IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!

IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!

Kuna msomi mmoja anaitwa walter Rodney aliaandika kiatbu chke zamani sana na nasikia alifundisha pia UDSM. Pamoja na kitabu kuwa outdated kitarehe, aliyoyaandika yamesimaa hadi sasa jana na juzi.

Ni sababu mojawapo kwa nini hata tukiwa na Migodi 20 ni Wacanada, Waustralia na na waisrel ndio watafaidika. Hata yakipatikana mafuta Ni BP and the likes ndio watafaidika. Sasa ukichanganya na mikataba mibovu na ubinfsi wa baadhi ya viongozi wetu.........
...... It is typical of underdeveloped economies that they do not (or are not allowed to) concentrate on those sectors of the economy which in turn will generate growth and raise production to a new level altogether, and there are very few ties between one sector and another so that (say) agriculture and industry could react beneficially on each other.

Kama hata kiwanda cha baiskeli hatuna, Laini tunakuwa mahodari wa kuagiza ma VX , kama hata maziwa ya ng'ombe tunaagiza kwa pesa za kigeni kwa kisingizo cha soko huria, Kama hata Nyama ya Kuku na mayai na hata nyama ya Ngome nayo kwenye supermareket ni za kugazia hatuwezi kutoka.....
....Furthermore, whatever savings are made within the economy are mainly sent abroad or are frittered away in consumption rather than being redirected to productive purposes

Bigest industry kwenye nchi kama Tanzania ni Administration. Pesa Nyingi zaidi inakwenda kulipa wabunge, walimu,wahasibu na watoa huduma . watu wachache wako wenye sekta hasasa za uzalishaji. Na hao wazalishaji hasa Kilimo kwanza bao ni siasa ......So ni sisi tulio mijini wavaa tai ni mzigo.
...Much of the national income which remains within the country goes to pay individuals who are not directly involved in producing wealth but only in rendering auxiliary services-civil servants, merchants, soldiers, entertainers, etc.

Mfano huu ndio wasi wasi wangu zile ahadi za kisiasa za za ajira milioni bili na nyinginezo bila kuzingtia mambo ya msingi zimeongeza mzigo
.........What aggravates the situation is that more people are employed in those jobs than are really necessary to give efficient service; and to crown it all these people do not reinvest in agriculture or industry. They squander the wealth created by the peasants and workers by purchasing cars, whisky and perfume.

Ingawa hizi ni takwimu za zamani na si za tanzania lakini huu fano wa matatizo halisi tuliyoanyo.Na mbaya zaidi tunarudi kule kule . bunge anazidi mshahar Afisa elimu wa mkoa au Afisa Kilimo wa Mkoa au Mganga Mkuu wa Mkoa. Ours is a political driven economy
It has been noted with irony that the principal ‘industry' of many underdeveloped countries is administration. Not long ago, 60%, of the internal revenue of Dahomey went into paying salaries of civil servants and government leaders. The salaries given to the elected politicians is higher than that given to a British Member of Parliament

Badala ya kudeal na issue kila kitu siasa.Mfano huu dhaihiri wa ratio ya mbunge per wananchi upo hata zanzibar . M tu anakuwa mbunge kwa kura 8,000. Kwa nini tuna majimbo mengi ya kisiasa wakati matatizo yetu ni hata ukiunganisha mikoa au mikao mitatu ni yale yale common, elimu, afya, maji, kilimo, Nihshati?
....the number of parliamentarians in the underdeveloped African countries is also relatively high. In Gabon, there is one parliamentary representative for every 6,000 inhabitants, compared to one French parliamentary representative for every 100,000 Frenchmen.
 
"Deficit" ni tatizo tu pale ambapo lina "impact" growth, ili upate faida inabidi uwe na "deficit" mwanzoni, kila unachokiingiza nchini iwe ni bidhaa au mkopo unahisabiwa kama "value" iliyoingizwa nchini. Hiyo "impact" haiwi kubwa pale inapoonekana kuwa "measures" za kuikabili "deficit" zipo na ndio maana ukaona hiyo sentensi ya mwisho "Structural reforms are moving forward, notably to strengthen debt management capacity."

Ni kama vile leo umenunuwa kiwanda cha kuzalisha bidhaa, kwenye hesabu yale matumizi na "depreciation" yanaonekana ni hasara mpaka hesabu zitapo "break even", kwa mfano huo tazama kwa kipindi hiki cha miaka mitano iliyopita Tanzania imewekeza kwenye nini na nini au "activity Drivers", jee, kutakuwa na faida katika huo uwekezaji? Ndio. Ndio maana ukaona hiyo niliyoweka blue. Ikiwa hamna hizo "activity drivers" unawekewa vikwazo na IMF mpaka wakupe masharti mapya kama tulivyowekewa 1997 na IMF, tulikuwa hatuna "activity drivers" zozote.

Je nikuulize Sie tunakopa kwa ajili ya kuwekeza au tunakopa kufidia mashimo ya bajeti? Vile vile nikuulize Our economic growth rate is 6.3% and rate of inflation is 17% Je growth ya tanzania inatokea wapi? Hebu tupe mchakato wa hizo activity drivers zinazosukuma uchumi kukuwa by 6.3% na vile vile kuweza kumanage debt kama unavyofikiria wewe. IMF wamesema hivi na nanukuu:-

"Under the PSI program through June 2011, the Bank of Tanzania's reserve money targets were met and foreign commercial borrowing was kept well within program limits. However, partly due to the shortfall in commercial borrowing, domestic financing of the budget was higher than planned and the target for accumulating net international reserves was missed. Structural reforms are moving forward, notably to strengthen debt management capacity.

"Discussions during the mission focused on ensuring that public spending does not exceed the available fiscal space; setting the right policy mix for reducing inflation; and the financial implications of Tanzania's emergency power plan.

"It was agreed that the budget deficit in 2011/12 should be allowed to exceed the earlier programmed level (6 percent of GDP) to help finance the emergency power plan and accommodate expanded social spending. At the same time, savings will be implemented in non-priority programs, ensuring that the deficit is reduced from year-ago levels to around 6½ percent of GDP. This fiscal tightening will also help the disinflation effort.

"The authorities intend to pursue prudent fiscal policies in 2012/13 and beyond to stabilize Tanzania's rising public debt, projected to end this year at close to 42 percent of GDP. The government has agreed that recurrent spending in the 2012/13 budget should not exceed the financing provided by revenues and grants. This will require continuing efforts to prioritize spending and/or increase revenue collections.

"The authorities will maintain tight liquidity conditions to help reduce the demand for foreign exchange and stem inflationary pressures. The floating exchange rate regime will be maintained, and the accumulation of international reserves will benefit in the coming months from new donor funding and other credits.

"The government's emergency power plan combines public and private investment in new thermal power capacity, with initial investments having already reduced the frequency of load-shedding. The purchase cost to the state power utility of the new power supplies is relatively high, and the government recognizes that early steps will be needed to strengthen the power utility's finances.
"Reflecting discussions in these and other areas, the authorities and the mission reached understandings, ad referendum, on economic policies and reforms that could be supported under the PSI. The IMF Executive Board is expected to take up the third PSI review in January 2012."

Mwisho wa kunukuu.

Kwa hivyo basi serikali yenyewe inaliona tatizo la madeni ya nchi. IMF wanachokipendekeza na kukubaliana na serikali ndio hichi tunachokisema hapa kuwa serikali inahitaji kusave hela na kupunguza gharama zisizo na umuhimu pamoja na kutatua tatizo la umeme. Let us hope they keep their promise to the IMF we shall see!!!
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!

Marekani wanapigana vita miaka 10 sasa na vita ni ya kukopa hawakua na hizo hela kwenye reserve yao( vita hizi ni $1.4 trillion), tanzania tumepigana miaka 10 hii ? acha ushabiki wa kijinga hii thread haikuwa na ushabiki wa namna unayofikiria wewe...

hawa ndiyo watu wanachochea vita nikisikia zile nchi wananyongana ni hawa wa namna hii.jamii inafikiria kimantiki wenyewe wanaendeshwa na hisia zaidi.
 
