Imeshika kasi: Tuendelee Ushujaa wa "Ka-Corona, tusitishane, tuchape kazi" tukiteketea; au tubadili msimamo na tusitisishe Mikusanyiko tuokoke?

Sijui kwanini kuna watu duniani wanaamini Mungu anapinga sayansi.

Tunaweza hata kuthubutu kumuomba Mungu atuongoze kupitia maarifa ya sayansi tugundue dawa au kinga ya gonjwa lolote haraka.

Maandiko matakatifu yanasomeka ukiwa na imani unaweza hata kuhamisha mlima.

Tuwe na imani basi kuwa kama waafrika tunaweza kumwomba Mungu tutumie mikono yetu na akili zetu sawasawa kutatua matatizo yetu.

Kupitia binadamu wa kwanza na ile dhambi ya kwanza tulishapewa adhabu ya kula kwa jasho. Yaani suluhu zote utazipata kwa kusotea. No short cut.

Ukifuatilia nchi za Ulaya, Amerika na Asia unasoma na kusikia zipo katika harakati ya kupata chanjo na dawa ya janga la Korona hata kama itachukua miaka.

Nchi za Afrika sidhani kama zina hata mpango wa baadae kujihami au kupata suluhu ya hili janga. Sanasana ni kuomba miujiza itokee.

Huwa ninajiuliza Mungu muweza ya yote atambariki asiye jituma na kuomba au atambariki anayejituma na kuomba kile anachojituma kifanikiwe?





Sent using Jamii Forums mobile app
 
AACHIE mahabusu na wafungwa yani warud makwao au nimeelewa vibaya?

huu hata upukutishe nchi nzima,hilo halitakaa litokee maana ...
 
Tuendelee kuchapa kazi ila mikusanyiko ni marufuku na sheria iwekwe na isimamiwe

sanitizer za buku kila mtu awe na yake mfukoni,Mask lazima kwa yeyote anaetoka nnje

ya nyumba yake,ukikutwa huna mask "udakwe" uwezo wa kuzuia maambukizi upo vzr tu

ila nadhani kuna idadi inasubiriwa ifike ndio tuanze kutishiana na kuleteana ubabe mandaazi.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest:
Mimi ni mwandishi wa habari, na kunapotokea janga lolote, hatua ya kwanza ni "appreciating the situation" hivyo mimi ni miongoni mwa wale tuliompongeza Rais Magufuli kwa hatua za Tanzania ilizochukua kwa kutotishika na janga la Corona na kumsifia Magufuli shujaa, wakati marais wa nchi jirani wametishwa, wakatishika. Rais Magufuli alionesha ushujaa wa hali ya juu kwa kwa kuonesha assuarance "KaCorona ni kaugonjwa kadogo, tusitishane, Watanzania tuendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga", huku rais Magufuli akionyesha mfano wa kutokutishika kwa kulihutubia taifa siku ya Jumapili ambayo ndio siku ya mapumziko. And then, siku ya Jumatatu ambayo ni siku ya kazi, by basking on the sun recreating himself kwenye majabali ya Ikulu ya Chamwino.

Uandishi sio fani static na conservative kama sheria, ni fani dynamical na current ambayo misimamo ina change with time. Kwa rate ya maambukizi ya siku zile, kwa uamuzi ule, ni kweli Rais Magufuli alikuwa shujaa, lakini kwa rate hii tunayokwenda nayo sasa, ya maambukizi ya Corona kwa local transmissions, we seriously need ku-reposition misimamo yetu. Corona sio kaugonjwa kadogo, ni liugonjwa likubwa; ni balaa, ni janga la kitaifa na kimataifa. Hatuwezi kukabiliana nalo kwa kuchapa tu kazi with life as usual, now we have to make some sacrifices to save the lives of our people.

Hatua ya kwanza kwa sasa, ni tuzuie mikusanyiko yote isiyo ya lazima ikiwemo mikusanyiko ya nyumba za ibada na sehemu za starehe, bar, nightclubs na kumbi za burudani.

Tusitishe shughuli zote za mikusanyiko mihimu inayoweza kusubiri, hii ni pamoja na kusitisha kesi zote katika mahakama zote, tuwaachie huru mahabusu wote ambao sio hatarishi kwa maisha ya watu; tuwaachie huru wafungwa wote magerezani kote, wakiwemo wafungwa wa vifungo vya maisha, kwa wafungwa hawa na wale wa vifungo virefu, kupewa likizo. Corona ikiisha, watarejea magerezani kwa wafungwa kukamilisha vifungo vyao, mahabusu kurejea kwenye umahabusu wao na kesi kuendelea, na kwa wale ambao watatokomea na kutorejea, ihesabiwe huu ndio mpango wa Mungu kwa watu wake, tusubiri hadi maafa ya kiwango cha juu yatukute ndipo tuchukue hatua hizi.

Ule msimamo kuwa rais Magufuli ni shujaa wa Corona barani Afrika bado unaendelea, na hata katika vita ukiwa kwenye mstari wa mbele wa mapambano, kuna mashujaa wa aina mbili:

1. Mashuja Wapiganaji Fighters, wao kazi yao na motto yao ni ku-Fight, Fight, Fight -- no retreat, no surrender. Pigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike hata kama all will be wiped, mtakuwa mmekufa kishujaa mkipigania taifa lako na mtakumbukwa milele kama mashujaa wa taifa. Ndivyo walivyofanya kina Mkwawa, Mtemi Mirambo, Kinjekitile, na wengine. Je, tuendelee kumchagiza Rais Magufuli kushikilia msimamo huu wa kufa kishujaa na hata Tanzania tukiteketea, tumekufa kishujaa, au?

