I'm Confused, Niolewe ama niendelee kumsubiri?

I'm Confused, Niolewe ama niendelee kumsubiri?

Shida mwanaume kamjibu kua wazae kabla ya haimake sense mtu atake azae lakini ndoa imshinde,so kua baba anaweza kua mume hawezi,huyo dada aolewe kama moyo wake umemruhusu na akili yake ikakubali aolewe tu ya mbele anajua Allah
You are being very logical. Hawa wanaosema asiolewe hata hawana hoja. Eti hoja miaka 23.

Of course binti asiolewe eti kwa sababu mtu kaleta posa, halafu kwani posa mnaielewaje wazee?? Posa inaweza pokelewa na family ya binti ikachukua muda kumchunguza huyo jamaa anaetaka mke.

Posa inaweza kukubaliwa na then walii wa binti akaja akasema kijana hukidhi viwango. Posa ni kishika uchumba tu
 
Hawa wanaume huwa hawamaanishi wanachokisema! Ingekuwa lengo ni mtoto angeshazaa hata kwingine! Pengine ni kumpima tu bidada uwezo wake wa kufikiri!!
Hakuna kitu. Huyo swala anaetaka kumzalisha huyu binti hafai hata kuendelea nae mahusiano. Huyo jamaa hampendi huyu binti take it from me!
 
Watu wa ajabu kabisa! Yaani mnamshauri aache ndoa aendelee kufanya uzinzi?
Huyo mzinzi mwenzie hana future kabisa kwa huyu msichana, ndiyo maaana anataka kumzalisha kinyume na utaratibu. Ushauri wangu kama huyo mtoa posa unahisia nae OLEWA. Pili kuanzia leo achana na huyo mtaka mtoto hana heshima na kawadharau wazazi wako.
Umri ulionao ni muda sahihi wa kuolewa. Asikudanganye mtu eti bado mtoto. Kama mtoto mbona unalalakitanda kisichokuwa cha baba yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake mna nini lakini mnatuperekesha puta kama wajeshi, mapenzi sio vita, yani unataka kuolewa haraka haraka bila subira na kijana mwingine kisa ametaka amekutamkia anakuoa na huyu uliokaa nae miaka miwili kwenye uchumba unaona hafai, sioni sababu ya kukimbilia ndoa kama vipi subiri mwenzako ajipange uliweza kaa nae kipindi chofe hicho mpe muda, wanaume tunapenda tujipange kabla, inaonyesha ulikua unamsaliti maana huyu aliekuja umewezaje kumkubalia haraka ndoa, nakushauri hata ukae miaka 80 hujaolewa wait for the right time cha msingi uolewe na mtu sahihi pia, ndoa zina mambo wewe waulize walioingia kwenye ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Dada yangu alikuwa na boyfriend wakazaa,mimba ina mwezi1 jamaa kaleta posa kabisa lakini hakuoa mpk baada ya miaka miwili sababu anajipanga.

kumbe akawa na mwanamke mwingne na dada pia! Baada ya kuachana na huyo mwingine akamuoa Dada ila badae ya mwezi6 akawa na michepuko mwingine na unasemekana umeathirika! So ndoa imekufa mume hataki kupima!

Huko kujipanga anaona na wengine, hata kama atakuoa anaweza akawa hana mapenzi nawe tena. Kumbuka akimaliza kujipanga na pesa atakuwa nayo

Msome mchumba mpya tabia then ukiridhika olewa!!
 
