IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Nov 7, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimesikiliza taarifa ya saa 2 TBC 1, maafisa wa IMF walikuwa na mazungumzo na maafisa wa BOT wakatangaza kwamba serikali imeishiwa.

  Mapato ya ndani ukichanganya na fedha za nje ni ndogo kuliko matumizi. Kwa hiyo serikali imelazimika kukopa benki za ndani hivyo kuwanyima waekezaji fedha kutoka mabenki.


  Chadema walipokuwa wanasema tuondoe posho na kupunguza safari waliona mbali, sasa serikali inatumia tu mara Australia wanaenda msafara wa watu 80 wakati nchi haina pesa,
   
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Na bado, Muda si mrefu Mkullo ataomba pesa nyingine nje ya zile 13 trillion za walipa kodi alizopewa mwaka jana for his budget - tumtarajie any time within the next 3 months aki submit a mini budget coz ya uchumi uchwara uliopo sasa; na sababu kubwa ni kutokana na yeye na taasisi chini yake kutokuwa makini na suala la inflation kwani costing zote za budget yake ya 2011 - 2012 ilifanyika in the context of inflation targets way below of what is happening now, so utekelezaji wa ahadi za Rais kwenye uchaguzi mwaka jana hautafanyika kwa ufanisi na kupelekea rais kuonekana alikuwa muongo kumbe ni uzembe wa watendaji wake; ahadi za igunga ndio kabisa; nchi gani inayotumia kila siku kuliko inavyopokea na huku pia inaachia vyanzo vya kodi kama vile madini na kukamua kodi kwenye vibiriti na bia za ndizi ambapo watumizi wa bidhaa hizi wala hawafaidiki na hizo kodi?

  Uchumi wetu unaelekea kugumu sana, especially for the rural mass and the urban poor all of which the budget never really cares much about them coz kwa mfano, katika bajeti nzima, 60% ambayo ni over 8 trillion shillings zilienda kwenye posho na mishahara, na just over 4 trillion ndio zilienda kwenye matumizi ya maendeleo; hii haina tofauti na yanayoimbwa katika ule wimbo wa starehe gharama, sasa upande mmoja misaada inaanza kuwekwa kwenye package ya ushoga, huku kwingine sijui nini kitatokea; huu ndio uchumi wetu uchwara;
   
 3. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Watanyosha tu maelezo maana wanakijitabia cha kuficha ugonjwa. Wakiulizwa vipi mko hoi wanajidai wako fit. Ngoja wataumbuka mchana kweupe.
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Kuna siku JK na Mkulo watakuwa wanaangaliana tu bila cha kufanya pale nchi itakapo kufa kifo cha mende....uchumi unaelekea kusimama wakuu.
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii kitu ya kukopa kwenye benki za kibiashara tena za ndani! Na kutumia mikopo hiyo kwa ajili ya kuagiza mafuta nje, lina madhara sana. Wanajamvi wengi waliliona hili na kulitolea msimamo lakini walitupuuza. Sasa ngoja tuone kitakachofuata baada ya hatua hiyo ya IMF
   
 6. A

  Amelie Senior Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado watoa misaada wenyewe wana debt crisis,sijui tutapeleka wapi bakuli
   
 7. mkonomtupu

  mkonomtupu JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Na usiku huu wamewaalika mashoga kibao wa Cameron kumalizia vijisent vye2. Walaaniwe CCM wote na mashoga zao
   
 8. O

  OSCAR ELIA Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wachumi wetu mko wapi?mbona mambo yanazidi kuwa magumu kwa walalahoi.Haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania ?
   
 9. gmosha48

  gmosha48 JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 180
  Mkuu, umeongea point sana, ila kuna mahali umepiga msituni kidogo. Unaposema kuwa asilimia 60 ya bajeti imekwenda kwenye mishahara na Posho, na kiasi kilichosalia kikaenda kwenye maendeleo siyo kweli. Kwa heasabu nyepesi kabisa, unachotaka kuwaambia watanzania ni kwamba Bajeti ya Tanzania= Posho+ Mishahara+ Maendeleo. Kama hiyo ndiyo tafsiri yako ya Bajeti, utakuwa umepotoka. Tafsisi sahihi ni hii:

  bajeti ya Tanzania= Mishahara+Posho+ Matumizi ya kawaida ( mafuta, vitabu, madawa, ukarabati nk)+ maendeleo. Kwa tafsiri halisi ya serikali( kwa mujibu wa vitabu vya bajeti) bajeti yetu = Personal Emoluments ( Mshahara na mafao)+ Other charges ( ghrama za uendeshaji) + developement Expenditure( Maendeleo). Kwa miaka mingi sasa, bajeti ya maendeleo imekuwa ni kama asilmia 20 tu ya bajeti nzima.

