Nyangumi,
Maneno yako kweli tupu hata yule wa CUF aliyekuwa akisafirisha watu nje yalimkuta hayohayo leo vipi CCM bado wanawakumbatia hawa jamaa?...
Kutokana na hali hii naomba mtu afungue mada inayozungumzia BUNGE letu na yanayotokea huko ili watu wapate kufahamu kinachoendelea... leo hii ktk pita pita zangu nimeona kitu hiki ndani ya IPPmedia kidogo kinanipa tumaini kuwa ngoma hii bado kabisaaaa!..
Nimenukuu kipande hiki:-
Akinukuu kifungu cha 57(2)E, Spika alisema iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu, Waziri au Naibu Waziri naye anakoma kushika wadhifa wake.
"Sasa baada ya kuwa mheshimiwa Waziri Mkuu amemuandikia Rais barua kwamba anajiuzulu na jioni hiyo hiyo ombi lake kukubaliwa na kwa mujibu wa Katiba kwa kutumia kifungu hicho cha 57(2)E ni dhahiri kwamba Bunge hili sasa hatuna serikali.
Sasa waheshimiwa wabunge kwa kuwa serikali imebaki na Rais na Makamu wake ambao nao hawamo ndani ya Bunge, ibara ya 63 (2) ya Katiba inatamka kazi zetu kama Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, ikiwa ni pamoja na kuwahoji maswali Mawaziri lakini sasa hawapo,`` alisema Spika na kupigiwa makofi yaliyoambatana na vicheko.
Akizungumia hoja ya kujadili ripoti ya mkataba wa Richmond alisema: ``Kushauri huko ni pamoja na kuendelea kuyajadili haya mapendekezo ya kamati teule ili tukishauri yale yatakayokubalika wawepo wa kuyatekeleza� Sasa hawapo, kwa msingi huo natangaza kuahirisha Bunge nipate nafasi ya kushauriana na taasisi mbalimbali,``
Asubuhi bungeni jana, Bw. Lowassa, hakuonekana hali kadhalika Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika naye hakuonekana.
Hata hivyo, Bw. Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, walikuwepo. Baadhi ya Mawaziri walivikimbia viti vyao na kujiunga na wabunge wa kawaida kwenye viti vya nyuma.
Lakini kwa upande wake, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge ambaye ni mbunge wa Bariadi Magharibi mara baada ya kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge huku akijua kabisa hana tena wadhifa wake wa uwaziri, hakusumbuka kwenda kwenye kiti anachokalia siku zote ambacho kiko mbele. Badala yake Bw. Chenge alikwenda nyuma kabisa ya viti vya wabunge ambako hakuna viti akaamua kuketi chini ya zulia.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye, Bw. Chenge aliangaza na kubaini kuwepo kwa viti kadhaa vikiwa havina wabunge waliovikalia, aliinuka na kwenda kukalia kiti cha Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz ambaye hakuwepo ndani ya ukumbi.
Nje ya Bunge zilisikika dua zisemazo ``kaka, dada nakuombea Mungu, Mwenyezi Mungu atakurudisha. Tutakuona na safari hii utapanda ngazi.`
Asubuhi kabla ya kuanza kikao cha Bunge, Mawaziri `waliotimuliwa` waliingia eneo la bunge kinyonge, tena kwa miguu baada ya kuegesha magari yao binafsi nje ama ya serikali yaliyokuwa na namba za STK. Utaratibu uliozoeleka ni vigogo hao kuingia na `mashangingi` yao na kuyaegesha katika eneo maalum la magari ya viongozi.
Wengi hao walionekana wanyonge, wakitembea kwa makundi makundi huku wakijadili hili na lile, hali ambayo ilidhihirisha hofu ya kutemwa kwenye baraza jipya linalosubiriwa kwa hamu.
Haya haya Simba na Yanga uwanjani....fainali ndio hiyooooo!