Imeshika kasi: Tuendelee Ushujaa wa "Ka-Corona, tusitishane, tuchape kazi" tukiteketea; au tubadili msimamo na tusitisishe Mikusanyiko tuokoke?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali,
Kufuatia kuingezeka maradufu wa kasi ya sasa ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona, Je, tuendelee kuupongeza msimamo wa rais Magufuli wa ushujaa wa Ka Corona ni Ka Ugonjwa Kadogo, Tusitishane, Watanzania Tuendelee Kuchapa kazi kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu ya jinsi ya kujikinga huku maambukizi yakizidi kushika kasi, au kwa hali ya sasa, kwa kasi hii ya maambukizi ya Corona ya locally transmissions, sasa tumshinikize rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli, JPM, abadili msimamo, sasa tukubali sio ka Corona ni ugonjwa wa Corona, ni janga na kasi ya kuenea inatisha, hivyo tukubali kutishika, tusitishe mikusanyiko yote yenye misongamano ikiwemo ya nyumba za ibada, tusitishe kesi zote mahakama zote, tuwaachie huru mahabusu wote na wafungwa wote ambao sio hatarishi, na kubadili some strategies ikiwemo kuanzisha some lockdown kwa mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwemo nyumba za ibada, baa, night clubs na maeneo ya starehe ili kuwaokoa watu wetu?.

Declaration of Interest:
Mimi ni mwandishi wa habari, na kunapotokea janga lolote, hatua ya kwanza ni "appreciating the situation" hivyo mimi ni miongoni mwa wale tuliompongeza Rais Magufuli kwa hatua za Tanzania ilizochukua kwa kutotishika na janga la Corona na kumsifia Magufuli shujaa, wakati marais wa nchi jirani wametishwa, wakatishika. Rais Magufuli alionesha ushujaa wa hali ya juu kwa kwa kuonesha assuarance "KaCorona ni kaugonjwa kadogo, tusitishane, Watanzania tuendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga", huku rais Magufuli akionyesha mfano wa kutokutishika kwa kulihutubia taifa siku ya Jumapili ambayo ndio siku ya mapumziko. And then, siku ya Jumatatu ambayo ni siku ya kazi, by basking on the sun recreating himself kwenye majabali ya Ikulu ya Chamwino.

Uandishi sio fani static na conservative kama sheria, ni fani dynamic na current ambayo misimamo ina change with time, place and circumstances, hivyo kwa rate ya maambukizi ya siku zile za mwanzo, kwa uamuzi ule, ni kweli Rais Magufuli alikuwa shujaa wa Corona, ni kweli mwanzo huu ugonjwa wa Corona ulikuwa ni ka ugonjwa kadogo, Watanzania hatukuwa na haja ya kutishika, lakini kwa rate hii tunayokwenda nayo sasa, ya maambukizi ya Corona kwa local transmissions, we seriously need ku-reposition misimamo yetu. Corona sio kaugonjwa kadogo tena, ni liugonjwa likubwa; ni balaa, ni janga la kitaifa na kimataifa. Hatuwezi kukabiliana nalo kwa kuchapa tu kazi with life as usual, now we have to make some sacrifices zikiwemo some lockdown of some sort to save the lives of our people.

Hatua ya kwanza kwa sasa, ni tuzuie mikusanyiko yote isiyo ya lazima ikiwemo mikusanyiko ya nyumba za ibada na sehemu za starehe, bar, nightclubs na kumbi za burudani.

Tusitishe shughuli zote za mikusanyiko mihimu inayoweza kusubiri, hii ni pamoja na kusitisha kesi zote katika mahakama zote, tuwaachie huru mahabusu wote ambao sio hatarishi kwa maisha ya watu; tuwaachie huru wafungwa wote magerezani kote, wakiwemo wafungwa wa vifungo vya maisha, kwa wafungwa hawa na wale wa vifungo virefu, kupewa likizo. Corona ikiisha, watarejea magerezani kwa wafungwa kukamilisha vifungo vyao, mahabusu kurejea kwenye umahabusu wao na kesi kuendelea, na kwa wale ambao watatokomea na kutorejea, ihesabiwe huu ndio mpango wa Mungu kwa watu wake, wala tusihangaike kuwatafuta, tuwahesabu tuu kuwa ni watu wasiojulikana, kama tuweweza kuwaachia wale wasiojulikana wa shambulio la Lissu, tunashindwa nini kuwasamehe mahabusu wote na wafungwa wote, unless miongoni mwao wapo mahabusu na wafungwa waliofanya ukatili mkubwa zaidi ya alichofanyiwa Lissu.

Kwa rate hii ya kasi ya maambukizi ya local transmissions, something must be done differently and quickly to change the situation maana sasa tunaelekea kwa wenzetu, and honestly mwanzo niliamini Corona ni ugonjwa wa Wazungu na wazee, but now...we have to do some changes tusubiri hadi maafa ya kiwango cha juu yatukute ndipo tuchukue hatua hizi.

Ule msimamo wa mwanzo wa rais Magufuli kwa Tanzania ni shujaa wa Corona barani Afrika bado unaendelea, na hata katika vita ukiwa kwenye mstari wa mbele wa mapambano, ukiona kuna dalili ya kuzidiwa, unabakiwa with only two options, uendelee kupigana kishujaa, uangamizwe, uteketezwe ubaki historia ya ushujaa au ukubali matokeo, u retreat or surrender. Kuna mashujaa wa aina mbili, na wote ni mashujaa:

1. Mashuja Wapiganaji Shupavu, hawa ni Fighters, wao kazi yao na motto yao ni ku-Fight, Fight, Fight -- no retreat, no surrender. Pigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike hata kama all will be wiped, mtakuwa mmekufa kishujaa mkipigania taifa lako na mtakumbukwa milele kama mashujaa wa taifa. Ndivyo walivyofanya kina Mkwawa, Mtemi Mirambo, Kinjekitile, na wengine. Je, tuendelee kumchagiza Rais Magufuli kushikilia msimamo huu wa kufa kishujaa na hata Tanzania tukiteketea, tumekufa kishujaa, au?

2. Mashujaa Wapiganaji Makini, hawa ni the Intelligent Fighters ambao hawapekeki askari vitani hadi kwanza wajue nguvu ya adui, ili kuepuka kupeleka vitani askari wake kwenye a loosing battle wakaishia all kuwa wiped out na nchi nzima kugeuzwa mateka.

Kundi hili wakati wakiwa kwenye mstari wa mbele, wakiona dalili na kuzidiwa, kuliko kuendelea kupigana hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike hata kama they'll all be wiped ila watakumbukwa kama mashujaa wa taifa, intelligent fighters, wata retreat kwa kurudi nyuma kwenda kukusanya nguvu na kujijenga upya, au wata surrender na kuchukuliwa mateka hai kuliko mashuja wafu.

Je, sisi Watanzania tungemtaka rais wetu Magufuli awe ni shujaa yupi, shujaa mpiganaji Shupavu au Shujaa Mpiganaji Makini?.

Kama tunamtaka aendelee kuwa mpiganaji shupavu tuendelee hivi hivi hata wote tukiishia kuwa wiped, tutakuwa tumekufa kishujaa kulifia taifa letu.

Au tungemtaka rais wetu awe shujaa mpiganaji makini, kwa hali ilivyo sasa, jee tumshinikize Rais Magufuli kwanza akubali matokeo ni Corona na sio ka Corona, abadili misimamo ya awali kutokana na the escalating situation ya maambukizi ya Corona tubadili strategies tusalimike au tuendelee kushupaza shingo zetu tukielekea machinjioni?

Hitimisho:
Namalizia hoja yangu hii ya bandiko hili. Kwa kasi ya sasa ya Corona; je, tuendelee kumchagiza Rais Magufuli ashikilie msimamo ule ule wa ushujaa wa "Tusitishane, Corona ni kaugonjwa kadogo, Watanzania tusitishike tuendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu ya jinsi ya kujikinga" hivyo japo tunateketea, lakini Rais Magufuli ni shujaa Mpiganaji Shupavu au sasa tukubali matokeo kuwa ni ugonjwa wa Corona na sio ka Corona, ugonjwa unatisha hivyo Rais Magufuli akubali kubadilika, awe Shujaa Mpiganaji Makini, tusitishe mikusanyiko, ibada, starehe, achia mahabusu, wafungwa, before it's too late; au tusubiri idadi ya maafa... ndipo...?

Paskali.
 
Lazima hatua za udhibiti ziongewe ikiwemo kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima hilo ni lazima tulifanye haliepukiki.

Tuache siasa tuchukue hatua kali zaidi kabla maji hayajazidi unga.
 
Mkubwa huwa hakosei, Kama tulikubali haka ni kaugonjwa kadogo kasitutishe, Leo tukisarenda na kulamba matapishi yetu tutaaminika?

Nina imani serikali inamipango mingi na mizuri tuu juu ya kupambana na huu ugonjwa wa Covid19.

Chamsingi tuchukue tahadhari,tuzingatie maelekezo ya serikali na wataalamu wa Afya.
 
Mkuu Paskali, Rais wetu ni mbobevu wa sayansi kemia. Kwa kiwango cha usomi wa shahada ya uzamivu katika sayansi hii, yeye ni mtafiti na mzoefu mkubwa wa mambo ya maabara.

Naamini ijapokuwa yupo ktk kipindi cha mapumziko kutokana na majukumu yake makubwa ya taasisi nyeti anayoiongoza. Bado atakuwa anafanya shughuli za kitafiti ktk kutafuta suluhu ya kudumu ya janga hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuendelee Kumchagiza Rais Magufuli Ashikilie Msimamo Ule Ule wa Ushujaa wa Tusitishane, Corona ni Kaugonjwa Kadogo, Watanzania Tusitishike Tuendelee Kuchapa Kazi kwa Kuzingatia Maelekezo ya Wataalamu ya Jinsi ya Kujikinga
Mpaka sasa tayari jibu lishapatikana mkuu.
 
Hamna kasi tutaudhibiti soon within 1 week, Tatizo wapinzani wa nchi hii ni wavivu sana. Wananchi pigeni kazi.
Strategy ya kuudhibiti toka kwa rais hii hapa

IMG-20200416-WA0008.jpg
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom