Ilani ya CHADEMA 2010-2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 17, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huwa sishtuliwi na mambo mengi ya kisiasa; lakini kama nilichokiona kwa macho yangu ndicho kitakachokuwepo kwenye Ilani ya Chadema basi naweza kusema tu kuwa ni ya "kuthubutu, inatisha na inawaweka CCM pabaya". Kama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE".

  Mwaka huu watu watapigia kura sura au watapigia sera!


  UPDATE:

  Download ILANI YA CHADEMA 2010 - 2015 kwa kubonyeza hapa
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Shida yenyewe ipo hapa!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aaah Mwanakijiji umeanza ku ballyhoo kama ilivyo kawaida yako.....
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  :glasses-nerdy:
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Changamoto kubwa ipo kwenye uelewa wa watanzania walio wengi juu ya hayo mambo ya ilani na sera za chama. Wananchi wengi hawajui hizi habari, wanachojali wamepata tshirt, khanga na kofia za kijani basi hicho ndo cha maana kwao. Pamoja na ilani hizo nzuri, hakikisheni kwamba na nyie mwaka huu mnawekeza vya kutosha kwenye mabango, tshirt, kofia na khanga. Hayo ndo mambo ya msingi zaidi kwa wananchi wa vijijini.

  Kwa namna moja au nyingine ni vema mkatambua ukweli kwamba mtaji mkubwa wa CCM ni umaskini na ujinga wa watanzania. Ndiyo maana CCM haitakaa ifanye jitihada ya kumaliza umaskini nchini wala jitihada za kupunguza umaskini kwa kuwa hali hiyo ndiyo inayowafanya wao waendelee kutawala. Wanatumia ujinga wa watanzania kuelekeza chuki kwa vyama vya upinzani kwamba ni vyama vya kuleta vita. Wananchi wa kawaida wanaohofia vita hawawezi kukubali kuchagua chama kitakacholeta vita. Kunahitajika elimu na strategy zaidi kuliko sera pekee. Take care.
   
 6. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  chadema oyee! sisiemu ziiii!
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji unaenda mbali saana kwa kuwaza Ilani.

  Kamwe nchi hii, ilani haitaiangusha CCM. Leo hii tuulizane hapa hata kabla yakufika kule vijijini, ni nani aliisoma Ilani ya CCM ya 2005 na nani anaweza kuizungumzia utekelezaji wake! Jibu ni kuwa utashangaa saana. Wengi kati yetu tunapenda kusoma mistari miwili na kufunika na hao ndio tunajiita wasomi. Sasa, vipi kuhusu wanakijiji?

  Matatizo ni makubwa saana katika kujisomea kwa Taifa letu na ndio maana hata umakini hakuna. Tena basi si kusoma tu hata kuandika. Jipe fursa upitie hata magazeti yetu utashangaa.

  Kwahiyo binafsi naona CCM itaondoka madarakani kwa njia za kupayuka tu na kuzungumza na wananchi zaidi juu ya haki zao bila hata ya kuwaeleza ilani inasema nini!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  It is about time. Nchi inahitaji mtikisiko! Nafurahi pia Cheche zinarudi mtaani.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ilani ndio sababu, nia na kuonyesha uwezo wa kutaka kushika madaraka ya kuongoza nchi..

  Hata kama watu wanachagua vichwa safari hii Chadema hawako nyuma sana hivyo ushindani utabakia ktk Ilani za chama. Na kama ujuavyo wananchi wana CHUKI!

  Naogopa tu hiyo chuki ya hawa waitwao Wajinga waliolala, isije kuwa ni zaidi ya kura zao ikawa za Wanyamulembe..
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Aug 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi kuwa Tanzania haina tofauti yoyote na Kenya au Zimbabwe linapokuja swala la uchaguzi. Ni bora kuhakikisha kuwa vyama vyote vinajiimarisha vya kutosha kulinda na kudhibiti na upigaji na uhesabuji wa kura kwa karibu sana.
   
 11. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  WanaJF, mimi niko nje lakini najitahidi kukaa karibu na mikoa yote ya Tanzania kupitia mitandao mbali mbali kama hii, najaribu kuifutilia breaking news toka kwenu na vyanzo vingine vya habari. karibu wiki nzima nimejaribu kuhoji watu mbali mbali katika mikoa ya mbeya(kuna marafiki), Dodoma(kuna marafiki), Shinyanga [Kahama na Kishapu(Home)], mwanza(Nilisoma), Tabora (nilisoma), Dar es salaam ( ninakofanya kazi), Arusha (nimefanya kazi), na Manyara( nimefanya kazi). Watanzania wengi ni wavivu wa kujisomea ndo maana wenye vijarida vyenye vituko wanauza, haviitaji kufikiria sana ni kucheka tu na kusisimuka basi.

  Kote huko nilikuwa naulizia jinsi Chadema ilivyojipanga au upinzani ulivyo nanguvu, cha kusikitisha mkoa wangu (Shinyanga) wanasema wanataka chama cha Nyerere. Iliniuma sana lakini nitafanyeje! nikabaki kutafuta sababu tu, ambayo nimeona niiweke hapa! CCM imefanikiwa kukaa muda mrefu kwa kuwanyima watu elimu bora, inawapa watu elimu ya kuendeleza umasikini badala ya kuwaondelea umaskini.

