IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!

IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!

Kwanza wewe uangalie Tanzania wanakopa kwa matumiza gani halafu tazama IMF wanasemaje:

"...the Bank of Tanzania’s reserve money targets were met and foreign commercial borrowing was kept well within program limits..."

Nlikuwa nakuhurumia lakini sasa naanza kukuogopa! Itabidi meya wa jiji atusaidie kufanya uchunguzi wa mfumo wako wa kufikiri. Mimi nina wasiwasi kwamba unatumia tekn0logia nyingine kwenye kufikiri, siyo ile aliyosema mheshimiwa Masaburi.
 
Nna uhakika kuwa huelewi kilichoandikwa hapo kwa Kiingereza, hilo ndio tatizo lako kubwa.
 
Faiza,

Unaijua Capital account position ya Britain , Germany na USA hebu lete figures basi tulinganishe na current account deficit yao halafu tulinganishe na Tanzania yetu.
 
Ni wapi hapo, wacha.

wewe akili yako siyo nzuri. soma hapo kwennye red halafu ukalawle ishakuwa usiku sasa.

Tanzania, kwa sasa tunafanya vizuri sana katika uchumi na dalili zote zinaonesha tutaendela kufanya vizuri, tunaona Gas, Oil zinavyochangamkiwa, viwanda vipya, uzalishaji wa chuma, na mengine kadha wa kadha, mambo ambayo ni ndoto ya kila mwenye kutaka neema katika nchi yake, yote yanafanyika ni nini kinawasumbuwa? mawazo mgando?
 
wewe akili yako siyo nzuri. soma hapo kwennye red halafu ukalawle ishakuwa usiku sasa.

Mkuu,

Huko unakoenda sipo kama mtu ana msimamo wake muheshimu tu haina haja ya kutukanana unachafua hali ya hewa mzee. Tuheshimiane ili mjadala uwe mzuri tukianza matusi tutaelekea kubaya ndugu yangu. Gentlemen usually say we agree to disagree.
 
ndugu zangu sasa tatizo liko wapi? serikali ? wasomi wetu ? au sisi wananchi? maana naona nyingi ni lawama tu bila solution
 
Wataalam

  • Tunaweza kusema hizi iissue zinatokana na extenal factors zaidi na si internal factors?
  • Kwa nini hakuna uhusiano wa Thamani ya dhhabau na kupanda au kushuka kwa shilingiVs Dollar? Value ya Tsh yetu inategemea nini?
  • Uchumi wa Tanzania unategemea au unadeshwa na sekta ganii kuu japo mbili au tatu ?
 
Mkuu,

Huko unakoenda sipo kama mtu ana msimamo wake muheshimu tu haina haja ya kutukanana unachafua hali ya hewa mzee. Tuheshimiane ili mjadala uwe mzuri tukianza matusi tutaelekea kubaya ndugu yangu. Gentlemen usually say we agree to disagree.

mkuu kama nimetukana mahali 'report abuse'. au hauoni hicho ki-button.

mimi najiheshimu bana usiniletee uchuro mkuu wangu.

samahani sana.
 
wewe akili yako siyo nzuri. soma hapo kwennye red halafu ukalawle ishakuwa usiku sasa.

Ama kweli huna hoja, wewe unajuwa kuchimba mafuta? una zana za kuchimbia mafuta? kama Serikali haijachangamka kuwaleta watafutaji na wachimbaji utachimba kwa kucha? unanchekesha!
 
ndugu zangu sasa tatizo liko wapi? serikali ? wasomi wetu ? au sisi wananchi? maana naona nyingi ni lawama tu bila solution

Tatizo ni watu wanaozuwa namna hii:

"Nimesikiliza taarifa ya saa 2 TBC 1, maafisa wa IMF walikuwa na mazungumzo na maafisa wa BOT wakatangaza kwamba serikali imeishiwa. "

Ukiisoma ripoti ya IMF ni tofauti na hayo. Kama si uzushi usiokuwa na maana ni nini?
 
Faiza,

Unaijua Capital account position ya Britain , Germany na USA hebu lete figures basi tulinganishe na current account deficit yao halafu tulinganishe na Tanzania yetu.