2. Intelligent Fighter ambao hawapekeki askari vitani hadi kwanza wajue nguvu ya adui, ili kuepuka kupeleka vitani askari wake kwenye a loosing battle wakaishia all kuwa wiped out na nchi nzima kugeuzwa mateka.

Kundi hili wakati wakiwa kwenye mstari wa mbele, wakiona dalili na kuzidiwa, kuliko kuendelea kupigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike hata kama they'll all be wiped ila watakumbukwa kama mashujaa wa taifa, intelligent fighters, wata retreat kwa kurudi nyuma kwenda kukusanya nguvu na kujijenga upya, au wata surrender na kuchukuliwa mateka hai kuliko mashuja wafu. Je, sasa tumshinikize Rais Magufuli abadili misimamo ya awali kutokana na the escalating situation ya maambukizi ya Corona au tuendelee kushupaza shingo zetu tukielekea machinjioni?

Hitimisho:
Namalizia hoja yangu hii ya bandiko hili. Kwa kasi ya sasa ya Corona; je, tuendelee kumchagiza Rais Magufuli ashikilie msimamo ule ule wa ushujaa wa "Tusitishane, Corona ni kaugonjwa kadogo, Watanzania tusitishike tuendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu ya jinsi ya kujikinga" Au Sasa Rais Magufuli akubali kubadilika, tusitishe mikusanyiko, ibada, starehe, achia mahabusu, wafungwa, before it's too late; au tusubiri maafa ndipo...?

Paskali.
Kuna muda nakaaa natafakari nchi hii yupo Rais kweli kwangu mm Rais ni Baba kwa mjibu wa katiba yetu ni mfariji mkuu na huu ni utamaduni wa Duniani kote......sio mara moja Rais wetu majanga makubwa yanapotokea anakuwa yuko kimya saa nyingine anatoa kauli tata rejea tetemeko kule Kagera ama ubomolewaji wa watu wa kimara yote.hii imenipa tabu kumfikiria sana Rais wetu embu angalia kauli zake za ugonjwa wa korona kwamba ni wa kawaida yapo magonjwa mengi mara hatufungi mipaka ndege zije tu,Leo ugonjwa ushasambaa ndio wanazuia ndege
Kama mfariji mkuu wa taifa alitakiwa awe anapata coverage kwenye media juu ya huu ugonjwa angalia Marais wenzake tusiende mbali hapo Rwanda au Kenya au Uganda alafu yy kajipa likizo yupo kijijini kwao ni sawa na Baba kuikimbia familia nyakati za shida kuwa kwake likizo kumepelekea viongozi wadumavu kama makonda mongela kujionesha mbele ya umma
Tumuombe mungu maana Baba kaikimbia familia
Stay home ugonjwa ni hatari ukifa unazikwa na serikali chukua tahadhari



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Praise team....Mmemchagiza miaka mitano ameishia kuharibu uchumi wa nchi na kutukana watz mchagizeni zaidi ili alipe wakulima wa korosho, asiwashushe matajiri na kuwa mashetani, aongeze mishahara ya wafanyakazi, wanafunzi wote wapate mikopo vyuoni....
Nyie lumumba ni hamnazo sana
 
Mkuu Paskali, Rais wetu ni mbobevu wa sayansi kemia. Kwa kiwango cha usomi wa shahada ya uzamivu katika sayansi hii, yeye ni mtafiti na mzoefu mkubwa wa mambo ya maabara.

Naamini ijapokuwa yupo ktk kipindi cha mapumziko kutokana na majukumu yake makubwa ya taasisi nyeti anayoiongoza. Bado atakuwa anafanya shughuli za kitafiti ktk kutafuta suluhu ya kudumu ya janga hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaàa.......anafanya utafiti kajichimbia maabara kuu ya pale chato
 
Kuna muda nakaaa natafakari nchi hii yupo Rais kweli kwangu mm Rais ni Baba kwa mjibu wa katiba yetu ni mfariji mkuu na huu ni utamaduni wa Duniani kote......sio mara moja Rais wetu majanga makubwa yanapotokea anakuwa yuko kimya saa nyingine anatoa kauli tata rejea tetemeko kule Kagera ama ubomolewaji wa watu wa kimara yote.hii imenipa tabu kumfikiria sana Rais wetu embu angalia kauli zake za ugonjwa wa korona kwamba ni wa kawaida yapo magonjwa mengi mara hatufungi mipaka ndege zije tu,Leo ugonjwa ushasambaa ndio wanazuia ndege
Kama mfariji mkuu wa taifa alitakiwa awe anapata coverage kwenye media juu ya huu ugonjwa angalia Marais wenzake tusiende mbali hapo Rwanda au Kenya au Uganda alafu yy kajipa likizo yupo kijijini kwao ni sawa na Baba kuikimbia familia nyakati za shida kuwa kwake likizo kumepelekea viongozi wadumavu kama makonda mongela kujionesha mbele ya umma
Tumuombe mungu maana Baba kaikimbia familia
Stay home ugonjwa ni hatari ukifa unazikwa na serikali chukua tahadhari



Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tulikosea kumchagua Magufuli uchaguzi ujao tusirudie makosa
 
Tumuombe mungu maana Baba kaikimbia familia
Stay home ugonjwa ni hatari ukifa unazikwa
Screenshot_20200416-211952.png
 
Back
Top Bottom