Ilani ya CHADEMA 2010-2015

It is an open secret that the majority of the people of Tanzania, educated and uneducated, old and young, are fed up with CCM... My Question has always been, what makes them win despite this obvious fact?

CHADEMA, if they want to be an alternative to CCM, have to identify the source of CCM's long life victory; and then root it out.

The Ilani thing has never been CCM's winning card if my thinking is right; they have so far lacked a strong opponent; but from which perspective? is it their expertise in stealing, cheating, campaigning, rigging,- you name it?

If it is money that makes people vote, CHADEMA kazi mnayo; because all this EPA, DOWANS, RADAR, TANROADS, ... scandals that you know of , plus the ones that you dont know, CCM, like its longer version of a name, ie CHAMA CHA MAJAMBAZI, has a hand in them.

Kama Ilani itakuwa ndio nyenzo ya watu kupigia kura; well, CHADEMA anzisha mbadala wa TOT uanze kuiimba na kuitangaza na mapema; ukisubiri watu waisome, ndugu yangu, kutosoma ni donda sugu Tanzania; at least thats my experience

Point to be taken into consideration with CHADEMA i hope. It is true that a secret of their victory should be id'd before hand.
 
Hii ni Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA (2010-2015)
 

Attachments

  • ILANI_CHADEMA_2010-2015.pdf
    321.1 KB · Views: 128
Utoro na Watoto wa kike kuacha shule kwa sababu ya mimba Moja ya tatizo linaloikabili elimu yetu ni utoro wa wanafunzi. Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi umefikia kiwango cha asilimia 35.5, na baadhi ya mikoa na wilaya hadi asilimia 56.7. Takwimu zinaonyesha pia kwamba mimba za utotoni ni moja ya sababu kubwa za watoto wa kike kuacha shule, ambapo asilimia zaidi ya 15 ya watoto wote walioacha shule mwaka 2009 ilisababishwa na mimba za utotoni. Bahati mbaya serikali ya CCM haina jibu ya tatizo hili, zaidi ya Rais Kikwete kuendelea kuwakemea wale wanaowapa watoto wa shule mimba. Kukemea hakuwezi kumaliza tatizo la mimba za utoto, maana waswahili walisema maneno matupu hayavunji mfupa hata kama ni makali kiasi gani. Kinachoshangaza zaidi ni kwamba Rais Kikwete, badala ya kuja na suluhu ya tatizo, anawalaumu watoto wanaopata mimba kwa kuwaambia kuwa wanapata mimba kwa sababu ya ‘kiherehere chao' (Nipashe, Jumatatu, 07 Juni 2010).
 
SURA YA KUMI NA MOJA

VIPENGELE MAALUM

Mpango wa miaka kumi wa kuinua Tanzania

Pamoja na vipaumbele vilivyoanishwa katika sura zilizopita, CHADEMA imeyaanisha maeneo kumi na moja ambayo yatapewa msukumu maalumu. Maeneo haya ni yale ambayo yana umuhimu wa pekee na yakipewa msukumo maalumu yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi na kutokomeza umaskini hapa nchini. Maeneo haya yatatekelezwa kama miradi maalumu ya maendeleo ambayo itasimamiwa moja kwa moja na Serikali.
i) Dar-es-Salaam

Mojawapo ya miradi mikubwa ni ya ujenzi wa jiji la kisasa la Dar ili kulileta jiji letu kubwa zaidi katika ulimwengu wa karne ya ishirini na moja.Katika kuboresha maandhali na makazi katika Jiji la Dar es Salaam, Serikali ya CHADEMA itafanya yafuatayo:
  • Itaanzisha mradi wa ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua na maji machafu ili hatimaye tatizo la mafuriko yanayotokea mara kwa mara na yenye kuharibu miundo mbinu na kuchafua mazingira yakomeshwe. Lengo ni kuhakikisha kuwa katika miaka kumi ijayo Jiji lote la Dar lina mfumo wa kisasa wa kukusanya na kusafirisha maji machafu na ya mvua kutoka kwenye majengo na makazi ya watu.
  • Mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taka utaanzishwa pamoja na kutenga maeneo maalum nje ya jiji ya kutupa taka (madampo). Tutahakikisha kuwa Halmashauri za Manisapaa Jijini Dar es Salaam hazinunui magari ya kawaida ya kukusanya taka kama ilivyo sasa bali tutahakikisha halmashauri hizi zinanunua magari ya ‘compactors' ambayo yanasindilia taka na kuzisaga kabla ya kuzitupa. Hii itasababisha magari kuweza kukusanya taka nyingi zaidi na kwa utaratibu maalum wa siku kwa siku. Wananchi watatakiwa kuhifadhi taka za majumbani katika mifuko maalum ili ziweze kukusanywa katika maeneo ya mitaa yao. Tatizo sugu la katika Jiji la Dar es Salaam ni tabia ya wakazi kuanza kuzoea kuishi na uchafu. Katika kukabiliana na tatizo hili, hatua kali za kisheria zitawekwa kwa wale wanaotupa taka ovyo mitaani.. Pamoja na Halmashauri serikali itaweka utaratibu ili makampuni ya kisasa yenye kuzingatia vigezo vitakavyowekwa yanakuwepo ili kutoa huduma ya kukusanya taka kutoka mitaa, maeneo, na taasisi mbalimbali.
  • Ili kuondoa msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam, tatizo ambalo linasababisha upotevu mkubwa wa muda, kero na uchafuzi wa mazingira, Serikali ya CHADEMA itatekeleza mipango ifuatayo:
i) Kuanza kwa mradi mkubwa wa kutandaza barabara za lami katika Manisapaa zote za Jiji katika maeneo ya makazi ya watu. Hii itaendana na mradi wa urasimishaji wa makazi ya watu ili yaendane na hali ya kisasa.
ii) Ujenzi wa barabara mpya ya kuingia katikati ya Jiji la Dar kutoka Barabara ya Sam Nujoma, Sinza, Tandale na kuweka njia panda ya kisasa eneo la bonde la Jangwani.
iii) Kuanzia Ubungo hadi katikati ya jiji barabara ya Morogoro itaongezewa njia mpya za upande mmoja (unidirectional) zikienda sambamba kutoka na kuingia katikati ya jiji. Bararaba hii (Outer Drive) itakuwa ni kwa ajili ya matumizi ya watu na magari ambayo yana lengo la kuingia sehemu yoyote katikati kabla ya kufika jijini, au magari yanayoharibikia kwenye Morogoro Road. Kwa kujenga njia hizi barabara ya Morogoro itageuzwa na kuwa Express Way kuanzia Ubungo bila ulazima wa kusimama mara kwa mara.
 
Wadau isambazeni kwenye address list zenu ili watanzania wengi wapate fursa ya kuipata. Kuna wengi hawana access ya kuipata hapa
 
Kutoa chakula kwa watoto wa shule za msingi kupunguza utoro na kusinzia madarasani ni jambo jema kwa Elimu yetu.

Kama tungezipata Ilani za CCM na CUF hapa ingekuwa nzuri halafu tunaangalia wanayokubaliana wote, wanayotofautiana, mazuri na mabaya ya kila upande. Kwasababu kwa sasa hivi vyama ndivyo vyenye muelekeo wa kuongoza nchi hii kwa namna moja ama nyingine.
 
Yaani kweli CHADEMA hajajipanga. Wazindua kampeni Jpili lakini mapaka leo hawana Ilana ila wana rasimu tu. Kweli Tanzania ina vyama vya upinzani. sasa nimelewa kwanini wamechelewa kuanza kampeni zao kumbe hata ilani haijakamilika. Bure kabisa

Nani kakwambia bado ni rasimu? Yaani unakurupuka tu?
 
Ni Ilani Nzuri sana... Tatizo ni namna ya kuisambaza na kuhakikisha ujumbe uliomo unawafikia walengwa wapiga Kura wote kabla ya 30/10/2010.
 
Kwa kweli ilani ni nzuri kama kweli wataweza kuitekeleza. Cha kujiuliza itawafikiaje watu wa chini ambao wengi hawataweza kuisoma ilani hii?
 
Naipa tano, imetulia tatizo ni kuisambaza kwa wapiga kura ambao ni wavivu wa kusoma kama mimi hapa. Afadhali leo nimeipitia japo kidogo, ila nina muda wa kutosha.
 
Nimefurahia sana mipango ya makazi na mipangomiji katika ilani hii. Ila tu hawajazungumzia kabisa sheria za mikopo ya nyumba ya muda mrefu [mortgages] . Sheria hii ingekua mkombozi wa kupata makazi bora kwa mamilioni ya watu bila kulazimika kufanya ufisadi. Tujiulize watu wanaojenga majumba ya mabilioni sasa hivi bila kuwa na mortgage wanatoa wapi mapesa hayo? Ni wazi kwamba tusipozungumzia swala hili ufisadi utaendelea hata kama CHADEMA watachukua nchi.
 
Ndio naanza kuisoma hapa. Nime-convert kwenda kwenye PDF. Inapatikana publicly, yani hata kwa wasio members wa JF. Watumie ndugu, jamaa na marafiki.


Thanks Ngolinda.

PS: You can download the file from that link for as many times as you wish, it is on a server with unlimited monthly transfer.
 
Tutumaini tu kuwa CHADEMA watai condence na kuifanya isomeke na kueleweka kwa watu wenye kiwango cha chini kielimu na kiuchumi. MUNGU Kibariki CHADEMA, MUNGU ibariki Tanzania.
 
duh.. watu kweli sharp!!! Lakini nadhani Ilani yenyewe (rasmi) imeweka pembeni mambo mengine..
 
Back
Top Bottom