Ilani ya CHADEMA 2010-2015

we uko upande upi?

unaposema Go slaaa unamanisha kweli?

Wewe... read between the line and think out side the box!
Kuwa support CHADEMA haina maana uko ndani kwenye kutengeneza sera, ilani etc. Nimetoa wazo ambalo kwa mtazamo kama wako waweza ona ni dogo. Watendaji waliomo humu should take this positively na kulifanyia kazi, na si la kuonwa kwa mtazamo finyu.

Mkuu soma kati ya mistari.
 
kinachoniudhi ni huko mjini,
hamna umoja kabisa
unafiki tu


Mtu anyeona RA, BM, EL wana haki ndani ya chama. Kiasi cha kuwafanya the biggest fish, wenye kujua rais ajaye atatoka katika kundi gani ni wa kuogopwa kama Cancer na HIV. Edson najua ipo siku utaelewa haya tunayosema. Pole mkuu.:playball:
 
Mwanakijiji ukiipata tuwekee nasi tuione ili kuitumia kuwavunja vunja hawa wanazi wa CCM, naamini mwaka huu CHADEMA wamejipanga vizuri nasi huku vyuo vikuu tuko pamoja kuwasaidia hamna shida.Wamebana wataachia.
 
Huwa sishtuliwi na mambo mengi ya kisiasa; lakini kama nilichokiona kwa macho yangu ndicho kitakachokuwepo kwenye Ilani ya Chadema basi naweza kusema tu kuwa ni ya "kuthubutu, inatisha na inawaweka CCM pabaya". Kama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE". Cheche za Fikra itatoka na exclusive mapema Alhamisi baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Bw. Freeman Mbowe, Tundu Lissu na wengine..

Mwaka huu watu watapigia kura sura au watapigia sera!

yes.. unaitwa "MTANANGE WA DEMOKRASIA"..!!! quote me!
hebu tuwekee hiyo kitu hapa tujilambe
 
Nafikiri hao wanakijiji sasa wanaamka ila si kwa ile rate tuliyotizamia au kufikiria. Sisi tuna wajibu wa kuelimisha jamii wakiwemo hao wanakijiji jinsi gani wanavyokandamizwa na mamlaka chini ya chama tawala.

Mwanakijiji, ukituwekea hiyo kopi hapa mapema naamini utakuwa umefanya jambo la mbolea maana twaweza kupeleka elimu huko vijijini kwa malinganisho ya hizo ILANI za UCHAGUZI ikiwa ni pamoja na dhamira ya hao wanatuomba KURA kwa vyama vyote.
 
Mama yangu anamiaka 75 na kajiandikisha kupiga kura yeye naye anadai hata iweje hakuna chama kama CCM anadai je wewe mwanagu unaweza kunikataa mimi kuwa si mamako,kwake yeye CCM ndiye mama wa siasa na vyama vyote kwa hiyo vyama vingine havina nguvu au ubavu wa kushindana na chama mama,loh nikaishiwa hamu,nikajaribu kumueleza maovu yote yanayofanywa na CCM kwani hata muda wa kunisikiliza hakuwa nao akaniambia we mwanangu lakini kwa hilo la kuisema CCM unaenda mbali akafunga mazungumzo,kwa hiyo ni kweli hata Chadema wangekuja na ilani ya uchaguzi nzuri kiasi gani bado kuna safari ndefu kwa wananchi walio wengi kujua ilani kwanza nini au ina manufaa gani,tukumbuke enzi za Mkapa alisema ilani ya CCM haitekelezeki na bado tukamchagua mgomnea wa CCM kwa kishindo,ingekuwa ni nchi zingine zenye uelewa juu ya Ilani ,CCM ingekuwa isha zikwa zamani kwenye kaburi futi sita ardhini.