Austerity measures 2.0 inakuja sasa maana yake hawa IMF hawana lingine zaidi ya hizi issue na uwa zinazidisha tu umaskini na migawanyiko katika mataifa. mpaka leo bado hatujarecover na austerity measures za 1980s. kazi kubwa
 
FaizaFoxy, kuitetea serikali ya CCM inatakiwa uwe na roho ngumu kama ya paka shume mweusi, nakushauri ukubali wachambuzi wanayokwambia, hata mwanangu anapenda lile tangazo la hakielimu ambalo mwanafunzi anamuuliza mwalimu "Mwalimu kama ndiyo hivyo mbona sisi maskini" wakati tuna madini ya kila aina?

Mwanangu pia (7) alikuwa anauliza swali hilo hilo - na mimi nimempa majibu haya haya kwamba uongozi mbovu kwenye kila sekta - tena nampa na mfano wa umeme, maji, usafiri dar nk -- amenielewa. wewe bado tu unatetea nini hapa mkuu kama si ubishi usio na maana.
 
SASA hapo uchumi uchwara upo wapi?! Hivi kweli hapo panahitajika close look kama ilivyosema?! Mbona kila ki2 kipo wazi?! In 2010/2011 makusanyo ya serikali(domestic revenue) yalikuwa makubwa (8.3 Trillion) wakati bajeti was only 11.6 Trillion......kwa lugha ya hesabu nyepesi ni kwamba, wakati makusanyo yalikuwa ahueni, bajeti ilikuwa ndogo!!! In 2011/2012, makusanyo ya serikali yalikuwa madogo(only 6.7 Trillion) as compared to 2010/2011. Hata hivyo, ili shughuli ziweze kuendelea, bajeti ilipanda frm 11.6 Trillion to 13.5 trillion!! Kwa lugha ile ile ya hesabu nyepesi (am confident kwamba wengi wetu humu namba zinatupiga chenga) ni kwamba, wakati makusanyo(domestic revenue) yameshuka, bajeti imeongezka na ndio maana Domestic Revenue as % of total budget ime-drop from 72% to 49%!!!! Kwa uchumi wa kwako wewe, wa kuangalia % growth in Domestic Revenue as % of total budget ni kwamba as far as Domestic Revenue ilishuka, then, Bajeti nayo ingekuwa ndogo!!!!! Broda, hapo hakuna uchumi uchwara, labda concern yako iwe ni kushuka kwa domestic revenue!!! Na kwa mtu anayefahamu mambo ya uchumi hawezi kushangaa, i hope wewe ni mchumi, lakini hata kama sio, try to study economic graphs......cjawahi ona any economic graph ambayo ina-rise exponentially; always mambo ya fluctuations ni ya kawaida katika uchumi wowote ule dunian, unless kama unataka kusema our economy is very exceptional ambao ni never affected by other economic factors (controllable and uncontrollable factors). Try to investigate even our personal economy; always fluctuations broda!!! Tuache kulalamika na kulaumu, let's find out de way ya kuongeza vyanzo vya mapato ya serikali, upunguzwaji wa posho ni chanzo kidogo sana cha kuongeza mapato.......Let's sit down na kuangalia stable and sustainable additional domestic revenue sources. Nilipitia bajeti ya upinzani huku nikitarajia huko ningekuta njia mbadala, lakini nao waliishia porojo za kisiasa na wala hakukuwa na vyanzo vya maana vya kuongeza mapato!!!

Suala hapa ni dogo sana - How do we finance our budget? how much of that comes from domestic sources vis - as - vis external sources? And how is our debt servicing from our exports behaving?
It doesnt need kujua sana hesabu au kuwa mchumi kugundua kwamba huu ni uchumi uchwara; Ndio, prior to 2011 tulikuwa tunapiga hatua nzuri in relation to mchango wa mapato yetu katika bajeti kwani hata ukiwa na matumizi kiasi gani, kama mapato ni yako mwenyewe you are better off, otherwise uchumi wetu ni ule wa 'starehe gharama'. Kwa mwendo wa sasa, what the 49% tells us ni kwamba yes tumesimama pale pale on 28% when it comes to dependency on AID; now given the over crowding effect that the government has on domestic credit to the private sector, and given the importance of Ndullu to begin discouraging the government kupunguza kuitegemea BOT pamoja na commercial banks ili kusaidia to maintain both the GDP growth and control money supply, the government might fall back again into donors' hands na hata ikibidi kusaini kukubali ushoga and thus raise the 28% of AID contribution to our budget katika bajeti ijayo ya 2012-2013 above 28% contrary to Mkullo's goals of bringing down this rate into single digits; tusubiri tuiangalie hii figure kwa umakini pamoja na ile ya 49% next june.

