kurudi kwenye zama za utawala wa Mkapa wa kibabe na ufisadi uliotukuka.
 
Wewe kweli BONGOLALA...

kwanini watu huwa hawapendi kujibu hoja aliyotoa mtu?
sasa mtu katoa maoni yake ya kwanini anaona lowasa anafaa,kataja na sifa za kuisimiamia hoja yake,badala kujibu hoja mtu unaishia tu kusema kweli bongolala,
ndio maana mimi nimesema watu wanaompinga lowasa[waliochangia mpaka sasa]wanaonesha hawana hoja,ila tu ni chuki waliyonayo kwa mtu,bia sababu wa la hoja ya msingi,watu wameamua tu kupinga,hawaoneshi mbadala,zaidi wanabaki tu kusema watu wanaomtetea lowasa ni mafisadi/wametumwa na mafisadi,as if lowasa ndiye baba wa mafisadi au ndiye fisadi pekee,na wapinzani wake kisiasa ni wasafi kama sufi,
mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni.
 
Back
Top Bottom