Kuna msemo hua tunasemaga shahada mwisho ni mara tatu tu, ya mbele hayo ni majukumu ya Mungu hayaingiliwi sote tumo humu hatujui jama jioni tutafika au tukafariki kabla ya kula cha mchana, of course ndoa s kuvaa shela wala pete ibataka kujitoa nyie wahusika yeye mwenyewe kama kishaona anastahili ana watamudu aolewe zake tu wapo watu waliwasubiri wapenzi wao waliowapenda wafikie huko na mtu akawakataa wote abakie na huyo isifae pia bas kama yeye anaona asiolewe na wengine amuoe yeye wakat mwengije riziki hufunguka baada ya ndoa kwa hiyo hata kama miaka 23 midogo akubali kuendelea kuziniwa tu? Huyo kaka amuoe kama anamhitaji wataishi hivo hivo
Congrats! Unatema madini sana kwenye huu juzi

Fahimat msikilize huyu dada yako nakuhusia
 
Sku hizi nimeacha kujiombea peke yangu, namuombea na ubavu wangu kwa pamoja Allah atuepushie mitihani ilo mikubwa, midogo, nisioijua na ninayoijua, mitihani ijayo na ilopita azidi kutudumisha kwa pamoja

Mungu akipenda hiyo long way to go atuzidishie imani, mahaba na uvumilivu ili tuzikane
Amina, nawaombea amani tele

God is a God of hearts
 
Dah,! ,haya ndio madhara ya kuwa na mahusiano kabla ya ndoa,, sehemu kama hiyo mwenyezi Mungu Ndo Hufanya Kazi ,ulianza mahusiano bila Mungu!, unataka umalize bila yeye,?,, maana huo sio utaratibu wake, ndoa sio jaribio, wengi wanatamani nafasi yako wafanye maamuzi sahihi! hujachelewa fanya toba ya kweli ,kulingana na imani yako , ruhusu Mungu afanye kazi hutojuta , Marriage To Be Real, Must Be Spiritually Based!

Umeongea maneno kuntu sana mkuu,agiza soda kwa Mangi hapo mwambie nitalipa.
 
الزَّانِي لَا يَنْكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنْكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharimishwa kwa Waumini.

-Sura An-Nur, Ayah 3
 
Watu wa ajabu kabisa! Yaani mnamshauri aache ndoa aendelee kufanya uzinzi?
Huyo mzinzi mwenzie hana future kabisa kwa huyu msichana, ndiyo maaana anataka kumzalisha kinyume na utaratibu. Ushauri wangu kama huyo mtoa posa unahisia nae OLEWA. Pili kuanzia leo achana na huyo mtaka mtoto hana heshima na kawadharau wazazi wako.
Umri ulionao ni muda sahihi wa kuolewa. Asikudanganye mtu eti bado mtoto. Kama mtoto mbona unalalakitanda kisichokuwa cha baba yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri mzuri sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam wakuu, moja kwa moja kwenye mada, naomba msaada wa kimawazo juu ya hili nalopitia wana jamvi wenzangu. Mm ni msichana miaka 23, nimekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa, (Boyfriend & Girlfriend, kwa maana kwamba sio mahusiano rasmi). Kiukweli nampenda sana huyu mkaka, ananipenda pia anavosema. Lakini tatizo linakuja kwenye Commitment. Mwenzangu anatamani mtoto kabla ya ndoa na mm nataka tupite njia za halali Nusra (Ndoa) kwanza ndo mengine yafuate. Wamekuja vijana watatu kwetu kuniposa sikuwakubalia nikiamini ninae wangu ambae ndo yeye, habari hizo anazijua lakini bado hakutilia maanani,

Sababu ya kutaka ushauri ni kwamba amejitokeza kijana mwingine mwenye nia ya kunioa, nilivompa taarifa kwamba nmeamua nakubali kuolewa kwasabb ya yeye kutonionesha ushirikiano, ananilaumu kwamba nimechukua maamuzi kwaharaka kwanini nisimvumilie. Kiukweli I'm confused, naomba ushauri nimkatae na huyu ili niendelee kumsubiria Boyfriend au ni Move on? Karibuni.

NB: New ID for a Reason. Please don't doubt.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nafikiri umempa nafasi ya kutosha kutafakari. Huyu wa nne akipita inaweza kuwa ndio byebye. #OLEWA.
 
Olewa. Achana na huyo boyfriend. Utakuja nikumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom