Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,904
- 7,746
Na mie uvivu wangu umetoka wapi?
Mtoa post amewakilisha kilichoandikwa kwenye gazeti...not his idea..Sasa kwa vile ni Zitto mnataka isijadiliwe...mbona JK katoka kwenye gazeti anabembea tayari watu wana comment heavily...kwani JK hajajadiliwa huko nyuma?mbona hamsemi agenda zake zisitishwe?....lets be a little bit democratic...kama issue ya Zitto ilijadiliwa kabla si umredirect mtoa thread easily na sio kukashifu watu..pengine ilipojadiliwa alikuwa sio member wa JF....
Tuache jazba na utemi humu....nasi twaweza pia
Dk. Slaa amvaa Zitto
• Asema CHADEMA ipo tayari kwa uamuzi wowote
na Tamali Vullu
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kipo tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ya kuamua kujiuzulu nyadhifa zote katika chama hicho ama la.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, siku moja baada ya Zitto kukaririwa na vyombo vya habari jana kuwa amekuwa akiandaa barua ya kujiuzulu nyadhifa zote ndani ya chama hicho, ikiwamo na ya ubunge. Zitto pia alituma nakala ya maelezo hayo kwa gazeti hili.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Dk. Slaa alisema tangu Zitto aanze kunukuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa anamuunga mkono aliyekuwa Ofisa Habari wa chama hicho, David Kafulula, amekuwa kimya licha ya kumtumia barua pepe kutaka kufahamu ukweli juu ya suala hilo.
"Zilipotolewa taarifa hizo kwenye vyombo vya habari mama yake Zitto, Shida Salum, alieleza kuwa mwanawe hausiki kwa kuwa e-mail yake imekuwa ikiingiliwa na watu na kutuma ujumbe huo," alisema.
Mama huyo pia aliwasilisha madai hayo katika kamati kuu iliyokutana Desemba 2 na kwamba kutokana na hali hiyo alilazimika kumtumia taarifa kwa barua pepe (e-mail) Zitto ili ampe ukweli wa suala hilo, lakini tangu wakati huo amekuwa kimya.
"Baada ya kutolewa kwa madai hayo na kuwasilishwa katika kamati kuu, Desemba 2, nilimtumia e-mail Zitto, lakini mpaka leo (jana) hajanijibu," alisema Dk. Slaa.
Alisema kutokana na hali hiyo, ameanza kupata wasiwasi kuwa huenda mama huyo anadanganywa na mtoto wake huyo (Zitto).
Hata hivyo, alisema asipopata majibu kutoka kwa Zitto atajua kuwa maelezo hayo yana ukweli na kusema kwamba CHADEMA ni taasisi, haitayumba kwa kuondoka kwa mtu yeyote. "Wakati ule aliondoka Kabourou (Amani Walid Kabourou) na CHADEMA imeendelea kuwapo…anaweza kuondoka Freeman Mbowe na Dk. Slaa, lakini CHADEMA itabaki," alisema.
Aidha, alisema suala hilo linakuzwa ili chama hicho kiachane na ajenda ya kupigania ufisadi nchini na kujikita katika mizozo ya aina hiyo.
"CHADEMA haitaacha kupiga vita ufisadi na ndiyo maana hivi karibuni tumetoa tamko la kuitaka serikali ijibu hoja kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) kuichafua Tanzania kuhusu kupeleka silaha kwa kundi la waaasi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)," alisema Dk. Slaa.
Jana, Zitto alikaririwa na gazeti moja (si Tanzania Daima) kupita barua pepe akieleza kuchukizwa na siasa chafu zinazoendelea ndani ya chama hicho na kwamba yupo tayari kujivua nyadhifa zote ndani ya chama hicho ikiwamo ubunge. Mbunge huyo kijana, alikaririwa akieleza kuwa uamuzi wa kumfukuza Kafulila haukuwa wa haki na kwamba ataendelea kumuunga mkono kama atagombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR - Mageuzi na si mgombea wa CHADEMA. Hivi karibuni, chama hicho kilimtimua Kafulila na Danda Juju, ambao walikuwa wapambe wakuu wa Zitto katika uchaguzi mkuu wa chama hicho, akiwania nafasi ya uenyekiti wa taifa kabla ya kuamua kujitoa badaa ya vikao mbalimbali vya wazee wa chama hicho vilivyomsihi asigombee ili kutokigawa chama katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=11002
Fafanua ndugu yangu, wameishiwa kivipi?Slaa na Mbowe wameishiwa..wanaogopa vivuli vyao..shame on them
wameshindwa ku-handle internal party conflicts itakuwaje waki pewa madaraka!Fafanua ndugu yangu, wameishiwa kivipi?
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kipo tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ya kuamua kujiuzulu nyadhifa zote katika chama hicho ama la.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa
-Tanzania Daima
Zitto,
Kwa maana nyingine ni kuwa uongozi wa juu CHADEMA wanakuambia fungasha uondoke.
Dr. Slaa alishayaongea haya maneno kwenye vyombo vingine vya habari. Lakini naona kaona labda inaonekana kama ni uvumi tu wa vyombo vya habari vinavyoipinga CHADEMA.
Sasa kaamua kwenda kuyanena kwenye gazeti la Mbowe ili pasiwe na utata. Wenzako hawakutaki tena.
Ushauri wangu ni kuwa, usijibu lolote la kwenye vyombo vya habari mpaka wawasiliane na wewe wakifuata taratibu za kiofisi. Jaribu sana ku-avoid vyombo vya habari, watakutega huko. Good lucky.
Mkuu this is very sad kwa upinzani, yaani mnapishana lugha ndani halafu mnajibizana mtaani... tena mbele ya watoto
CHADEMA! You have got to put your act together, enough is enough!!!
My advice kwenu, just give media a black-out, hata kwa hilo gazeti lenu!!
Let their asses be exposed so that we know them better ... what about that!!! Lol!!
Let their asses be exposed so that we know them better ... what about that!!! Lol!!
Zitto,
....
Ushauri wangu ni kuwa, usijibu lolote la kwenye vyombo vya habari mpaka wawasiliane na wewe wakifuata taratibu za kiofisi. Jaribu sana ku-avoid vyombo vya habari, watakutega huko. Good lucky.
Mbona sijakuelewa mkuu, au labda IQ yangu imepungua siku hizi!