Uchaguzi 2020 Ili kuondoa kelele za kutotendewa haki, nawashauri CHADEMA na ACT wekeni Mawakala kila Kituo ili kujiridhisha, Uchaguzi Mkuu ni huru na wa haki

Hawa hata mwenyekiti wa tume angekuwa Edwin Mtei, mkurugenzi wa tume awe Allute Mugwai Lissu wajumbe wawe prof Safari na prof Baregu na ofisi za tume ziwe ufipa wasingeweza kutoboa kwa Magufuli uchaguzi huu.
Mkuu mwaimu Jt, humu duniani, hakuna kitu kizuri kama ukweli wenyewe halisi, huu ndio ukweli wenyewe, naamini hata Lissu mwenyewe, ukweli huu, anaujua kuwa kwa track record ya Magufuli, Tundu Lissu alikuwa hawezi kumshinda kwa kura za Kukubalika, ila kwa kura za kuchangamsha na na za huruma kwa yaliyomtokea.

Huwezi kushindanisha ukweli vs ubatili halafu ubatili ukashinda!.

P
 
Ushauri wako print ukaflash chooni

Taifa hilo bado Lina wajinga sana kupitilizaaa
Hivi ni nchi gani ambayo uchaguzi ulifanyika alafu aliyeshindwa akasema ameshindwa kihalali? Tuanzei nchi za Ulaya, Amerika, Asia, na Mashariki ya Kati na baadaye huku Afrika. Ni vigumu aliyeshindwa kuridhia matokeo kirahisi, hivi karibuni kumekuwa na shida Israel kwa sababu hii hii, vilevile kure Ujerumani! Na sasa hivi tujiandae kuona maajabu huko Marekani wkati Trump atakapokataa matokeo!
 
Wanabodi
  1. Ushauri huu wa bure nimeuekekeza kwa vyama viwili tuu vya Chadema na ACT, kwasababu kwa maoni yangu hivi ndio vyama viwili pekee ambayo vimeonyesha at least some seriousness ya kiasi fulani kwa upinzani, kwa vyama vingine vyote vya upinzani, ikitokea vikashinda hata kiti kimoja cha ubunge au udiwani, ushindi huo utatokana na personal merits za mgombea individually na sio kutokana na strength ya chama chake. Tukiongelea upinzani Tanzania ya leo, tunaongelea Chadema na ACT Wazalendo.
  2. Ukiondoa CCM, hakuna chama kingine chochote cha siasa nchini Tanzania ambacho kina the ability, capacity na capabilities za kusimamisha wagombea majimbo yote na kata zote, hivyo pazia la NEC litakapofungwa, kuna wagombea wa CCM wa ubunge na udiwani watapita bila kupingwa hivyo kwenye majimbo yao, wagombea watatangazwa moja kwa moja na hawatapigiwa kura, ila kura za urais zitapigwa. Hii itakuwa ni dalili ya kwanza ya uthibitisho wa udhaifu wa upinzani wa Tanzania na nyota njema ya dalili ya ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi Mkuu huru na wa haki
  3. Kwa vile zoezi la upigaji kura kwa kura zote zinapigwa vituoni very transparently na zinahesabiwa hapo hapo vituoni very transparently mbele ya mawakala, na matokeo hadi ya urais yanabandikwa kwenye ubao wa matangazo very transparently ili kila mmoja aone,
  4. Hakuna namna yoyote ya kufanya rigging ya matokeo ya kura zilizopigwa vituoni kwa uhuru na uwazi na matokeo yakabandikwa ubaoni.
  5. Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, kuruhusu matokeo yote hadi ya urais kuhesabiwa vituoni na kubandikwa ubaoni, hii maana yake ni NEC inaendesha zoezi la uchaguzi very transparently with no any schemes and nothing to hide.
  6. Na kwa vile CCM itakuwa imepata ushindi wa kishindo, hivyo Bunge lijalo litakuwa ni one party CCM dominated parliament, ili to make sense of Bunge la vyama vingi, tutamshauri mshindi kuwateua baadhi ya alioshindana nao au wapinzani makini kati ya zile nafasi zake 10 za uteuzi ili wakalete changamoto Bungeni ya kulichangamsha Bunge kuonekana ni Bunge la vyama vingi kweli
  7. Na kufuatia Watanzania kuonyesha imani kubwa kwake na kwa CCM, then awamu ijayo, hakuna haja ya kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. He has nothing to loose kwa kuiacha demokrasia ushamiri
  8. Tutapata Tanzania ya neema yenye kuzingatia demokrasia, haki za binaadamu na uhuru mkubwa zaidi wa habari, and if ikimpendeza pia atawapatia Watanzania Katiba mpya, and you never know, anaweza kushangaa, mwaka 2025, nchi inzima ikafanya maandamano kushinikiza ukomo wa vipindi viwili vya urais uondolewe kwasababu katiba ni ya watu na sauti ya watu ni sauti ya Mungu, Vox Pupuli is Vox Dei
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Nilipenda sana makala na hoja zake zikigusa maeneo mengi. Leo ni upande mmoja tu kusifia.
Nikiona makala yake huwa nasoma tu kichwa naishia.
Mkuu Mzamifu, karibu katika makala hii, uangalie jinsi ninavyosifu!.
P
 
Paskali, Paskali, Paskali.
Umepatwa na nini?
Ni Mtanzania gani mwenye akili timamu ambaye anasema kuwa tarehe 28 Oktoba 2020 kulikuwa na Uchaguzi Mkuu?
Ni Mtanzania gani mwenye akili timamu ambaye anakubaliana na "matumizi ya bilioni 350 kwa kile kilichofanyika Oktoba 28'?
Ni Mtanzania gani mwenye akili timamu ambaye anakubaliana na alichokifanya Ndugai na Halima Mdee 'et al'?
Nimeona AG akinukuliwa na Gazeti la Uhuru juu ya haki za Halima Mdee na wenzake!
Mwanasheria Mkuu ambaye aliukunja mkia wake mithili ya mbwa mwoga wakati Tume ya Uchaguzi ikiinajisi Katiba ya Nchi kwa kuhakikisha kuwa Mawakala wa Vyama vya Watu hawaingii kwenye Vituo vya Kupigia Kura.
Ni Mtanzania gani mwenye akili timamu, mwenye uzalendo na nchi yake, mwenye uchungu na masikini wa Nchi hii ambaye anaweza kuunga mkono matumizi ya shs. bilioni 13.68 za mishahara ya Wabunge hao19 kuhalalisha ubatili wa tarehe 28 Oktoba 2020?
Nakumbuka 'novel' ya " Cry, the beloved Country".
Napata faraja nikijifunza kutoka kwenye Historia kuwa "daima, dhuluma itashindwa".
Mungu Ibariki Tanzania
Mkuu fundimchundo , nimeguswa na bandiko lako hili, mimi ni realist, ma realists wote, hata kama hau support kilichofanyika, lakini when kumetokea kitu kilichotokea, and there is nothing anyone can do to change the situation, ma realists wote tunakubali matokeo, katika muktadha wa appreciating the situation and suggest the best way forward out of the situation.

Vyama vya siasa sio mali ya watu, viongozi, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote yatafanywa kwa kutanguliza maslahi ya umma.
Kwenye hili, maslahi ya umma ni kwa wapinzani hao wachache waliopata fursa ya kuingia Bungeni, waingie waka salvage what is left of opposition in Tanzania.

Nimekuleta hapa ili kukujulisha, kuwa tulishauri pia the best way forward, ukitoa ushauri mzuri, hata kama haukufuatwa, wewe unakuwa umetimiza wajibu wako.

Mimi nimetimiza wajibu wangu.
Kama kosa langu ni kuukubali ukweli jinsi ile ulivyo, nalikubali kosa hili.

