Simple
JF-Expert Member
- Feb 6, 2009
- 249
- 121
Sera ya Kilimo
Kilimo chetu kidemorora, kwa nini?- Watanzania wengi bado wanalima kwa kutumia jembe la mkono.
- Kilimo bado kinategemea huruma ya mwenyezi Mungu kupata mvua.
- Soko finyu la mazao ya kilimo Mengi yanaozea shambani, au kuuzwa kwa bei ya kutupa.
- Mifumo mibovu ya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.
- Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha ya wakulima wa mazao ya chakula na yale ya biashara.
- Bado tunategemea mazao ya biashara tuliyorithi kutoka kwa wakoloni.
- Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao ya wakulima kuoza kabla ya kufika sokoni.
Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima?
- Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT.
- Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini.
- Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji.
- Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake.
- Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo.
- Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje.
- Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga.
- Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya.
- Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao.
- Tutalinda soko la ndani la bidha zetu.
- Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa.
Naombeni ufafanuzi kwa wanaofahamu data zaidi kuhusu sera hii,,mfano ni jinsi gani ulinzi wa soko letu la ndani utafanyika.