Mdondoaji hata iweje leo hii huwezi kuilinganisha na "capital" ya hizo nchi na Tanzania lakini hapa tunaongelea "deficit" na kumbuka kila unapokuwa na "Capital" kubwa ukiwa na "deficit" nayo itakuwa kubwa.

Mfano bajeti billion 100, matumizi yako billion 108 hicho ni kiwango chako cha asilimia 8 deficit, ni billion 8 tu. Lakini unapokuwa na bajeti ya billion 1000 ukawa na "deficit" ya asilimia 3 tu, tayari unaongelea billion 30, kwa hiyo dificit ni deficit kiwa tajiri au maskini tena ina "impact" kubwa kwa tajiri kuliko maskini. Linganisha billion 30 na billion 8, tena hiyo ni asilimia 3 tu, sasa chukua Uingereza bajeti yao na asilimia 13 ya "deficit" halafu tazama ni kiasi gani hicho.

Nna uhakika umenielewa.
 
inanikumbusha Ugiriki, hapa kilicho bakia ni nchi itangaze kufilisika, ila kuhusu matumizi watafunguka mda c mrefu,

wakitangaza kufilisika watangazetna matumizi yaliyopelekea kufilisika alafu ukiwaulza kuwa nchi imefilisika watakanusha yle wakubwa wameshasay
 
Tatizo la serikali kukosa fedha linazidi kujidhihirisha tena katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kama ilivyokuwa kwenye mitihani ya Taifa kidato cha Pili iliyoanza leo semina kuendesha bila hata chuba ya maji ya 200, chai na chakula. Wakuu wa shule na wasimamizi wasaidizi kusimamia bila serikali kutenga bajeti yoyote ya malipo kwa shule za sekondari. Kituko kingine kiko kwenye mitihani ya Taifa Darasa la Nne. Katika mitihani iliyokuwa ikisambazwa jana na maafisa kutoka idara ya elimu ya msingi katika halmashauri mbalimbali, waliwaeleza walimu wakuu kuwa ndio watakao simamia badala ya walimu waliokuwa wakichukuliwa toka shule tofauti na wafundishazo. Wameambiwa kila mwalimu mkuu abadilishane na mkuu mwenzake wa shule ya jirani. Waliambiwa kuwa seriakali haijatowa fedha za kuwasafirisha wala za kuendesha semina ambazo huambatana na kula kiapo cha kutunza siri za mitihani kama sheria inavyotaka. Mwalimu mkuu mmoja anayefundisha shule wilaya moja iliyopo mkoani Morogoro alieleza kuwa wameambiwa watajilipa pindi pesa itakapotolewa na serikali ya ruzuku kwa shule zao, aliendelea kupasha kuwa hiyo ni danganya toto. Afisa aliyekuwa kwenye msafara wa kusafirisha mitihani hiyo alipasha kuwa hata wao hawakupewa pesa yoyote zaidi ya kuambiwa malipo yatashughulikiwa baadae "tunaomba gari isipate hitilafu turudi mjini salama la sivyo tunaweza kufa njaa". Mpaka JK amalize muda wake tutafika kweli jamani? siku nazo hazikimbii.
kweli THE TANZANIA WE WANT KIZAZI HIKI KWA MFUMO HUU KUTAKUA HAKUNA CHA KUJIVUNIA(CCM POLITICS +MAMBO YA MUHIMU KAMA ELIMU,AFYA NA UCHUMI=KUCHOTA MAJI KWA KIKAPU,
 
Iliyofilisika si serikali bali watanzania wanaolea CCM pamoja na kutenda makufuru yote. Kama umma hautaamka na kudai nchi yao watauzwa kwa shilingi mbili ili wezi wenye madaraka waendelee kutanua. Wakati nchi inafilisika, rais Vasco da Gama ndiyo anazidisha safari nje na kutanua mikoa wilaya na wizara. Hivi huyu jamaa ana akili au tunatawaliwa na chizi wa kawaida asiyejua kinachoendelea. Nisionekane natukana. Ni Tanzania pekee ambapo nchi inaweza kukaa kizani kwa mwaka na kuamua kulipa mabilioni kwa waliosababisha kiza na wananchi wakazidi kunyamaza. Hakuna nchi taahira duniani zaidi ya Tanzania so to speak. Heri serikali ifilisike maisha yawe magumu huenda watu wetu wataamka toka kwenye kuishi kizani kwa matumaini yasiyo na maana. Je ni kwanini watu wetu hawapambani na serikali dhalimu au nao madhalimu kivyao vyao?
 
Kwanza wewe uangalie Tanzania wanakopa kwa matumiza gani halafu tazama IMF wanasemaje:

"...the Bank of Tanzania’s reserve money targets were met and foreign commercial borrowing was kept well within program limits..."
tunapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa jimama ili tuendeleze kuachia maeneo ya uchimbaji madini bure jimama
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!
It's Marekani and not Merekani. Wewe ndio unachekesha tena bigtime unalinganisha uchumi wa United States of America na Tanzania?!! fanya research kabla hujaandika. Tz. tupo katika hali mbaya kupita maelezo hilo linaeleweka sasa usichokiona wewe ni kipi? Waliopo ndani na nje ya Tz. wanaliona hilo
 
tunapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa jimama ili tuendeleze kuachia maeneo ya uchimbaji madini bure jimama

Hayo yashaachiwa zamani na Mkapa, sasa turekebisha tu , kama alivyofanya Kikwete, juzi wametangaza kutoka Australia wanaanza kulipa kodi, na wale wengine wameshaanza mwaka huu.

Sasa na wewe si ukachimbe na kucha.
 
It's Marekani and not Merekani. Wewe ndio unachekesha tena bigtime unalinganisha uchumi wa United States of America na Tanzania?!! fanya research kabla hujaandika. Tz. tupo katika hali mbaya kupita maelezo hilo linaeleweka sasa usichokiona wewe ni kipi? Waliopo ndani na nje ya Tz. wanaliona hilo

Sikiliza kijana, uchumi mkubwa unapotetereka athari zake ni kubwa sana kuliko kauchumi kako ka Tanzania. Na pia kumbuka Tanzania uchumi wetu ni mzuri kwa sasa, hilo usiwe na wasiwasi nalo. Mambo mema yote yanajionesha waziwazi.

Point hapa i hiyo habari ya Post #1 na ukweli kama ulivyooneshwa kwenye ripoti ya IMF ni vitu viwili tofauti.
 
Iliyofilisika si serikali bali watanzania wanaolea CCM pamoja na kutenda makufuru yote. Kama umma hautaamka na kudai nchi yao watauzwa kwa shilingi mbili ili wezi wenye madaraka waendelee kutanua. Wakati nchi inafilisika, rais Vasco da Gama ndiyo anazidisha safari nje na kutanua mikoa wilaya na wizara. Hivi huyu jamaa ana akili au tunatawaliwa na chizi wa kawaida asiyejua kinachoendelea. Nisionekane natukana. Ni Tanzania pekee ambapo nchi inaweza kukaa kizani kwa mwaka na kuamua kulipa mabilioni kwa waliosababisha kiza na wananchi wakazidi kunyamaza. Hakuna nchi taahira duniani zaidi ya Tanzania so to speak. Heri serikali ifilisike maisha yawe magumu huenda watu wetu wataamka toka kwenye kuishi kizani kwa matumaini yasiyo na maana. Je ni kwanini watu wetu hawapambani na serikali dhalimu au nao madhalimu kivyao vyao?

Hujawahi kuiona Serikali iliyofisika usingesema hayo. Ulikuwepo wakati tunapanga foleni ya unga wa njano wa msaada kutoka Merekani? ulikuwepo wakati tunavaa vitambaa vya "kirimplini"? ikiwa joto mpaka unaisikia inaungua mwilini, ikiwa baridi inaongeza kibaridi.

Hujawahi wewe kukesha kwenye foleni ya sukari, halafu unakuta wenzako wamepanga mawe kukuwahi na ukifika zamu yako unakuta kumbe sio sukari ni foleni ya mafuta ya nazi.

Hii nchi kijana, ilifilisika wakati wa Nyerere, tulikuwa wote kama wagonjwa kwa kukosa lishe bora.

Gilasi za kunywea maji hakuna madukani, tunatumia vifuu. Hujaiona wewe Serikali iliyofilisika na utajiri inao.
 
Back
Top Bottom