Na hakuna anaelalamika hapa, kinachoendelea ni watu kujenga hoja based on takwimu hizo hizo za serikali na tunakunwa kwasababu kwasababu hizi ni pesa zetu walipa kodi, especially ambao tunaishi Tanzania hivi sasa.
 
Hizo hela zenyewe wanazokopa hatuoni wanachokifa,zaidi zaidi kuzigawana wenyewe.
 
Na bado, Muda si mrefu Mkullo ataomba pesa nyingine nje ya zile 13 trillion za walipa kodi alizopewa mwaka jana for his budget - tumtarajie any time within the next 3 months aki submit a mini budget coz ya uchumi uchwara uliopo sasa; na sababu kubwa ni kutokana na yeye na taasisi chini yake kutokuwa makini na suala la inflation kwani costing zote za budget yake ya 2011 - 2012 ilifanyika in the context of inflation targets way below of what is happening now, so utekelezaji wa ahadi za Rais kwenye uchaguzi mwaka jana hautafanyika kwa ufanisi na kupelekea rais kuonekana alikuwa muongo kumbe ni uzembe wa watendaji wake; ahadi za igunga ndio kabisa; nchi gani inayotumia kila siku kuliko inavyopokea na huku pia inaachia vyanzo vya kodi kama vile madini na kukamua kodi kwenye vibiriti na bia za ndizi ambapo watumizi wa bidhaa hizi wala hawafaidiki na hizo kodi?

Uchumi wetu unaelekea kugumu sana, especially for the rural mass and the urban poor all of which the budget never really cares much about them coz kwa mfano, katika bajeti nzima, 60% ambayo ni over 8 trillion shillings zilienda kwenye posho na mishahara, na just over 4 trillion ndio zilienda kwenye matumizi ya maendeleo; hii haina tofauti na yanayoimbwa katika ule wimbo wa starehe gharama, sasa upande mmoja misaada inaanza kuwekwa kwenye package ya ushoga, huku kwingine sijui nini kitatokea; huu ndio uchumi wetu uchwara;
well said Mpoki
 
No wonder our economy inakwenda segemnege! Pengine niulize,kwa points hizo hapo juu, maisha ya Mtanzania wa kawaida yatakuwa magumu. Mambo mengine yanayohusu upunguzaji wa matumizi ni masuala ya kisera. Ni mpaka tutakapotengeneza katiba yetu mpya. Sasa je,katika mhula wa pili wa mwaka wa fedha,kuna chochote kinachoweza kufanyika? Ama ni kweli kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukitegemea VYANZO VISIVYO RASMI ili tu kufanikisha malengo ya kisiasa..na sasa ufadhili huo haupo tena,na kulazimika kuchota katika bajeti yetu?[vyanzo visivyo rasmi mfano, Harare, Tripoli, Mafisadi Papa,n.k. ambavyo vyote havina uwezo tena kutokana na sababu mbalimbali] Mwaweza kunikosoa pia.
 
Nimesikiliza taarifa ya saa 2 TBC 1, maafisa wa IMF walikuwa na mazungumzo na maafisa wa BOT wakatangaza kwamba serikali imeishiwa.

Mapato ya ndani ukichanganya na fedha za nje ni ndogo kuliko matumizi. Kwa hiyo serikali imelazimika kukopa benki za ndani hivyo kuwanyima waekezaji fedha kutoka mabenki.


Chadema walipokuwa wanasema tuondoe posho na kupunguza safari waliona mbali, sasa serikali inatumia tu mara Australia wanaenda msafara wa watu 80 wakati nchi haina pesa,
Billion100 kuazimisha miaka 50 ya uhuru, hii nchi mpaka kuna wakati nahisi kama nipo ndotoni
 
Mchambuzi

NImekukubali

Asante kwa Data zako na Uchambuzi wako kwani umetufungua wengine
 
r
NGOJA nipitie kwa umakini taarifa ya IMF kupitia Newsletter niliyoipata leo kuna mchana wa saa saba!!!

