In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Angalia usomi usikufumbe macho, I am not a lawyer and I am not talking legalese in case you are confusing my simple english with technical terms

Look up the word precedent


http://dictionary.reference.com/browse/precedent

Sio lazima kuwe na hukumu au tume iwe mahakama, hii tabia inaweza kuwa justified kwa sababu hii kamati ingawa si mahakama, ina nguvu za kimahakama ndiyo maana imeweza kuwahoji watu katika kiapo.Ni kamati ya bunge for gods sake, kamati ya watu wanaotunga sheria yenye nguvu za kimahakama!

Second, the word is rebuttal not rebattle.Ninaongelea ripoti kutompa nafasi Lowassa kujibu implications zilizomo katika ripoti hiyo kwamba Lowassa amehusika.Lowassa probably did not choose the confrontational route because he knows he is guilty, and he needed to save face, thus the front that he was not given a chance to clear himself.Understand that I am not advocating on Lowassas side, I am merely pointing out the weakness of Mwakyembe's prosecution that the report itself, which is supposed to contain solid facts, did not take the time to question Lowassa and get his of the story and legally speaking it is very much unbalanced.Kuna law and legalese (unachoongea wewe complete with Latin Maxims, halafu kuna "the spirit of the law" haya ni mambo yanayo transcend law na legalese na kwenda kwenye concept nzima ya rule of law, due process na fairness.Hata Mwalimu mkuu (ambaye si mahakama wala tume ya bunge) hawezi kuhukumu kesi ya wanafunzi waili kwa haki ikiwa kama hajamsikiliza mmoja, no matter the evidence presented.Ama sivyo itakuwa kulazimisha mambo tu.

Ukiiangalia hii move katika spirit ya rule of law Lowassa ana point.Ukiangalia justice utaona kufuata sheria kungeweza kutishia justice, Mwakyembe amemuonyesha Lowassa how the west was won gangsta style.

Mwakyembe anajua kudeal na watu wenye kuvimbisha vichwa kama Lowassa.
Kama una deal na watu wasiofuata utaratibu ukifuata utaratibu umekwisha. Urahisi na uhalali wa kudeal na watu hao ni kufuata njia wanazotumia wao kuwafanya watu wengine wajinga.

By pass them.

Hiyo rule of law unayoiongelea ni ipi?

"Ukiangalia justice utaona kufuata sheria kungeweza kutishia justice"

Hii sentensi imeshindwa kabisa kupanda ngazi kwenda upstairs
Nielimishe una maana gani?
 
Madela tatizo ni kuwa Punda alikuwa na kifaduro na inabidi tuwe makini kwani kesho keshokutwa kifaduro hiki kinaweza kutoka kwa punda na kumpata mtu.

Mimi nimefurahi mambo yalivyoenda, ningefurahi zaidi kama Lowassa angenyimwa hata kitu cha kujisema, maana sasa hivi anadai kuwa hakupewa nafasi ya kujieleza.

Mimi naongelea kesho keshokutwa kutakuwa na watu hawampendi mtu, watamuundia tume, kumframe na kumtoa madarakani bila hata kumpa nafasi ya kujitetea.
 
Kila mtanzania alipewa nafasi ya kujieleza, kutoa ushahidi au maoni yake. Na tuhuma hizi zililengeshwa kwake tangu mwanzo wa SCAM hii. Kama hakuitwa angechukua initiative ya kujisafisha.Kwa mtu kama Waziri Mkuu sifikirii kama alikuwa hajui yeye ni mtuhumiwa namba 1 kwa ushahidi wa kimazingira. Hivyo alipaswa asafishe hali ya hewa kama kweli alikuwa msafi.
 
Jamani mnaomtetea Lowasa mnatutonesha vidonda. Asanteni mlotambua kuwa tume haikumhukumu bali kumshutumu. Na kisheria kushutumiwa inaruhusiwa ili kukupa nafasi yakuweka kumbukumbu sawa. Lowasa alipaswa sasa kujibu shutuma na kuthibithisha kaeleweka vibaya tu ila ni mwema. short of that shutuma zimethibitika na sasa astahili hukumu. Msimamizi mkuu wa taratibu za kiutendaji za serikali na aloapa kuzisimamia akiweka mbele maslahi ya uma leo anatarajia tuwe wapuuzi kiasi gani kubariki ufisadi aloonyesha. Maswali yote tume ilojiuliza na kuyatafutia vielelezo, Lowasa angekuwa safi angeshayaundia tume na kuwasimamisha kazi wengi. Kwamba yaliendelea mpaka ilipofika mhh.

Ila lowasa mjanja. Aligeuza hoja iwe ni kumuonea wivu kuwa kawa waziri mkuu na hivyo akiutema uwaziri mkuu basi watu waridhike. Nooooo. Tunachotaka ni mali zirudi zilipostahili na yeye alodhalilisha taifa awahi anapostahili. Keeekoooo.
Kisingov
 
Kuna watu wanaoangalia mambo juu juu na kuwa swept na euphoria of the moment.Watu kama hawa ndiyo walipimgia kura Bush aende Iraq bila kusoma Patriot Act na leo wanajilaumu.


It happenned, this is good for the country.What would have been better for the rule of law is if Lowassa would have had a chance to present his case to the Mwakyembe committee before it was presented to parliament.This a simple matter of due process and rule of law, that every accused deserves a hearing.Lowassa did not get a chance to supposedly clarify himself.So lets stop kidding ourselves kwamba Mwakyembe did things A-OK, because he did not!

so, u think lowassa resigned because of bunge tume////

homework find out jk role since oct 2007, when lowassa was officially done.

also find out who paid 3.5 million usd to the us embassy to acquire that marine house along chole drive and what the cia wrote to jk. karibu mca isimamishwe kwa mambo ya el.

so this saga has so many angles.
 
so, u think lowassa resigned because of bunge tume////

homework find out jk role since oct 2007, when lowassa was officially done.

also find out who paid 3.5 million usd to the us embassy to acquire that marine house along chole drive and what the cia wrote to jk. karibu mca isimamishwe kwa mambo ya el.

so this saga has so many angles.


Tupe habari nzima ya hiyo $3.5M na nyumba ya Chole usitupe kiduchu.
Mwenyewe si umeona Bango letu JF linasema "Where we dare to talk openly?"


Lakini hili tu la Richmonduli linatosha kumpeleka Keko au Ukonga kwa miaka yote iliyobaki ya uhai wake.
 
Hapa naomba tuwe wazi kabisa...ukijaribu kuikosoa ripoti ya mwakyembe tafadhali uwe umeisoma ki-uhakika. Ndugu yangu ripoti inasema kwa hali inavyoonyesha kuna uwezekano mkubwa sana kwamba bwana mkubwa Lowassa alishiriki kwa njia moja au nyingine...na ile ni ripoti ya kamati teule...sasa yeye alichokimbia ni hiyo sehemu moja kwamba akutendewa haki kwa kutoitwa kuhojiwa.

lakini kwa nini angalau akugusia yaliyomo kwenye hiyo ripoti. Hiyo ripoti ina zaidi ya kurasa mia na imegusia maeneo mengi sana. Kwa hiyo tungemuelewa kama yeye angesema kwamba kwa kuwa yeye ni kiongozi wa ngazi ya juu serikalini anaona kwamba yaliyoibuliwa kwenye ripoti ya Mwakyembe ni ya muhimu na kwamba inabidi yafanyiwe utafiti wa kina ili kkupata ukweli kabisa...na angemalizia kwa kusema basi naona tume haijamaliza kazi yake naomba ije inioji ili tupate ukweli....

Mimi sikubaliana kabisa na hoja za utetezi zinazotolewa hapa...hasara ni kubwa inayolipata Taifa na wanaohumia ni wananchi wa hali ya chini....sioni haja ya kumtetea...aende akale hizo pesa ambazo ameiba lakini ipo siku haki itachukua mkondo wake...

Tusitetee kila kitu bwana....
:confused:
 
Mwakyembe anajua kudeal na watu wenye kuvimbisha vichwa kama Lowassa.
Kama una deal na watu wasiofuata utaratibu ukifuata utaratibu umekwisha. Urahisi na uhalali wa kudeal na watu hao ni kufuata njia wanazotumia wao kuwafanya watu wengine wajinga.

By pass them.

Hiyo rule of law unayoiongelea ni ipi?