  Inauma sana kuona mkoa kama shinyanga unakuwa ni kama jimbo la CCM vile. kwa hiyo chadema au vyama vya upinzani tuna kazi, ilani najua itasaidia kwa wajanja wachache, lakini kwenye mikoa kama shinyanga nadhani kuna haja ya kuwafanyia utafiti kabla ya kampeni ili kuweza kuwapa upeo.

  Hiyo ni shinyanga, lakini kuna maeneo kibao,mikoa mingi ya namna ambayo ni kama majimbo ya ccm watu hawaelewei, wanatishiwa vita kama vya rwanda, wanaohongwa, wanaokamatwa na kubambikwa kesi yaani ni uonevu kwenda mbele. Lakini yanawezekana, maisha bila ccm yanawezekana kabisa. TWENDE KAZI chadema.
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  The late J. K. Nyerere commended Chadema to lead the country and now it is a high time to do it!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wananiudhi kweli watu wanaodharau "wanakijiji" wenzangu.. wakati wabunge 60 wa CCM na wengine wamebwaga na wanakijiji hao hao; ni wanakijiji hadi hivi sasa ndio wanaongoza Tanzania kwa kuchagua upinzani! Walio mjini ndio wa kulaumiwa kwa kuendelea kwa utawala wa CCM hivi sasa. Msitushakizie.
   
 14. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Mama yangu anamiaka 75 na kajiandikisha kupiga kura yeye naye anadai hata iweje hakuna chama kama CCM anadai je wewe mwanagu unaweza kunikataa mimi kuwa si mamako, kwake yeye CCM ndiye mama wa siasa na vyama vyote kwa hiyo vyama vingine havina nguvu au ubavu wa kushindana na chama mama.

  Loh nikaishiwa hamu,nikajaribu kumueleza maovu yote yanayofanywa na CCM kwani hata muda wa kunisikiliza hakuwa nao akaniambia we mwanangu lakini kwa hilo la kuisema CCM unaenda mbali akafunga mazungumzo, kwa hiyo ni kweli hata Chadema wangekuja na ilani ya uchaguzi nzuri kiasi gani bado kuna safari ndefu kwa wananchi walio wengi kujua ilani kwanza nini au ina manufaa gani.

  Tukumbuke enzi za Mkapa alisema ilani ya CCM haitekelezeki na bado tukamchagua mgomnea wa CCM kwa kishindo, ingekuwa ni nchi zingine zenye uelewa juu ya Ilani, CCM ingekuwa ishazikwa zamani kwenye kaburi futi sita ardhini.
   
 15. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama kuna watu wanaofikiria kwamba watanzania ni wajinga milele, wasubiri masaa 12 ya tarehe 31 October 2010. Ikiwa refer (Tume ya usimamizi) atakuwa mkweli wa haki sawa kwa wote na atadhibiti itikadi ya kichama ya kuiba kura ili kishindo kionekane, na ikiwa hatamwangalia nyani usoni katika kupiga filimbi, safari hii Tanzania inayo matumaini makubwa kuwaonyesha wanaofkiri wanayo hati miliki ya kuiongoza nchikwamba hawasemi kweli daima.

  Ofcourse huwezi kumdhibiti mwizi 100%, kwani inadaiwa mwizi akifika nyumbani kwako kuiba akakosa ufanikisha zoezi hilo ni lazima afanye uharibifu japo kidogo, ataiba hata kandambili iliyochoka sana iliyosahauliwa mlangoni. Tukiongea sana tunadhaniwa ni mashabiki, so let us wait and see. Time will confirm and tell it all.
   
 16. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama watu hawatapigia kura pilau na pombe za kienyeji, na sh 5000 za kununulia kilo ya nyama
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Babu karibu sana kyadema
   
 18. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kuwa kweli tunasoma kurasa chache halafu tunafunika.

  Sidhani kama hilo linasababishwana uvivu wetu hapana, ni kwa sababu hizo kurasa mbili zote ni pumba, na ni aya zile zile za toka Uhuru na ambazo tumezizoea, kama hivi "mkakati unafanywa ili kuboresha huduma za afya na maji vijijini" Sasa hapo unaniambia nini, what is tangible thing hapo ambacho mimi msomajiwa ilani nitaondoka nacho ili kesho na keshokutwa nikubane wewe mgombea kama ulideliver.

  Na ni aina hiyo hiyo ya staili ya kujibu maswali bungeni, mfano "mchakato unafanywa ili kubaini ni madai gani ya walimu halali na si halali" Seriously, what is that? So ilani ya CCM haina kitu kipya, ina vision ya 2015 na 2025, come one, kama huwezi kuwaondolea wananchi kero leo, utawezaje kuiondoa kero miaka 20 ijayo wakati anayeomba kura hatakuwepo madarakani.

  I can assure you, ilani ya Chadema ikitoka kila mwenye kuipenda na kuitakia tanzania mema atasoma, mbona wengi waliusoma ule waraka wa wakatoliki isipokuwa Kingunge? Kama first two pages zitakuwa pumba kama za CCM then hata hiyo ya Chadema wataifunika tu.

  USIWADHARAU WATANZANIA, WANA AKILI ZA KUTOSHA NDUGU LOL
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sio kweli Mimi mama yangu aliyepiga kura siku zote CCM amesema mwaka huu atapiga Chadema na anajuta miaka yote hiyo alipokuwa mwalimu na kusimamia uchaguzi na kuwasaidia watu wapige CCM. kwa hiyo unategemea una mama wa aina gani na yuko eneo gani
   
 20. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  ilani inataka utekelezaji hivyo kama inatekelezeka tuikaribisha kwa hamu saana
   
Loading...