Baada ya kupata taarifa rasmi kuwa ZZK amevuliwa nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA, Vyama vinne vinamsaka ili ajiunge navyo na kujiongezea nguvu..
1. CCM
CCM ina kiu ya kumpata ZITTO ili iweze kunyakua majimbo ya KIGOMA... Matumaini ya makada wa CCM ni kumpata Zitto na baadaye Kafulila (swahiba muhimu wa Zitto) kugeuza chuki ya wana Kigoma dhidi ya CCM... MMoja kati ya watu nilioongea naye ni mpinzani mkuu wa Jenista Mhagama - Peramiho - ndani ya CCM (ambaye ni msomi mwenye PHD)... kwa maoni yake Zitto hawezi kupata nafasi za juu ndani ya CCM kwa miaka 15 ijayo ila ni mtu muhimu katika kuirudisha CCM kigoma... "Nafasi ya urais ina watu wengi sana, hawezi kupata".... Ubunge nafasi iko wazi.
2. NCCR Mageuzi
Nimepata maoni ya wafuasi wachache wa NCCR Mageuzi - mmoja ni mfuasi wake aliyekuwa kiongozi wa CDM mkoa wa Mbeya na sasa amehamia Dar kikazi na zaidi ya yote ni mwanachama wa NCCR Mageuzi... Yeye anasema, "tulijua yatatokea haya, tuna matumaini makubwa sana ataungana nasi.... Akija NCCR Mageuzi, ukanda magharibi wote kuanzia Katavi hadi kagera, Mwanza na Shinyanga tunachukua"... Anaongeza kwa kusema, uenyekiti kwa sasa hawezi kupata, ila kugombea urais nafasi iko wazi.
3. CHAUMA
Chama hiki kinaongozwa na Hashim Rungwe (mtu wa Kigoma). Pia kuna taarifa kuwa kuanzishwa kwake kuna mkono wa Kafulila na Zitto Kabwe (wote kutoka mwisho wa Reli)... Chama hiki kinamatumaini makubwa ya kumpata ZITTO... ingawa wanakiri kuwa ni kazi ngumu kukikuza chama hiki kwa muda mfupi uliobaki. "Nafasi yoyote akitaka tunampa" ...
4. CUF
Chama hiki kina mtaka kwa udi na uvumba.. mmoja wa viongozi niliyeongea naye leo - Buguruni.. ameniambia kuwa wanatarajia kupeleka ujumbe rasmi kuonana naye ndani ya wiki hii...... Tukimpata tunaweza kujiimarisha zaidi.