"Ukiangalia justice utaona kufuata sheria kungeweza kutishia justice"

Hii sentensi imeshindwa kabisa kupanda ngazi kwenda upstairs
Nielimishe una maana gani?

Madela the beauty of your posts ni kwamba una capture wisdom kwa statements fulani very simple

Kama una deal na watu wasiofuata utaratibu ukifuata utaratibu umekwisha. Urahisi na uhalali wa kudeal na watu hao ni kufuata njia wanazotumia wao kuwafanya watu wengine wajinga.

Hapa umemaliza mkuu, Mwakyembe hakufuata process lakini angefuata asingefika alipofika.Ndiyo maana nimeandika countless times before, the end justifies the means.

Kuhusu law and justice, law ndiyo inayomfanya mafia crook aliye fanya ushenzi a get away with it kwa sababu hamna evidence, justice goes beyond the law, and it rewards everyone according to their deeds.
 
bugurunikwamnyamani

Naona JF kama kawaida yetu tumeingia na vigele gele wakati ukweli ni kuwa MWAKYEMBE kama mwanasheria anajua fika kuwa kulikuwa na umuhimu wa kumhoji mtuhumiwa mkuu katika hili skendo bwana LOWASSA lakini hakufanya hivyo

Huu si uzushi wala nini na LOWASSA mwenyewe alisema hilo katika hotuba yake

sasa guys lets take a back seat and look at huyu MWAKYEMBE na kamati yake walikuwa wanajaribu kuficha nini ? huwezi kuendesha mambo haya based on emotions na kwangu naamini kuwa one is innocent till proved otherwise na in this case Lowassa hakutendewa haki. Simpendi na sina ulazima wa kumpenda lakini haki yake mpeni

Hebu soma majibu aliyopewa waziri mkuu mwathirika bungeni kutoka kwa Mhe Seleli
 

Attachments

  • seleli.doc
    2.9 KB · Views: 96
JE NANI ANJUA KIREFU CHA RICHMOND?

RICH stands for RICHARD
MOND stands for MONDULI

kazi kwenu sasa
 
so, u think lowassa resigned because of bunge tume////

homework find out jk role since oct 2007, when lowassa was officially done.

also find out who paid 3.5 million usd to the us embassy to acquire that marine house along chole drive and what the cia wrote to jk. karibu mca isimamishwe kwa mambo ya el.

so this saga has so many angles.

Lowassa resigned so that more dirt should not be dug up on him.
 
Pundit,
samahani mkuu lakini unapozungumzia Law na Justice unakuwa unatuchanganya kidogo kwani Bungeni kuna sheria zake na utaratibu wa bunge ni tofauti kabisa na utaratibu nje.
Ebu nikuulize wewe imekuwaje siku hiyo Lowassa afike Bungeni na mkewe? lini waziri mkuu aliwahi kuja bungeni na mkewe na alifika hapo kwa mwaliko wa nani hata aangushe kilio!... mjomba EL aliyajua yote mapema na alikuwa na muda mrefu wa kujisafisha kabla hajafikia kujiuzuru..
Nitakupa mfano wa scandal moja ya Watergate kama unaikumbuka vizuri.. kulikuwepo na report mbili za FBI na pia Senate Watergate Committee's staff investigators ambao wote hawa hawakumhoji Nixon ktk uchunguzi wao isipokuwa baada ya kuwakilisha report zao Kamati maalum ilichaguliwa na Senate kwa madhumuni ya kuwahoji mashahidi, investigator na Nixon mwenyewe on Presidential Campaign Activities. Yaani baada ya kuwakilishwa report na kupitiwa hapo ndipo Nixon alikuwa mtuhumiwa. Baada ya senate kuangalia mapendekezo ya nyaraka zote mbili toka FBI na SWCSI ambao wote walihojiwa pia na kamati maalum iliyofuatia.
Kwa hiyo ilitakiwa Lowassa asubiri Bunge litoe uamuzi wa kuhoji uchunguzi mzima kuwaita wahusika wa pande zote kama kweli alitaka haki na hiyo neutral justice. Lakini kabla ya Spika hajazungumza kitu mjomba kesha andika barua kwa rais yaani hapo aliposimama alikuwa anawataarifu tu hatua alizozifanya tayari. Kaamua kujitoa uwaziri mkuu kutokana na hizo alizoziita tetesi na minong'ono. How can a Prime minister resign his position based on rumors?.. come on then, ni nani mbaya wetu kama kweli huyu mjomba anaipenda nchi yake. Unapojitoa hali unafahamu kabisa kuwa wewe huna makosa sii kuitakia mabaya nchi yako unayodai kuipenda?...Je, si kweli kuwa kutuachia mchawi ndani ya serikali ikiwa madai yake yana ukweli?...Kilio chake cha kuipenda CCM na nchi yake ni bure na tutakuwa wendawazimu kama tutashirikia na baadhi vichaa wa CCM ambao wanampongeza ati kwa kujiuzuru.. Mnampongeza kitu gani na kumwita jasiri hali mtu huyu ni mhujumu uchumi??. Je, mbona sikuwasikia hawa hawa wabunge kina Mongella wakimpongeza Mzee said Mamwindi aliyemuua Dr. Kyaruu na kujisamisha yeye na silaha alotumia?... na kwa nini walimnyonga hali ujasiri wa kukubali makosa unapongezwa bungeni!... Ga damn it!
samahani mkuu sikuwa namaanisha wewe bali hao Mawaziri wabunge ambao bila aibu wanampongeza FISADI...
 
