Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,303
- 18,459
"Hii ni Ilani ya CCM ya saba ya uchaguzi mkuu tangu nchi yetu iliporejea katika mfumo wa vyama vingi vya siasa na kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Katika Ilani zote hizi, CCM imeongozwa na Dira ya kuiona Tanzania yenye ustawi kwa wote, nchi inayozingatia na kuheshimu utu, haki na usawa, na Taifa imara linalojitegemea na kuheshimika kimataifa.
Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wenzangu wa Mkutano huu, kama ilivyo kwa vyama vingine vya siasa nchini, CCM ilishiriki na kushirikishwa katika mchakato wa maandalizi ya Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Dira 2050). Aidha, CCM inakubaliana na maudhui ya msingi ya Rasimu ya Dira 2050. Hivyo basi, Ilani hii ni nyenzo ya CCM ya kuanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Ndugu Mwenyekiti: Nieleze kidogo kuhusu mchakato wa kuandaa Ilani hii. Sehemu kubwa ya maudhui ya Ilani hii yametokana na maoni ya wanachama wa CCM, wananchi na wadau mbalimbali. Kwa mfano: Vijana wetu wa UVCCM waliandaa makongamano mbalimbali kutoka pande zote za Tanzania na kutoa maoni yao. Msisitizo wao mkubwa ulikuwa ni kwamba Ilani ije na suluhu ya ajira kwa vijana. Tulikutana na Mabaraza ya Wazee, wanawake na makundi mbalimbali maalum.
Kwa umuhimu wa pekee, nitambue mchango uliotolewa na Asasi za Kiraia (AZAKI). Tumekutana nao mara tatu, tukawasikiliza kwa umakini mkubwa, tukahojiana nao na walitupatia nakala ya Ilani yao. Tumezingatia maoni ya wadau wote.
Ndugu Mwenyekiti: mbali na kukutana na makundi mbalimbali katika kupata maoni, maudhui ya Ilani hii ni matokeo ya utafiti. Kabla ya kuanza zoezi la kuandika Ilani, utafiti mpana ulifanyika uliolenga kukusanya maoni ya wananchi kisayansi kuhusu masuala na maeneo ambayo wangetaka yazingatiwe katika Ilani ya mwaka huu. Kwa kifupi, niseme tu Ndugu Mwenyekiti kwamba, pamoja na kwamba imeandaliwa na CCM, Ilani hii imeakisi matamanio na matarajio ya wananchi. Ni Ilani ya watanzania!"- Prof Kitila Mkumbo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM 2025/30 leo Mei 30, 2025 Mjini Dodoma.