Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Kuwa na Ilali nzuri ni kitu kimoja, cha muhimu hao CHADEMA wanatakiwa wawe wamejipanga vizuri kuweza kuiuza hiyo ILANI kwenye kampeni zao, vinginenvyo hiyo ilani wataisoma ''MENDE'' tu kwenye makabati na haitakuwa na maana yeyote hata kama ina tisha!
 
Mama yangu anamiaka 75 na kajiandikisha kupiga kura yeye naye anadai hata iweje hakuna chama kama CCM anadai je wewe mwanagu unaweza kunikataa mimi kuwa si mamako, kwake yeye CCM ndiye mama wa siasa na vyama vyote kwa hiyo vyama vingine havina nguvu au ubavu wa kushindana na chama mama.

Loh nikaishiwa hamu,nikajaribu kumueleza maovu yote yanayofanywa na CCM kwani hata muda wa kunisikiliza hakuwa nao akaniambia we mwanangu lakini kwa hilo la kuisema CCM unaenda mbali akafunga mazungumzo, kwa hiyo ni kweli hata Chadema wangekuja na ilani ya uchaguzi nzuri kiasi gani bado kuna safari ndefu kwa wananchi walio wengi kujua ilani kwanza nini au ina manufaa gani.

Tukumbuke enzi za Mkapa alisema ilani ya CCM haitekelezeki na bado tukamchagua mgomnea wa CCM kwa kishindo, ingekuwa ni nchi zingine zenye uelewa juu ya Ilani, CCM ingekuwa ishazikwa zamani kwenye kaburi futi sita ardhini.
Nchi hii siku zote inaangushwa na mikoa ya Mwaza, tabora na Shinyanga. Kuna almost 75% ya wapiga kura halafu hawana uelewa wowote juu ya maswala ya kisiasa, wao bora liende.
 
Sasa ndo hapo mnataka mdahalo la JK ataeleza nn na llani yake ya kiimra?
Ndo maana kaingia mitini aibu atakayo pata na llani yake ataificha wapi!
 
Wananiudhi kweli watu wanaodharau "wanakijiji" wenzangu.. wakati wabunge 60 wa CCM na wengine wamebwaga na wanakijiji hao hao; ni wanakijiji hadi hivi sasa ndio wanaongoza Tanzania kwa kuchagua upinzani! Walio mjini ndio wa kulaumiwa kwa kuendelea kwa utawala wa CCM hivi sasa. Msitushakizie.
Ni kweli kabisa MMkj, hebu angalia Majiji kama Dar na Mwanza, kama kwa huo tunaoita uelewa wao wangeonyesha nguvu zao za kura na kuukataa ubabaishaji wa CCM unadhani hali ingekuwaje? Ngome kuu za upinzani zilipaswa kuwa katika miji mikubwa na sio kama ilivyo sasa.
Na kama majiji yetu yangekuwa na nguvu za upinzani hadithi ingekuwa nyingine kabisa.
 
Licha ya kuwa na ilani nzuri CHADEMA wanatakiwa wajipange kimkakati na watawanye resource zao kwa namna kuwa kunakuwa na group ambazo zitatembelea wananchi wote wa nchi hii ili kuuza sera hizo hasa vijijini. Ukweli ni kuwa Dr Slaa hawezi kupita kila kona ya nchi hii peke yake kwa siku sabini.

Kunatakiwa kuwe na safu ya uhakika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anafikiwa. Hii itasaidia kuondoa woga wa wapiga kura. Watu wengi wanateseka lakini wana hofu ya ccm huko vijijini na wanaogopa usipopigia kura ccm utaadhibiwa. Hii nimeshuhudia katika ziara yangu hivi karibuni Huko vijijini. Baado wananchi wanaambiwa mkichagua upinzani wataleta vita. Hivyo kama mnataka amani chagueni ccm
 
Nina wasiwasi kuwa Tanzania haina tofauti yoyote na Kenya au Zimbabwe linapokuja swala la uchaguzi. Ni bora kuhakikisha kuwa vyama vyote vinajiimarisha vya kutosha kulinda na kudhibiti na upigaji na uhesabuji wa kura kwa karibu sana.

Angalizo/Vision

Chadema wamewashinda CCM kwa kupata Kura nyingi za nafasi ya Rais, na wabunge wengi pia;
Habari mpya ni kwamba sio Chadema walioshinda, ni CCM; Kura za Tanga zilikuwa bado kuhesabiwa wakati tunatoa taarifa ya kwanza


Hilo ni Angalizo tu kwa Chadema nikimaanisha kwamba mipango yote mizuri watakayo panga 'haina maana' kama hakuna mkakati Madhubuti wa kulinda Kura, hata kama mkakati huo utawaudhi baadhi ya watu.. especially the so called 'Wanaharakati wa Human rights'

Get prepared
 
WANAJIANDAA KUCHEZA RAFU, wanajiandaa kwa mikakati yao ya kishetani, CHADEMA ni makini naamini wameng'amua. othewise ccm Wanaenda kushindwa, na wakianguka wale , hawataamka.
 
Tatizo watanzania wengi ni wanafiki...

They say one thing and they act differently...:mad2:
 
wandugu tuwekeeni attachement ya hiyo ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHETU-CHADEMA, 2010
 
Hivi wapiga kura wengi wa Tanzania hasa kule vijijii ambako ushindi wa tsunami wa ssm upo wanafahamu maana ya ilani? For sure watachagua sura na kile walichozoea?? Tatizo ni kwamba wazalendo wengi wenye uelewa wa kupiga kura na maana yake huwa hawapigi kura!!!?? Tuamke sasa, tujitolee katika kulikomboa taifa hili. Yaani tukishindwa tena kufurukuta safari hii basi itachukua muda sana kuiweka ssm chali kwa awamu nyingi zijazo.
 
Changamoto kubwa ipo kwenye uelewa wa watanzania walio wengi juu ya hayo mambo ya ilani na sera za chama. Wananchi wengi hawajui hizi habari, wanachojali wamepata tshirt, khanga na kofia za kijani basi hicho ndo cha maana kwao. Pamoja na ilani hizo nzuri, hakikisheni kwamba na nyie mwaka huu mnawekeza vya kutosha kwenye mabango, tshirt, kofia na khanga. Hayo ndo mambo ya msingi zaidi kwa wananchi wa vijijini.

Kwa namna moja au nyingine ni vema mkatambua ukweli kwamba mtaji mkubwa wa CCM ni umaskini na ujinga wa watanzania. Ndiyo maana CCM haitakaa ifanye jitihada ya kumaliza umaskini nchini wala jitihada za kupunguza umaskini kwa kuwa hali hiyo ndiyo inayowafanya wao waendelee kutawala. Wanatumia ujinga wa watanzania kuelekeza chuki kwa vyama vya upinzani kwamba ni vyama vya kuleta vita. Wananchi wa kawaida wanaohofia vita hawawezi kukubali kuchagua chama kitakacholeta vita. Kunahitajika elimu na strategy zaidi kuliko sera pekee. Take care.
So TRUE. God help us. But sadly , God helps those who help themselves.
 
Wanachohitaji CHADEMA ni mpango madhubuti wakujitangaza...wawe na mawakala kila mahali, especially vijijini.
Wanahitaji KUSIKIKA ili KUELEWEKA ili kuwapa wananchi SABABU YA KUWAPA WAO MADARAKA.Wanatakiwa wawajulishe
watu kwamba CHADEMA IS THE TO GIVE and make their lives better ,NOT TO TAKE and make it worse than it already is...which is what Chama Cha Mafisadi is all about.

PIGA KURA KAMA UNAICHUKIA TANZANIA KAMA ILIVYO NA UNATAMANI MABADILIKO!
 
Mkuu Ilani ndio sababu, nia na kuonyesha uwezo wa kutaka kushika madaraka ya kuongoza nchi..

Hata kama watu wanachagua vichwa safari hii Chadema hawako nyuma sana hivyo ushindani utabakia ktk Ilani za chama. Na kama ujuavyo wananchi wana CHUKI!

Naogopa tu hiyo chuki ya hawa waitwao Wajinga waliolala, isije kuwa ni zaidi ya kura zao ikawa za Wanyamulembe..

Mkuu nakubaliana nawe kuwa watu wana chuki, na hasira, mfano mdogo tu ni chaguzi za Busanda, Tarime, Kiteto na Biharamulo. Hata hao wa vijijini wamechoka na si lazima sana wasome hata wakiambiwa tu itatosha. Kwenye Biblia kuna mstari unaosema "Heri asomaye na kuyasikia maneno ya kitabu hiki". Mimi nasema ambaye hatasoma atasikia na watanzania sasa wako tayari kwa mabadiliko.

Go CHADEMA!!! Go Slaa
 
Huwa sishtuliwi na mambo mengi ya kisiasa; lakini kama nilichokiona kwa macho yangu ndicho kitakachokuwepo kwenye Ilani ya Chadema basi naweza kusema tu kuwa ni ya "kuthubutu, inatisha na inawaweka CCM pabaya". Kama ndiyo hiyo, basi itabidi CCM warudi darasani kuandika Ilani yao upya maana kama watu watapigia kura Ilani.. basi mtanange huu wa demokrasia 'UNOGILE". Cheche za Fikra itatoka na exclusive mapema Alhamisi baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Bw. Freeman Mbowe, Tundu Lissu na wengine..

Mwaka huu watu watapigia kura sura au watapigia sera!

yes.. unaitwa "MTANANGE WA DEMOKRASIA"..!!! quote me!

Timing ya kutoa hizi sera zao ni muhimu sana kuzingatia! Kumbu kumbu zangu bila aibu CCM/CUF walisema wao ndo waanzilishi wa vita vya Ufisadi! Kwasababu hawa CUF-CCM ( naandika hivi kusudi maana kuna ndoa kati yao) wanaweza copy na kuweka kwenye ilani zao. Wasubiri hadi kampeni rasmi zianze.
 
Mwanakijiji unaenda mbali saana kwa kuwaza Ilani. Kamwe nchi hii, ilani haitaiangusha CCM. Leo hii tuulizane hapa hata kabla yakufika kule vijijini, ni nani aliisoma Ilani ya CCM ya 2005 na nani anaweza kuizungumzia utekelezaji wake! Jibu ni kuwa utashangaa saana. Wengi kati yetu tunapenda kusoma mistari miwili na kufunika na hao ndio tunajiita wasomi. Sasa, vipi kuhusu wanakijiji? Matatizo ni makubwa saana katika kujisomea kwa Taifa letu na ndio maana hata umakini hakuna. Tena basi si kusoma tu hata kuandika. Jipe fursa upitie hata magazeti yetu utashangaa. Kwahiyo binafsi naona CCM itaondoka madarakani kwa njia za kupayuka tu na kuzungumza na wananchi zaidi juu ya haki zao bila hata ya kuwaeleza ilani inasema nini!

CHADEMA mliomo humu ndani please take this a challenge and work on it. Tengenezeni ilani version ya kuwawezesha wadanganyika wa kule namanyere kuelewa, i am sure you will defeat them. Go Slaa...
 
Angalizo/Vision

Chadema wamewashinda CCM kwa kupata Kura nyingi za nafasi ya Rais, na wabunge wengi pia;
Habari mpya ni kwamba sio Chadema walioshinda, ni CCM; Kura za Tanga zilikuwa bado kuhesabiwa wakati tunatoa taarifa ya kwanza


Hilo ni Angalizo tu kwa Chadema nikimaanisha kwamba mipango yote mizuri watakayo panga 'haina maana' kama hakuna mkakati Madhubuti wa kulinda Kura, hata kama mkakati huo utawaudhi baadhi ya watu.. especially the so called 'Wanaharakati wa Human rights'

Get prepared

I couldn't agree more...you can get everything right but ukikosea hapo tu umekwenda na maji. What transpired in the primaries epitomizes the magnitude and complexity of the whole problem
 
hahahahaha
wacha nicheke mie

kuna mijitu humu inaonekana ina machungu na nchi hii lakini wapi unafiki tu.

subirini octoba
 
CHADEMA mliomo humu ndani please take this a challenge and work on it. Tengenezeni ilani version ya kuwawezesha wadanganyika wa kule namanyere kuelewa, i am sure you will defeat them. Go Slaa...


we uko upande upi?

unaposema Go slaaa unamanisha kweli?
 
Je wanachama na wakereketwa wa CHADEMA NA SERA ZAKE walijiandikisha kupiga kura? Je, CHADEMA kinaweka takwimu au kumbukumbu ya "potential" wapiga kura wao kiasi kwamba waweze kuwazungukia na kuweka "birika vuguvugu" saa zote , ili siku ya kupiga kura basi kweli wajitokeze kwa wingi kukipigia chama chao kura?
Bila hivyo, ilani itawazingua lakini haitawaletea mabadiliko wanayotamani.Kadhalika, huwezi kutegemea ilani tu ndio iwabadilishe mawazo wanachama wa vyama vingine - ushabiki wa vyama ni kama ushabiki wa vitu vingine iwe ni mpira au mziki kuna loyalty fulani ambayo ni ngumu kuipindua kirahisi.Ndivyo nionavyo mimi.
 
Back
Top Bottom