Mzee said Mamwindi aliyemuua Dr. Kyaruu na kujisamisha yeye na silaha alotumia?... na kwa nini walimnyonga hali ujasiri wa kukubali makosa unapongezwa bungeni!...

MKANDARA umenitonesha kidonda inabidi kuanzishwa na topic nyingine kuhusu hio issue
 
MMASAI,
Inaudhi mkuu wangu hawa jamaa wanampongeza mtu kama huyu..hali Richomnd toka waingize mitambo yao ni mwaka sasa hivi na tunalipa milioni 152 kwa siku!.. Haya tazama hizo cost za uchunguzi ambazo zimewapeleka watu hadi US na kadhalika wamwite jasiri hali angekuwa kama Mwamwindi ambaye khakuchelewesha uchunguzi alijisalimisha siku ile ile..at no cost!...Hivi kweli hawa watu wanaipenda nchi tyetu?
wanajutia gharama zilizotufika ama ndio mchezo kwao umekwisha!
Ama kweli hatuna wabunge nadhani ipo haja ya kusimamisha bunge na kuanza uchaguzi mpya!...
 
..naona spin machinery imeingia JF lakini this time haitasaidia.EL ni millionaire mkubwa sana tena kaupata kwa njia za ufisadi na ingekuwa nchi za wenzetu angekuwa anaelekea jela kwa miaka mingi sana lakini bahati yake JK ndio amemalizana naye hapo,sasa aingie mtaani wakaibiane na mamilionea wenzake kina Rostamn aziz...mtu ananunua nyumba ya 3.5m$ unafikiri ana pesa kiasi gani?
 
" Kweli ni huzuni, kwa kuanguka kwake morani, kulipotokea pale bungeni, akasema moyoni, nafukuzwa kazi kwa uzushi, akalia kwa huzuni, hata mwisho akachoka, pale juu kizimbani akabwaga nyanga kwa huzuni"!
 
opinion poll ya JK imepanda juu ajabu....anashangaliwa sana...sasa jamani nilishasema hapo mwanzo hakuna nchi rahisi kutawala kama bongo...yaani wananchi hawaangalii mbali..hawajiulizi maswali je Mkuu Muathirika atafanywa nini au itakuwa kama zamani ameboronga, ameiba case closed?go to your ranch leave like a king na walinzi wawili FFU na afisa usalama wawili and us tax payers will pay the bills.

Kiti si muhimu mimi nitaka kujua serikali yetu itafanya nini kuhusu yale mapesa yetu.

Kampeni ya sasa tunataka pesa zetu...mnajua leo watu wengi hapa bongo wameshasahau Buzwagi.BOT.KIWIRA..... JF jamani ALUTA CONTINUA
 
Hii Spin ya kuwa Lowassa hakutendewa haki is stale! Commission si mahakama, na aliulizwa maswali hakujibu. He knows he is guilty na afadhali akae kimya.