  Kwenye tafsiri yako, utakuwa umesahau fedha za uendeshaji ( other charges ) ambazo ni karibia asilimia 40 ya pesa pesa zote za matumizi ya kwaida yaani ( recurrent Expenditure)

  Viginevyo, point zako ni za msingi sana.
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Serikali haina cha kufanya,watabakia kutumia dola kujilinda huku wakiomba Mungu mambo yabadilike kwasababu wao wanaamini tatizo la uchumi ni la kidunia.
   
 12. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Unakopa ili katika matumizi ya bajeti yako ya trilioni 13.5, over 8 trillioni goes to posho na mishahara and the rest ndio kwenye shughuli za maendeleo ya walipa kodi? Come on now. Angalia Marekani wanapokopa wanafanya nini na matumizi yao. Kukopa kwa serikali yoyote sio tatizo, unakopa kwenda kufanyia nini? na unachokifanya kitasaidia kuweza rudisha mkopo au atleast punguza mkopo in the future parallel to lifting the rural mass?
   
 13. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  inanikumbusha Ugiriki, hapa kilicho bakia ni nchi itangaze kufilisika, ila kuhusu matumizi watafunguka mda c mrefu,
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  r
  NGOJA nipitie kwa umakini taarifa ya IMF kupitia Newsletter niliyoipata leo kuna mchana wa saa saba!!!

  Concluding Statement by the IMF Mission to Tanzania
  Press Release No.11/401
  November 7, 2011


  ........................
  "An International Monetary Fund (IMF) mission, led by Mr. Peter Allum, visited Dar es Salaam during October 26–November 7, 2011 to conduct discussions for the third review under the Policy Support Instrument (PSI).[SUP]1[/SUP] The mission met with Finance Minister Mkulo, Bank of Tanzania Governor Ndulu, and other senior officials, as well as representatives of the private sector, civil society, and development partners. The mission wishes to thank the authorities for their warm hospitality, close collaboration, and the high quality of the discussions."

  "At the conclusion of the mission in Dar es Salaam, Mr. Allum issued the following statement:


  "Despite recent power shortages, Tanzania's economy continues to grow strongly, expanding 6.3 percent in the first half of 2011. Core inflation, measured excluding food and energy components, remains in single digits, while headline inflation has approached 17 percent (year-on-year), boosted by global energy prices, food price effects from the drought in the Horn of Africa, and the recent depreciation of the shilling. Public spending has risen as a share of gross domestic product (GDP) in recent years to deliver significant growth in local government health, education and other social programs as well as scaled up investments in roads and other infrastructures. However, overall recurrent spending has outpaced revenue and grant financing, contributing to growing fiscal deficits and a rising public debt stock."


  "Under the PSI program through June 2011, the Bank of Tanzania's reserve money targets were met and foreign commercial borrowing was kept well within program limits. However, partly due to the shortfall in commercial borrowing, domestic financing of the budget was higher than planned and the target for accumulating net international reserves was missed. Structural reforms are moving forward, notably to strengthen debt management capacity.

  For more information, visits
  Press Release: Concluding Statement by the IMF Mission to Tanzania


  Hiyo sasa ndio taarifa rasmi ya IMF, ambayo si ya ki CHADEMA CHADEMA bali iliyotokana na utafiti wao. Ndio taarifa inayopaswa kuchambuliwa kwa hivi sasa na kuwekwa kwenye mizani na kuangalia inaegemea wapi!!!
   
 15. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Na bado,

  Tunaposema tatizo lipo ujue lipo mfano mdogo ni our country debt to gdp ratio now stands at 40% of the total GDP excluding the $500 Billion Euro bond. Mwaka huu sijui figures ikifika mwisho wa mwaka zitakuwa wapi but kuna uwezekano tukawa 74.5% of the total GDP. Our external debt is estimated to be $7 Billion (2010 IMF figures).

  Our tax revenue as percentage of GDP is 12% meaning from $23.06 Billion of GDP only 12% of it is collected by the revenue board. About $2.76 Billion. Tunachokikusanya kidogo mno kama kodi lakini kasi yetu ya kukopa ni kubwa mno. Bado hatuzungumzia Current account deficit na mengineyo.

  Tunarudia tena kuna umuhimu wa serikali hii kupunguza matumizi yasiyo na msingi. That includes wabunge wa viti maalum kuokoa hii serikali isurvive na kutoishiwa hela. Serikali ipunguze matumizi ya anasa na badala yake iwekeze katika sekta za maendeleo.
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Nanukuu, "Amenikumbusha mama mmoja siku moja Hotelini jioni akiwa na watoto wake, watoto walikuwa wakisumbua na kutoka toka kwa kwenda kwenye giza nje. Mama yao alipofikiria njia ya kuwatisha ili wasiende nje aliwaambia “ Nyie njoni haraka CCM watawachukua” Wale watoto wakarudi haraka wanakimbia. Tuliosikia tulicheka kisha tukamwuliza kwa nini watoto wamerudi haraka kwa neno hilo. Akasema nataka watoto wangu wakue wakijua kuwa CCM ni kitu kibaya." mwisho wa kunukuu
   
 17. sam2000

  sam2000 JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Once a country uses more than 50% of its budget to pay salaries and allowances, its a sure fact its economy is destined to fail miserably. That is what we have been doing for as long as we can remember. Sometimes you wonder all those Drs and Professors of economics are when the country is heading to the dogs. A whole professor of economic and he cant do any meaningful thing about our economy!
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280

  Sawa sawa mkuu. Ebu tusaidiane kuchambua hili:

  Mkullo June 2011


  Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, katika mwaka 2011/12 Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi
  bilioni 13,525.9 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 8,600.3 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha shilingi bilioni 3,270.3 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali, taasisi na wakala za Serikali na shilingi bilioni 1,910.4 kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali.

  Aidha, jumla ya shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,054.1 ni fedha za nje.

  Mapato:
  A: Mapato ya Ndani 6,775,952
  (i) Mapato ya Kodi (TRA) 6,228,836
  (ii) Mapato Yasiyo ya Kodi 547,116
  B: Mapato ya Halmashauri 350,496
  C: Mikopo na Misaada ya Nje 3,923,551
  D: Mikopo ya Ndani 1,204,262
  E: Mikopo ya Masharti ya Kibiashara 1,271,634
  JUMLA YA MAPATO YOTE 13,525,895

  F: Matumizi ya Kawaida 8,600,287
  (i) Mfuko Mkuu wa Serikali 1,910,376
  (ii) Mishahara 3,270,292
  (iii)Matumizi Mengineyo 3,419,619
  Wizara 2,727,472
  Mikoa 49,981
  Halmashauri 642,166

  G: Matumizi ya Maendeleo 4,924,608
  (i) Fedha za Ndani 1,871,471
  (ii)Fedha za Nje 3,054,137
  JUMLA YA MATUMIZI YOTE 13,525,895

  ---
  Ukisoma katika ufunguzi utaona kuna takwimu zimefinywa finywa, hazielezwi zimeenda wapi na mantiki yake ni matumizi ya kawaida in the form of posho, mishahara, repairs za majengo haya na yale, dhfa za kitaifa n.k - kwa ufupi i still hold kwamba 60% of the budget goes to other things than maendeleo ya Mtanzania. Thats the bottomo line.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,244
  Trophy Points: 280
  Yes, Marekakani ni kweli wanakopa, ila wao hawakopi kwa sababu wameishiwa bali wanakopa ili kutia stimulus package kwenye uchumi wake. Mwaka juzi walikopa China kwenye ile bail out ya mdororo wa uchumi.

  Sisi tutakopa kwa vile tumeishiwa!. Bajet yetu ni tegemezi kwa 40% toka kwa unkal, aliyoyasema ankal kama masharti mapya, tumeyasikia, tumetunisha misuli na sasa tutakopa benki zetu za ndani za interest ya 20%!.

  Japo mimi si mchumi, lakini impact ya mkopo huo ni kilio cha kusaga meno!.
   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Unajua Pasco, uchumi uchwara wa Tanzania hauhitaji mtu kuwa mchumi kujua nini kinaendelea kwani hata hesabu za total budget mwaka jana zilikosewa ikabidi zikajumlishwe upya; does that need an economist au just a rational thinker pasco.
   
Loading...