Kama ni kweli unashindwa kumconvince mama yako mzazi, basi hapo ndugu yangu mwenye matatizo ni wewe. Mimi nakumbuka vugu vugu la vyama vingi lilivyopokelewa na watu sehemu mbali mbali na hasa vijijini baada ya propaganda za CCM. Wana kijiji ninapotoka waliamini kabisa kuwa hivyo vyama vitaungwa mkono tu na wakorofi watakaowaletea tu vurugu na vita na kwa kweli wengi wa waliojiunga navyo walikuwa ni wale walioshindikana kwenye jamii. Kwa bahati nzuri mimi nilikuwa na mahusiano mazuri na wana kijiji na kila mara nilipofika kijijini wapo wengi tu waliokuja kunisalimia wakitaka kujua kulikoni huko mijini.

Kwa kifupi ndugu yangu mfianchi, sikupata taabu hata kidogo kuwabadilisha mawazo wanakijiji nikianzia kwa wazazi wangu ambao waliijua na kuitambua CCM kuwa ndiyo serikali. Wakigombana ndugu walipelekana ofisi ya CCM, wakidaiana walifikishana ofisi ya CCM, wakiibiwa mifugo waliripoti ofisi ya CCM - yaani kila kitu ni CCM. Najisifu kuwa baada ya kukaa nao kwa wiki moja niliweza kuwafungua macho kwani walianza kwa kujiuliza iweje huyu kijana wetu tunayemfahamu fika kuwa si mtu wa vurugu aunge mkono upinzani ? Kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa 1995, wanakijiji wengi waliweza kuamua kukinyima kura CCM.

Naamini tuliopata bahati ya kufunguka macho na tulio na uchungu na serikali ya CCM inakotupeleka, tukiamua kila moja wetu kwenda kijijini na kila moja kutimiza wajibu wake kwa kuongea nao ana kwa ana, CCM itaangukia pua. Miaka kumi na mitano iliyopita ilikuwa tofauti sana na sasa kwani kwa kiwango mwamko wa wananchi ulikuwa mdogo lakini sasa wananchi wengi wako macho zaidi. Tunayo pia bahati nzuri ya kumpata kiongozi mahiri na anayekubalika na chama ambacho kimeonyesha kujitoa mhanga katika kutetea wanyonge kuliko nyakati za nyuma. La muhimu tujipange kikamilifu kwani hili genge la mafisadi halitakubali kirahisi na litatumia kila mbinu kung'ang'ania kubaki madarakani - tukiwaruhusu tumekwisha.
 
Watu wanaanza kusifia Ilani hata hawajaisoma bado, da mapenzi kweli upofu.

Haya Mwanakijiji, Mtanange ndio nini nishasahau maana yake... Waweza nikumbusha?
 
Mag3,
Hata mimi nina dada yangu pale Mugumu, aliwahi kuwa mwenyekiti wa tawi la CCM. Umri wake ni miaka 72. Lakini amechoshwa na wizi wa CCM na anajua sakata la mbuga za Grumeti na mkuu wa nchi kwenda kupumzika huko kila mara . Amesema hawapigii kura CCM mwaka huu na anasubiri kampeni zianze asaidie CHADEMA.
 
kama wengi walivyosema, watu wengi sio wazuri wa kusoma sana, na hata wakisoma wengi pia sio wazuri wa kuchambua na kuelewa lugha za kisiasa, cha muhimu kampeni ziwe zinatofautiana kutokana na mazingira, kama ukienda kwenye jumuiya ya wasomi nadhani hapo panahitajika uchambuzi wa sera, ukifika vijiji kama vya kilimanjaro ukaongelea mambo ya maji na shule kwa kweli utakosa mshiko , lakini ukifika usukumani na kuongelea mambo ya maji na jinsi utakavyoweza kuwasidia watakuona unaongea cha maana, Sera ziwepo na zitafsiliwe kwa makini, lakini kampeni ya muhimu ni kujua kila eneo lina shida gani na kuielezea udhaifu wa CCM kushindwa kutatua shida zao kwa miaka yote iliyokuwa Madarakani.
 
