Uchaguzi 2020 Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni huru na wa haki

Hawa hata mwenyekiti wa tume angekuwa Edwin Mtei, mkurugenzi wa tume awe Allute Mugwai Lissu wajumbe wawe prof Safari na prof Baregu na ofisi za tume ziwe ufipa wasingeweza kutoboa kwa Magufuli uchaguzi huu.
Mkuu mwaimu Jt, humu duniani, hakuna kitu kizuri kama ukweli wenyewe halisi, huu ndio ukweli wenyewe, naamini hata Lissu mwenyewe, ukweli huu, anaujua kuwa kwa track record ya Magufuli, Tundu Lissu alikuwa hawezi kumshinda kwa kura za Kukubalika, ila kwa kura za kuchangamsha na na za huruma kwa yaliyomtokea.

Huwezi kushindanisha ukweli vs ubatili halafu ubatili ukashinda!.


P
 
Ushauri wako print ukaflash chooni

Taifa hilo bado Lina wajinga sana kupitilizaaa
Hivi ni nchi gani ambayo uchaguzi ulifanyika alafu aliyeshindwa akasema ameshindwa kihalali? Tuanzei nchi za Ulaya, Amerika, Asia, na Mashariki ya Kati na baadaye huku Afrika. Ni vigumu aliyeshindwa kuridhia matokeo kirahisi, hivi karibuni kumekuwa na shida Israel kwa sababu hii hii, vilevile kure Ujerumani! Na sasa hivi tujiandae kuona maajabu huko Marekani wkati Trump atakapokataa matokeo!
 
Nilipenda sana makala na hoja zake zikigusa maeneo mengi. Leo ni upande mmoja tu kusifia.
Nikiona makala yake huwa nasoma tu kichwa naishia.
Mkuu Mzamifu, karibu katika makala hii, uangalie jinsi ninavyosifu!.
P
 
Mkuu fundimchundo , nimeguswa na bandiko lako hili, mimi ni realist, ma realists wote, hata kama hau support kilichofanyika, lakini when kumetokea kitu kilichotokea, and there is nothing anyone can do to change the situation, ma realists wote tunakubali matokeo, katika muktadha wa appreciating the situation and suggest the best way forward out of the situation.

Vyama vya siasa sio mali ya watu, viongozi, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote yatafanywa kwa kutanguliza maslahi ya umma.
Kwenye hili, maslahi ya umma ni kwa wapinzani hao wachache waliopata fursa ya kuingia Bungeni, waingie waka salvage what is left of opposition in Tanzania.

Nimekuleta hapa ili kukujulisha, kuwa tulishauri pia the best way forward, ukitoa ushauri mzuri, hata kama haukufuatwa, wewe unakuwa umetimiza wajibu wako.

Mimi nimetimiza wajibu wangu.
Kama kosa langu ni kuukubali ukweli jinsi ile ulivyo, nalikubali kosa hili.

P
 
Wewe ni adui wa Demokrasia
Siasa tuliosoma zamani tulifundishwa maadui wa Demokrasia ni
1 wapenda madaraka
2 vizabizabina
3 Akina bendera fuata upepo


Paskali bila shaka wewe ni kizabizabina
 
Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru?

Umejibu hili?
Mkuu Kiranga, kwa vile wengi wanauzungumzia uchaguzi based on kilichotokea, mimi nimeanza kuuzungumzia zamani na matokeo ya uchaguzi wa 2020, niliishayajua tangu ile 2015 baada ya Jembe JPM, kuingia ulingoni.
Karibu pande hizi
P
 
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Aisee. Hii kali. Mkuu Paskali sasa nimejua kuwa ingawa huwezi kusema ukweli, lakini ni wazi kwamba umeshazichoka siasa za Tanzania kama wasomi wengi walivyoamua "kuachana"nazo. Lakini wewe, badala ya kuchukua low profile, umeamua sasa kuwakera wale wote ambao bado unaona wana "MATUMAINI HEWA"; ambao bado wanaamini mabadiliko yatatokea hivi karibuni. Sio kwa deception hii. Dah.

Tangu lini wapinzani "ambao ni vichwa vya ukweli" wakaingia bungeni kwa tiketi za uteuzi wa Rais na viti maalum? Usitudanganye. Haiwezekani wewe usahau habari ya "amlipaye mpiga zumari ..."! Halafu, Queen Sendiga naye ni kichwa? Kweli? Mara hii umeshamsahau au kumtelekeza Upendo Peneza? Au rangi imekuchanganya?

Mimi naishia hapa. Wewe endelea na misheni yako ya kuwaudhi wapenzi wa CHADEMA na wote wanaoishi na matumaini "feki" ya kuiona Tanzania bora hivi karibuni. Lakini ingekuwa uungwana zaidi kama ungewaacha na huzuni zao badala ya kuwafanyia kejeli kwa vilio vilivyopitiliza kuliko wenyewe wenye msiba wao. Kwa makala zako tata, usishangae wengi wakikuona mlozi/mchawi kumbe umeamua kuwa sarcastic tu.
 
Pascal nasikitika kukuambia kuwa
Hua nashindwa kukuelewa unashindwaje kuielewa CCM jinsi inavyowatendea wapinzani kinyume kabisa na matakwa ya katiba na wewe unakaa kimya tu.
Mkuu lee van cliff , karibu mitaa hii uone kimya changu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…