Ila private sector kuna watu wanakula maisha balaa

Ila private sector kuna watu wanakula maisha balaa

Uzur wa wana jf wakiwa kwenye keyboard hakuna kitu kikubwa kwao, hata ungesema home boy anakunja 10,000,000/= wangesema we hujaona home boy anakunja 15,000,000/= kwenye waleti

Acheni ujinga

Nilitaka kuchangia nikagundua ligi tofauti hii.

Kwanza hela ziwekwe kwenye US $ zikiwekwa kwenye shilingi za Tanzania hela haijafika hata US $ 1,000 inaitwa milioni.

Inatuchanganya tuliozoea kusoma milioni ya kweli (USD) 😂😂😂
 
Nimeshangaa sana na hiyo pesa nimetoka kuacha baa sa hii😅
Sikutaka kuchangia huu uzi ila inabidi,

Bwashee waambie vijana waje huku tukomae na box,
Hilo hela ni income ya siku 4 tu,

Mleta mada unatakiwa ubadilike kifikra na kitabia ili na wewe upige hatua kwenye maisha yako,na kuacha kushangaa vipato vya wengine,kuna kitu kinakukwamisha ila hujakigundua tu bado,
  1. Acha kufuatilia ili kujua mishahara ya watu wengine,haitakusaidia kitu,sana sana inaweza kukukatisha tamaa tu,be yourself,kitendo cha wewe kuanzisha huu uzi na kuweka pay slip ya mtu,kina ashiria kua wewe ni mtu wa aina gani,hapa issue sio kwamba hiyo hela ni nyingi au ndogo,bali ni issue ya wewe mpaka kuanzisha huu uzi kujadili mshahara wa mtu!
  2. Ishi wewe kama wewe,panga mipango yako,malengo,nidhamu na usiri wa mambo yako,usianike mambo yako mitandaoni wala kuanika mambo ya wengine,usipoteze muda wako kufuatilia maisha ya wengine,haitakusaidia kitu,Be yourself.
Good Luck.
 
Kwa ambaye hana hela ataona kubwa sana. Lakini kiukweli hakuna kitu hapo
Upo sahihi kabisa,

Mkuu,hela kua nyingi au ndogo inategemea mtu na mtu na pia inategemea majukumu ya mtu,mipango yake na yupo level ipi kwenye maisha,
So,mleta mada kwa level yake kusema hiyo hela ni nyingi kwake,anakua yupo sahihi,

Ila aache kufuatilia maisha ya wengine,atachelewa sana,
He needs to deal with his own life.
 
Unashangaza🤔
Hii mbona malipo ya kawaida sana?
Tatizo watu wamekariri kuwa ajira za Gvnmnt ni bora sana, lakini siku hizi upepo umebanilika, huko Gvnmnt ndiyo kuna njaa sana na kupiganiana kazi za posho, posho zenyewe ndogo, yani ni shida tupu.
 
Hii ni mbaya sana saaana mkuu. Ukiona mtu anafungua biashara tu ili tu awe na biashara au kisa tu ana mtaji, hiyo biashara kukua katika viwango vikubwa sana sio rahisi kuliko yule anayejua ni nini anakifanya.

Biashara inahitaji mambo mengi sana saaana, inahitaji utulivu wa akili mkubwa na kupiga hesabu vyema haswa.
Watu wanafungua biashara ili na yeye aonekane anafanya biashara ..miaka nenda Rudi , ila maisha yake hayasogei yako pale pale...biashara ya kupata hela ya kula tu...ndio biashara nyingi za bongo..biashara za mazoea ama biashara za kukopi...ni asilimia chache sana wanafanya business wako kwenye channel na wanafanya maendeleo
 
Back
Top Bottom