Kijijini ninakotokea sasa wamebadilika sana, kila nikienda nyumbani huwawananiuliza kuhusu CHADEMA na Dr Slaa. Wanataka kwa dhati mabadiliko ila watu walioenda darasa ndio wanaowakwamisha wakiwaambia CCM itaiba tu hata kama watachagua Chama cha upinzani.

Nafikiri vijijini kuna mabadiliko makubwa kuliko mijini, uwoga wa baadhi ya walioingia darasani ndio tatizo
 
Au ndiyo maana thithiem wanaanza kutuambia mambo ya treni ya umeme???

Mkuu imesahau... mbayuwayu ni bingwa wa kuagiza hata visivyotekelezeka!!! Mwaka jana aliwaambia wana CCM magomeni kuwa... serikali yake inashughulikia suala la traffic jams in Dar, ameagiza wizara ya miundo mbinu ijenge fly overs haraka. Jana nimechekeka sana; taarifa ya habari ya saa mbili usiku mbayuwayu kaagiza tena wizara ya elimu, elimu ya juu, wakae na TCU kuangalia marekebisho ya ada na mfumo wa elimu nchini. Yeye huwa anaagiza tu..... Hatudanganyiki tena.......
 
Huwa sishtuliwi na mambo mengi ya kisiasa; lakini kama nilichokiona kwa macho yangu ndicho kitakachokuwepo kwenye Ilani ya Chadema basi naweza kusema tu kuwa ni ya "kuthubutu, inatisha na inawaweka CCM pabaya". Kama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE". Cheche za Fikra itatoka na exclusive mapema Alhamisi baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Bw. Freeman Mbowe, Tundu Lissu na wengine..

Mwaka huu watu watapigia kura sura au watapigia sera!

yes.. unaitwa "MTANANGE WA DEMOKRASIA"..!!! quote me!

It is an open secret that the majority of the people of Tanzania, educated and uneducated, old and young, are fed up with CCM... My Question has always been, what makes them win despite this obvious fact?

CHADEMA, if they want to be an alternative to CCM, have to identify the source of CCM's long life victory; and then root it out.

The Ilani thing has never been CCM's winning card if my thinking is right; they have so far lacked a strong opponent; but from which perspective? is it their expertise in stealing, cheating, campaigning, rigging,- you name it?

If it is money that makes people vote, CHADEMA kazi mnayo; because all this EPA, DOWANS, RADAR, TANROADS, ... scandals that you know of , plus the ones that you dont know, CCM, like its longer version of a name, ie CHAMA CHA MAJAMBAZI, has a hand in them.

Kama Ilani itakuwa ndio nyenzo ya watu kupigia kura; well, CHADEMA anzisha mbadala wa TOT uanze kuiimba na kuitangaza na mapema; ukisubiri watu waisome, ndugu yangu, kutosoma ni donda sugu Tanzania; at least thats my experience
 
kwani kwenye ilani ya chadema hakuna MAHAKAMA YA KADHI?....wadau tunasubiri hilo ili tuwapigie kura kwani ni jambo la muhimu kwetu waislamu.............sisi,mahakama ya kadhi,oic tunataka vyama ambavyo vitaonesha kipaumbele..........
Huwa sishtuliwi na mambo mengi ya kisiasa; lakini kama nilichokiona kwa macho yangu ndicho kitakachokuwepo kwenye Ilani ya Chadema basi naweza kusema tu kuwa ni ya "kuthubutu, inatisha na inawaweka CCM pabaya". Kama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE". Cheche za Fikra itatoka na exclusive mapema Alhamisi baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Bw. Freeman Mbowe, Tundu Lissu na wengine..

Mwaka huu watu watapigia kura sura au watapigia sera!

yes.. unaitwa "MTANANGE WA DEMOKRASIA"..!!! quote me!
 
Tunauziwa mbuzi kwenye gunia. Unasikia sauti unaambiwa beberu hilo. A policy is any good if it can be implemented.
 
Back
Top Bottom