Kwa kweli mkuu mimi mtu akija akiniomba ushauri kati ya biashara na ajira, moja kwa moja ntamwambia ajira. Ajira ina security kubwa hasa ya serikali.
Biashara ili utoboe haswa unahitaji utulivu na uvumilivu mkubwa, kichwa kinapaswa kitulie kweli kweli mkuu. Biashara sio kitu rahisi kabisa kabisa mkuu.
Ila yote katika yote, kuajiriwa na kujiajiri inategemea na Mungu amekuandikia wapi, kama amekuandikia uajiriwe basi jishikize zaidi tu hapo huku ukitafuta biashara unayoweza kuifatilia na kuifanya vyema. Kuna watu Mungu amewatengenezea namna ya kujiajiri.