Ilikuwaje baada ya kukutana nae Live? Yaani face 2 face..

Ilikuwaje baada ya kukutana nae Live? Yaani face 2 face..

Mimi hapa jf tulianza PM, then number za simu, tukawa tunachart, tunaongea, siku nakutana naye kwa kweli sikujuta ingawa relation yetu haikukaa sana, but alikua mcute,bibie ukiiona hii post usininunie sijafanya "name calling"
 
Kwangu ipo tofauti kidogo..
Kwa mara ya kwanza nameet na yule manzi, ilikuwa 2009 pale kigogo mbuyuni. Hakika alikuwa binti mrembo mwenye weupe asilia, mrefu macho yake kama ananikonyeza vile!.. Nilifurahi sana kumuona nae pia alionyesha furaha pia, nawasiliana nae mpaka kesho..
Mkuu mtoto mtamu uyo hakupiga show ya kibabe skuiyo
 
Mie nilikutana nae siku hiyo kila moja akamwona mwenzake tofauti na alivyotegemea yaani kila mtu hakuvutiwa na mwenzake issue ikaishia pale pale kila mtu akapita hivi hakuna aliyemtafuta mwenzeke .Swala la mahusiano mtandaoni sio issue wengi ni vioja mno sitaki hata kusikia.
 
Haya mambo wakati mwingine ni magumu. Nikawa nawasiliana na binti mmoja "moto". Yaani tunaongea masaa kwenye simu zile za tochi mpaka siku zingine ananiambia eti ngoja leo nikulaze naimbiwa vinyimbo vitamu, naelezwa anavyonitamani yaani mzuka balaa. Hatimaye siku ya siku ikafika tukutane yeye anatoka Bagamoyo kuja pale Mlimani. Uwii kumbe ni mmama anayeweza hata kunizaa kabisa. Nikampeleka kwenye kamkahawa fulani pale karibu na kituo cha polisi. Japo alikuwa mweupe na mtako wa kufa mtu lakini sikuwa na mzuka tena kutokana na umri wake. Wakati nampa nauli ya kurudia Bagamoyo nikamuona analia. Kumuuliza vizuri ndo ananiambia yeye ni mwathirika wa UKIMWI na anaomba nimsaidie. To cut the long story short niliendelea kuwa rafiki yake na nilikuwa namtumia vihela vya matumizi kila inapowezekana na alikuwa anamtuma binti yake. Mpaka alipozidiwa akalazwa Muhimbili nikaenda kumuona analia na kunishukuru mno. Hata alipofariki kwenye mazishi yake ndugu zake wananiangalia na kunipa heshima sana. Binti yake alitaka kweli tuwe marafiki lakini nilimkatalia kata kata na hatimaye tukapotezana.

Mkasa huu ulinifundisha mambo mengi na hata kunifanya kuwa binadamu bora zaidi na leo hii passion yangu maishani ni kusaidia watu wasiojiweza kabisa kabisa moja kwa moja. Huko ndiko huwa namalizia disposable income yangu na ni tabia inayoliwaza moyo sana na kuleta ridhiko la kweli. Naamini Mungu Alimtumia yule mama ili kunifundisha kitu na kuyabadilisha maisha yangu. Na kuanzia wakati huo sijawahi kukutana na mtu tunayewasiliana mtandaoni tena!
Duh! Kastory chako kana shule ndani yake nimekapenda[emoji122] [emoji122]
 
Mimi mtu alikosea namba akasema haina neno tuwe marafiki basii kuna kipind mm nikaenda musoma na yy yupo huko nilijutaa kumuona mwanaume andunje mfupii mnoo na mm nilienda na watu wawili mm wa tatu walichekaa rafiki zangu tupoondoka hatukurud tulikula na kunywa tukaaga kurud hakuna alierud
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Andunje mfupi mno
 
Back
Top Bottom