Ilikuwaje baada ya kukutana nae Live? Yaani face 2 face..

Ilikuwaje baada ya kukutana nae Live? Yaani face 2 face..

Haaaa, mm nilikua na chat na bibie flan. Niliiba namba yake kwenye group flan la whatsapp.
Tukaanza kuchat mara kuongea, kuonana, nilistuka sana. Kiukweli sijawahi kuona binti mrembo kama yule, akaniambia Mora amemuonesha mm ndio mme wake.
Nikatuma majeshi anaposoma, anapofanya kaz na anapokaa, wakaleta taarifa yupo Poa.
Mwaka huu tunafunga ndoa baada ya kukaa mwaka kwenye mahusiano
Hongera,,kila mmoja akilizikaa,, huwa poa Sana'a,,ila ukikunbana ya kwetu utabaki unacheka tuy
 
Asante Shunie. Nililelewa na kusomeshwa na single mom tena kwa eka moja ya pamba kila mwaka ili nipate karo ya shule. Makuzi haya ndo yamenifanya niwe hivi nilivyo na heshima na upendo wangu kwa wanawake haumithiliki. Mambo yalipobadilika kwa yule mama nilianza kujiuliza vipi angekuwa ni mamangu, dada au rafiki? Na maisha yetu hapa duniani ni nini kama hatuwasaidii binadamu wenzetu wanaosumbuliwa na magonjwa na madhila mengine ya umasikini? Na hii ndiyo dini ya kweli ati!
Story yako imenisikitisha sana mkuu Mungu azid kukubariki kwa yote unayoyafanya
 
Haaaa, mm nilikua na chat na bibie flan. Niliiba namba yake kwenye group flan la whatsapp.
Tukaanza kuchat mara kuongea, kuonana, nilistuka sana. Kiukweli sijawahi kuona binti mrembo kama yule, akaniambia Mora amemuonesha mm ndio mme wake.
Nikatuma majeshi anaposoma, anapofanya kaz na anapokaa, wakaleta taarifa yupo Poa.
Mwaka huu tunafunga ndoa baada ya kukaa mwaka kwenye mahusiano
[emoji121]
MKUU,
WEKA PICHA NA NAMBA YAKE YA SIMU HAPA ILI TUMPE NASAHA NJEMA.
 
Hamna wewe utapewa first priority
Sasa unarudia makosa yaleyale kwani nyie mshawahi kuonana? Au safari hii unataka ukutane na anaetembea kavaa baby diapers (au mnaita pampers) yaani tayari keshaharibika kabisa bora huyo wa kwanza kalegea mikono na macho tu sio valve ya kuzuia uchafu usichuruzike ovyo?
 
Sasa unarudia makosa yaleyale kwani nyie mshawahi kuonana? Au safari hii unataka ukutane na anaetembea kavaa baby diapers (au mnaita pampers) yaani tayari keshaharibika kabisa bora huyo wa kwanza kalegea mikono na macho tu sio valve ya kuzuia uchafu usichuruzike ovyo?
Eehh kean lazima tuonane, si humu humu jf bhasi not outside
 
Story yako imenisikitisha sana mkuu Mungu azid kukubariki kwa yote unayoyafanya
Usisikitike Shunie. Ni mapito tu ya hapa duniani. Na wakati mwingine, kama vile chuma cha pua, wengine inabidi tupite katika fukuto la mfua vyuma ili tuweze kung'ara huko mbele ya safari. Asante sana!
 
Mimi mtu alikosea namba akasema haina neno tuwe marafiki basii kuna kipind mm nikaenda musoma na yy yupo huko nilijutaa kumuona mwanaume andunje mfupii mnoo na mm nilienda na watu wawili mm wa tatu walichekaa rafiki zangu tupoondoka hatukurud tulikula na kunywa tukaaga kurud hakuna alierud
acha ubaguzi
 
Haya mambo ni magumu. Nikawa nawasiliana na binti mmoja "moto". Yaani tunaongea masaa kwenye simu zile za tochi mpaka siku zingine ananiambia eti ngoja leo nikulaze naimbiwa vinyimbo vitamu, naelezwa anavyonitamani yaani mzuka balaa. Hatimaye siku ya siku ikafika tukutane yeye anatoka Bagamoyo kuja pale Mlimani. Uwii kumbe ni mmama anayeweza hata kunizaa kabisa. Nikampeleka kwenye kamkahawa fulani pale karibu na kituo cha polisi. Japo alikuwa mweupe na mtako wa kufa mtu lakini sikuwa na mzuka tena kutokana na umri wake. Wakati nampa nauli ya kurudia Bagamoyo nikamuona analia. Kumuuliza vizuri ndo ananiambia yeye ni mwathirika wa UKIMWI na anaomba nimsaidie. To cut the wrong story short niliendelea kuwa rafiki yake na nilikuwa namtumia vihela vya matumizi kila inapowezekana na alikuwa anamtuma binti yake. Mpaka alipozidiwa akalazwa Muhimbili nikaenda kumuona analia na kunishukuru mno. Hata alipofariki kwenye mazishi yake ndugu zake wananiangalia na kunipa heshima sana. Binti yake alitaka kweli tuwe marafiki lakini nilimkatalia kata kata na hatimaye tukapotezana.

Mkasa huu ulinifundisha mambo mengi na hata kunifanya kuwa binadamu bora zaidi na leo hii passion yangu maishani ni kusaidia watu wasiojiweza kabisa kabisa moja kwa moja. Huko ndiko huwa namalizia disposable income yangu na ni tabia inayoliwaza moyo sana na kuleta ridhiko la kweli. Naamini Mungu Alimtumia yule mama ili kunifundisha kitu na kuyabadilisha maisha yangu. Na kuanzia wakati huo sijawahi kukutana na mtu tunayewasiliana mtandaoni tena!
Aise basi inabidi mimi nawe mtandao utukutanishe tena lols
 
Sitaki kukumbuka, kuna mkaka nilikuwa nachat nae fb, sasa nilisafir kwenda mkoa furan for my own issues koz na yy yupo huo mkoa so ikabidi tuonane, jmn mm nikawa upande wa pili wa barabara sasa anakuja anavyovuka sasa anakimbia ka mdada, ile kunifikia kumbe ni shoga...lol nilidelete namba ake siku ile ile
hiyo picha kwenye profile ni yako....nauliza tu
 
Nakumbuka ilikuwa 2004,, pind nasoma,, Form,,6 Sengerema,, sec,,Mwanza,, Ndipo Nikaamua kukutana live na Binti,, live Mwanza mjini na binti aliye kosea,, Namba na kunipigia kwenye cm yangu,,ya Philips,,JAMAN,,sijawahi Mbaya mbaya kama huyo,,Et Nilikuwa nimebeba na Marafiki zangu,, Si unajua Kama mnarudi Likizo Nyumbani,, unakuwa na Rafiki,,Ilibidi Nijifiche hapo,tu bandari ya kwenda Bukoba,,Maana hiyo siku ilikuwa siku ya Meli na Kwetu ni Siku ya Treni,,, Kwa kweli nilijifunza mpaka Leo sijawahi shobokea Demu aliyokosea na kunipigia hata kama ana sauti nzuri vipi,,,Hebu Niambie Kama Dada ulifanyaje? Na kama Kaka ulifanyaje? Maana nilijuta hiyo siku,,
Watu wa huko kanda ya ziwa mnapenda kutengeneza hadithi za maisha yenu sana. Yaan hata kama ni kweli utaiweka kama riwaya fulani hivi amazing
 
Back
Top Bottom