Concluding Statement by the IMF Mission to Tanzania
Press Release No.11/401
November 7, 2011


........................
"An International Monetary Fund (IMF) mission, led by Mr. Peter Allum, visited Dar es Salaam during October 26–November 7, 2011 to conduct discussions for the third review under the Policy Support Instrument (PSI).[SUP]1[/SUP] The mission met with Finance Minister Mkulo, Bank of Tanzania Governor Ndulu, and other senior officials, as well as representatives of the private sector, civil society, and development partners. The mission wishes to thank the authorities for their warm hospitality, close collaboration, and the high quality of the discussions."

"At the conclusion of the mission in Dar es Salaam, Mr. Allum issued the following statement:


“Despite recent power shortages, Tanzania’s economy continues to grow strongly, expanding 6.3 percent in the first half of 2011. Core inflation, measured excluding food and energy components, remains in single digits, while headline inflation has approached 17 percent (year-on-year), boosted by global energy prices, food price effects from the drought in the Horn of Africa, and the recent depreciation of the shilling. Public spending has risen as a share of gross domestic product (GDP) in recent years to deliver significant growth in local government health, education and other social programs as well as scaled up investments in roads and other infrastructures. However, overall recurrent spending has outpaced revenue and grant financing, contributing to growing fiscal deficits and a rising public debt stock."


“Under the PSI program through June 2011, the Bank of Tanzania’s reserve money targets were met and foreign commercial borrowing was kept well within program limits. However, partly due to the shortfall in commercial borrowing, domestic financing of the budget was higher than planned and the target for accumulating net international reserves was missed. Structural reforms are moving forward, notably to strengthen debt management capacity.


Opinion on bolded italic phrase:

Planning ambayo inategemea third parties katika hali mbaya ya uchumi wa Dunia, ILHALI rasimali tulizokuwa nazo, nyingine ziko kwenye uzalishaji lakini hatupati tunachostahili, mianya mibovu ya kimfumo na rasimali watu wezi wanaotunyima kiasi kikubwa cha pesa (Udhaifu wa Serikali), chunguza pesa tunazopoteza bandarini, TRA, madini,

Wazo: Serikali ijadili na mabenki njia nzuri zaidi ya kuwa na mfumo bora wa kutoa mikopo mikubwa kwa wazawa wenye mawazo mazuri na yanayotekelezeka
: Serikali itekeleze mbinu(kwa hakika zipo) zitakazo tupa pesa zaidi kwenye madini
: Mifumo inayoleta mianya ya utendaji mbovu wenye madhara makubwa kipesa ibadilishwe haraka iwezekanavyo TRA, TPA
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!

marekani kitu gani Tz tukiamua kusimama sisi kama sisi tunaweza kinachututiza ni viongozi wetu wanavyoweka maslahi yao binafsi (ufisadi) mbele, rasilimali za kutosha tunazo
 
Tatizo la serikali kukosa fedha linazidi kujidhihirisha tena katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kama ilivyokuwa kwenye mitihani ya Taifa kidato cha Pili iliyoanza leo semina kuendesha bila hata chuba ya maji ya 200, chai na chakula. Wakuu wa shule na wasimamizi wasaidizi kusimamia bila serikali kutenga bajeti yoyote ya malipo kwa shule za sekondari. Kituko kingine kiko kwenye mitihani ya Taifa Darasa la Nne. Katika mitihani iliyokuwa ikisambazwa jana na maafisa kutoka idara ya elimu ya msingi katika halmashauri mbalimbali, waliwaeleza walimu wakuu kuwa ndio watakao simamia badala ya walimu waliokuwa wakichukuliwa toka shule tofauti na wafundishazo. Wameambiwa kila mwalimu mkuu abadilishane na mkuu mwenzake wa shule ya jirani. Waliambiwa kuwa seriakali haijatowa fedha za kuwasafirisha wala za kuendesha semina ambazo huambatana na kula kiapo cha kutunza siri za mitihani kama sheria inavyotaka. Mwalimu mkuu mmoja anayefundisha shule wilaya moja iliyopo mkoani Morogoro alieleza kuwa wameambiwa watajilipa pindi pesa itakapotolewa na serikali ya ruzuku kwa shule zao, aliendelea kupasha kuwa hiyo ni danganya toto. Afisa aliyekuwa kwenye msafara wa kusafirisha mitihani hiyo alipasha kuwa hata wao hawakupewa pesa yoyote zaidi ya kuambiwa malipo yatashughulikiwa baadae "tunaomba gari isipate hitilafu turudi mjini salama la sivyo tunaweza kufa njaa". Mpaka JK amalize muda wake tutafika kweli jamani? siku nazo hazikimbii.
 
Nijuzeni kufahamu kiwango cha Elimu ya watu hawa wawili;
1. Waziri Mkulo
2. Gavana Ndulu.

Waziri Mkulo sioni kama ni thinker au kama ni mtu mwenye hamu ya kuinua hali ya uchumi wa nchi lakini huenda an kiwango duni cha elimu.

Huyu Prof. Ndulu, ametokea wapi? Is he the best for the BoT? Au tumeokota tu ili naye afaidi. Isije ikawa wateuzi walitishika na neno profesa!
 
waambie waendelee kujitolea mkuu, kwani ualimu si tulishasema ni wito. kwa kipindi hiki cha huyu mk.were dhana hii inaenziwa kweli ili hali wengine wakiendelea kuponda raha. mwambie avumilie maana uozo ni kama umejaa kila mahali kwa sasa
 
To have a fridge at home was extravagant at the time of Nyerere, to use Colgate was extravagant, to have a car was extravagant, to have a TV was extravagant. Extravagant is what you perceive and how stagnant you are it is never the rule of economics. Remember how a big failure Nyerere was economically?

It is highly suicidal to economize on expenditures to your economy, to fuel economic growth you have to be extravagant in all aspects. How can you have a growth without spending? simple economy rule; "the more you spend the more you earn the more you earn the more you spend". That is the only way you can measure your growth, you can never ever measure growth by not spending. Be real.

Sasa nimegundua jinsi gani Nyerere anabezwa na baadhi ya wenzake CCM, na nadhani pia wapo viongozi wa CCM vilevile, na sababu zao ni ngumu kuelewa. Ila bila shaka, wengi wao ni wale wasio kuwa na maadili ya uongozi kwahivyo Jina la Nyerere kuwa mwiba mkali kwao. Ni ajabu kwamba hata viongozi wa CCM wapo wanaobeza mafanikioa ya Nyerere; Tunampima Nyerere kwa vipimo vya Colgate, TV na Magari? Ina maana kwamba sifa za viongozi wa leo ni upataikanaji wa Colgate, TV na Magari? Nilibahatika kwenda Kiteto na maeneo mengine mengi sana Tanzania huko vijijini na maisha yao kule hayana tofauti na mwaka 1961; Isitoshe, hizo Colgate hazishikiki (huku wengine wakitumia vitu mbadala); TV ndio usiseme kwani sio zaiadi ya 12% ya watanzania wana umeme, leave alone uwezo wa kununua TV sets;

Well, Nyerere admits hata mwenyewe kwamba kuna mambo ya maana alifayanya na mengine ya kipumbavu lakini akashangaa awamu za mbele yake zinaacha ya maana na kuchukua ya kipumbavu; we can talk about what made him fail lakini sidhani kama ni mahala pake hapa, kwa sasa tuangalie yafuatayo kwa ufupi tu; ila kwa kifupi ni Nyerere alivyokwisha sema - yanachukuliwa ya kipumbavu, yanaachwa ya maana.
Nyerere aliipokea hii nchi ikiwa na 95% of Tanzanians as wanavijiji, and 5% as urbanites; Sina haja ya kuziweka takwimu hapa kuonyesha ni jinsi gani mpaka anaondoka social development indicators zilivyokuwa juu kama vile literacy rates at upper 60s percent - one of the highest in Africa; Leo hii, illiteracy in Tanzania is about 30%; and about 24% of Tanzanians hawana elimu of any kind (hawajasoma hata darasa la kwanza); tunazidi kushangilia shule za kata from a quantitative side, and we totally ignore the qualitative side of it; social indicators nyingi sana zinawasuta wale wanaosema leo hii tumepiga hatua kuliko enzi za Mwalimu kijamii – tukitazama suala la afya, elimu in qualitative terms hakuna la maana sasa compared to zamani, ila kama hoja zenu ni quantitative, Hurray, mmewapata wajinga.

Uchumi wa Mwalimu ulikuwa una trickle down to the 95% of the rural masses, huu wa sasa sio pro – poor growth na hatuna haja ya kuweka takwimu hapa kuonyesha hilo kwani zipo wazi kila sehemu; Mpaka mwaka 1985 wakati Mwalimu anaondoka, Tangia Mwalimu kaondoka, hakuna much changes katika composition mfano ya manufacturing on GDP as we can see kwenye figures (see table below);

Kilimo - mhango wa kilimo kwenye GDP umepungua na kufikia 28.9%; kwa kawaida hii huwa ni ishara nzuri lakini pale tu kama Kilimo ndicho kinachozalisha then tukipata earnings from there ndio ziende kuamsha na kuendeleza sectors nyingine kama viwanda, mining etc, hivyo ndivyo economic development comes about na ndivyo nchi zote zilianza na kilimo na later kuwa industrialized; hivyo ndivyo green reveolution occurs – increase in productivity ya kilimo, then kizalishe na kuleta hela kwa wingi na hela hizo ziwe invested kufungua sekta nyingine za uchumi (sio kutegemea misaada au wawekezaji kufanya hilo); We see in the table below kwamba between independence and now, imepungua from 48% to around 29%; but hizi namba hazina maana yoyote kwani hazina mahusiano yoyote na kilimo kuwa productive na kutupatia uwezo wa kupata fedha ili zijenge viwanda vyetu, zichimbe madini yetu, zifungue taasisi zetu muhimu za umma; the change from 48% to 29% in agricultural composition kwenye GDP hazina association yoyote katika haya; why? Because we don't invest in zaidi ya Mwalimu alivyokuwa anawekez mkazo; tumebaki na porojo tu za Kilimo Kwanza huku matrekta mengi yakienda kwa watu wasio walengwa; Tuangalie mfano in 1961, agricultural machinery, tractors per 100 sq. km of arable land was 31.8; as of 2004 it was down to 23; productivity ya kilimo compared to miaka ya nyuma imepungua sana – ebu fikiria in 1961 Cereal production (metric tons) was 1.1 million; by 2009, that figure had only reached to 6.2 million; mind you, in 1961, population yah ii nchi was around 9million, by 2009, 40million plus; hata tukiangalia annual growth in the kilimo sector (see the table below), hatuna cha ajabu cha kujivunia na kumbeza Mwalimu;

Manufacturing – hakuna anything impressive tofauti na Mwalimu Nyerere; at most imezidi kuporomoka; manufacturing composition yake on GDP haina tofauti sana na miaka ya nyuma nab ado hatujafikia kiwango cha Mwalimu cha 10.8% (see table below);

Service Sector – hakuna ubishi kwamba hii sekta imepanuka zaidi kuliko wakati wa Mwalimu lakini tusisahau kwamba service economy is a new phenomenon, hata nchi zilizoendelea halikuwa jambo la maana zaidi ya industrialization Kwahiyo kwa uwezo wake na bidii yake, a 22% level ya Mwalimu during the 1970 – 1980 period inastahili pongezi;

YearKilimo as % of GDPKilimo annual growth rateManufacturing as % of GDPManufacturing growth rateService Sector % of GDPService sector growth rate
1960 – 1970 (Nyerere)43.6%3.7%8.7%10.4%15.7%7.2%
1970 – 1980 (Nyerere)43.4%3.4%10.3%4.4%22%15.7%
200630.4%3.88.5%8.4%46.7%7.1%
200729.6%4.08.5%8.7%46.7%8.4%
200829.7%4.58.6%9.9%47.1%7.9%
200928.7%3.29.5%8%46.9%7.1%

Source: Various World Development Reports

Napenda kuzidi kusisitiza kwamba kinachofanya watu waone kuna mabadiliko katika pato la taifa (GDP) ni mchango wa sekta ya madini katika GDP, but the question comes – this production is for who? Mwalimu aliamua madini yasiguswe kwani yatakuwa abused hivyo ‘yakae tu huko chini kwani hayaozi' mpaka watanzania waweze produce wataalum wa kuyafanyia kazi wao wenyewe na kwa faida yao wenyewe; sasa yanaguswa na wawekezaji, na yanakuwa abused, ndio tunashangilia economic growth ya over 6% since mwaka 2000 kama ni mafanikio wakati hii inatokana na mchango wa madini in terms of production peke yake, not income from the sekta? Huu ndio uchumi uchwara.
It's obvious kuna watu wanadanganyika sana na GDP growth bila kuangalia nini kimeipelekea ku behave that way: angalieni hali za wananchi kama zinabadilika, na sio wa mjini, the 70% plus in rual areas! Otherwise hakuna that much of a difference between miaka ya Mwalimu sasa, especially in his first 20 years in terms of Maendeleo na mchango wa kilimo, manfucaturing;

Ni muhimu lakini tukaangalia impact ya kilimo on GDP kushuka from 48% to 29%; again, kwa kawaida haya ni Maendeleo lakini tumeone kwetu sisi hakuna lolote hapo; inatakiwa composition ya GDP ikishuka, kwingine ipande na ajira kwenye hizo sekta nyingine kama viwanda, mining, services zipande; ebu tazama jedwali la hapo chini la hali ya sasa relative to ile ya Mwalimu where about 80% of the labour force was in the agricultural sector, je leo tumepiga hatua kweli?

Table1: Employment in Tanzania According to Sectors (%)
SECTORDAR-ES-SALAAM (%)OTHER URBAN AREAS (%)RURAL AREAS (%) TOTAL(%)
Agriculture, Hunting, Forests 7.1 38.0 81.8 67.9
Fishing 0.5 1.3 1.4 1.3
Mining 0.5 2.6 0.6 0.9
Manufacturing 4.2 3.9 0.6 1.4
Production of electricity, gas and water 1.0 0.9 0.5 0.6
Construction 4.6 2.8 1.0 1.6
Trade (retail and wholesale) 27.9 18.6 3.6 8.3
Hotel and restaurants 4.5 3.3 0.6 1.4
Transport and communication 6.7 2.9 0.4 1.4
Financial services 0.7 0.2 0.1 0.1
Estate leasing 0.3 0.2 0.1 0.1
Administration, Defence and Public safety 5.4 3.2 0.5 1.4
Education 2.3 2.6 1.1 1.4
Health and social welfare 1.8 1.8 0.4 0.7
Other services 30.3 15.5 6.9 10.4
Private household employing other persons 2.1 2.1 0.4 0.9
Diplomatic offices and foreign service organizations 0.1 0.1 0.0 0.0
Total 100.0 100.0 100.0 100.0

Source: Household Budget Survey + World Bank Data.

The table above proves kwamba GDP composition imeshuka from 48% to 29% sio kwa sababu ajira kwingine zimeongezeka kutokana na mafanikio ya kilimo (agricultural revolution) ambayo yamesaidia kupanua sekta nyingine; instead, ukweli ni kwamba kushuka kwa hii composition ni kwamba watanzania wengi vijijini wamekimbia kilimo kwasababu hakilipi, lakini kama tunavyoona kwenye hizo figures, hawajaenda kwenye viwanda wala service sector wala madini bali kwenye informal sector huko ambapo the so called service sector inawabeba kama wauza vocha, maji ya uhai, magazeti na wabeba zege;

Faizyfoxx, pia on your point kwamba:
"It is highly suicidal to economize on expenditures to your economy, to fuel economic growth you have to be extravagant in all aspects. How can you have a growth without spending? simple economy rule; "the more you spend the more you earn the more you earn the more you spend". That is the only way you can measure your growth, you can never ever measure growth by not spending. Be real."
Hata sijui nianzie wapi kukujibu hili, na wengi sana humu tayari wamelielezea sana; cha ajabu ni kwamba, ni wazo hili hili ulilonalo hapa ndilo linalotupelekea sisi kama nchi kufilisika kiuchumi kwani tunakopa kuliko tunavyoweza lipa na tunatumia kuliko tunavyoingiza;
 
Back
Top Bottom