Hata mimi nimekereka mno na sifa walizomwagia Fisadi Mkubwa EL! Ni aibu kubwa sana!
Hizo opinion polls kwamba JK kapanda chati ni ujinga tu! Mitaani watu wanasema wanataka akina Lowassa wakamatwe na wafilisiwe! Labda wahame nchi! Lakini tutawabana hapahapa!
 
Lowassa!!! huyu mtu nadhani jeuri ilimponza sana.Hii issue ya Richmond alikuwa na muda mzuri tu wa ku deal nayo kabla haijalipuka.Since 2006!
Yeye kama PM,angeweza sana kuibomoa kidogo kidogo mpaka ikaisha kabisa.Cha ajabu ni kwamba yeye alijua kwa kuwatumia PCB watamaliza hii issue,na yule bwege akaenda mbele ya waandishi wa habari kusema kuwa mkataba wa Richmond ni safi,na hauna athari zozote kwa taifa hili.Wote wakajua kuwa sasa basi,na mjadala umefungwa!
Huku nyuma kwenye one of the threads humu,ilisemwa kuwa issue ya Richmond ilikuwa raised na Anna Abdallah kwenye kikao cha NEC au CC,sina uhakika,na wajumbe waliambiwa kuwa mhusika ni yeye,Lowassa. Nasema kuwa Lowassa ni jeuri,kwa sababu within a year alikuwa tayari kajijengea maadui wengi sana within chama na serikali,na mmoja wa hao ni Spika ambaye yeye Lowassa kwa kushiriakiana na Rostam Aziz walikuwa wanafanya mpango awe impeached.
KWa mtazamo wangu,ile tume ya Mwakyembe ilikuwa ni matokeo hayohayo ya uadui alionao na Sitta.Tutakumbuka kuwa Chenge alijaribu kufanya bila mafanikio ile report isisomwe,akitoa sababu kuwa miswaada ya serikali inatakiwa kusomwa kwanza,na wale walikuwa wameshapandikiza watu wao,na hio miswada ingekuwa dragged on mpaka kufunga bunge(mtazamo wangu).I'm sure kama spika angekuwa ni Anna Makinda siku ile wangemburuza tu na hio,lakini Sitta akaitupilia mbali,na wakina Lowassa wakapigwa na butwaa!
Sasa yule baba,angekuwa ni mtu mwenye busara,ile hotuba yake ya kujitetea asingesema yale aliyosema ya kuanza kuwa-acuse wakina Mwakyembe,yeye angejitahidi atoe an emotional kubwaga-manyanga speech ili aondoke somewhat gracefully,matokeo yake aliyoyasema yamezidisha chuki kutoka kwa wananchi.
Msabaha ndie pekee aliyesema ya maana.
Huyu PM(kwanza hata sijui ataitwa nini,maana sio mstaafu)kajitia aibu yeye,familia yake,pia kamtia aibu kubwa sana bosi wake ambaye against many wishes,hata predecessors wake he still chose him as his PM in 2005.Within a year ya uPM wake,jamaa alishajiingiza kwenye dili.Sasa basi bora hata hio kampuni ingekuwa ni kubwa inayoeleweka,lakini kampuni ambayo inashindwa hata kumkatia ticket ya ndege director wake kwenda South Africa!
Yatasemwa yooote,lakini the guy has simply disgraced himself,mimi ningekuwa yeye,ninge-dye zile mvi sasa hivi tu.Kama hizo pesa bado anazo,basi azile na zimtokee puani,lakini tumshukuru kwa kitu kimoja,kwamba sasa ukii-Lowassa hii nchi,people with real interests at heart for this country will maul you!
 
hayo ndiyo majibu ya LOWASA

mwakyembe hajaeleza kwa nini hakumhoji huyu mtuhuimiwa mkuu na hiyo ni fault

kama unazo barua weka na si kutishia

Unafikiri angehojiwa ripoti ingetoka kama hiyo. Ingepelekwa hospitali na kutibiwa na kutoka kitu tofauti kabisa. Mwakyembe ni mwanasheria na anajua anachokifanya. Bora anyamaze, yaishe kuliko kumgeuza geuza nyoka wakati unajua kuwa huyu ni nyoka na hana miguu.
 
Back
Top Bottom