Wewe ni adui wa Demokrasia
Siasa tuliosoma zamani tulifundishwa maadui wa Demokrasia ni
1 wapenda madaraka
2 vizabizabina
3 Akina bendera fuata upepo

Paskali bila shaka wewe ni kizabizabina
 
Wanabodi
ninatoa ushauri very honestly kwa wapinzani, kuwa ni kweli uchaguzi mkuu huu utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki kama alivyoahidi rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, tumwaminie na tusiwe na shaka yoyote kabisa licha ya yeye pia kuwa mmoja wa wagombea.
  1. Na kwa vile CCM itakuwa imepata ushindi wa kishindo, hivyo Bunge lijalo litakuwa ni one party CCM dominated parliament, ili to make sense of Bunge la vyama vingi, tutamshauri mshindi kuwateua baadhi ya alioshindana nao au wapinzani makini kati ya zile nafasi zake 10 za uteuzi ili wakalete changamoto Bungeni ya kulichangamsha Bunge kuonekana ni Bunge la vyama vingi kweli
  2. Na kufuatia Watanzania kuonyesha imani kubwa kwake na kwa CCM, then awamu ijayo, hakuna haja ya kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. He has nothing to loose kwa kuiacha demokrasia ushamiri
  3. Tutapata Tanzania ya neema yenye kuzingatia demokrasia, haki za binaadamu na uhuru mkubwa zaidi wa habari, and if ikimpendeza pia atawapatia Watanzania Katiba mpya, and you never know, anaweza kushangaa, mwaka 2025, nchi inzima ikafanya maandamano kushinikiza ukomo wa vipindi viwili vya urais uondolewe kwasababu katiba ni ya watu na sauti ya watu ni sauti ya Mungu, Vox Pupuli is Vox Dei
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru?

Umejibu hili?
Mkuu Kiranga, kwa vile wengi wanauzungumzia uchaguzi based on kilichotokea, mimi nimeanza kuuzungumzia zamani na matokeo ya uchaguzi wa 2020, niliishayajua tangu ile 2015 baada ya Jembe JPM, kuingia ulingoni.
Karibu pande hizi
P
 
Wanabodi
Declaration of Interest
Naomba kuanza na ku declare interest kuwa mimi ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM ambaye ni muumini wa haki na demokrasia ya kweli ndani ya Bunge. Nautoa ushauri huu kwa dhati ya moyo wangu, licha ya ukada wangu kwa chama changu, CCM.
  1. Na kwa vile CCM itakuwa imepata ushindi wa kishindo, hivyo Bunge lijalo litakuwa ni one party CCM dominated parliament, ili to make sense of Bunge la vyama vingi, tutamshauri mshindi kuwateua baadhi ya alioshindana nao au wapinzani makini kati ya zile nafasi zake 10 za uteuzi ili wakalete changamoto Bungeni ya kulichangamsha Bunge kuonekana ni Bunge la vyama vingi kweli
  2. Na kufuatia Watanzania kuonyesha imani kubwa kwake na kwa CCM, then awamu ijayo, hakuna haja ya kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. He has nothing to lose and everything to gain, kwa kuiacha demokrasia ushamiri.
  3. Tutapata Tanzania ya neema yenye kuzingatia demokrasia, haki za binaadamu na uhuru mkubwa zaidi wa habari, and if ikimpendeza pia atairekebisha Tume ya Uchaguzi NEC, kuifanya inclusive, na atawapatia Watanzania Katiba mpya, and you never know, anaweza kushangaa, mwaka 2025, nchi inzima ikafanya maandamano kushinikiza ukomo wa vipindi viwili vya urais uondolewe kwasababu katiba ni ya watu na sauti ya watu ni sauti ya Mungu, Vox Pupuli is Vox Dei
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Swali moja rahisi sana kwako Paskali. CHADEMA ikifa, Watanzania na taifa kwa ujumla tutapata hasara gani? Unaamini NI LAZIMA CHADEMA iendelee kuwepo (exist)?

Maelezo yote hayo marefu sana uliyotoa na ambayo umekuwa ukiyatoa zaidi ya mwaka kuhusu CHADEMA, yanadhihirisha kuwa kwa mazingira ya kisiasa tuliyo nayo Tanzania, HAIWEZEKANI tuwe na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini ambao ni BONA FIDE GENUINE.

Halafu, VERY CURIOUSLY, siioni juhudi yako ya dhati kuwaasa wenye dhamana ya kutengeneza mazingira sahihi ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania ili kuwezesha vyama kama CHADEMA kuwepo na kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Hapo ungeeleweka badala ya kupania kwa makala kadhaa zilizojaa jazba nyingi kutaka CHADEMA IWEPO na ikubaliane na dola tu hata katika mazingira hatarishi kiasi gani!

WHAT’S YOUR REAL MOTIVE?
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.

Aisee. Hii kali. Mkuu Paskali sasa nimejua kuwa ingawa huwezi kusema ukweli, lakini ni wazi kwamba umeshazichoka siasa za Tanzania kama wasomi wengi walivyoamua "kuachana"nazo. Lakini wewe, badala ya kuchukua low profile, umeamua sasa kuwakera wale wote ambao bado unaona wana "MATUMAINI HEWA"; ambao bado wanaamini mabadiliko yatatokea hivi karibuni. Sio kwa deception hii. Dah.

Tangu lini wapinzani "ambao ni vichwa vya ukweli" wakaingia bungeni kwa tiketi za uteuzi wa Rais na viti maalum? Usitudanganye. Haiwezekani wewe usahau habari ya "amlipaye mpiga zumari ..."! Halafu, Queen Sendiga naye ni kichwa? Kweli? Mara hii umeshamsahau au kumtelekeza Upendo Peneza? Au rangi imekuchanganya?

Mimi naishia hapa. Wewe endelea na misheni yako ya kuwaudhi wapenzi wa CHADEMA na wote wanaoishi na matumaini "feki" ya kuiona Tanzania bora hivi karibuni. Lakini ingekuwa uungwana zaidi kama ungewaacha na huzuni zao badala ya kuwafanyia kejeli kwa vilio vilivyopitiliza kuliko wenyewe wenye msiba wao. Kwa makala zako tata, usishangae wengi wakikuona mlozi/mchawi kumbe umeamua kuwa sarcastic tu.
 
  1. Na kwa vile CCM itakuwa imepata ushindi wa kishindo, hivyo Bunge lijalo litakuwa ni one party CCM dominated parliament, ili to make a good sense of Bunge la vyama vingi, tutamshauri mshindi JPM, kuwateua baadhi ya alioshindana nao au wapinzani makini kati ya zile nafasi zake 10 za uteuzi ili wakalete changamoto Bungeni ya kulichangamsha Bunge kuonekana ni Bunge la vyama vingi kweli
  2. Na kufuatia Watanzania kuonyesha imani kubwa kwake na kwa CCM, then awamu ijayo, hakuna haja ya kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. JPM ana uwezo wa kuiletea maendeleo Tanzania, na bado akaiachia demokrasia ikashamiri, He'll have nothing to lose and everything to gain kwa kuleta maendeleo, huku akiiiachia demokrasia ushamiri.
  3. Tutapata Tanzania ya neema yenye kuzingatia demokrasia, haki za binaadamu na uhuru mkubwa zaidi wa habari, and if ikimpendeza pia anaweza kuirekebisha Tume ya Uchaguzi NEC, kuifanya more inclusive na funga kazi ni akiisikia sauti Mungu moyoni kwake, kuacha the biggest legacy, ni kama atawapatia Watanzania Katiba mpya, and you never know, anaweza kushangaa, mwaka 2025, nchi inzima ikafanya maandamano kushinikiza ukomo wa vipindi viwili vya urais uondolewe kwasababu katiba ni ya watu na sauti ya watu ni sauti ya Mungu, Vox Populi is Vox Dei
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Pascal nasikitika kukuambia kuwa
Hua nashindwa kukuelewa unashindwaje kuielewa CCM jinsi inavyowatendea wapinzani kinyume kabisa na matakwa ya katiba na wewe unakaa kimya tu.
Mkuu lee van cliff , karibu mitaa hii uone kimya changu.
P
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom