I'm Confused, Niolewe ama niendelee kumsubiri?

I'm Confused, Niolewe ama niendelee kumsubiri?

Yaani kama kuna mtu anataka uzae naye kabla ya ndoa basi kama una sumu karibu muwekee tu hana faida kwako, kama kweli ana nia njema na wewe muambie utasubiri huku akiwa amefunga zipu yake.
Kwa aliyekuja kukuposa kama kweli moyo wako umeridhia na umejihakikishia ni mtu mwema kwa uchunguzi wako basi olewa acha hilo jangili liendelee kusubir wa kuzaa naye kabla ya ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona dalili za mshkaji (Aliyeleta posa) kutaka kumuoa mke wa mtu (boyfriend wa mtu). Hapa angoje kusalitiwa tu mana wapenzi hawataachana kamwe isitoshe ni long time relationship yaani wameshibana hawa.
Muhimu Kijana usikurupuke tu kuoa ukaja oa mke wa mtu baadae ukaja ishia kulialia mbona wanawake wako wengi lakini?
 
Rebeca 83 dunia ya sasa wanaanza mambo wakiwa wadogo mnoo, kuna story nyingi humu kuwahusu watoto wa primary. sasa 23 mbona umri mkubwa tu

Kuanza mambo ukiwa mdogo sio sababu, kuolewa sio kuduu peke yake, kuolewa ni lifetime commitment,unaanzisha familia, kulea watoto na familia sio jambo rahisi kama hujakomaa
 
Kama haeleweki olewa na alie nania ya kukuoa utashangaa unafunga 30+ afu mwenzio hana habari na ww

[emoji375][emoji375]
 
Salaam wakuu, moja kwa moja kwenye mada, naomba msaada wa kimawazo juu ya hili nalopitia wana jamvi wenzangu. Mm ni msichana miaka 23, nimekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa, (Boyfriend & Girlfriend, kwa maana kwamba sio mahusiano rasmi). Kiukweli nampenda sana huyu mkaka, ananipenda pia anavosema. Lakini tatizo linakuja kwenye Commitment. Mwenzangu anatamani mtoto kabla ya ndoa na mm nataka tupite njia za halali Nusra (Ndoa) kwanza ndo mengine yafuate. Wamekuja vijana watatu kwetu kuniposa sikuwakubalia nikiamini ninae wangu ambae ndo yeye, habari hizo anazijua lakini bado hakutilia maanani,

Sababu ya kutaka ushauri ni kwamba amejitokeza kijana mwingine mwenye nia ya kunioa, nilivompa taarifa kwamba nmeamua nakubali kuolewa kwasabb ya yeye kutonionesha ushirikiano, ananilaumu kwamba nimechukua maamuzi kwaharaka kwanini nisimvumilie. Kiukweli I'm confused, naomba ushauri nimkatae na huyu ili niendelee kumsubiria Boyfriend au ni Move on? Karibuni.

NB: New ID for a Reason. Please don't doubt.



Sent using Jamii Forums mobile app
Nakushauri uolewe kama huyo muoaji unamwona yuko serious.Usidanganyike kumsubiri kijana asyeonesha commitment ipo siku utajuta,wanawake huenda na time,kadri miaka inavyoenda uzuri wako waweza kuwa unachuja pia.Itafika muda kila kijana hatakuhitaji tena hata huyo unayemsema boyfriend wako.Nakushauri uolewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka wewe ni mtoto wa kiislam basi fanya kama vile ulivyopata mafundisho, mkatalie mtoto wa nje ya ndoa, kwanza mwanao atakosa haki zake nyingi kwa baba yake km atazaliwa nje ya ndoa, wewe mwenyewe halikadhalika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu inawezekana ukawa upo sahihi,lakini issue hapa ni huu utaratibu wa mtu kutaka kupeleka posa kwao na hawafahamiani kabisa hajui tabia zake ?

Ndio tukawa tunajiuliza huu utaratibu wa kizamani bado upo, labda nikuulize Mkuu wewe unaweza kutaka kuoa binti usiyemfahamu kabisa?[/QUOTE
Mimi naweza sababu mwanamke anatakiwa kutii na kuniheshimu halafu Mimi ndio napenda
 
[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13] imebidi nicheke kwa sauti.. huu umri wake jaman anataka ndoa lol..

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha ya ndoa siyo lelemama kwa umri huo bado sana, ila kuna watu wanasema umri huo tayari umri wa mwanamke kuolewa ni kuanzia miaka 27 anakuwa amesha komaa kiakili..

Miaka 23 bado anaakili za kitoto akikaa kwenye ndoa miaka miwili visa vinaanza
 
Sku hizi nimeacha kujiombea peke yangu, namuombea na ubavu wangu kwa pamoja Allah atuepushie mitihani ilo mikubwa, midogo, nisioijua na ninayoijua, mitihani ijayo na ilopita azidi kutudumisha kwa pamoja

Mungu akipenda hiyo long way to go atuzidishie imani, mahaba na uvumilivu ili tuzikane
Bado you ave a long way to go... Ila mtambue ndoa ni baraka na ni mpango wa Mungu na sio shetani, wanawake wasio ndani ya ndoa wanatakiwa wasali sana ili Mungu azidi kumsogeza mtu wako kama chaguo lako..







God is a God of hearts
 
Darasani anafanya nini? Mtu wa miaka 23 anatakiwa awe amemaliza chuo mwaka jana mwezi wa 10.

Wewe ulicheleweshwa shule au ulifeli ukarudia au ukaenda diploma?
Nilitaka kulisema hili. Hivi miaka 23 watu kweli wanachukulia kidogo au mna agenda tu ya pembeni?? Hebu waambie waache uzwazwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom